Nini asili ya jina Tanganyika na Nani alilitunga jina hili?

Kwa hiyo comrade unatuambia kwamba jina Tanga lilikuwepo kabla ya jina Tanganyika? Na kama ni hivyo sasa mkoa wa Tanga ulikua uko ndani ya nchi inayoitwaje?

Kabla ya 1885 Africa ilikuwa na nchi rasmi zifuatazo: Ethiopia, Liberia na Egypt....kwingineko yalikuwa 'maeneo" tu bila mipaka rasmi
 
Historiaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! huku sio kwangu, labda mngeniuliza Newton laws of motion na makitu mengine kama hayo ila huku duuuuuuuuuuuuuuuuh!!!!!!!!!!!!!! mweupe.
 
Kumekuwepo na maswali mengi juu ya jina la tanganyika na baadaye tanzania
sisi twajua yakwamba jina tanzania lilitokana na munganiko wa nchi mbili tanganyika na zanzibar,
sasa swali nikwamba Tanganyika ilitokana na nini?
Na nini maana ya Tanganyika?
Na ninani aliyependekeza jina Tanganyika?

Tanganyika ilitokana na maneno hayo mawili yaani Tanga na Nyika.

Tanga au kutanga ni pale unapokuwa baharini na mashua ukitoka pande moja kwenda pande ingine kwa kutumia pawa au kwa kiingereza twasema "sailing".

Nyika ni eneo kubwa la ardhi ambalo mtu anaweza kutembea kwa miguu bila kutumia baiskeli wala gari kutafuta anachotafuta iwe amepotea au nakwenda kutafuta mji ulio karibu.

Hivyo twasema anatangatanga nyikani akitafuta njia.

Sasa akaja yule mgunduzi bwana SPEKE na mawakala wengine kama Stanley na wengine ambao waliingia ndani ya eneo lote la Afrika Mashariki kwenda ndani na SPEKE akaelekea UJIJI na kwa wao waliona kwamba eneo lolote lililoko kando ya ziwa basi ni nyika na Tanga ni kule kuzunguka lile eneo.

Lakini SPEKE alipofika Ujiji Kigoma na kushangaa maajabu ya ziwa lililokuwa kandoni mwa njia aliyopita akitanga kutafuta makoloni akaona atunge jina la ziwa hilo na kuliita Tanganyika na likakubalika kule Ujerumani kwa wakubwa wake.

Baada ya vita kuu ya kwanza mwaka (1918 kupigana) lakini mgogoro uliendelea na 1919 kulifanyika mkutano baina ya wajerumani na nchi washirika ikiwemo Uingereza na kukawepo mkataba uitwao Versailles ambao uliweka wazi nani anamiliki wapi na kwa vipi.

Kwahio Ujerumani ikapoteza sehemu yao waliyoiita Germany East Africa na Uingereza ikachukua eneo hilo na wakaamua kuliita Tanganyika, hivyo waingereza walitubatiza jina hilo la Tanganyika hadi wanatupatia uhuru.

Nafikiri waliona ni rahisi kulitamka jina hilo na kwamba wasingeweza kumshusha hadhi bwana SPEKE ambae alijivunia kugundua ziwa ambalo aliliita Tanganyika.

Hivyo kwa kifupi bwana SPEKE alibatiza ziwa kuwa Tanganyika na Waingereza walibatiza eneo lote la nchi yetu kwa kuiita Tanganyika, wenyewe wakitamka TA_NGA_YI_KA.
 
kwahiyo hili ziwa Tanganyika lilikuwa likiitwa hivyo toka mwaka gani?
Maana hata jina la ziwa limetokana na watu kulipa jina,
Maswali mengine ya ajabu kweli. Vipi ndugu yangu, je kwenye post yangu uliyokwoti niliandika nini? Nilisema kuwa nitalifanyia utafiti kujua lilianza lini lakini ni la siku nyingi kwa vile record zilizoko zinaonyesha kuwa hata mwaka 1859 lilikuwepo ingawa lilianza kutumika kama nchi mwaka 1922 tu.
 
Tanganyika ni eneo lililohusisha mkoa wa Kigoma, Tabora na sehemu za Rukwa. Hii habari niliipata huko Kigoma. Mzee mmoja anasema eneo lingine la Tanganyika ya leo liliitwa Azania. Hivyo Tz Bara =Tanganyika +Azania.

Researchers watujuze.

Hacha kupotosha asili ya neno tanganyika ni Tanga na Nyika.........Tanga=Sail........Nyika= Wilderness Sail in the wilderness...au ni nyika baada ya pwani ya Tanga soma link hiyo Tanganyika Territory - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Kama utafiti wako ni kusoma Wikipedia basi huna kiwango cha kujibizana na mimi katika mambo ya historia. Wanaojuia historia hawatumii Wikipedia kama reference. Hata hapo juu nimekuwekea reference nzuri original inayoonyesha kuwa neno Tanganyika lilikuwepo mwaka 1859, karibu miaka sabini kabla ya Tanganyika Territory, nikakuahidi kufanya research zaidi ili kutafuta reference za nyuma zaidi kuona neno hilo lilianzia wapi, halafu wewe unakazania reference nyepesi kama Wikipedia. Iwapo Wikipedia ndilo lingekuwa jibu basi hata kusingekuwa na haja ya kujadili mada hii.

Kama uko siriasi kujua mambo, usiwe mtu wa pupa; jaribu kuwa positive na kuyaangalia kwa mapana yake muda wote.
 
Wakati facebook inapotosha watoto wa primary na secondary kwa kuwapotezea muda, Wikipedia inawapotosha undergraduates na graduates wanaopenda shortcut ya madesa!

Kama kuna kitu siipendi kwenye mitandao ni Wikipedia!
 
Ni kweli, watoto wa siku hizi wanapenda sana njia za mkato za kusoma kwenye internete na kuchukulia kuwa huo ndio ukweli.

Nimefanya utafiti wa kutosha na sasa ninaweza kuwaambia wote mageuzi1992, Dingswayo, Richard, King Kong III, mnyinda na wengineo mliochangia post hii kwa kadri ya uwezo wenu kuwa neno "Tanganyika" halina uhusiano wowote maneno ya "Tanga" na "Nyika" kama inavyoripotiwa Wikipedia na kweingineko, nitajaribu kwenda kusahihisha huko Wikipedia nikiweza, kwa vile mtu yoyote anaweza kufanya hivyo.

Ni kweli kuwa jina la nchi Tanganyika limetokana na kuwepo kwa ziwa Tanganyika, lakini asili ya neno Tanganyika lenyewe ndilo lililokuwa na utata. Kwa vile sina muda wa kutosha kuandika historia yote kwa kirefu, nitadondosha kidogo tu kuwa jina "Tanganyika" limetokana na neno "Changanyika." Nitatoa maelezo kwa kina huko mbeleni, ila lina sababu kubwa mbili ni: (1) kuchanganyika kwa waarabu na wamanyema pale ujiji (2) kuchangayika kwa maji ya maziwa ambayo yalikuwa hayajulikani ya ukerewe na ya Nyanja kwenye ziwa hilo la ujiji.

Kwa vile maelezo yake ni marefu yanayohitaji supporting documents na graphics, nitayatoa kwa kina nikipata nafasi nzuri ya kufanya hivyo. Nikiahidi hapa JF mara nyingi huwa ninatimiza hasa iwapo nimeshakamilisha utafiti wangu. Kwa vile sasa hivi nimeshakamilisha utafiti huo, nitaleta ripoti kamili siku chache zijazo. Nitawaacha na ramani hii inayoonyesha ziwa hilo likiitwa jina la kijerumani.
 
Attachments

  • Slug_map.jpg
    Slug_map.jpg
    150.4 KB · Views: 131
Mkuu Kichuguu ahsante kwa ufafanuzi wako ingawa hujamalizia kama unavyosema utajaza maneno mengi.

Mimi pia nimesoma historia na tatizo ni kwamba wale wajifunzao leo bado wanakosa msaada mkubwa wa maktaba za kueleweka na sisi wenye nafasi ya kuangalia maktaba zilizojaa taarifa mbalimbali hatuna budi kuzitumia.

Bado nafanya jitihada za kupata picha halisi kuhusu eneo letu kabla halijaitwa Tanganyika na baada ya kubatizwa jina hilo, kama unavyofahamu historia ni jana, leo na kesho na historia pia hujirudia, ila nimepitia sehemu mbalimbali zikiwemo Maktaba na mengine.

Ukweli unabakia kuwa Tanganyika ni maneno mawili ya Tanga na Nyika na ni Mwingereza John Speke alieobatiza jina hilo.

Wazungu waliposikia habari za kuwepo maziwa makubwa ndani ya eno la Tanzania ya wakati huo hasa ziwa Nyanza ambalo leo laitwa Victoria, walimtuma mwingereza bwana Speke ambae alikuwa ni mtaalam wa ugunduzi na ujasusi. Speke alikuwa akishirikiana na jasusi mwingine mwingereza aitwae Burton ambae kwa pamoja walikuwa wakibishana wapi chanzo cha mto Nile kinaanzia.

Kwahio waliondoka Zanzibar mwezi June 1857 kuelekea Dar-es-Salaam hadi Ujiji na safari hiyo iliwachukua miezi sita kufika kwenye ziwa ambalo wangeliita Tanganyika. Hivyo John Speke alilipa Ziwa hilo jina la Tanganyika mwezi February mwaka 1858. Na ni bwana John Speke huyohuyo aliendelea na safari baada ya kumwacha bwana Burton ambae alianza kuugua na mwezi July mwaka huohuo akagundua ziwa Nyanza na kuamua kuliita Victoria kumuenzi malkia wa wakati huo.

Sababu kuu ninavyofikiri ni kwamba waliamua kutumia jina la tanganyika kwa kumaanisha kwamba Ujiji ndio makao makuu ya shughuli za serikali ya GEA.

Wajerumani walipokuwa wakiingia ndani ya Tanzania ya leo (wakati huo hapakuwa na jina kamili) wakitokea Zanzibar walikuwa wakipita maeneo mengi tu ya uzaramo (Dar es-salaamya leo) ambayo ndiyo ilikuwa mji mkuu wa kuingia Uzaramo (au USARAMO kama walivyoiita) hadi walipofika Ujiji, na ndipo walipoamua kuanzisha GEA na kuendelea kupaita sehemu ya Tanzania Bara ya leo Tanganyika na hiyo ilikuwa 1885 baada ya mkutano wa Berlin Conference.

Walikuwa wakimaanisha nchi iliyozungukwa na ziwa na hata ile Germany East Africa ilipoanziswha walitumia sehemu ya Tanzania bara ya leo kwa jina la Tanganyika. Pia ukumbuke mote humo walimopita hawakukuta ziwa kubwa na refu namna namna ya hilo la Tanganyika na hata kwenye moja ya Ramani zao utaona wametaja ziwa hilo kama Tanganyika See.

Hivyo hata mwingereza alipochukua tanganyika baada ya vita kuu ya kwanza na ule mkataba wa Versailles walikuwa wakifahamu kwamba Tanganyika ilikuwa ni kainchi kamili na hata mwaka 1925 yule gavana wa kwanza alipewa Tanganyika ili aendeleze kazi.
 
Ni kweli, watoto wa siku hizi wanapenda sana njia za mkato za kusoma kwenye internete na kuchukulia kuwa huo ndio ukweli.

Nimefanya utafiti wa kutosha na sasa ninaweza kuwaambia wote mageuzi1992, Dingswayo, Richard, King Kong III, mnyinda na wengineo mliochangia post hii kwa kadri ya uwezo wenu kuwa neno "Tanganyika" halina uhusiano wowote maneno ya "Tanga" na "Nyika" kama inavyoripotiwa Wikipedia na kweingineko, nitajaribu kwenda kusahihisha huko Wikipedia nikiweza, kwa vile mtu yoyote anaweza kufanya hivyo.

Ni kweli kuwa jina la nchi Tanganyika limetokana na kuwepo kwa ziwa Tanganyika, lakini asili ya neno Tanganyika lenyewe ndilo lililokuwa na utata. Kwa vile sina muda wa kutosha kuandika historia yote kwa kirefu, nitadondosha kidogo tu kuwa jina "Tanganyika" limetokana na neno "Changanyika." Nitatoa maelezo kwa kina huko mbeleni, ila lina sababu kubwa mbili ni: (1) kuchanganyika kwa waarabu na wamanyema pale ujiji (2) kuchangayika kwa maji ya maziwa ambayo yalikuwa hayajulikani ya ukerewe na ya Nyanja kwenye ziwa hilo la ujiji.

Kwa vile maelezo yake ni marefu yanayohitaji supporting documents na graphics, nitayatoa kwa kina nikipata nafasi nzuri ya kufanya hivyo. Nikiahidi hapa JF mara nyingi huwa ninatimiza hasa iwapo nimeshakamilisha utafiti wangu. Kwa vile sasa hivi nimeshakamilisha utafiti huo, nitaleta ripoti kamili siku chache zijazo. Nitawaacha na ramani hii inayoonyesha ziwa hilo likiitwa jina la kijerumani.

Mkuu umeipata wapi hii Changanyika?
 
ngoja na mm nikatafiti zaidi maana mwanzoni nakumbuka niliambiwa Tanga nyika limetokana na ma explorer walipofika kwa mara ya kwanza kwenye pwani ya Tanganyika ,walikuta wenyeji wanawaambia tanga yani walikua wanataka kuwasaidia kutia nanga sikumbuki vizuri ni lugha gani ya pwani,ila kwa wao maexplorer wakawa wanajua wanaambiwa hapa ndio tanga

na hao wazungu walipotaka kwenda kuingia interior wakawaomba msaada wenyeji wawasaidie kuwafikisha wanapotaka kwenda wanapotaka wenyeji ambao ni maakuli wa kusaidia kubeba mizigo wakawa wanawaambia nyika yani maporin maeneo ya ndani, basi hao maexplorer rwakachukua upande wa pwani ni nchi ya tanga na huko kuingia ndani kuna nchi inaitwa nyika,walipomiliki eneo lote wakaunganisha hayo maneno kuyaita Tanganyika
 
Mkuu Richard, record yako siyo sahihi kabisa.

Neno Tanganyika siyo muungano wa maneno mawili ya Tanga na Nyika, ni neno lililokuwa linatumiwa na watu wa ujiji kwa maana ya kuchanganyika. Wakati huo Ziwa lile lilikuwa likijulikana kama Ziwa la Ujiji. Mtu alieanza kuliita ziwa lile kuwa ni Ziwa Zanganyika ni Mr. Cooley katika article aliyoandika mwaka 1845 (zaidi ya miaka 10 kabla ya Burtone na Speke hawajatembelea eneo hilo). Mr Cooley aliandika article yake iliyoitwa "Memoir on the Geography of K'yassi" kwenye toleo la 15 la jarida la Journal of the Royal Geographical Society, mwaka 1845. Mr Cooley alikuwa amemuhoji mtu mmoja wa Lamu aliyejulikana kama Khamis Bin Tani alijifanya kuwa anajua maziwa yoye hayo. Wakati huo eno la pwani lilikuwa likijulikana kama Zanguebar. Cooley aliandika

The Mucarang'a, or people of Monomoezi; still retain the com-
mercial habits for which they were formerly so much noted.
They descend annually in large numbers to Zanzibar. The
journey to the coast and back again takes 9 or 10 months, includ-
ing the delay of awaiting the proper season for returning. It
would appear that they start on the journey down in March or
April, probably at the end of the heavy rains, and return in Sep-
tember. They are decently clothed in cotton of their own manu-
facture ; but the most obvious mark of their superiority above
other nations of Eastern Africa is, that they employ beasts of
burden, for their merchandise is conveyed to the coast laden on"
asses of a fine breed. From a town or tribe called Zanganyika;
on the opposite or south-western side of the lake (which near Oha
is 3 days voyage across), they obtain copper, ivory, and oil of a
red colour. They are said to have formerly used for money
''little balls, like glass, of a reddish colour."* There is no
difficulty in guessing what is here meant to be described. The
most famous mountain of Eastern Africa is Kirimanjara, which
we suppose, from a number of circumstances, to be the highest
ridg« crossed by the road to Monomoezi. The top of this moun-
tain is strewed all over with red carnelian, the rounded pebbles
of which were doubtless the money referred to. The importation
of beads has probably caused the disappearance of the carnelian
currency.

Zanganyika.jpg

Kwenye mkutano wa Royal Geographical Society uliokutana December 15, mwaka 1856 (miaka mitatu kabla Speke na Burton hawajafika kweny ziwa lile,) Dr Livingstone naye alizungumza hivi:

DR. LIVINGSTON: When I was on my way from Linyanti to Loando, I met
with an Arab, who was going to return home towards Zanzibar across the
southern end of the lake " Tanganyenko," and who informed me that in the
country of the Banyassa (Wun' Yassa?) there is an elevated ridge which trends
towards the N.N.E. The lake lies west of it, and in the northern part is
called Kalague. They cross the southern end of it, and when crossing they
punt the canoe the whole way, and go from one island to another, spending
three days in crossing. It seems, from the description I got from him, to be a
collection of shallow water, exactly like Lake Ngami, which is not deep either,
as I have seen men punting their canoes over it. It seems to be the rem-
nant of a large lake, which existed in this part, before the fissure was made to
allow the Zambesi to flow out. That part of the country is described by
many natives as being exceedingly marshy. The Makoloko went up to the
Shuia Lake and found all the country exceedingly marshy, and a large lake
seems to be actually in existence, or a large marsh with islands in it. But it
can scarcely be so extensive as has been represented, as in that case I must
have crossed part of it or heard more of it.

Account ya kwanza kuhus jina Tanganyika iliandiwaka na Captain Richard Francis Burton mwaka 1860 katika kitabu chake maarufu cha "Lake Regions of Central Africa" na hasa kwenye ukurasa wa 367, kama nilivyouambatanisha hapa.
attachment.php

Tanganyika.jpg

Record zote hizo hizo za kihistoria nilizotaja hapo ninazo ila kama nilivyosema kwenye post yangu ya awali, naomba nipate muda wa kuzipanga vizuri, kwa vile siwezi kuzimabatanisha hapa kutokana na ukubwa wake.
 
Ndugu Ritz na mwananthropolojia.

Majibu nimeyaweka hapo juu; mkitaka details zaidi ya hapo basi subirini kidogo nipange maneno lakini page ya kutoka kitabu cha Burton cha mwaka 1860 inatoa majibu mengi kabisa ikitumiwa vizuri kwa kusaidiana na melezo mengine ndani ya post yangu hapo juu.
 
Last edited by a moderator:
Neno Tanganyika linamaanisha 'nyika ya Tanga'. Watembezi 'explorers' wa kizungu waliokuja wakti wa zamani, walishukia Tanga, na wakaingia bara kutafuta chanzo cha mto Nile. Maeneo yale waliyotembea wakayaita 'nyika ya Tanga' au Tanganyika. Soma zaidi hapa:

Tanganyika Territory - Wikipedia, the free encyclopedia

Yes ndio maana watu wa Tanga wanawaita watu kutoka Tabora,Singida,Rukwa na kwingineko huku katika kanda hizo Wanyika
 
Mkuu Richard, record yako siyo sahihi kabisa.

Neno Tanganyika siyo muungano wa maneno mawili ya Tanga na Nyika, ni neno lililokuwa linatumiwa na watu wa ujiji kwa maana ya kuchanganyika. Wakati huo Ziwa lile lilikuwa likijulikana kama Ziwa la Ujiji. Mtu alieanza kuliita ziwa lile kuwa ni Ziwa Zanganyika ni Mr. Cooley katika article aliyoandika mwaka 1845 (zaidi ya miaka 10 kabla ya Burtone na Speke hawajatembelea eneo hilo). Mr Cooley aliandika article yake iliyoitwa "Memoir on the Geography of K'yassi" kwenye toleo la 15 la jarida la Journal of the Royal Geographical Society, mwaka 1845. Mr Cooley alikuwa amemuhoji mtu mmoja wa Lamu aliyejulikana kama Khamis Bin Tani alijifanya kuwa anajua maziwa yoye hayo. Wakati huo eno la pwani lilikuwa likijulikana kama Zanguebar. Cooley aliandika

The Mucarang'a, or people of Monomoezi; still retain the com-
mercial habits for which they were formerly so much noted.
They descend annually in large numbers to Zanzibar. The
journey to the coast and back again takes 9 or 10 months, includ-
ing the delay of awaiting the proper season for returning. It
would appear that they start on the journey down in March or
April, probably at the end of the heavy rains, and return in Sep-
tember. They are decently clothed in cotton of their own manu-
facture ; but the most obvious mark of their superiority above
other nations of Eastern Africa is, that they employ beasts of
burden, for their merchandise is conveyed to the coast laden on"
asses of a fine breed. From a town or tribe called Zanganyika;
on the opposite or south-western side of the lake (which near Oha
is 3 days voyage across), they obtain copper, ivory, and oil of a
red colour. They are said to have formerly used for money
''little balls, like glass, of a reddish colour."* There is no
difficulty in guessing what is here meant to be described. The
most famous mountain of Eastern Africa is Kirimanjara, which
we suppose, from a number of circumstances, to be the highest
ridg« crossed by the road to Monomoezi. The top of this moun-
tain is strewed all over with red carnelian, the rounded pebbles
of which were doubtless the money referred to. The importation
of beads has probably caused the disappearance of the carnelian
currency.

View attachment 97875

Kwenye mkutano wa Royal Geographical Society uliokutana December 15, mwaka 1856 (miaka mitatu kabla Speke na Burton hawajafika kweny ziwa lile,) Dr Livingstone naye alizungumza hivi:

DR. LIVINGSTON: When I was on my way from Linyanti to Loando, I met
with an Arab, who was going to return home towards Zanzibar across the
southern end of the lake " Tanganyenko," and who informed me that in the
country of the Banyassa (Wun' Yassa?) there is an elevated ridge which trends
towards the N.N.E. The lake lies west of it, and in the northern part is
called Kalague. They cross the southern end of it, and when crossing they
punt the canoe the whole way, and go from one island to another, spending
three days in crossing. It seems, from the description I got from him, to be a
collection of shallow water, exactly like Lake Ngami, which is not deep either,
as I have seen men punting their canoes over it. It seems to be the rem-
nant of a large lake, which existed in this part, before the fissure was made to
allow the Zambesi to flow out. That part of the country is described by
many natives as being exceedingly marshy. The Makoloko went up to the
Shuia Lake and found all the country exceedingly marshy, and a large lake
seems to be actually in existence, or a large marsh with islands in it. But it
can scarcely be so extensive as has been represented, as in that case I must
have crossed part of it or heard more of it.

Account ya kwanza kuhus jina Tanganyika iliandiwaka na Captain Richard Francis Burton mwaka 1860 katika kitabu chake maarufu cha "Lake Regions of Central Africa" na hasa kwenye ukurasa wa 367, kama nilivyouambatanisha hapa.
attachment.php

View attachment 97874

Record zote hizo hizo za kihistoria nilizotaja hapo ninazo ila kama nilivyosema kwenye post yangu ya awali, naomba nipate muda wa kuzipanga vizuri, kwa vile siwezi kuzimabatanisha hapa kutokana na ukubwa wake.

asante mkuu
 
tafiti znaitajka kupata ukweli, naona wengi wanasemea tanga na kigoma.. Wakaazi wa maeneo haya mchango wao unaitajka.
 
Kupoteza record za historia ni sawa na kuwa utumwani. Due to Nyerereism. Alipoteza histioria yote ili tusijue tulikotoka, tulipo, tunakoenda na nini kifanyike. Kumbuka enzi za kulipia hadi radio ushuru wa kutumia kwa mwaka, hakuna TV, magazeti ni ya serikali, nguo ni za dhiki kuu, hakuna madawa, magari mazuri na ya gali ni peugeot 505, hakuna kununua range rover etc. Ali mradi ushenzi. Tushukuru sana Umoja wa Mataifa kwa kumtishia vikwazo hadi tulipompata Mwinyi na akabadilisha mfumo mzima. Ikiwa mtu mwenye ego kama ya Mwinyi angepokea kutoka kwa wakoloni tungekuwa sawa na Malaysia kwa sasa. Maisha bora kwa kila Mtanganyika.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom