Nini chanzo cha kuvunjika kwa ndoa kwa jamii ya sasa?

88 girl

New Member
May 27, 2011
3
1
Inaonyesha kuwa ndoa nyingi za siku hizi hazidumu kwasababu ya umasikini ambao unapelekea ndoa nyingi kuvunjika .je hiyo ni sababu ya mzingi inayopelekea kuvunjika kwa ndoa nyingi kwa jamii ya sasa ?
 
ndoa nyingi za siku hizi hazidumu kwasababu ya umasikini ambao unapelekea ndoa nyingi kuvunjika
utafiti gani unaonesha hivyo? mwaga data zako humu tuone,
 
Hofu ya Mungu imekwisha.
Heshima kwa mume, mke, ndugu imeshuka.
Sababu ziko nyingi zaidi ya umaskini.. nafikiri wenye uwezo kiasi ndio wanaongoza kwa sababu ya kiburi na tamaa ya mali na ngono.
 
Sidhani kama ni sababu. 80% ya watanzania vijijini ni fukara wa kutupwa, ndoa zao zinavunjika? Kuiga iga ndo kunawaponza.
 
Inaonyesha kuwa ndoa nyingi za siku hizi hazidumu kwasababu ya umasikini ambao unapelekea ndoa nyingi kuvunjika .je hiyo ni sababu ya mzingi inayopelekea kuvunjika kwa ndoa nyingi kwa jamii ya sasa ?
Umasikini sio sababu.
  1. Siku hizi mwanamke anakulazimisha umuoe, zamani mwanamme unamlazimisha
  2. Siku hizi kuolewa ni fasheni
  3. Tafouti ya mwanamke na mme haipo tena
Kifupi maadili hayapo tena, ukiwa na mke unakuwa stressed zaidi ya kuwa peke yako.
 
Inaonyesha kuwa ndoa nyingi za siku hizi hazidumu kwa sababu ya umasikini ambao unapelekea ndoa nyingi kuvunjika .je hiyo ni sababu ya mzingi inayopelekea kuvunjika kwa ndoa nyingi kwa jamii ya sasa ?

Hapo kwenye RED - Umetoa wapi takwimu za kujua ndoa zinavunjika sana, umetumia kipimo gani?

Hapo kwenye BLUE - umejuaje kuwa ni umaskini?

Ni vizuri kuja na statistics nzuri ku-support conclusion yako hiyo. . Kwa kifupi, tungeomba source, ya kuonesha ndoa zinavunjika sana
 
cheating zimezidi,kwa upande wa wanaume na wanawake pia.kutokuvumiliana,kutokuwa tegemezi kwa mtu kunakufanya bora uachie ngazi.upungufu wa maadilifu kwa kutokuheshimiana{mmojawapo anakuwa na wapembeni na haiwi siri}
 
1.Watu wengi wanaingia katika ndoa bila kujua majukumu na wajibu wao kama mume au mke.
2.Wengi wao kushindwa kuvumilia mapungufu ya kibinadamu aliyonayo mwenzake.
 
Ndoa nyingi zinavunjika ila sababu zipo nyingi tu,
1.umaskini
2.tamaa.
3.kuwa mbali na mpenzi wako.
4.fumanizi
5.ugumba,
6.ndugu kuingilia kwenye ndoa za watu wengine.
7.
8.
9.
n.k
 
UKISOMA HII HABARI INAWEZA KUKUPA PICHAKIDOGO SABABU KAMILI KAMA SIO ROBO
MKAZI wa kijiji cha Ubinga kata ya Mhugi, Tabora, Bundala Mwandu (26) amejinyonga baada ya walezi wake kumkataza kuoa mke wa pili.

Akithibitisha jana kutokea kwa tukio hilo, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Nzega, Issa Muguha, alisema Mwandu alikutwa amejinyonga Juni 13 saa nne asubuhi katika kijiji hicho.

Muguha alisema, kabla ya kujinyonga, Mwandu alikuwa na mke mmoja na alitaka kuoa wa pili, lakini alipopeleka taarifa hiyo kwa walezi wake, hawakukubaliana na uamuzi huo.

Baada ya taarifa hiyo kukataliwa, Mwandu alifikia uamuzi wa kujinyonga kwa kutumia kamba ya gome la mti.

Akizungumza na gazeti hili, babu wa Mwandu, Bulabo Kinimba, alisema alipopata taarifa ya mjukuu wake kutaka kuoa mke wa pili, alimshauri asubiri mpaka baadaye.

Kinimba alisema alimshauri kwamba kwa sasa umri wake hauruhusu kubeba majukumu makubwa ya familia mbili.

"Nilimwambia asubiri baadaye ndipo angeze mke wa pili, kwani bado ana umri mdogo, nashangaa kijana wangu amefikia uamuzi huu," alisema babu huyo.
 
Bundala Mwandu (26

JAMANI JINA LIMEKUWA KALI DINI GANI HUYU...?
 
1.Watu wengi wanaingia katika ndoa bila kujua majukumu na wajibu wao kama mume au mke.
2.Wengi wao kushindwa kuvumilia mapungufu ya kibinadamu aliyonayo mwenzake.
siko mbali nawe umeniwai tu, umaskin si tatizo mbona hata matajir pia humwagwa
 
Inaonyesha kuwa ndoa nyingi za siku hizi hazidumu kwasababu ya umasikini ambao unapelekea ndoa nyingi kuvunjika .je hiyo ni sababu ya mzingi inayopelekea kuvunjika kwa ndoa nyingi kwa jamii ya sasa ?

As far as I know, umaskini has nothing to do with kuvunjika kwa ndoa. ndoa nyingi zinavunjika kwa sababu ya TAMAA. watu wanapendana kwa sababu ambazo ni temporary kama vile pesa, sura nzuri, shape nzuri, kazi nzuri , kumiliki vitu kama magari n.k. na pindi pakitokea hali ya kuyumba kidogo kwa hivyo vitu hapo basi penzi nalo huzimika ghafla, au mmoja wapo nae akimudu kuwa na pesa au gari basi haoni sababu ya kuendelea kuwa na yule aliempendea pesa. ingekuwa umaskini unavunja ndoa wazee wetu wasingeishi hata kutuzaa sisi. mimi mwenyewe nahisi nisingeishi na mume wangu hadi leo kwa kuwa wakati tukioana hatukuwa na chochote zaidi ya kitanda na kabati lakini tuko pamoja kwa muda sasa na tuna kila kitu kizuri ambacho tunakihitaji ktk maisha yetu watoto, nyumba nzuri, magari, pesa, tuna amani na furaha tele na hatukumbuki tena umaskini wetu tulikoanzia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom