Ningekuwa Mh. Mbowe; Kipande cha Hotuba yangu ya Leo Kingekuwa Hivi……

Walimsimamisha Zitto Ubunge wakajua watammaliza na kukimaliza CHADEMA, leo tena wanarudia makosa yale yale. Wanamfungia LEMA wanadhani watammaliza yeye na Chama chake! Ni akili gani watu hawa wanazo? Ni kwa nini hawajifunzi kutokana na historia? Lakini tusiwalaumu ndio mwisho wao wa kufikiri ulipofika.
 
Naunga mkono hotuba ukombozi ni hatua,safari yake imeshaanza kwa mguu wa kulia
 
Tutakutafutia nafasi ya kuandika na kuedit hutuba ya Kamanda wetu safi sana

Umenisoma vema. Nina masaa mawili ya kujitolea kila wiki kwa ajili ya kushiriki harakati za ukombozi. Kama CDM watanihitaji, basi NDIYO ndo litakuwa jibu langu.
 
English Learner nimekusoma!
Lakini hotuba yako ina mapungufu ya kiufundi. Huwezi kutoa hotuba halafu ukasamehewa kwa kusahau ku-address lengo la mkusanyiko ule. Mkusanyiko huo unalenga kuwaambia Wana wa A-town jinsi CDM ilivyopokea maamuzi ya Mahakama Kuu Kanda ya Ars juu ya kesi ya ubunge wa Godbless Lema. Kwenye hotuba ni LAZIMA itajwe bila kutafuna maneno ikiwa chama kinaikubali hukumu au la. Then, lazima zitajwe hatua ambazo CDM inazichukua kufuatia maamuzi hayo. Na mwisho (si kwa ubora lakini) watoe wito kwa umma wa Wana A-town washikamane pamoja katika kuhakikisha kuwa mikakati moja,mbili, tatu..... inatekelezwa kwa nguvu yao. Na hiyo ndiyo tafsiri halisi ya Pipoooooooooooooz Pawa!!!!!!!!!!!!
 
Nimechukua pointi hapo, kama sehemu ya cdm iliyopo kila nukta ya ardhi ya nchi hii ujumbe utafika ,
thanx mkuu!
 
duh nime ipenda sana hii mkuu kama watakata rufaa itakuwa jambo zuri pia na kazi mpya ya mh. lema ita work out 100% japo kuna kitu kina nishinda kuelewa kama wale waliopinga ubunge kwa sababu walizozitoa sina imani kama ni raia wa kawaida wenye akili timamu, nina imanikubwa sana kuwa wale walitumwa na walikuwa na training kwa muda wote tangu uchaguzi kwaiyo baada ya kufaulu shule waliyo enda ndipo walipo kuja na hoja ya kupinga ubunge wa lema

=shule yao ilifadhiliwa na Magamba

=wakili wao na hakimu ndio walikuwa wana wafundisha kwa muda huo wote

sasa nadhani kuna haja ya CDM kuweka mawakili internation wa kesi kama hizi zakupikwa ili zikipakuliwa wale wao
kweli hii imekula kwao

nawakilisha
 
".....Mh. Lema, chama kitakupa jukumu jipya. Toka sasa Jimbo lako la Utumishi litakuwa Tanzania nzima. Kwa kadri Allah atakavyokuwezesha, utakwenda kila mkoa, kila wilaya, kijiji na kila tarafa. Ukaamshe, uanzishe, uimarishe na kukomaza fikra za ukombozi. Hii kampeni yako itaitwa "Operation Ukombozi"……………."
Jana katika Mkutano wa CDM Dodoma, Mh. mbowe kazidi kukazia kipande cha pendekezo langu juu ya hotuba kwa kusema:

"Ninajua mna hamu ya kusikia kuhusiana na mbunge wenu Lema, (wananchi wanaitikia ndiyo), tumempatia kazi maalum kwa kumpa helikopta, muziki mkubwa na matarumbeta," alisema.

"Anakwenda kuamsha ari ya mageuzi nchini, hakuna kulala hadi kieleweke. Wangejua ni balaa kwa hili walilolifanya wangemuacha bungeni," aliongeza Mbowe
 
Back
Top Bottom