Nini Cha kujifunza toka kwenye Picha hii?

Hamna chochote cha kujifunza hapo. Sio kila picha apigwayo au apigayo raisi ina mafunzo.
 
Wewe ni Great thinker!!

Kama angekuwa baba angeenda kulala siku zote hizo tuko gizani? Angeendelea kutanga tanga dunia nzima akikomba pesa sawa na bajeti ya kujenga vyumba kibao vya madarasa au kulipa walimu kama 500 kwa mwezi? (trip yake inatumia ~50ml wakati mshahara wa mwalimu ni ~200,000/-). Kweli wajinga ndio waliwao!

Hapa rais hatuna kabisaa jamni kifupi nchi imemshinda kabisaa maana msafara wake unaweza kulipa walimu wetu na madaktari, lakini wapii ye anaona bora akashangae mtandao wa google!!! hivi nasikia amealikwa Kingstone ni kweli tusubiri tuu sijui atarudi na Ganja jamni hehhe tutafika tuu poor walimu wetu walidhani watakombolewa na mama wa kwanza lakini hali imezidi kuwa mbaya. Kweli alieshiba hamkumbuki kwenye njaa!!
 
8D6U1237.JPG


Photo OP. Good for JK.

Swali ni kuwa, ni nini watoto kama huyo walichotengenezewa na Mh. JK kitakachowanufaisha hapo baadaye? Hadi hivi sasa amewaletea yafuatayo;
  1. Elimu Duni
  2. Matibabu Duni
  3. Ufisadi
  4. Ukosefu wa umeme
  5. Ongezeko la Deni la nchi
  6. Wizi wa madini
 
hata kubrashi viatu vyake pia hawezi au hataki?hebu angalia hicho cha kushoto.sijui huyo Aide de Camp hapo nyuma nafanya nini.Yule wa Mkapa alikuwa sharp
 
at this stage i careless kuhusu hizo deal zao...sie tunataka umeme ama sivyo ei ya simenti itatuua

...acha ikuue tuu,hiyo 85% isiyopata hata huo mgawo wa saa moja mbona wanaishi tuu na ndio wanawalisha na jembe lao la mkono!
 
KIPO KITU CHA KUJIFUNZA
Lazima tukubali ukweli wakati mwingine wandugu!Kiongozi yeyote duniani ana sura tofauti tofauti. Mchukue G.W.Bush alikuwa na sura zake. Sura moja wamarekani walimfagilia, na sura nyingine hawakumfagilia.
Katika picha hii lazima tuukubali upande mwingine mzuri wa sura ya Rais wetu. Toka aingie madarakani amejionyesha ni Rais aliyetofauti na Marais wote waliotutangulia katika Taifa letu. Ni Rais wa watu wote asiye na matabaka. Ni Rais wa watu kwa maneno mepesi nikisema. Ingawa kwa upande mwingine wa sura imekuwa ikimgharimu na kujikuta akiitumia fursa hyo kukumbatia mambo yasiyo ya msingi na ni ya hatari kwa taifa kwa ujumla.
Lakini katika picha hii nakubali Rais wetu ni Rais wa watu. Hana mipaka.
 
acha kejeli

umeme mitambo ya Dowana na IPTL ipo semanyiemnaojiita wapiganaji hamtaki iwashwe.

hebumpumzisherais wetu sie
Hivi huoni hoja yako ni ya kijinga?

Huyo unayemuita 'Rais wetu' si ndio most powerful person ktk ranks za kiuongozi ktk Taifa letu? Sasa yeye kashindwa nini kwenda kubonyeza kitufe kuwasha hayo maDOWANS? Mwe!
 
JK ni mtu wa WATU. Alitakiwa tu asiwe RAIS MTENDAJI ili aendelee na kazi hizi za kubusu watoto, kutembelea wagonjwa, kuhudhuria misiba, kuzima mwenge,...Awepo WAZIRI MKUU MTENDAJI. Tunaweza kuibadili KATIBA yetu sasa?
 
JK ni mtu wa WATU. Alitakiwa tu asiwe RAIS MTENDAJI ili aendelee na kazi hizi za kubusu watoto, kutembelea wagonjwa, kuhudhuria misiba, kuzima mwenge,...Awepo WAZIRI MKUU MTENDAJI. Tunaweza kuibadili KATIBA yetu sasa?

Duh, sasa kwanini tubadili katiba kwa ajili ya ugoigoi wa mtu mmoja?
 
Mnafki tuu kama kweli anaupendo na watoto bas angempa msingi bora wa elimu, chakula na malazi,, hiyo yote hapo anatafuta kampeni tu ya mwakani, kwani akimfunga kamba za viatu ndo mtoto atashiba??? hebu tuamke jamani mbona ni jambo dogo tuu??? tumuulize tu huyo dogo kapata mlo gani kwa siku ndo tuweze kumsifia kama kweli ni baba anaejali watoto!!!


Jamani tuwe na kiasi.
Where is our sense of moral justice.
Mtu unazaa mtoto kwa raha zako na unategemea Raisi au kodi za wananchi walishe mtoto huyo?
Kejeli kama hizi si tu zinaelezea chuki ya mtu kwa kiongozi lakini vile vile upeo mdogo wa utatuzi wa matitizo ya nchi kuanzia ngazi ya mtu mmoja mmoja.
Pole sana mama!!
 
Kama alivyokwenda "kutibiwa" muhimbili, anajaribu kujishusha ili aonekane kama mwenzetu vile..........
 
Jitume tumikia wakubwa na wadogo, Inawezekana timiza wajibu wako...
 
kwani cha ajabu nini hapa we mtoa mada?au ndo kila kitu watu tuwe critic tuuuu,ujinga na utoto huo,ebu waza mambo ya manufaa eti,kwani kumfunga didamu mtoto kunasababisha shida gani?He is a caring father,close to people,not afraid to touch anyone!angekuwa Obama ungesifia kisa foreigh=ner,acha tabia yako chafu wewe mtoa mada!!
 
waziri mkuu yupo na ndo mtendaji wa serikali. kama hatimizi majukumu yake nafikiri tusimtwishe mzigo rais

Hata kama ni jukumu la waziri mkuu na hatalitekeleza nani anatakiwa kumuwajibisha? We John Kitabi wewee unajua unachokiongea???
 
Ni mfano ulioko kwenye Msahafu wa Kikristo. Mkubwa mtumikie mdogo na hapo umewajibika. Asiyewapenda watoto wadogo kama hawa ni vigumu kuurithi ufalme wa Mbinguni. Ulipomsaidia mtoto mdogu yule ulinisaidia mimi, karibu katika ufalme wangu.

Yako mengi, lakini je, labda pia ni kampeni? Kwani kama kitendo hicho kinafanyika tu pale penye makamera, ni unafiki dhahir. Kama ni utaratibu wake basi hekoooo! Huwezi kujua, anayefungiwa kamba za viatu vyake anaweza kuwa the future Presidaa.

Waheshimu wale uliowaacha chini maana huwezijua watakufaa vipi utakapokuwa unashuka chini. Nyie watoto waheshimu wakubwa zenu, maana wanaweza kuona unachopungukiwa na kukusaidia, wameona na kupitia mambo mengi hata kujua mabaya mengi na mazuri mengi .........

Leka
 
Jk is a human too; does this act stop him for been a president? Kwanza watu wana akili finyu ina maana ukiwa Rais huna hisia za kibinadamu, huwezi kuiona walio chini, huwezi hata kutambua kwamba unaweza kufanya jambo kama binadamu wa nyama na mifupa tu? Tumekuwa mno na roho mbaya ya kudhani rais si binadamu, hana hisia wala chohote kama binadamu wa kawaida. Naomba nielezwe, kufunga kamba za viatu vya mtoto amefanya kosa gani. Je, kufanya hivyo ndiyo maana hakuna umeme? Watu wawe na fikra za maana tuache kupayuka bila staha!
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom