Nini Cha kujifunza toka kwenye Picha hii?

waziri mkuu yupo na ndo mtendaji wa serikali. kama hatimizi majukumu yake nafikiri tusimtwishe mzigo rais
Hauijui KATIBA yetu. Nadhani JK kuna kitu alijifunza kwa kuzifunga zile kamba za viatu vya yule mtoto. Kwamba hatuna kiwanda cha viatu Nchi hii kama ilivyokuwa BORA SHOES enzi za Mwalimu.
 
Kitendo hiki kinaweza kufanywa tu na mtu anayejali,hebu tazama wale watu wa serikali nyuma yake.
Si rahisi kuamini kuwa miaka ya 60 mimi nikiwa mdogo sana umri wa mtoto huyo, vilevile nilkutana na Mwalimu uso kwa uso nikiwa ndani ya nguo za Young Pioneers.Na Mwalimu alifanya kama JK anavyofanya sasa.
That boy will remember this for his entire life.
na uzee wako huo unaona kufungwa kiatu na raisi ni kitu cha maana sana......eti atakumbuka maisha yake yote.......tukisema tunataka matendo sio maneno sio hayo ya kufunga watoto viatu au kuwapa pipi bana aaaghhh!!!!!!!!
 
kwanza huyo mtoto anaonekana ana njaa, asubuhi alipiga uji wa limao.amechezeshwa gwaride kwenye jua kali, midomo imekauka, ana kiu, anaweza akaanguka kama raisi wakati wowote.
 
kwani cha ajabu nini hapa we mtoa mada?au ndo kila kitu watu tuwe critic tuuuu,ujinga na utoto huo,ebu waza mambo ya manufaa eti,kwani kumfunga didamu mtoto kunasababisha shida gani?He is a caring father,close to people,not afraid to touch anyone!angekuwa Obama ungesifia kisa foreigh=ner,acha tabia yako chafu wewe mtoa mada!!

77 mbona unamlaumu bure mtoa mada? inonesha hukumwelewa na maamuzi yako ni kutazama shilingi pande moja. Baada ya kupitia hoja za wachangiaji nimejifunza mengi, hiyo picha ina maana kubwa sana. Na kila mtu kwa mtazamo wake anaweza kusema lolote, mtoa mada hakuiponda hiyo picha wala hakuipa sifa aliichoomba ni kwamba umejifunza nini? tuambie umejifunza nini kwa hicho kinachoonekana kwenye picha ili tujue upeo wako. unajua unaweza kumsifia hata mjinga akifanya baya na ukamdharau mwerevu kwa kufanya zuri, yote ni upeo na mitazamo tu. Kama Rais amefanya hivyo toka moyoni, basi ni jambo zuri la kuigwa, nampongeza.
 
Jamani tujitahidi kufanya upembuzi yakinifu 2010 tuchague watu watakaoweza kutatua hizi kero. tuangalie mbadala wa CCM.
 
na uzee wako huo unaona kufungwa kiatu na raisi ni kitu cha maana sana......eti atakumbuka maisha yake yote.......tukisema tunataka matendo sio maneno sio hayo ya kufunga watoto viatu au kuwapa pipi bana aaaghhh!!!!!!!!

It takes a human being to appreciate another.
If at all you have no human feeling for goods deeds then thats just too bad.
 
kwanza huyo mtoto anaonekana ana njaa, asubuhi alipiga uji wa limao.amechezeshwa gwaride kwenye jua kali, midomo imekauka, ana kiu, anaweza akaanguka kama raisi wakati wowote.

Ungetupa picha na mtoto wako wewe yukoje?
 
8D6U1237.JPG

Muungwana analenga kampeni mwakani.
Bila shaka Cap J Komba atatumia hii picha kuandaa wimbo wa kutuzuga 2010.

Tumpe kura kikwete tumpe kura
.. anapenda na anawajali watoto
Tumpe kura kikwete tumpe kura
.. atawapa elimu bora watoto

Muungwana anajua hesabu kuliko mnavyofikiri.
 
BWANA Yesu alisema atakayempokea mmoja kati ya watoto hawa, amenipokea mimi, Huyu jamaa kajishusha kwa watanzania, ina maana yuko chini kwa watu wote, HII NI SEHEMU YA KAMPEINI
 
wengi hapa wamemuona na kujifunza kwa rais tu mi nimemuona huyu mlizi/mpambe wake nae kainamisha kichwa anamuangalia rais badala ya kuangaza macho huko na huko[kuwasiliana na wenzake ili kuhakikisha hali ya usalama wa mkulu,
 
Jamaa hana kazi! Wakati watu wanahangaika kutafuta suluhu ya umeme yeye wala hana lolote analojua! Adrenalin level yake ni zero na huyo ndiye kamanda wetu katika vita!!

kwani kazi ni nini? ulichoona wewe ni umeme tu ndo kazi? au huyo mtoto ambaye anaitwa taifa la kesho haitaji kuonyeshwa mapenzi hata ya kufungwa kamba za viatu ili ajue kuwa wakati wake utakopofika nafsi ya upendo ndo inajenda nchi?

au hujui kuwa penye upendo ndo umoja unakuwepo, na penye umoja ndio hayo ya umeme hutatuliwa?

vipi familia yako unaionyesha upendo unaostahili?

kwa upande wangu Rais ni wa watu wote so kila kitu kina nafasi yake na wakati wake so hiyo nihaki ya mtoto katika mazingira hayo unayoyaona hapo.
 
BWANA Yesu alisema atakayempokea mmoja kati ya watoto hawa, amenipokea mimi, Huyu jamaa kajishusha kwa watanzania, ina maana yuko chini kwa watu wote, HII NI SEHEMU YA KAMPEINI

Pia aliwahi kumpa mtoto pipi, si mnakumbuka?
 
kazoea kucheza na watoto...mnakumbuka miezi miwili iliopita alimpa mtoto pipi.
 
Jamaa inaonyesha yuko poa ila kajizonga na kuzongwa. Anatamani sana kuwa mtu bora ila kwa sasa hawezi. Katika biblia kwenye mfano wa mpanzi ni sawa na zile mbegu zilizosiwa mibani zikamea ila zikasongwa na miiba hadi zikafa. Swali. Kosa ni la nani kati ya aliyesia mbegu na aliyeweka miba hapo?
 
wengi hapa wamemuona na kujifunza kwa rais tu mi nimemuona huyu mlizi/mpambe wake nae kainamisha kichwa anamuangalia rais badala ya kuangaza macho huko na huko[kuwasiliana na wenzake ili kuhakikisha hali ya usalama wa mkulu,

sio kazi za mpambe kuhakikisha ulinzi na usalama,kazi yake ni kumuandalia mkubwa mambo madogo madogo kama kumshikia kamkoba kenye nyaraka ambazo sio siri saaana.
 
kwani kazi ni nini? ulichoona wewe ni umeme tu ndo kazi? au huyo mtoto ambaye anaitwa taifa la kesho haitaji kuonyeshwa mapenzi hata ya kufungwa kamba za viatu ili ajue kuwa wakati wake utakopofika nafsi ya upendo ndo inajenda nchi?

au hujui kuwa penye upendo ndo umoja unakuwepo, na penye umoja ndio hayo ya umeme hutatuliwa?

vipi familia yako unaionyesha upendo unaostahili?

kwa upande wangu Rais ni wa watu wote so kila kitu kina nafasi yake na wakati wake so hiyo nihaki ya mtoto katika mazingira hayo unayoyaona hapo.

CKabula,

Ukweli hii picha ni nzuri sana na kwa kuwa imefanywa na Rais wetu ni kitu cha kufurahisha sana. Huo ni upande mmoja wa shilingi na sijapinga!

Kama umefuatilia mijana kwa umakin, watu wanasema kuwa nchi iko kama vitani hivi. Kwa hiyo picha ya maana sana sasa hivi ni kumwona rais anashughulikia hilo tatizo na siyo kucheza cheza na watoto. Labda jaribu kutafuta maanda ya adrenalini. It never gives a chance for Santa to celebrate with kids!
 
Hii picha inaonyesha kuwa huyu mkuu,anasisitiza kuwa yeye ni baba anayejali familia,na watoto sikuzote ni wakutupiwa jicho kila wakati coz they are not care!!
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom