Ningekuwa Katika Nafasi ya JK Ningeangalia Ivory Coast, Tunisia, Egypt…Moto Unawaka..

niweze

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
1,008
116
a. Ningekuwa Nimeona Jinsi Gani Wananchi Hawapendi Serikali ya CCM, Sera zake na Zaidi Rushwa na Ufisadi Mbaya Tuliouleta. Ningeona Mapinduzi Yana Karibia na Kujaribu Kuhepusha Janga Kubwa…
b. Ninge Mualika Dr Slaa, Chadema na Kuunda Serikali ya Muda…
c. Ningeshirikiana na Dr Slaa Kuandaa “Kamati ya Katiba” kwa Pamoja …
d. Ningeshirikiana na Dr Slaa Kuandaa “Uchaguzi wa Uraisi na Wabunge” kwa kutumia Tume Mpya ya Uchaguzi…
Lengo Kubwa ni Kuunda “Katiba Mpya na Nchi Mpya.” Kuondokana na Loop Holes Zote Zinazosababisha Wananchi Kuibiwa na Viongozi wa Chama Kimoja (CCM) Kufanya Ujangiri kwa Wananchi Wao. Taifa ni letu sote na Hakuna Mwananchi yeyote au Familia Yeyote ambayo haiumii kutokana na majanga tuliyaona kwa miaka 50. Umaskini umeendelea na Viongozi peke yao wananufaika kwa kuibia nchi yao kwa kusaini mikataba ya uongo kama Dowans. Elimu, Afya, Ajira na Uchumi Vyote vimekuwa vitu visivyo na Umuhimu tena kwa Viongozi (CCM)wa Taifa Letu. Chaguzi zote zimekuwa ni za kuiba kura na sio demokrasia ya kweli…Tunahitaji JK Usikie kama unasikia au usome jamii fórum au washahuri wako wapitie jamii kupata ushahuri…

tunisia-revolution-babes.jpg

protest-in-egypt.jpg

south-african-protest.jpg


"People Always Win"
 
Sikio la kufa hilo!!!!!!Ila ukweli siku za mafisadi kutawala zinahesabika popote pale, hili wimbi halitamponya JK na chama chake cha mifisadi.
 
Back
Top Bottom