Nini kifanyike kunusuru nchi yetu?

Mjomba wa taifa

JF-Expert Member
Apr 20, 2012
231
161
Tangu kuingia madarakani kwa serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Kikwete kumekuwa na udhaifu mkubwa unaojidhihirisha hadi kufikia baadhi ya wabunge kutamka waziwazi pasipo kupepesa macho wala kumung'unya maneno ndani ya ukumbi wa bunge kuwa Rais ni dhaifu.

Hivi tatizo lipo wapi? kwa Rais? au watendaji wake ndio dhaifu? au wananchi ndio dhaifu?

Ni vyema tuone tumejikwaa wapi ili tusijerudia tena makosa haya.

Mheshimiwa Pinda aliwahi kutamka kuwa Rais Kikwete amekuwa mpole sana, je ni kweli? Nini tofauti ya upole na udhaifu?

Ni fursa kwa wana-JF kuchambua idara/eneo moja baada ya jingine na kutoa ufumbuzi nini kifanyike kunusuru taifa letu japo kwa eneo hata moja kwa kila mmoja.

ikumbukwe kuwa Kanzu ya Ijumaa hufuliwa Alhamis.
 
Udhaifu mkubwa upo kwa rais kwani kateuwa timu yake isiyokuwa na maslahi kwa taifa. Pia waTZ wote ni dhaifu kwakutojua wajibu wao na kushindwa kuhoji pale serikali inapoboronga
 
Tangu kuingia madarakani kwa serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Kikwete kumekuwa na udhaifu mkubwa unaojidhihirisha hadi kufikia baadhi ya wabunge kutamka waziwazi pasipo kupepesa macho wala kumung'unya maneno ndani ya ukumbi wa bunge kuwa Rais ni dhaifu.

Hivi tatizo lipo wapi? kwa Rais? au watendaji wake ndio dhaifu? au wananchi ndio dhaifu?

Ni vyema tuone tumejikwaa wapi ili tusijerudia tena makosa haya.

Mheshimiwa Pinda aliwahi kutamka kuwa Rais Kikwete amekuwa mpole sana, je ni kweli? Nini tofauti ya upole na udhaifu?

Ni fursa kwa wana-JF kuchambua idara/eneo moja baada ya jingine na kutoa ufumbuzi nini kifanyike kunusuru taifa letu japo kwa eneo hata moja kwa kila mmoja.

ikumbukwe kuwa Kanzu ya Ijumaa hufuliwa Alhamis.

Dhaifu wewe ambaye hujui kupambanua wanasiasa wanaotaka umaarufu na wanasiasa wenye hoja. Hivi na wewe unakubali kuwa JK ni dhaifu? Mnyika alikuwa anataka kujirudisha kwenye kiwango baada ya kashfa ya wizi wa kura jimboni kwake.
VIVA JK.
 
kinachotakiwa hapo ni kubadilika kwa mfumo mzima kuanzia presedent mpaka grass root that will be best way to clear our nation.
 
Sio kosa lako Mamaisara bado mgeni JF. Kuna tofauti kubwa kati ya blog za udaku na JF.
 
Hivi inaingia akilini gas ya mtwara ijengewe bomba ije kutumika daslam?
 
Tangu kuingia madarakani kwa serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Kikwete kumekuwa na udhaifu mkubwa unaojidhihirisha hadi kufikia baadhi ya wabunge kutamka waziwazi pasipo kupepesa macho wala kumung'unya maneno ndani ya ukumbi wa bunge kuwa Rais ni dhaifu.

Hivi tatizo lipo wapi? kwa Rais? au watendaji wake ndio dhaifu? au wananchi ndio dhaifu?

Ni vyema tuone tumejikwaa wapi ili tusijerudia tena makosa haya.

Mheshimiwa Pinda aliwahi kutamka kuwa Rais Kikwete amekuwa mpole sana, je ni kweli? Nini tofauti ya upole na udhaifu?

Ni fursa kwa wana-JF kuchambua idara/eneo moja baada ya jingine na kutoa ufumbuzi nini kifanyike kunusuru taifa letu japo kwa eneo hata moja kwa kila mmoja.

ikumbukwe kuwa Kanzu ya Ijumaa hufuliwa Alhamis.

mi naona ni mwendelezo tu wa serkal za nyuma
 
Mjomba wa taifa Mkuu, mada yako ni nzuri na muhimu sana, lakini kwanza ingependeza ungeikuza kidogo na ingefaa zaidi kuipeleka kule kwa Great Thinkers ambako itachambuliwa na kujadiliwa kwa kina, bila udaku.

Pia ninakuomba (na wengine) kupitia angalau moja ya mada hizi za:
https://www.jamiiforums.com/great-thinkers/256191-mawaziri-ovyo-wa-ccm-wapi-tunakosea-kama-nchi.html
https://www.jamiiforums.com/great-thinkers/227287-kwanini-mikoa-yetu-haiendelei-kiuchumi.html
https://www.jamiiforums.com/great-thinkers/38756-kwanini-watanzania-ni-maskini.html
https://www.jamiiforums.com/great-t...ado-ni-chama-cha-wakulima-na-wafanyakazi.html
 
Dhaifu wewe ambaye hujui kupambanua wanasiasa wanaotaka umaarufu na wanasiasa wenye hoja. Hivi na wewe unakubali kuwa JK ni dhaifu? Mnyika alikuwa anataka kujirudisha kwenye kiwango baada ya kashfa ya wizi wa kura jimboni kwake.
VIVA JK.

Uharo wa nguruwe..
 
Sio kosa lako Mamaisara bado mgeni JF. Kuna tofauti kubwa kati ya blog za udaku na JF.

Unamwambia huyo aliyerusha thread au mimi? manake naona yeye ndo kaposti thread ki-udaku zaidi. Anataka kutuambia kuwa anajua nchi hili ilikotoka na ilipo na inatakiwa kwenda wapi? Aanatakiwa kuelewa kwanza sababu za kule ilikokuwa zilikuwa zipi, sababu gani zinapelekea nchi kuwa hapa ilipo, ana analinganisha ni nchi ipi barani afrika? asije akaanza kututajia viibaraka Kagame waliotumiwa na Wazungu leo hii wameanza kumgeuka. Asije akanitajia Kenya ambayo hata jana nilisikia wamepigana vita ya wenyewe kwa wenyewe. Unainusuru Tanzania katika mambo yapi?

Siwezi kuendelea kulumbana na mapandikizi kama ww.
 
Mjomba wa taifa Mkuu, mada yako ni nzuri na muhimu sana, lakini kwanza ingependeza ungeikuza kidogo na ingefaa zaidi kuipeleka kule kwa Great Thinkers ambako itachambuliwa na kujadiliwa kwa kina, bila udaku.

Pia ninakuomba (na wengine) kupitia angalau moja ya mada hizi za:
https://www.jamiiforums.com/great-thinkers/256191-mawaziri-ovyo-wa-ccm-wapi-tunakosea-kama-nchi.html
https://www.jamiiforums.com/great-thinkers/227287-kwanini-mikoa-yetu-haiendelei-kiuchumi.html
https://www.jamiiforums.com/great-thinkers/38756-kwanini-watanzania-ni-maskini.html
https://www.jamiiforums.com/great-t...ado-ni-chama-cha-wakulima-na-wafanyakazi.html
Mimi naona kama CCM bado imara sana tena sana tu na ndiyo maana hapa JF baadhi ya watu wametumwa tu kukidhoofisha kwa majungu, fitina, na chuki binafsi. Toeni facts na kutupa mbadala sahihi wa CCM kama kitaonekana kushindwa kwa baadaye ila siyo hiki chama cha ukoo wa akina Mtei, Ndesamburo na Lissu.
 
Nchi,Serikali ilijikwa pale ambapo walijipa ushindi kwenye kinyanganyiro cha urais kwa njia ya wizi,dhuruma.njia pekee ya kuweka sawa ni kuwang'oa madarakani kwa nguvu ya umma,watu tuandamane kwenda ikuru,tumtoe jk kisha ufanyike uchaguzi huru na wa haki.
 
Dhaifu wewe ambaye hujui kupambanua wanasiasa wanaotaka umaarufu na wanasiasa wenye hoja. Hivi na wewe unakubali kuwa JK ni dhaifu? Mnyika alikuwa anataka kujirudisha kwenye kiwango baada ya kashfa ya wizi wa kura jimboni kwake.
VIVA JK.

nafkr wewe darasani ulienda kujifunza kusoma na kuandka tu ulipomaliza ukahitimu pengine umebatizwa kwa jina la magamba ndo maana uko na mawazo mgando.Kawaulize hata watoto wa chekechea watakuambia udhaifu wa jk
 
Mimi naona kama CCM bado imara sana tena sana tu na ndiyo maana hapa JF baadhi ya watu wametumwa tu kukidhoofisha kwa majungu, fitina, na chuki binafsi. Toeni facts na kutupa mbadala sahihi wa CCM kama kitaonekana kushindwa kwa baadaye ila siyo hiki chama cha ukoo wa akina Mtei, Ndesamburo na Lissu.
Mamaisara, sikatai juu ya Uimara wa CCMlakini kwa maoni yangu na facts unazozitaka, ni kuwa chama kimejijengea uadui na Watanzania kwa mfululizo wa rushwa, ubadhirifu, ufisadi...na yote haya wanayafanya dhidi ya Watanzania. Imefika pahali CCM kinatumia ubabe na kulazimisha kikubalike badala ya ridhaa hasa ya Watanzania. Sikatai pia kuwa CCM inaweza kuendelea kubakia madarakani kwa misingi hiyo niliyoeleza hapo juu. Chama kukaa madarakani miaka mingi sio tatizo, Chama cha Asasi za Kimapinduzi (Partido Revolucionario Institucional) cha Mexico kilikaa madarakani kwa miaka 60 (1929-1989), lakini muda wote katika demokrasia na kukubalika, siku kilipowaendea kinyume wananchi kilikataliwa visandukuni bila ya kutumia pesa, rushwa na jeshi kukilinda.

Kwa wale waliozaliwa kabla na baada ya uhuru hadi miaka 7 baada ya kuundwa kwa CCM (1977-1984), Watanzania wengi hatukujali, "tuliapa na kuahidi kuilinda CCM mpaka kufa," lakini baada ya hapo CCM ikaachana na Watanzania: Wakulima na Wafanyakazi na kukumbatia matajiri na "wawekezaji." Ni Mtanzania gani leo mvuja jasho atakubali unapomuambia afunge mkanda, wakati wanaotoa amri hiyo hawafanyi hivyo, watoto wao wanasoma nje au shule za International wakati watoto wetu wanasota ndani ya vumbi na kunyeshewa mvua, wao wakishikwa na homa tu wanakimbilia India wakati sisi hatuna pesa ya kununua hata aspirini? Kama kuna mvuja jasho ambaye hayaoni na kama anayaona hayo na bado ana imani na CCM, huyo anafaa kupelekwa Milembe.
 
Tumpe nchi shibuda tu awe rais
makamo wake lusinde mpaka 2015
labda wanaweza badili kidogo uchumi......
V
SENGEREMA
 
Back
Top Bottom