Nini hasa maana ya utu?

jmushi1,

Asante Mkuu kwa mchango. Vipi hii ya mbunge na wapiga kura wake? Wapiga kura wake watakuwa hawana utu (hawa-act kama mtu) kama wakitaka ufanyike uchaguzi mwingine ili wamchague mbunge mwingine atakayeweza kuwawakilisha?
 
Mkuu kutaka uchaguzi ufanyike ni ndani ya utu kwasababu ni misingi ya demokrasia na haki ya mpiga kura ama "rights" za watu hao wapiga kura.

Kwetu sisi kuwa "Mtu" kwakweli ni lazima ufanye mambo ambayo jamii inaya perceive kama rights za "watu"
 
Binadamu hujitofautisha na mnyama kwa kule kuthamini utu na kutenda matendo yenye heshima mbele ya binadamu wengine kwa jinsi ambavyo yeye (binadamu) anavyotaka athaminiwe kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za kimaumbile.

Jee [utu] una uhusiano na ubinafsi. Iwapo mimi sijali mtu kuniheshimu ni sahihi kutomheshimu mwengine? Taratibu za kimaumbile hapa zinamaanisha kitu gani?

Naandika mtazamo wa kisaikolojia kwa vile wananchi wengi tumepoteza haiba ya utu na heshima wetu, yaani upendo, kujali na huruma! Binadamu tuna wajibu wa kiutu kuwa na upendo, huruma na kuwajali watu wengine kwa jinsi ya ubinadamu

Kwa "jinsi ya ubinaadamu" ina maana gani? Hivi huu ubinaadamu unapimwaje? Inawezekana mtu mmoja akawa na ubinaadamu mwingi zaidi ya mwengine?
 
Nilitoa maeelzo amabayo yanaweza kuchangia kwenye hapa!!

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/192427-lowassa-atabiri-vita-tanzania-5.html#post2812077 Re: Lowassa atabiri vita Tanzania

By Fe Lady Labda tutambue wakati wa serikali ya Sumaye tatizo la ajira lilikuwaje,ilipokuja serikali ya Lowasa lilipungua?Now Pinda Limeongezeka?LOWASA Anatafuta sababu,alifanya nini kucreate ajira?

Hali ilivyo inahitaji BUSARA zaidi ya kusema ukweli!

By MZALAMO
Lowasa ni tatizo kubwa sana katika jamii ya kitanzania kuliko hata kikwete!

Naafiki!

By Noti mpya tz Huyu kaamua atoke na issue ya vijana anadhani itampeleka ikulu kweli watanzania tunayo kazi sitarajii huyu jamaa kuungwa mkono na vijana maana ameshiriki kuwatesa na sasa anataka kuwatumia atimize malengo yake

Lowasa anatumia AKILI lakini hana BUSARA! Ameongea ukweli usio na Busara hata kidogo!! Kuujua ukweli si issue ..hata yeye can not handle what he pointed and expressed so well ..This make the matter even worse..cause he is worse naturally!!

By Melanoxylon Ajira kwa vijan kwani yeye ndo kaona tatizo leo? Ninavyofaham yeye kama mwkilishi wa wananchi ameishauri nini serikari au hata raisi rafiki yake. Nothing wizi tu... What a prezda fisad aiyekuwa na aibu. With me mchango wake tumeupokea but for u prezda ashindwe kwa jina la yesu

... Naafiki .. Mchango upokelewe ... na Yesu afanye vitu vyake on this issue!!

By MPIGA ZEZE
Yes, Man Made Money and, in turn, Money Made Man Mad! Kama poor peasants wanavyokiwezesha Chama Cha Magamba kuendelea kuwa madarakani kwa pupewa kofia, kanga, fulana, na ubwabwa, ndicho hiki tunaanza kukiona kwa Kanisa Katoliki (kanisa lenye heshima kubwa duniani) kutaka kutumiwa kama kondomu kwa sababu ya "Money"!!!! Kanisa Katoloki limegeuka kuwa kichaa. Shame on you!!!

... Siamini wala sioni nianzie wapi ...kuona ..kanisa ..litumike kupitishia ukweli mkubwa kama huo ..lakini usio na busara ..na hata mtoa mada mwenyewe knows kwamba ..cant change that truth!! ..Smart, clever BUT NOT Intelligent ...and this is really SHAMEFUL!!

By Zion Daughter Hatudanganyiki!!!

... I also tend to believe so!! Time and space wont allow kudanganyika any longer!!

Watanzania tuwe macho na hili fisadi papa!
Hii ni muhimu sana!! ... Nafikiri itatekelezwa!!

Kuwa na AKILI bila busara za UTU na UBINADAMU ... Ni Tatizo linaloikuba dunia yote kwa kasi ya haraka! Lakini viongozi wote NGULI wenye akili nyingi sana lakini wasio na utekelezaji kwenye nyaja ya UTU na UBINADAMU wanapukutika na kuangamia kwa AIBU na kasi ya Ajabu. Kuwa na AKILI za kutosha kunaweza kukupatia PhD! Lakini si lazima Uwe na UTU na UBINADAMU kwakuwa unaakili inayoweza kundika mtihani wa PhD!

Iko hivi Baba mwenye PhD , anayewahi kufika nyumbani akala chakula cha watoto, akanawa akawa wa kwanza kupanada kitandani wa kwanza kulala huko anakoroma na watoto wakarudi nyumbani wakakosa chakula na kulia kwa mayowe kama wale vijana wa Mbeya...hakumuondolei Baba huyo PhD Yake kwani ganda bado liko ukutani. Hakumfanyi Dingi Kutokuwa na AKILI. Lakini UTU na UBINDAMU wake Bure kabisaa! Akili ya Phd 100% na Utu na ubindamu 0%. Hafai kuwa Baba,hafai kuwa kiogozi, mbunge waziri wala Rais!

Mawaziri wangapi ndani ya baraza wana PhD na akili nyingi sana? Dosens.. Wanakula chakula cha watoto kivipi? Wanasaini mikatataba mibovu ...wawekezaji wanapata faida ya 100% kwa mika 100 ijayo na Yeye mwenye PhD na Akili nyigi sana ..anapewa RV 4 new model 2. Moja ya Mkewe na Moja ya Kwake. Kwani hiyo inamuodolea Phd Yake ? No! Akili Mingi ...Utu/Ubindamu..0%

Lowasa ametumia Akili yake vizuri sana hapo kanisani kuuweka hadharani ukweli mkubwa sana! Hilo halinipi tatizo ... Vipi kuhusu chakula cha watoto wazalendo wananchi wa kitanzania? Utu na Ubinadamu wake ndio unasukuma na kuipa akili, fikra na matendo mwelekeo wa anachokifanya! Mwelekeo wa KIUTU ambao ndio chimbuko la Taifa liitwalo Tanzania. Utanzania ni UTU, Utanzania ni Ubinadamu na asiye na sifa hizo za KIUUNGU na akae kando kwenye kuutafuta UONGOZI waTaifa hili. Kwani HIZI NI ENZI MPYA!!!
 
Azimio jipya hebu nieleze kwa malezo mafupi Utu ni nini? Unatokana na nini? na Unapimwaje?

Mara nyingi nimeona kuwa contemplation ya UTU inaeleweka kwa mifano ... !

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...alifu-wa-wana-ccm-si-uhalifu.html#post2783844

Re: Kaimu Kamanda wa Polisi Arusha: Uhalifu wa wanaCCM si Uhalifu!!!!

Kamanada ana AKILI nzuri na timamu, lakini anatatizo la Utu na Ubinadamu katika kutumia Hekima na Busara. Mambo ambayo hayaendi kwa misukumo ya Kiakili na lililotazo la vinogozi wengi kwa sasa. Tatizo hili hatimaye lianakuwa shina la Usugu wa Matatizo megi ya Kijamii na Kitaifa.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Hapo itabidi uwaulize wenye dini. lol. Kwenye kitabu cha Chachage na Cassam titled: African Liberation: The Legacy of Nyerere at page 51 wanasema: "Ujamaa embraced aspects of the Swahili concept of utu or common humanity (or Ubuntu as is called in South Africa). This [utu] is based on the philosophy of forgiveness, reconciliation and willingness to share." Tunaweza ku-define utu kama kusameheana, kusuluhishana na kusaidiana? Japokuwa wapo wengine watasema utu simply mean Uhuru Through Ujamaa. lol

Mfano: Mwingine wa UTU wa Kitanzania , kile kinachodhaminiwa kuwa Ubindamu wa Maadili ya Kitanzania!

Re: Ni bora kufa mapema kuliko kuona ndoa ya ushoga tanzania!-dk mvungi

https://www.jamiiforums.com/habari-...ya-ushoga-tanzania-dk-mvungi.html#post2783820

Its all about moral authority and general credibility.

To come out firm loud and clearly claiming ... this isn't Tanzanians morals values, first as an individual you must posses that cleanliness to some degrees ..and how do you know your leader is serous and believe in what is talking?

Check with his moral superiority .. in politics, social and economical issues.. does he dilly dally or is firm and clearly outspoken for the benefit of whole community?

If he has failed in all that..! Definitely he lucks character, nobility and credibility!

That being the case?! .. Where will he get the slightest strength and meaningful moral values to speak out against what type of marriage ...! I know we know .. most of them arnt serious ...
 
Utu ni neno pana na linaweza lisiwe na tafsiri moja tu.
Kimantiki utu ni ile hali ya kujali ubinadamu, kwenda kinyume na hapo ni kutokuwa na utu, waingereza wanaita against humanity.
Tunapo zungumzia ubinadamu ni ile hali ya kuwa sisi binadamu tuna ufahamu mkubwa kuliko wanyama, kwamba hatuwezi kuishi kama wanyama tuna misingi yetu kama binadamu, kwa kuwafanyia wenzetu yale tunayopenda kufanyiwa na si yale usiopenda kufanyiwa.

Mimi si mtaalamu wa lugha nashindwa namna mzuri ya kuliweka hili neno lieleweke uzuru
Sasa kwa mfano FF anapo muita marehemu alikuwa mlevi au kichaa na ametoa kauli hiyo akijua si kweli wakati wenzake ndugu na na jamaa wanaomboleza kifo cha ndugu yao mpendwa, hapo ni kukosa utu, amekosa ile hali ya kawaida ya ki binadamu kutoa kejeli wakati wenzake wako katika wakati mgumu, na kumfanya marehemu ni kama hana thamani kwani alijitakia.

Kwa issue ya mbunge, ukiangalia kwa manti mleta hoja anajua kabisa sheria zipo zinazotoa mwongozo kwenye jambo la ugonjwa kwa viongozi, lakini yeye ameweka kando kwamba kuna mtu kama yeye anapigania maisha yake apone na anapaswa kupewa sapoti kama binadamu yeyote, lakini kwake kwakuwa si wachama chake anaona anyang'anye ubunge kwa kuwa hafai ni mgonjwa na watafute mwingine

Utu ni zaidi ya sheria inavyo weza kutafsiri, utu ni namna mtu anavyoweza kutendea wenzake kwa kadri ya matarajio ya jamii husika inavyotarajia binadamu wa kawaida kufanya

Azimio Jipya,

In deed, hasa hapo kwenye red kama alivyosema Jenerali Ulimwengu:

"No self-respecting African man would let another man pay for his and his wife's and his children's upkeep.

Indeed, a man who allows that to happen would be considered as having been married by the provider man, call them economic homos.Rejecting the one, reject the other too."
 
@paulss,

Asante Mkuu kwa anaylisis yako nzuri. Hapo kwenye red wapo wanaosema kuwa law is based on humanity. Kwa mfano, kuna even sheria za crimes against humanity.
 
Utu ni zaidi ya sheria inavyo weza kutafsiri, utu ni namna mtu anavyoweza kutendea wenzake kwa kadri ya matarajio ya jamii husika inavyotarajia binadamu wa kawaida kufanya

]

Iwapo utu ni zaidi ya sheria inavyoweza kutafairi, tunaweza kumshitaki mtu kwa kosa la ukosefu wa utu?
 
Asante Mkuu kwa anaylisis yako nzuri. Hapo kwenye red wapo wanaosema kuwa law is based on humanity. Kwa mfano, kuna even sheria za crimes against humanity.
Iwapo utu ni zaidi ya sheria inavyoweza kutafairi, tunaweza kumshitaki mtu kwa kosa la ukosefu wa utu?
Ni kweli wakuu kuwa Laws zimewekwa ili watu waweze kuishi kwa utu, na karibu makosa yote ya jinai ni yale yanayohusu ukosefu wa utu.
Lakini kuna ukosefu mwingine wa utu haujatafsiriwa na sheria kama makosa ya jinai, mfano wa FF na anayedai mbunge atimuliwe kwa ugonjwa.au sakata la miss voda na meli kuzama nk, inatofautiana uzito tu
Na si wakati wote sheria zinasimamia utu, na ndio maana kuna wanaharakati wanapinga baadhi ya sheria kwakuwa zipo kinyume na utu(humanity)

Tatizo linakuja kuwa vitu visivyoweza kutafairika kisheria vinaacha uwanja mpana wa kila mtu kufikiri anavyotaka yeye

Kwa mfano kesi ya Mbunge. Mimi sioni kuwa ni ukosefu wa utu kumlazimisha ajiuzulu maadam anashindwa kufanya kazi yake tuliyomuajiri.

Badala yake kama kuna ukosefu wa utu basi ni kwa kuwaacha wananchi kukosa mwakilishi bungeni kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa
 
Niuzungumzie utu kama ambavyo wenzetu wanauita dignity

Naomba kwa kuanzia nikope tafsiri ya dignity kutoka kwa bwana Mette Lebech anaesema Dignity is the quality of worth (status/values) and honour (respect) intrinsic to every person which establishes the basic boundaries of humanity (Emphasis mine)

Unapoiangalia kwa undani tafsiri hii utagundua kuwa inazungumzia zaidi kile ambacho mtu anapaswa au anastahili kukipokea kutoka kwa watu wengine na anapaswa kukitoa kwa watu wengine.heshima kwa ile being ya mtu, yaani nikimaanisha ile treatment kwa kila mtu in a very fair manner jinsi alivyo na jinsi anavyostahili kuwa treated.
Tutatofautiana katika mambo yote lakini ukweli utakuja kubakia kuwa kuna basic values (status) ambazo kila mtu anastahili kupewa kwa kule tu kuwa binadamu (forget about other things). Kwa hiyo, kile kitendo cha kutoa heshima hiyo kwa watu wengine (pasipo kujali tofauti au kitu kinachofanya mtu huyo asistahili kupewa heshima hiyo) ndicho tunachoita utu.

Nimeweka hilo neno pasipo kujali kama anastahili au la, kwa kuzingatia ukweli kuna mazingira ambayo huwa tunadhani mtu akiwa katika hayo mazingira hastahili kutendewa kama mtu yaani kupewa heshima ya utu wake, lakini hilo ni kosa.tafsiri halali ya utu inahitaji mtu apewe haki yake heshima yake ya kuwa mtu hata kama amefanya jambo ambalo litatufanya tuone kuwa hastahili kupewa heshima ya huo utu na jamii husika. Utu huthibitika zaidi unapoweza kutoka nje ya vizingiti vyetu vinavyotutofautisha sisi kama binadamu (inaweza kuwa itikadi za kisiasa,

Kwa mfano, sio utu kumuacha mwizi kuwa kama mtu asie na hatia (kwa kuwa naye ameuweka utu wa watu wengine kwenye concern) na pia sio utu kumfanyia mwizi asivyostahili kufanyiwa (kwa mfano kumchoma mtu moto kwa kuiba badala ya kumpeleka kwenye vyombo vya dola kwa ajili ya kuchukuliwa hatua)

Au kwa mfano kuna mtu alitoa wazo hapa jamvini na kusema tuanze kuua watoto wa askari wanaopiga watu bila kutumia akilini sawa askari wetu wanaweza kuwa na makosa ila ukweli utabaki kuwa kufanya hivi sio utu. Hili ndilo kule kusema kanuni ya utu hufuata pia kanuni ya two wrongs cant make it right, yaani utu haumtumi mtu kurekebisha kosa kwa kutumia kosa (jino kwa jino)

Kimsingi; Utu ndicho kitu pekee kinachoweza kutuunganisha binadamu wakati kila kitu kinapokuwa kimeamua kututenganisha na kuweka kutu au ukungu kwenye ubinadamu wetu. Unapoondoka utu huu kwa tofauti zetu, basi hatuwi tena watu bali Wanyama.

Na hapa ndipo ninapokubaliana na dhana ya Lebech kuwa Dignity is the fundamental value
of the human being, ni zaidi ya kitu chochote kile, wakati mwingine hata sheria au baadhi ya kanuni mama zinazotuongoza
 
Iwapo utu ni zaidi ya sheria inavyoweza kutafairi, tunaweza kumshitaki mtu kwa kosa la ukosefu wa utu?

Mkuu Gaijin, naomba nisikujibu moja kwa moja ila niulize swali ili litujengee uelewa mpana zaidi

Kwa nini sheria zipo? Je si ili kulinda "utu" wa wananchi/wanajamii wa nchi/jamii husika?

hebu tusaidiane mtazamo hapo kwanza ndiyo tuone tunachukua njia gani katika kuamini hili
 
Nadhani ni vigumu kusema sheria kazi yake kulinda utu iwapo hatuwezi hata kuueleza utu ni nini. Kwa sababu tunaposhindwa kufasiri utu basi na sheria lazima itashindwa kuulinda

Chukua kesi ya FaizaFoxy kwa mfano; alichokifanya si makosa kisheria licha ya kuwa ameonekana kukosa utu.
 
Asante Mkuu kwa anaylisis yako nzuri. Hapo kwenye red wapo wanaosema kuwa law is based on humanity. Kwa mfano, kuna even sheria za crimes against humanity.

Tatizo linakuja kuwa vitu visivyoweza kutafairika kisheria vinaacha uwanja mpana wa kila mtu kufikiri anavyotaka yeye

Kwa mfano kesi ya Mbunge. Mimi sioni kuwa ni ukosefu wa utu kumlazimisha ajiuzulu maadam anashindwa kufanya kazi yake tuliyomuajiri.

Badala yake kama kuna ukosefu wa utu basi ni kwa kuwaacha wananchi kukosa mwakilishi bungeni kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa
Mkuu natumaini katika hili la mbunge zipo taratibu zimezingatia utu, kuwa akifikia hatua fulani basi kibinadamu hawezi tena kuendelea kuwa mbunge, sasa anapokuja mtu na kuanza kukejeli kwa ushabiki wa kisiasa kuwa atolewe tu kwasababua anaumwa si sahihi na haionyeshe ule ubinadamu kuwa huyu ni mtu kama yeye anapigania kupona na pindi ukishindikana kwa mujibu wa taratibu ataachia ubunge.

Mkuu sidhani kama utu ni uwanja mpana kila mmoja kujitolea tafsiri yake, hapana,
Mfano naishi na jirani yangu na mtoto wake anapata tatizo linalotaka kupelekwa hospitali haraka usiku na usafiri ni tabu, akija kuniomba niokoe jahazi kwakuwa nina gari kumrash mtoto wake hospitali, ninayo haki ya kusema mimi nimelala muda huu msinisumbue, lakini kwa mujibu wa kibinadamu nitaonekana na jamii sina utu.
Hebu msome mkuu
Cathode Rays kwenye mabandiko yake amejaribu kufafanua vizuri utu
 
Mkuu natumaini katika hili la mbunge zipo taratibu zimezingatia utu, kuwa akifikia hatua fulani basi kibinadamu hawezi tena kuendelea kuwa mbunge, sasa anapokuja mtu na kuanza kukejeli kwa ushabiki wa kisiasa kuwa atolewe tu kwasababua anaumwa si sahihi na haionyeshe ule ubinadamu kuwa huyu ni mtu kama yeye anapigania kupona na pindi ukishindikana kwa mujibu wa taratibu ataachia ubunge.

Hizo taratibu zimezingatia utu kwa mujibu wa nani? Kwangu mimi kwa mfano utu wangu ningeona nimpe mwaka mmoja kama hajapona uchaguzi ufanyike achaguliwe mwengine; wakati taratibu zimekuwa labda niseme na utu mwingi kuliko mie na kutoweka kikomo cha muda wa ugonjwa unaokubalika kisheria.

Hapa ndipo tunapokabiliana na uwanja mpana wa tafsiri kulingana na matukio na nani mwenye ku-impose tafsiri ya utu kwenye tukio husika
 
Nadhani ni vigumu kusema sheria kazi yake kulinda utu iwapo hatuwezi hata kuueleza utu ni nini. Kwa sababu tunaposhindwa kufasiri utu basi na sheria lazima itashindwa kuulinda

Chukua kesi ya FaizaFoxy kwa mfano; alichokifanya si makosa kisheria licha ya kuwa ameonekana kukosa utu.

Ukiangalia kwenye bandiko langu la kwanza hapo juu nimejaribu tu kidogo kutoa mtazamo wa "utu" wetu ni kitu gani....

Utu unaweza ukaandikwa kwenye katiba (kwa maana jamii yetu inatafsiri vipi utu na inaweka mambo gani kama kigezo cha utu) lakini zaidi msingi wake ni katika "utashi" wetu wa kibinadamu, kwa yale ambayo tutayatafsiri kama "utu" au "kukosa utu"

Zaidi ya yote kwa ufahamu wangu mdogo wa basic law, sheria zipo (plus sheria mama yaani katiba) ili kuhakikisha utu wa mtu unazingatiwa katika uendeshaji wa shughuli za binadamu, either by state machinery au kati ya watu wenyewe kwa wenyewe. Inasaidia kutoa tafsiri ya ni wapi mtu kavunjiwa utu wake na ni nini remedy (kwa aliyevunjiwa utu) na punishment (kwa alievunja utu). Kwa mfano anagalia sheria zote unazozifahamu kuanzia biashara, mikataba, ardhi, jinsia au ndoa n.k utagundua zinachokusudia ni kuweka usawa na kuhakikisha kila mtu anastahili kile anachostahili (kwa tafsiri ile niliyotoa kwenye bandiko langu la kwaza).....Tatizo ni wale waliokabidhiwa jukumu la utungaji na utekelezaji wake kuna mahali wanaharibu.

Hili ndilo MLK Jr anasema "
Law and order exist for the purpose of establishing justice and when they fail in this purpose they become the dangerously structured dams that block the flow of social progress"

All in all, cha msingi na cha kuelewa ni kuwa "Utu" sio lazima uwe kwenye maandishi kwa kile kinachoitwa "sheria" au "katiba", utu lazima uwe kwenye MOYO na UTASHI wa mwanadamu kwani hata kama utakuwa uko kwenye maandishi na hauko kwenye MIOYO na UTASHI wa watu, bado hauwezi kuonekana kwenye JAMII husika........DIGNITY IS A HUMAN "EMBLEM", a totality of our vibrancy as human race
 
Hizo taratibu zimezingatia utu kwa mujibu wa nani? Kwangu mimi kwa mfano utu wangu ningeona nimpe mwaka mmoja kama hajapona uchaguzi ufanyike achaguliwe mwengine; wakati taratibu zimekuwa labda niseme na utu mwingi kuliko mie na kutoweka kikomo cha muda wa ugonjwa unaokubalika kisheria.

Hapa ndipo tunapokabiliana na uwanja mpana wa tafsiri kulingana na matukio na nani mwenye ku-impose tafsiri ya utu kwenye tukio husika
Kwenye blue, mkuu dont complicate issues, utu ni kwa mujibu wa sisi binadamu kwa yale tuanayoyafanya na tunayofanyiwa na yakakubalika na jamii, utu ni nature huitaji kuwa na source mkuu, ninapo umwa kwa hali ya kawaida nategemewa kupona, hivyo kuna grace period ya kusubiria au daktari athibitishe vinginevyo kuwa huwezi tena kuendelea na position hiyo, sasa ukiumwa malaria kesho na mwingine anaweza kuja na hoja kama zako akaona wewe kuumwa wiki moja ni nyingi na akataka uchaguzi uitishwe kama wewe ulivoona mwaka ni mwingi.
Issue hapa sio muda tu, muda ni debatable nakubali lakini utu hapa ni kutambua chances yake ya ku recover, na mleta mada kiukweli aliileta kishabiki zaidi ndio maana zikaja tuhuma za utu.

Back
Top Bottom