Kujamba (kutoa ushuzi) kuna faida kiafya?

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,211
113,520
Kuuliza si ujinga walisemaga wahenga.

Hivi harufu ya ushuzi (hapa nazungumzia ushuzi wa mtu mwingine na si wa kwako mwenyewe) ina madhara yoyote ya kiafya kwa binadamu?

===========
July 14, 2014:
Wanasayansi wanasema kutoa ushuzi ni afya

Kila mmoja wetu kwa wakati fulani huhisi kuvimbiwa na gesi nyingi tumboni.

Suluhu ya pekee hapa huwa ni kujamba ili kupunguza gesi hiyo tumboni

Sasa Wanayansi katika chuo kikuu cha Exeter, nchini Uingereza, wanasema kuwa wamegundua harufu mbaya kama vile ya kujamba japo inachukiza kwa pua, ina manufaa makubwa kwa afya ya binadamu.

Wanasayansi hao wanasema kuwa harufu hiyo mbaya inaweza kuwa kinga dhidi ya magonjwa ya moyo na akili na hata Saratani.

Gesi au harufu mbaya ambayo hutokana na chakula kinachosagwa tumboni mwako inaweza kulinda baadhi ya viungo vya mwili wako.

Ndio! athari ni kile ambacho unakidhania: Eti watu wanauchukulia utafiti huu kumaanisha kuwa harufu mbaya inayotokana na mtu kujamba inaweza kuzuia magonjwa fulani mwilini kama vile Saratani.

Utafiti huo uliochapishwa katika mtandao wa chuo kikuu cha Exter uligundua kuwa gesi hiyo inayojulikana kama Hydrogen Sulfide ambayo pia hupatikana katika Mayai yaliyooza, inaweza kuwa muhimu katika kutibu baadhi ya magonjwa.

"ingawa gesi ya hydrogen sulfide inajulikana kuwa na harufu mbaya na hupatikana katika Mayai yaliyooza pamoja na harufu ya mtu kujamba, hutengezwa mwilini na inawezekana kuwa tiba kwa magonjwa fulani, ''asema Daktari Mark Wood,Profesa wa chuo hicho cha Exeter.

Gesi hiyo ina athari mbaya ikiwa katika viwango vikubwa , kwa mujibu wa utafiti huo.

Watafiti wanasema licha ya harufu hiyo mbaya ya kujamba kuchukiza, ina uwezo mkubwa wa kupunguza uwezekenano wa mtu kupatwa na magonjwa kama vile, Saratani,Kiharusi, mshtuko wa Moyo na kuumwa na mifupa

Chanzo: bbc

JE, UNAFAHAMU NINI KUHUSU KUJAMBA?

Kwanini tunajamba? kwanini "ushuzi" unanuka? Kujamba inaweza kuwa kitendo cha aibu kwa wengi wetu, lakini inaweza kukufanya ujisikie vizuri kujua kwamba ni tendo la kawaida sana kwa mwili wa binadamu kutenda.

1.Kujamba ni nini hasa?

Kujamba kunasababishwa na kubanwa kwa hewa, ambayo inaweza kutoka mwilini kwa njia nyingi. Baadhi ni hewa tuliyoimeza wakati wa kula au kunywa. Hewa ingine husababishwa na gesi kuingia kwenye utumbo wetu kutoka kwenye damu, na baadhi ya gesi huzalishwa na kemikali katika utumbo au bakteria. Kwa kawaida "ushuzi" unakua na asilimia 59 ya gesi ya nitrogen, asilimia 21 ni hydrogen,asilimia 9 ni carbon dioxide, asilimia 7 methane na asilimia 4 ni oygen.

Asilimia moja tu ya "ushuzi" inaweza kuwa hydrogen sulfide na mercaptans, ambayo ndio ina sulfur ndani yake,sulfur ndo hufanya "ushuzi" utoe harufu mbaya. Kujamba huambatana na sauti, hii ni kutokana na "vibration" katika njia ya haja kubwa. Ukubwa wa mlio wa kujamba hutegemea "presha" inayosukuma gesi itoke nje na pia ugumu wa misuli ya njia ya haja kubwa.

2. Kwa nini Ushuzi hutoa Harufu mbaya?

Harufu mbaya ya ushuzi hutegemea na ulaji wa mtu, vyakula vyenye sulfur kwa wingi ndio usababisha hili. Vyakula vyenye sulfur kwa wingi ni kama soda, maharage, kabichi na mayai.

3.Watu hujamba hadi mara 14 kwa siku

Mtu wa kawaida hutoa hata nusu lita ya ushuzi kwa siku. Inasemekana mtu akijamba mfululizo kwa kipindi cha miaka 6, anaweza kuzalisha nishati ya kutosha kutengeneza bomu la atomiki.

4. Ushuzi husafiri kwa mwendo wa futi 10 kwa sekunde. Harufu ya ushuzi huanza kusikika sekunde 10-15 baada ya mtu kujamba, hiyo ni kwa sababu inachukua muda mrefu kwa harufu kufikia pua.

5.Kujizuia Kujamba Inaweza Kuhatarisha Afya Yako.

Madaktari hawajakubaliana moja kwa moja kama kujizuia kujamba ni hatari kiafya. Baadhi ya wataalam wanafikiri kujamba ni sehemu muhimu katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula, hivyo kujizuia kujamba haitakuletea madhara. Wengine wanadhani kwamba kujizuia kujamba kunaweza kusababisha tumbo kujaa gesi, na pia inaweza sababisha bawasili (hemorrhoids).

6.Kwa Baadhi ya Tamaduni, Kujamba Sio Ishu

Wakati tamaduni nyingi zikichukulia tendo la kujamba lifanywe kistaarabu, kuna baadhi ya tamaduni hawaoni haya kujamba hadharani, na pia hufurahia tendo hilo. Mfano kabila la Yanomami huko America ya Kusini kwao husalimiana kwa kujamba na China unaweza kupata kazi ya kunusa ushuzi! Katika Roma ya zamani Mfalme Claudius akihofia kwamba kujizuia kujamba inaweza kuwa hatari kiafya, alipitisha sheria kwamba ni ruhusa kujamba kwenye "banquets".

7. Ushuzi Unawasha Moto
Kama ilivyoandikwa hapo juu. Methane na hydrogen inayozalishwa na ushuzi inaweza sababisha moto.

8. Mchwa Hujamba Kuliko Wanyama Aina Zote

Ni ngumu kuamini kuwa mchwa ndo anawajibika na matatizo yetu ya "Global Warming". Mchwa huongoza kwa kujamba kwa wanyama na hiyo huzalisha gesi ya methane.

9.Ukiubana Ushuzi, Utakutoka Usingizini

Hata ujitahidi kuubana vipi, ushuzi utatoka mara utapokua umepumzika, hasa ukiwa umelala.

10. Watu Hujamba Hata Baada ya Mauti Kuwafika

Maiti huendelea kutoa gesi hadi masaa matatu baada ya mtu kufariki dunia, hii huambatana na milio ya kujamba. Hali hii husababishwa na misuli kusinyaa.

UKIPATA MUDA JAMBA.

Credit to Mtandao


Pia soma
 
mwe...kitu ambacho hukipendi.. hakina fleva kwako lazima kina madhara kiafya..
 
hauna madhara wala nn ni kama unavyopga chafya kabla ya kuyatoa makamas kwa hyo hakuna tofaut sna na hvyo vtendo
 
kuuliza si ujinga walisemaga wahenga.

Hivi harufu ya ushuzi (hapa nazungumzia ushuzi wa mtu mwingine na si wa kwako mwenyewe) ina madhara yoyote ya kiafya kwa binadamu?
kwani hujui ushuzi ni toxic?
Ndo maana mkeo kadumaa kumbe una mpoison kila siku
 
Kuuliza si ujinga walisemaga wahenga.

Hivi harufu ya ushuzi (hapa nazungumzia ushuzi wa mtu mwingine na si wa kwako mwenyewe) ina madhara yoyote ya kiafya kwa binadamu?

If you have frequent heartburn, you may experience changes that affect your lifestyle too. Frequent heartburn may affect your ability to focus at work. And then there's the stress factor of heartburn that can make you seem ill-tempered or moody. You might even find it difficult to fully enjoy social occasions. There are also the effects of finding it hard to sleep due to heartburn.[SUP]2[/SUP] And the after-effects the next day of getting less sleep than you desire the night before.

Like the physical symptoms of heartburn, these effects can be just as discomforting to you, not to mention the people who care about you. So how much does frequent heartburn affect your life? Answering this will make it easier to give frequent heartburn the respect it deserves.
 
hauna madhara wala nn ni kama unavyopga chafya kabla ya kuyatoa makamas kwa hyo hakuna tofaut sna na hvyo vtendo

Wengine wakipiga chafya ni kama ushuzi tu aisee, au akipumua ni kama ushuzi
 
Una madhara makubwa, kuna jamaa aliwahi kuachia ushuzi na mtu aliyekuwa jirani yake akashikwa na mafua dakika hiyo hiyo...
 
If you have frequent heartburn, you may experience changes that affect your lifestyle too. Frequent heartburn may affect your ability to focus at work. And then there's the stress factor of heartburn that can make you seem ill-tempered or moody. You might even find it difficult to fully enjoy social occasions. There are also the effects of finding it hard to sleep due to heartburn.[SUP]2[/SUP] And the after-effects the next day of getting less sleep than you desire the night before.

Like the physical symptoms of heartburn, these effects can be just as discomforting to you, not to mention the people who care about you. So how much does frequent heartburn affect your life? Answering this will make it easier to give frequent heartburn the respect it deserves.

Kwanza kabisa hayo hujaandika wewe. Umeyanakili tokea sehemu.

Pili, hayahusiani kabisa na ushuzi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom