Nini Hasa Hutokea Mtu Anapokata Roho?

Babuji

Senior Member
Nov 27, 2008
197
3
Wanasayansi nchini Marekani wamejaribu kufanya uchunguzi kugundua ni kitu gani humtokea mtu anayekata roho na wamethibitisha kwamba kitendo cha kukata roho huwa si cha dakika moja tu puu mchezo umeisha, hufanyika kwa kipindi kirefu kidogo baada ya moyo kusimama na wakati mwingine huenda zaidi ya lisaa limoja.

Mtu anayefariki huwa kama vile yuko kwenye sinema ya maisha yake mwenyewe.

Kwa kusikililiza vielelezo vya watu ambao walihesabika kisayansi wamefariki lakini baadae wakazinduka, wanasayansi wanaendelea na uchunguzi wao wa kinachotokea wakati wa kukata roho.

Uchambuzi wa utafiti huo umeelezewa kwenye kitabu kinachoitwa “What Happens When We Die” kilichoandikwa na Dr. Sam Parnia wa Weill Cornell Medical Center.

"Asilimia 10 hadi 20 ya watu ambao awali walihesabika kisayansi wamekufa lakini baadae wakazinduka, walisema kwamba walikuwa kama wamezimia na baadhi yao walisema kwamba walikuwa wakijiona wako juu angani huku wakiwaangalia madaktari na manesi kwa chini wakihangaika kuitibia miili yao", alisema Parnia.

"Kisayansi wakati mtu anapofariki ubongo wake huwa haufanyi kazi hivyo kusingekuwepo na hali ya mtu kujiona amezimia" alisema Parnia.

Sayansi inasema kwamba wakati mtu anapopoteza mapigo ya moyo huhesabika amefariki, lakini kitu kinachowaumiza kichwa watafiti ni kujua nini huendelea kwenye ubongo baada ya moyo kusimama na cells kuanza kufariki.

Dr. Parnia na watafiti wake wanatafuta njia ya kugundua hali ubongo wa mtu ambaye yupo kwenye mlango wa kifo.

"Hivi sasa hakuna mwenye uhakika kwamba hali zinazosemwa kutokea wakati mtu anapofariki huwa ni za kweli au ni njia ya mwili kujaribu kujisahaulisha maumivu makali ya kukata roho", alisema Dr. Parnia.

Soma zaidi

http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3268926&&Cat=2
 
Back
Top Bottom