Nini amekifanya Mbunge wako jimboni kwako toka 2010 hadi sasa?

Na wenzake wanajua ndio maana hata unaibu waziri hawakumpa tena japo ana elimu yake ya kumtosha..
Kuna haja ya kukutana na wazee wakimeru watushauri la kufanya



Hakuna la kufanya maana walitoa tahadhari kabla hata ya uchaguzi hawakusikilizwa!
Wanasubiri tu uchaguzi urudiwe wamchague waliyemtaka maana huyu ni siku tu zinahesabiwa!
 
mbunge wangu FILEMON NDESAMBURO a.k.a babu mbunge wa MOSHI MJINI (chadema)ameboresha hospitali karibu zote za manispaa, hakuna kulipa ada kwenye shule za kata ,mji unakua kwa kasi ya ajabu,mji msafi, KM WABUNGE WOTE WANGEKUA WANAJALI MAJIMBO YAO KM NDESAPESA TANZANIA INGEKUA KM MAREKANI
 
Jimboni kwetu kuna wa wabunge watatu wawili hawaendi Bungeni ni Joseph Tadayo wa Trust Mark atorney na Cleopa David Msuya hawaendi Bungeni lakini wanafanya kazi zilizomshinda Maghembe. Huyu anayekwenda Bungeni yeye ni Majungu, Ushirikina tu hamna kitu

tadayo na huyo Msuya wanaendekeza siasa za kidini.
 
Mbungu wangu Prof. Maghembe amefanikiwa kugawa laptop mbovu ktk baadhi ya shule za kata.
Hongera Mbunge wangu.
 
Zinakataza kuomba mwongozo juu ya mwongozo.


Zinakataza lakini naibu spika aliruhusu mbunge wa simanjiro Bw. Ole Sendeka akaomba mwongozo bunge liunde kamati ya kuchunguza swala la Jairo wakati akichangia kwenye mwongozo wa Zito uliotaka bunge lisitishe kujadili shughuli zote za Serikali maana walituhumiwa nayo na kumpa Jairo nafasi ya kwenda mahakamani kuwashtaki wabunge kupitia kwa Filemon Luhanjo. Sendeka akaungwa mkono na hoja ikapita huku ile ya Zito ikafa kifo cha kutatanisha!


.
 
Mi jimbo langu linaongozwa na Malkia Makinda, Ninachomwomba jimbo lake la njombe kusini ni jimbo lililojaliwa na vyanzo vingi vya maji ikizingatiwa jimbo lake limezungukwa na safu za milima ya kipengere yenye kila namna ya uzuri lakini wakazi wake wana uhaba mkali sana wa Maji safi na salama yani ni aibu, Naomba ajitahidi kuondoa aibu hii.
 
mmmmmm hivi mbunge wangu wa UKONGA yuko HAI huko aliko, katokomea baada ya matokeo ya uchaguzi,
swali kwetu huku UKONGA sio mbunge katufanyia nini bali, yuko wapi
baada ya hapo tutafuatilia hilo la kutufanyia nini?
au tulichagua mzimu umeyeyuka
 
Mbunge wangu ni VICTOR MWAMBALASWA- LUPA [CCM] CHUNYA-MBEYA

Kama kawaida ya wabunge wengi wa TZ,mbunge wetu alionekana wakati wa kampeni na wakati fulani alikuja akakusanya wadau wake ndani ya Ofisi ya Chama na kuwashkisha elfu5 kwa kila mmoja.....Lakini mpaka leo hatujui aliko na hatujui anafanya nini kwa yale tuliyomtuma.Huku barabara mbovu na tumesikia wakandarasi waliokuwa wanajenga wameondoka kwa sababu hawajalipwa hatuna umeme Shule zetu watoto wanakaa chini,shule za Sekondari za kata zimegeuka mashine za kupachikia mimba watoto wetu wa kike wengi wanatoka mbali wanalazimika kupangisha vijumba vizivyokuwa na usalama kwa sababu ya gharama,huduma mbovu za afya,wajawazito wengi wanakufa njiani kwa sababu ya barabara mbovu wanapokimbizwa hospitalini hakuna maji safi na salama akina mama wanateka maji mbali sana kwa taabu.Hii ni term ya pili ya huyu mheshimiwa na mpaka sasa hakuna alichofanya
 
mi mbunge wangu ni AESHI ALFAN hapa sumbawanga kafanikisha dr kafumu hadi kapita igunga
 
Mbunge wangu wa Arusha. Mh. Godbless Lema amefanikiwa kuanzisha mfuko wa elimu ambapo mwaka huu watoto zaidi ya 100 (mia moja) wanaotoka kwenye familia zisizokuwa na uwezo wanasomeshwa sekondari na mfuko huo. Ukarabati kwenye wodi za hosp ya mkoa unamalizika. Hatua za awali za ujenzi wa "mlimani city" maarufu kama "Machinga complex" hapa Arusha zimeanza.
Kimsingi anaendelea vzuri na naamini atatufikisha mbali kimaendeleo!
asante kwa taarifa njema mkuu
 
Amesimamia kvipi?..... yaani kama nyapara au?
Mbunge haleti barabara, wala haleti umeme .... ungeuliza hizo barabara na huo umeme umefadhiliwa na nani,hizo projects ziliandikwa na nani na fedha zimetoka wapi?
Hapo ndio utajua what it took to get those projects going.
Sio mbunge anayelete miradi ya kiuchumi. Hapa watanzania inabidi tupeane shule.

sawa! Lakn yeye ndiye anaye yasimami? Na hlo ndo linalo washnda wabunge wengi!! Halla to Zitto!
 
Mbona Tanzania hakuna wabunge ila wasaka tonge, walalaji bungeni, waomba miongozo juu ya miongozo, wajenga sky over za kufikirika, nk.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom