Nini kilipelekea vijana wa Tanzania kuteka ndege ya ATC 1982 Mwanza?

Nimekupata mkuu...hata mimi nlivyoisoma hiyo article niliona haipo balanced....lakini nimeiweka ili tu watu watoe changamoto zao...kama kuna source nyengine watu waiweke....kilichonivutia kuhusu hiyo article ni mpangilio wake pamoja na Historia ya watekaji...nlikuwa sijui kuwa watekaji wote walikuwa na uhusiano wa kifamilia

Hakuna kilichoharibika, mkuu! Mbona umetusaidia kuna mengi tu ya kuyachukua hapo na labda isingekuwa wewe kuleta hiyo article mimi nisingekuwa na la kuchangia

Ila nilichojifunza mkuu, enzi za Nyerere habari zote za wapinzani wake aidha hazikuandikwa kabisa au zilipindishwa ili waonekane wabaya. Mfano Abdulrahman Babu ana mchango mkubwa sana kwenye taifa hili. Wakina Kambona, Mtei, etc
 
katika mapumziko ya wiki....leo nawaletea mkasa wa utekwaji wa ndege ya Atcl (1982) Mwanza fungu attachment ufaidi story hii.

Ndege ya Tanzania yatekwa kushinikiza Nyerere ajiuzuluKUTOKANA na hali ya kisiasa ilivyokuwa ikiendelea tangu kupatikana kwa Uhuru waTanganyika, kuna watu walioona kuwa hawaridhishwi na Serikali ya MwalimuNyerere-hasa vijana-kiasi cha kujasiria hata kuteka ndege ya abiria kwa lengo lakuishinikiza Serikali kufuata matakwa yao. Ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania,Boeing 737, ilitekwa mjini Mwanza na vijana watano wa Dar es Salaam.

Huo ulikuwa ni utekaji wa kwanza wa aina yake. Kabla ya hapo kulikuwa na utekajiuliofanywa na Serikali ya Tanzania mara mbili tofauti. Wa kwanza ulikuwa mwaka 1972na mwingine 1979. Lakini huu ulikuwa wa kipekee kabisa. Na ingawa ulikuwa wakisiasa, Serikali ya Tanzania haikutaka ijulikane hivyo.Baada ya maagano na ndugu, jamaa na marafiki, abiria walipanda katika ndege yaShirika la Ndege la Tanzania iliyokuwa na jina la Kilimanjaro, Boeing 737, kwenyeuwanja wa ndege wa Mwanza, Ijumaa ya Februari 26, 1982, saa 11 jioni.Uwanja wa ndege wa Mwanza ulikuwa na sifa mbaya kwa sababu haukuwa na usalamakiasi kwamba baadhi ya marubani walikuwa wakiutaja kama ‘kituo cha basi.'Makundi yaliyokuwa uwanjani hapo yalikuwa ya kawaida kama ya siku zote kwawasafiri wa kwenda Dar es Salaam. Wasafiri wengi walikuwa ni Wahindi, Waarabu naWaafrika wachache. Ingawa mambo yote yalionekana kuwa ya kawaida, jambo dogoliliifanya safari hiyo isiwe ya kawaida.

Ndege ya Kilimanjaro ilipaa angani kutoka uwanjani hapo saa 11.20 jioni ya siku hiyokwa kile kilichotazamiwa kuwa ni safari ya dakika 90 - maili 500, kutoka Mwanza hadiDar es Salaam.Lakini ikageuka kuwa safari ya juma zima - maili 9,500 - na kwa wakati mwingi abiriawa ndege wakisafiri ‘chini ya mtutu wa bunduki' kabla ya kuwasili Dar es Salaam.Dakika tano tu baada ya ndege kupaa angani, vijana wanne walisimama ghafla kwawakati mmoja. Mmoja wao alijipenyeza ghafla katika chumba cha rubani, halafuakaelekeza ‘bastola' yake kwenye kichwa cha mmoja wa marubani wa ndege hiyo,Kapteni Deo Mazula, na kumtaka awapeleke kwenye Uwanja wa Ndege wa JomoKenyatta mjini Nairobi.Baadaye ilikuja kujulikana kuwa majina ya watekaji wale ni Musa Memba (25),Mohamed Ali Abdallah (26) na ndugu yake Abdallah Ali Abdallah (22), Mohamed TahirAhmed (21) na Yassin Memba (21).

Kiongozi wao alikuwa Musa Memba.Wakati huo huo, watekaji nyara wengine, huku wakipunga ‘bastola' zilizotengenezwakwa vigogo vya miti na ‘mabomu' ya kutupwa kwa mkono, waliwatangazia abiria kuwawao ni viongozi wa ‘Vijana wa Harakati za Mapinduzi Tanzania' na kwamba shabahayao ni "kuhakikisha kuwa Rais Julius Nyerere anajiuzulu."Wakati hayo yakitokea, Rais wa Tanzania waliyemtaka ajiuzulu, Mwalimu JuliusNyerere, alikuwa Ikulu mjini Dar es Salaam akijiandaa kurudi nyumbani baada yakupokea risala kutoka kwa Chipukizi nchini waliomwahidi kuwa "Tutaendelea kuwawatiifu, wakakamavu na wenye bidii kwa kuwa tunafahamu mchango wetu unahitajikasana katika ujenzi wa nchi."Mpaka wakati anaondoka kwenda nyumbani kwake, Msasani, akiwa amefurahishwa narisala aliyosomewa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chipukizi, Frank Uhahula (15) wa darasala saba katika Sule ya Mingi ya Tumbi, Kibaha katika mkoa wa Pwani, MwalimuNyerere hakuwa amejua kilichotokea upande mwingine wa nchi -Mwanza.Watekaji nyara hao waliwaamuru abiria wote wakae kimya kwenye viti vyao na kufumbamacho yao na, kwa sababu ambazo hazikujulikana lakini za kustaajabisha,waliwalazimisha watumishi kuzima viyoyozi vya ndege.

Wakati hali ya hewa katikandege hiyo ilipoanza kuwa nzito na kukaribia kutovumilika tena, ndege hiyo ilitua mjiniNairobi kwenye Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta.Lakini katika kipindi cha dakika kadhaa baadaye, Rais Nyerere alipewa taarifa zakutekwa kwa ndege hiyo na kuambiwa kwamba tayari ilishatua Nairobi, Kenya. Waziriwa Mawasiliano na Uchukuzi, John Samuel Malecela, ambaye aliteuliwa rasmikushughulikia utekaji huo, alitumwa kwenda Nairobi kushughulikia tatizo hilo. MwalimuNyerere alitaka kuwa na hakika kwamba Serikali ya Kenya haingeruhusu ndege hiyoiondoke Nairobi.Wakati huo huo polisi wa Kenya wakifunga uwanja wa Ndege wa Kenyatta, na wanajeshiwalisambazwa uwanjani hapo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Robert Ouko,alikuwa uwanjani hapo akitokea Addis Ababa, Ethiopia, wakati ndege ya Tanzaniailipotua.Alipopewa habari za yaliyotokea, Dk Ouko hakusita, alikwenda kwenye chumba chakuongozea ndege kujaribu kushughulikia jambo hilo.

Akizungumza kupitia katika redioya ndege hiyo, mmoja wa watekaji wa ndege hiyo alijitambulisha kwa jina la LuteniWami, ofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania.Alisema kuwa ni lazima Rais Nyerere ajiuzulu vinginevyo ndege hiyo italipuliwa. DkOuko alijaribu kujadiliana na mtekaji huyo, lakini alijibiwa: "Tayari nimeshaua abiriawatatu na nitaendelea kuwaua wengine zaidi."Dk Ouko alistushwa na kauli hiyo. Ilimbidi amsihi mtekaji huyo akimwambia,"Usiendelee kuua zaidi." Lakini ukweli wa mambo ni kwamba hakuna mauaji yoyoteyaliyokuwa yametokea mpaka wakati huo.Kupitia mawasiliano yao ya redio ya upepo, mtekaji huyo alimwambia Waziri Ouko hivi:"Sasa namuua huyu rubani." Rubani mwingine aliyekuwa akisaidiana na Kepteni DeoMazula ni Oscar Mwamwaja (kuna vyombo vingine vya habari vya Ulaya vilimtaja kwajina la Mwangala Jotham).Lakini Dk Ouko akamjibu kwa kumwambia kuwa huo utakuwa ujinga kwa sababu"...rubani huyo atahitajika kuirusha ndege hiyo kwenda kwingineko." Mtekaji huyoakajibu: "N'naweza kuendesha ndege hii mwenyewe. Mimi ni luteni wa anga."Watekaji hao walitaka ndege hiyo ijazwe mafuta kwa ajili ya safari ya kwenda SaudiArabia. Akiwa hana lingine la kufanya, Waziri Ouko alikubaliana na matakwa hayo.Wakati huo huo katika mji wa Dar es Salaam, kumbukumbu za kijeshi zilianzakuchunguzwa kutafuta jina la Luteni Wami. Jina hilo halikupatikana popote.

Walahakukuwa na cheo chochote cha uluteni wa anga katika jeshi la Tanzania..Baada ya ndege hiyo kutua katika uwanja wa ndege wa Nairobi, Waziri wa Mambo yaNje wa Kenya, Dk. Robert Ouko, alijadiliana na watekaji hao lakini mwafakahaukupatikana.Kwa upande mwingine, hata baada ya majina ya watekaji hao kujulikana, Mkurugenzi waUpelelezi wa Makosa ya Jinai katika Jeshi la Polisi Tanzania, Ndugu Lemomo, katikataarifa yake, alisema:...Majina ya vijana hao ni ya kawaida na siyo rahisi kugundua maramoja katika kumbukumbu za Polisi iwapo waliwahi kuhusika na uhalifu wowote."Kadiri muda ulivyosogea, kiwango cha mjadala kati ya Dk Ouko na watekaji kiliwafanyawawe kama wenye wazimu. Mtekaji mmoja aliyedhani kuwa muda unawatupa mkono,kwa hasira kali alifoka: Tutailipua ndege hii sasa hivi ... Tutakufa sasa.

Leteni majeneza100..."Baada ya kuizuia ndege hiyo kwa muda wa saa kadhaa, ilipofika usiku wa mananeSerikali ya Kenya iliona haina la kufanya, na hivyo ikaiachia ndege hiyo iondoke Kenyaikatue nchi nyingine.Kabla haijaondoka, watekaji hao waliiachia familia moja ya Kiarabu ya watu sita kutokakatika ndege hiyo. Mmoja wa mateka hao, Khadija Mohammed Hassan, alisemawaliruhusiwa na watekaji kutoka katika ndege hiyo kwa sababu mtoto wake wa miezi 18,Mselem, alikuwa hanyamazi kulia, na kwa sababu hiyo watekaji walimwona kamaanawasumbua kwa hiyo wakamwacha aondoke.Lakini maofisa wa serikali ya Tanzania waliitilia mashaka familia hiyo.

Wasiwasi huouliongezeka zaidi wakati familia hiyo iliposema kuwa ilikuwa ikisafiri kwenda Dubai, nakwa kuwa tayari walikuwa Kenya, ingekuwa rahisi zaidi kwao kufika huko kupitiaMombasa.Bila wao kutaka, familia nzima ililazimishwa kupanda ndege ya Jeshi la Tanzania nakupelekwa Dar es Salaam. Kesho yake Mwalimu Julius Nyerere, akiwa nyumbani kwakeakitafakari ziara yake ya Pemba ya siku nne ambapo angeweka jiwe la msingi la kiwandacha mafuta ya karafuu, alitaka kujua zaidi yaliyotokea.Ingawa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wa Tanzania, John Malecela, aliwaambiawaandishi wa habari mjini Nairobi kuwa watekaji hao walitaka kujiuzulu kwa MwalimuJulius Nyerere, aliporudi Dar es Salaam alisema watekaji hao hawakutoa madai yoyote.Akiwa kama kiongozi wa kushughulikia utekaji nyara huo, Waziri Malecela alitoa taarifahizo hizo kwa Rais Nyerere;Wateka nyara hawakutoa madai yoyote.

Kwa kuwaamini maofisa wake, Nyerere aliaminipia kile walichomwambia kuhusiana na utekaji huo.Kikundi cha maofisa wa serikali ya Tanzania waliopiga kambi nyumbani kwa MwalimuNyerere, Msasani, kulingana na taarifa walizokuwa wakipokea, walianza kuchukuliakwamba utekaji huo haukuwa na kusudio lolote la kisiasa. Kwa kuwa hawakujua kisahalisi cha kutekwa kwa ndege hiyo, walibuni vya kwao.Walianza kuambizana wenyewe kwa wenyewe; wakamwambia na Rais Nyerere piakwamba ‘inawezekana' watekaji hao walikuwa na kiasi kikubwa cha dhahabu na almasiwalizotaka kuzitoa nchini.Waliamini pia kwamba walitumia utekaji huo kuvusha mali hizo na kwamba familia yaKiarabu iliyotaka kwenda Dubai kupitia Mombasa ilikuwa ni sehemu ya utekaji huo.Namna jambo hilo lilivyoshughulikiwa lilizusha maswali mengi huko Kenya. Dk Oukoalijiingiza katika mjadala na watekaji hao kwa sababu ndiyo kwanza tu naye alikuwaametua uwanjani hapo akitokea mkutanoni Addis Ababa.Siyo kwamba alifika uwanjani hapo rasmi kwa ajili ya hilo.

Ilikuwa ni sadfa tu kwambaOuko alitua uwanjani wakati ule ule ambao ndege iliyotekwa nayo ilitua.Hata hivyo utekaji huo haukutokea wakati mzuri kwa sababu mgogoro kati ya Kenya naTanzania kuhusu Jumuiya ya Afrika Mashariki ulikuwa haujapoa bado.Kitendo cha kuiruhusu ndege hiyo kuondoka mjini Nairobi kiliongeza idadi ya maswali.Lakini serikali ya Kenya haikujiingiza kwa undani katika kulizungumzia sana jambo hilo.Wakati watu wakitafakari kilichotokea, ‘Kilimanjaro' ilikuwa ikiambaa ambaa anganikuelekea Jeddah, Saudi Arabia. Ilipopata habari, Serikali ya Saudi Arabia iliikataliandege hiyo ruhusa ya kutua na kwa kuonyesha kuwa haikuwa ikitania, iliufunga uwanjawake.

Lakini wakati Kapteni Deo Mazula alipowasiliana kwa redio na uwanja huo nakuwaambia kuwa ndege yake imekwisha safiri umbali wa kiasi cha maili 1,600 tanguilipoondoka Nairobi na kwamba haikuwa na mafuta zaidi ambayo yangeiwezeshakuendelea na safari nyingine, serikali ya Saudi Arabia ilifyata mkia.Ndege hiyo iliruhusiwa kutua kwenye uwanja wa ndege wa Jeddah. Ruhusa hiyo ilikuwani kwa ajili ya kujaza mafuta tu. Walinyimwa hata ruhusa ya kufungua mlango wa ndegehiyo.Wakati huu hali ya hewa katika ndege ilishaanza kuwa afadhali. Viyoyozi vilikuwavimeanza kufanya kazi tena na watekaji walijaribu kuwasemesha abiria na kuwaambiashabaha yao ya kuiteka ndege.Lakini ujumbe waliojaribu kuutoa haukueleweka sawa sawa kwa abiria hao.

Watekajiwalijitambulisha kuwa wao ni wanachama wa Harakati za Kidemokrasia za Vijana waTanzania.Waliwaeleza abiria hao kuwa walitaka Rais Julius Nyerere ajiuzulu kwa sababu"Watanzania wanaishi katika hali ya shida na hawana chakula. Hata hivyo, mwisho wamazungumzo yao waliwaambia abiria kuwa wamekusudia kuipeleka ndegeMarekani.Wakati wakisema hivyo, watekaji waligundua kuwa abiria mmoja alitoabastola wakati walipokuwa Uwanja wa Ndege wa Mwanza ambayo ilihifadhiwa katikachumba cha rubani.Ilikuwa ni utaratibu katika viwanja vya ndege vya Tanzania kwa abiria yeyote kutoasilaha yake na kuikabidhi mpaka mwisho wa safari.

Kwa hiyo walimfuata rubani Mazula na kumtaka awape bastola hiyo. Mmoja wao, MusaMemba, alipoipokea alionekana kubabaika kama kwamba hakuwa na ujuzi wowote wanamna ya kuitumia na kuijaza risasi.Alipokuwa amejikunja upande mmoja wa chumba cha rubani akiishika-shika bastola hiyo(pengine akiichunguza na kuishangaa), ghafla ilifyatuka. Risasi iliyofyatuka iliupigamgongo wa rubani msaidizi, Oscar Mwamwaja na kumjeruhi
 

Attachments

  • Ndege ya Tanzania yatekwa.pdf
    145.5 KB · Views: 625
Story ni nzuri kweli, ila mbona ni A to C.....haijafika Z? badilisha heading japo.....maana duh
 
Ingawa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wa Tanzania, John Malecela, aliwaambia waandishi wa habari mjini Nairobi kuwa watekaji hao walitaka kujiuzulu kwa Mwalimu Julius Nyerere, aliporudi Dar es Salaam alisema watekaji hao hawakutoa madai yoyote. Akiwa kama kiongozi wa kushughulikia utekaji nyara huo, Waziri Malecela alitoa taarifa hizo hizo kwa Rais Nyerere;

Hii imenishtua kidogo. Kwa nini 'John' alimdanganya "Julius"
 
Good stuff ila vijana wengi wanaolilia kwenda uropa msiigize mtaumia. It was possible then not now. Maskini Memba mwenyewe alikolimbwa hivi hivi!
 
........Baadaye ilikuja kujulikana kuwa majina ya watekaji wale ni Musa Memba (25), Mohamed Ali Abdallah (26) na ndugu yake Abdallah Ali Abdallah (22), Mohamed Tahir Ahmed (21) na Yassin Memba (21). Kiongozi wao alikuwa Musa Memba............

Haya majina haya, mmmmmh ila coz ilikuwa serikali ya jembe basi waliipata fresh

 
Nasikia harufu ya al-shabab-shabab!
........Baadaye ilikuja kujulikana kuwa majina ya watekaji wale ni Musa Memba (25), Mohamed Ali Abdallah (26) na ndugu yake Abdallah Ali Abdallah (22), Mohamed Tahir Ahmed (21) na Yassin Memba (21). Kiongozi wao alikuwa Musa Memba............

Haya majina haya, mmmmmh ila coz ilikuwa serikali ya jembe basi waliipata fresh

 
Linatajwa kuwa moja ya majaribio yenye kustua vyombo vya dola vya nchi hii na linafananishwa na tukio la mnamo February 27, 1982 mjini Jidda lililoongozwa na Mousa Memba aliyekuja kufariki mwaka 1992 akiwa jela hapa Dar es Salaam


Japokuwa hadithi hubadilika badilika kila mtu akikusimulia, lakini kisa kinaelezwa hivi:

Vijana wanne wakizanzibar
waliovamia safari ya ndege ya Tz kutoka Zanzibar kuelekea Arusha, waliamua kuiteka ndege hiyo kabla ya kutua Arusha na kumwamuru rubani wa ndege hiyo awapeleke Ulaya,

Kutokana na kipigo, rubani alikubali na kuanza safari ya Ulaya,

Kinyume chake rubani aliwaleta Dar, akawaambia wapo nchi ya Ulaya huko na mafuta wameishiwa hivyo anatua ili wajaze mafuta,

Baada ya ndege kutua uwanja wa ndege Dar ulikuwa tayari upo chini ya ulinzi mkali, na wale vijana walikamatwa kama kuku kwani hawakuwa na silaha yoyote zaidi ya kisu, maembe dodo ambayo waliyatumia kama mambomu na bastola za bandia

Kiasi kwamba vijana walifanikiwa kuwatisha abiria wote nao wakaamini kuwa vijana wale walikuwa na mabomu na bastola kumbe matoi tu!

Japokuwa propaganda za kimagharibi zilibadili malengo ya watekaji ya kutaka kupelekwa Ulaya, sasa wao leo wanasema kuwa vijana waliiteka ndege ile ya Tz kwa lengo la kutaka Mwalimu Nyerere ajiuzuru wadhifa wake:

Hili linarudisha fikra zetu tujiulize kuwa viwanja vyetu vya ndege vinausalama wakutosha?
 
Linatajwa kuwa moja ya majaribio yenye kustua vyombo vya dola vya nchi hii,

Japokuwa hadithi hubadilika badilika kila mtu akikusimulia, lakini kisa kinaelezwa hivi:

Vijana wanne wakizanzibar waliovamia safari kutoka Zanzibar kuelekea Arusha, waliamua kuiteka ndege hiyo kabla ya kutua Arusha na kumwamuru rubani wa ndege hiyo awapeleke Ulaya,

Kutokana na kipigo, rubani alikubali na kuanza safari ya Ulaya,

Kinyume chake rubani aliwaleta Dar, akawaambia wapo nchi ya Ulaya huko na mafuta wameishiwa hivyo anatua ili wajaze mafuta,

Baada ya ndege kutua uwanja wa ndege Dar ulikuwa tayari upo chini ya ulinzi mkali, na wale vijana walikamatwa kama kuku kwani hawakuwa na silaha yoyote zaidi ya kisu, maembe dodo ambayo waliyatumia kama mambomu na bastola za bandia

Kiasi kwamba vijana walifanikiwa kuwatisha abiria wote nao wakaamini kuwa vijana wale walikuwa na mabomu na bastola kumbe matoi tu!

Hili linarudisha fikra zetu tujiulize kuwa viwanja vyetu vya ndege vinausalama wakutosha?


Mkuu wengine tunakosa fursa zaidi kwenye vyombo vya habari kwa mihangaiko.

Ongeza nyama kidogo, talehe gani/lini, akina nani kama majina yanaeleweka na hatuagani kama unataarifa zilifikiwa/chukuliwa zaidi.

Asante kwa taarifa mkuu.
 
Hao watekaji walishindwa hata kuchungulia madirishani kuona wako wapi?

They were fools.
 
Mbona hii story niliwasikia clouds fm hawa jamaa na kama sikosei walisema walitua Arusha wakajua washaa fika!
 
Umechanganya matukio mawili tofauti.

Utekaji wa ndege umetokea mara mbili hapa nchini.
 
Back
Top Bottom