Nini kifanyike kurudisha uhuru wa mtanzania

mkezwag

JF-Expert Member
Nov 15, 2011
3,245
1,080
Tanzania ni nchi huru,na hivyo hivyo watu wake wanapaswa kuwa huru katika kufanya maamuzi mbalimbali yanayo husu nchi yao na maisha yao kwa ujumla wake.Chakushangaza ni kama uhuru huo umetekwa na kuchukuliwa na watu wachache,ndiyo maana ukipita majimboni utasikia watu wakisema mbunge wao kapita kwa kuchakachua na si ridhaa yao,Wiki iliyopita tulishuhudia muswada wa wa marekebisho ya katiba ukipitishwa huku wananchi wengi mijini na vijijini wakilalamika hawakushirikishwa.Kundi la watu wachache wametufanyia maamuzi kwa mara nyingine,wapo wanaoamini hata Rais alichakachua kura ndiyo maana akaukwa urais.

Je kulalamika au kuendelea kulalamikia wasiosikia ni suluhisho?je nini kifanyike kurudisha uhuru wa Mtanzania wa Kawaida kujiamulia mambo yake,kama vile uhuru kamili(si uhuru kivuli) wa kuchagua nani amuongoze
 
Muswaada ule ni wa katiba ya ccm na cuf sii watanzania!iweje maoni ya dodoma dar na zanzibar useme ya watanzania?hiyo ni dharau kwa kabila la wasukuma walio wengi kuliko makabila yote kutotoa maoni
 
Back
Top Bottom