Nini kazi ya Mabalozi wanaoiwakilisha nchi nje ya nchi.

BLUE BALAA

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
1,222
762
Kama utamaduni tuna embassies katika nchi nyingi. Na nje ya Balozi kunakuwa na Balozi mdogo, Councillor na office staff. Binafsi sijui hasa hawa mabalozi huwa wanafanyaga nini? Hivi baada ya kumaliza muda wao huwa wanafanyiwa performance review?.

Maana yake huwa tunasikiaga kwenye vyombo vya habari wakati wameteuliwa kisha hatuwasikii tena mpaka wakiwa wamemaliza muda wao.

Mimi nina shida kidogo, lazima kwanza wenyewe wawe na tabia ya kujisuta - self appraisal, kwamba nimekaa huu muda JE HAVE I ARCHIVED? Nina wasiwasi hawa ni ma DC wetu wa nga'mbo!
 
Balozi zetu zinamaliza pesa hazina. Hakuna kazi wanafanya huko..Walimu, madaktari wanashindwa kulipwa mishahara kwa sababu ya matumizi mabovu kama haya yasiyo ya msingi. Ubalozi una watu lukuki wanafanya nini? halafu mkuu akitembelea hizo naye anaongozana na watu lukuki sasa si bora mkulu angekuwa anaenda mwenyewe akifika huko si kuna balozi na wafanyakazi walipashwa wafanye yote kubana matumizi...ukiangalia hata wengi waliopo kwenye hizo balozi wamewekwa kwa kujuana..nchi hii ina vituko sana. Hazina hakuna pesa lakini watu wanatanua
 
Balozi zetu zinamaliza pesa hazina. Hakuna kazi wanafanya huko..Walimu, madaktari wanashindwa kulipwa mishahara kwa sababu ya matumizi mabovu kama haya yasiyo ya msingi...

Pakawa punguza ukali. OhmyGawd! usitupe mti na jongoo. Nakubali kua Mkulu apunguze wapambe anapokwenda nje.

Lakini mi nadhani mabolozi na wasaidizi wake ni muhimu, kwa sababu ya viza na kwa ajili watanzania wanaoishi au kusafiri huko.

Blue Balaa, nakubaliana na pointi yako, wawe wana jiuliza what have i achieved all this time. Au wawe wanaulizwa. na hizo habari ziwe public. nafkiri Itawapa changamoto.
 
1.Kutoa Visa
2.Kutangaza nchi usika hasa kiutalii na uwekezaji
3.Kusaidia Raia wake wakiwa nje incase of matatizo

NB:2&3 Hayafanyiki
 
1.Kutoa Visa
2.Kutangaza nchi usika hasa kiutalii na uwekezaji
3.Kusaidia Raia wake wakiwa nje incase of matatizo

NB:2&3 Hayafanyiki

Mtanzania ukienda Ubalozini wanakuona kama umeenda kuwasumbua na mara nyingi wanakupuuza,, shida yako haisikilizwi, unless uwe na tabia ya kujichekesha chekesha na kujipendekeza kwao..
 
1.Kutoa Visa
2.Kutangaza nchi usika hasa kiutalii na uwekezaji
3.Kusaidia Raia wake wakiwa nje incase of matatizo

NB:2&3 Hayafanyiki

Mkuu umejibu sawa kufuatia swali lilivyoulizwa - nini kazi zao sasa kama mtoa mada anauliza kwa vili haoni wanachofanya jibu ni tofauti na wengi wamejielekeza huko kwani tunafahamu kuwa ni wawakilishi wetu shida ni kama tunaona wkituwakilisha ipasavyo

Mfano wa kuona kuwa raia wanaotembelea nchi hizo wanawasumbua linanikumbusha miaka ya nyuma Watanazania waishio Kenya walikuwa wanasumbuliwa na walipokwenda ubalozi wetu kutaka msaada wakaulizwa kama watu hwawataki nchini kwao mnafuata nini?

Kwa jibu hili unajiuliza hivi huyu anajua anachotakiwa kufanya akiwa kama ofisa wa ubalozi kweli?
 
Habari, Wana JF,

Naomba kujua kutoka kwenu mabalozi wetu ambao wanatuwakilisha katika nchi mbalimbali wanakuwa na majukumu gani hasa?

Mara nasikia tu wengine wanalalamika "nilienda ubalozi wa Tanzania lakini sikusaidiwa" n.k.

Nini hasa wajibu wao hawa watu?
 
Wataalamu wa Msuala ya kidplomasia wanatakiwa wakujibu, mimi nikijibu nitajibu kutokana na taaluma yangu ya ualimu wa shule ya msingi.
 
balozi zetu wamejaa waambata wa vyombo vya dola,Pia mabalozi wetu wateuliwa wametokea kwenye vyombo kama hivyo ndio maana hawanaga msaada customer care negative ubalozi unaenda kijeshi jeshi

ila kingine watu wanaolalamikia balozi haziwasaidii wanapeleka matatizo yao binafsi....Tusiwalaumu sana mabalozi wana bajeti finyu
 
1. Ku arrange safari za rais na viongozi wakuu

2.kukaribisha investors

3.kutangaza utalii

4. Kusaidia watanzania wanaofika katika nchi hizo
 
balozi zetu wamejaa waambata wa vyombo vya dola,Pia mabalozi wetu wateuliwa wametokea kwenye vyombo kama hivyo
ndio maana hawanaga msaada customer care negative ubalozi unaenda kijeshi jeshi

ila kingine watu wanaolalamikia balozi haziwasaidii wanapeleka matatizo yao binafsi....Tusiwalaumu sana mabalozi wana bajeti finyu
Mkuu,, kwahiyo mtu wa kawaida inakua vigumu kufanya kazi ubalozini ?
 
Hawa mabalozi kazi zao huwa ni nini kwani hawawezi kutuwakilisha kwenye jambo lolote linalotuhusu kuna haja gani ya viongozi kutoka kwenda huko kila siku, kunakuwa hamna maana ya kuteuliwa kwenda huko
 
Kuna ya kuwakilishwa na balozi
Kuna yanayomhusu mkuu wa nchi
Kuna ya mawaziri nk
Mbona hatuoni akina Biden au Liz Truss wakizunguka huku na huko?? Mabalozi hizo ndio kazi zao. Ukiona Biden au Liz Truss anaenda nchi fulani jua kua kuna interest kubwa ya nchi anaenda kuiongelea hawazunguki zunguki tu kila kona kama chief Hangaya, utasema alikula miguu ya kuku yeye na JK.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom