Ninatamani kuolewa, lakini ninaishi na virusi vya ukimwi

King Katika watu niliokuwa nawaheshimu wewe ni mmoja wapo lakini leo nimekushusha thamani kabisa.

Una hakika kuwa wafanyakazi wa TACAIDS wapo HIV+ (Ninabisha na ninauthibitisho wa hilo ukitaka)

Sidhani kama unajua hata kazi wala majukumu yake. For your infomation TACAIDS hakuna mtu ambaye hajaoa wala kuolewa. Muwe mnazungumza vitu mlivyo na uhakika sio kuropoka hovyo hovyo tu.

Ushauri kwa mdada:

Wengi wamekwambia hapo juu nenda pima magonjwa yote moyo, sukari nk ili ujue uko katika hali gani ikiwamo kuangalia CD4 zako ziko kiasi gani kwa sasa usije kuchelewa ukakuta zimeshuka sana ukapata magonjwa nyemelezi kwa maelezo zaidi NI PM

Dena Samahani kama nimekukwaza kuhusu TACAIDS,sijakwambia wafanyakazi wote ni HIV+ me nawajua watu pale ni HIV+ na waeoana na mie nimekuja kujua baada ya mke kusema mwenyewe kisa m/me wake kazaa na m/ke mwingine(bi mdogo) sasa bi mdogo alivyokuja juu ndo bi mkubwa akampa makavu live kwamba anagombania nini? Mtu mwenyewe anayemgombania ni +,so ikabidi nikae nae chini yule bi mkubwa wa TACAIDS ndo akaniambia hadi jinsi walivyokutana kwamba kuna program kama mtu ni + unakutanishwa na + mwenzako(kama tu unaitaji),sio wote read btn the lines
Huu sasa ndio unaitwa uungwana!

Tukirudi kwenye mada:

Mbufya mpendwa,
Katika yote utakayoshauriwa huko kwenye PM kama ulivyosema, Utakapoamua kufikia kufanya maamuzi, ODM mie nakushauri:
1. Shirikisha moyo wako (usije penda pasipopendeka, ni ugonjwa mbaya zaidi)
2. Shirikisha madaktari/washauri nasaha (hawa ni marefarii wa afya yako)
3. Mshirikishe Mwenyezi Mungu (huyu ni muweza wa yote)

Baada ya kusema hayo, napiga magoti kukuombea mafanikio mema. Nami pia napatikana kwenye PM, naweza kukupa ushauri na uzoefu zaidi kama utahitaji.

Karibu.
 
unyanyapaa una aina nyingi sana.
Mnampa pole ya nini? Yeye amewaambia hali yake na shida yake.

Nyie polee poleee!!!
 
Dena Samahani kama nimekukwaza kuhusu TACAIDS,sijakwambia wafanyakazi wote ni HIV+ me nawajua watu pale ni HIV+ na waeoana na mie nimekuja kujua baada ya mke kusema mwenyewe kisa m/me wake kazaa na m/ke mwingine(bi mdogo) sasa bi mdogo alivyokuja juu ndo bi mkubwa akampa makavu live kwamba anagombania nini? Mtu mwenyewe anayemgombania ni +,so ikabidi nikae nae chini yule bi mkubwa wa TACAIDS ndo akaniambia hadi jinsi walivyokutana kwamba kuna program kama mtu ni + unakutanishwa na + mwenzako(kama tu unaitaji),sio wote read btn the lines

King unanichekesha sana eti unawajua kuwa ni HIV+ uliwapima?? for your information mimi nafanyakazi hapo na nikwambie kitu walio wengi hapo wamekuja na ndoa zao siku nyiiingi waliooa wakiwa TACAIDS ni wachache sana tena ni vijana. Hata mimi sijakwambia kuwa watu wote ni HIV+??? Na huyo unayesema amezaa na small hausi he he he sijawahi sikia maana mimi niko Admini ningekuwa na taarifa zote maana taarifa na kumbukumbu za wafanyakazi nazitunza mimi so ningekuwa na taarifa.

King kiukweli umenikwaza sana katika hili, eti watu wanatafuta wakuoa hivi kuna mtu hana mke/mume hapa TACAIDS?? Umenishangaza kweli aisee dah.

Hiyo bluu inahusika hapa niambie kama huo mpango wa kukutanisha watu upo hapo?

Zifuatazo ni kazi za TACAIDS: -
  1. Kutunga miongozo kwa ajili ya mwitikio wa mapambano dhidi ya janga la UKMIWI na usimamizi wa athari zake Tanzania Bara
  2. Kutayarisha mkakati kwa ajili ya mipango na shughuli za udhibiti wa VVU/UKIMWI kwa mujibu wa mkakati wa Taifa.
  3. Kukuza uhusiano wa kitaifa na kimataifa miongoni mwa wadau wote kupitia uratibu bora wa mipango na shughuli zote za kudhibiti UKIMWI kwa mujibu wa mkakati wa Taifa.
  4. Kutafuta, kugawa kulingana na mahitaji na kufuatilia matumizi yake.
  5. Kusambaza na kubadilishana taarifa kuhusu janga la VVU/UKIMWI na madhara yake nchini Tanzania ili tuweze kudhibiti janga hilo.
  6. Kuhimiza na kuimarisha utafiti, ubadilishanaji taarifa na nyaraka na utunzaji kumbukumbu kwa ajili ya kuzuia na kudhibiti VVU/UKIMWI.
  7. Kuimarisha program za uraghbishi na elimu kwa kiwango cha juu.
  8. Kufuatilia na kutathmini shughuli zote za VVU/UKIMWI
  9. Kuratibu shughuli zote za kudhibiti janga la UKIMWI nchini Tanzania kwa mujibu wa mkakati wa Taifa.
  10. Kuwezesha juhudi za kupatikana tiba na chanjo na kuimarisha upatikanaji wa huduma na matunzo.
  11. Kuilinda haki za jamii ya watu walioathiriwa na walioathirika na VVU/UKIMWI
  12. Kujenga mazingira wezeshi kwa wanaoishi na virusi vya UKIMWI waweze kukubali hali
  13. Kuishauri serikali kuhusu masuala yote ya udhibiti wa VVU/UKIMWI Tanzania bara.
  14. Kubainisha vikwazo vya utekelezaji wa afua za VVU/UKIMWI katika sera za kinga, mipango na kuhakikisha ufikiwaji wa malengo yaliyowekwa.
  15. Kuimarisha shughuli zote zinazohusu huduma za kinga na udhibiti wa janga la UKIMWI katika yafuatayo:
  • Huduma za afya na ushauri kwa watu wanao ugua UKIMWI
  • Ustawi wa wafiwa, yatima na wategemezi waliobaki.
  • Kushughulikia masuala ya kijamii, kiuchumi, kiutamaduni na kisheria yanayohusu janga la UKIMWI
Kutekeleza shughuli na majukumu mengine yeyote yanayohusu kinga na udhibiti wa UKIMWI katika Tanzania bara kama Tume itakavyoona inafaa.

King nadhani umenisoma ukitaka data zaidi tuwasiliane.
 
@ King

Soma hii summary ya Mkakati wa taifa wa kudhibiti ukimwi 2008 - 2012
Mkakati wa Pili wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI (2008 – 2012)
Mkakati wa Pili wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI (NMSF) unahusu kipindi cha kuanzia mwaka 2008 hadi 2012. Unaendeleza mafanikio na uwezo wa Mwitikio wa Taifa wa Mapambano dhidi ya UKIMWI katika kipindi cha miaka mitano kilichopita (kuanzia mwaka 2003 hadi 2007) na kupendekeza hatua za kuchukuliwa ikiwemo mikakati ya kukabili vikwazo na matatizo vilivyopita. NMSF huu unaelekeza mikabala, afua na shughuli vitakavyofanywa na watendaji wote nchini. Mkakati huu umetayarishwa baada ya mapitio makubwa na mchakato wa ushauriano chini ya maelekezo ya wataalamu wa Kitaifa na Kimataifa.

Mpaka sasa UKIMWI ni tishio kubwa la maendeleo ya Taifa na umetangazwa kuwa ni janga la Taifa. Athari yake inasababisha kuenea kwa mateso miongoni mwa watu binafsi, familia na jamii nchini kote. Hata hivyo kuna dalili za matumaini. Kulingana na taarifa na takwimu za hivi karibu ushamiri wa VVU hauendelei na hata kufikia kupungua kidogo katika sehemu nyingi za Tanzania. Juhudi za kinga na upatikanaji wa matibabu yanayofaa vimepunguza athari ya UKIMWI miongoni mwa watu walioambukizwa. Hata hivyo, bado kuna Watanzania zaidi ya milioni moja walioambukizwa VVU na maambukizo mapya yanatokea nchini kila siku. Ukubwa wa janga hili na jumla ya athari zake katika kipindi cha miaka ishirini iliyopita bado vinaleta changamoto kubwa nchini, changamoto ambazo zinaweza kukabiliwa kwa njia ya kuongeza juhudi shirikishi.

Mafanikio na changamoto
Miaka mitano iliyopita ya Mwitikio wa Taifa wa Mapambano Dhidi ya UKIMWI iliongozwa na Mkakati wa Kwanza wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI (2003-2007). Katika miaka hii, kumepatikana mafanikio makubwa yaliyochangia kuimarisha juhudi za Kitaifa.

Miongoni mwa mafanikio makubwa katika maeneo manne yaliyodhamiriwa ni haya yafuatayo:

Mazingira yanayowezesha (masuala mtambuko):

Wizara, Idara na Wakala na Mamlaka za Serikali za Mitaa zimeanzisha kiasi fulani cha afua kwa ajili ya waajiriwa wao na sekta zao; VVU na UKIMWI vimefungamanishwa katika Mpango wa Muda mrefu wa Kupunguza Umaskini (MKUKUTA); TACAIDS imeweza kuwa mratibu mkuu wa mwitikio wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI; Waratibu wa UKIMWI wameteuliwa katika Wizara, na Idara, Wakala na Mamlaka za Serikali za Mitaa zote na Kamati za Kudhibiti UKIMWI ziliundwa; Kamati Shirikishi za Kudhibiti UKIMWI zilianzishwa katika Wilaya zote na katika baadhi ya Kata na Vijiji na mafunzo yalitolewa kwa wanakamati; Wakala za Uwezeshaji za Mkoa zilianzishwa katika Mikoa yote na zimetoa msaada mkubwa kwa Wilaya na Jamii;

Cheo cha Naibu Waziri wa Maafa na VVU na UKIMWI kilianzishwa katika Ofisi ya Waziri Mkuu; Umoja wa Wabunge wa Mapambano dhidi ya UKIMWI Tanzania ulianzishwa; Vyama vya Kiraia vingi vimekuwa vikijishughulisha na VVU na hivyo kutoa uelewa wa kutosha nchini vikiwemo vikundi vingi zaidi vya WAVIU; Fedha kwa ajili ya shughuli za VVU na UKIMWI ziliongezwa zaidi kutoka Serikali na Wahisani na fedha nyingi zaidi zilifikia jamii; Kulikuwa na upanuzi zaidi wa mfumo wa kufuatilia maambukizo ya VVU; Utafiti wa mara kwa mara ulifanyika kuhusu VVU na mwenendo (ukiwemo VVU na UKIMWI katika Utafiti wa Hali ya Afya ya Watanzania)na Utafiti wa Kiashirio cha VVU Tanzania; Kulikuwa na uunganishaji wa utoaji taarifa kuhusu VVU na UKIMWI katika mfumo wa afya; na Kulikuwa na uendelezaji na uanzishwaji wa mfumo wa ufuatiliaji kwa ajili ya shughuli zisizokuwa za afya (TOMSHA).

Kinga:
Matibabu ya maambukizo kwa ngono yaliongezeka katika hospitali na vituo vya afya vyote na asilimia 60 ya zahanati; Kumekuwa na ongezeko kubwa la upatikanaji wa kondomu za wanaume nchini (kutoka milioni 50 hadi milioni 150); Vituo vya Unasihi na Upimaji wa Hiari vimeongezeka zaidi ya mara tatu; Uzuiaji wa Uambukizo wa VVU kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto umeongezeka hadi kwenye asilimia 12 ya hospitali na vituo vya afya; Kutokana na utafiti mbalimbali, kulikuwa na uthibitisho kwamba vijana wameanza kubadili mienendo yao ya ngono (ongezeko la kuchelewesha shughuli za ngono, wapenzi wachache wa ngono n.k.) na programu za uendelezaji wa afya shuleni zilipanuliwa, na; Sekta binafsi na zisizo rasmi zimejihusisha zaidi na mapambano dhidi ya UKIMWI kwa kutoa programu za kinga na matunzo kwa waajiriwa na jamii kwa ujumla.

Matunzo na Matibabu:
Mpango maalumu wa Tiba ya Kuongeza Kinga ya Mwili umetekelezwa na zaidi ya WAVIU 70,000 wamepewa matibabu hadi mwisho wa 2006, na Miradi ya matunzo nyumbani imepanuliwa hasa na vyama vya kiraia.

Upunguzaji Athari:
Misaada iliongezeka kwa mayatima, watoto wanaoishi katika mazingira magumu na vikundi vingine vinavyoishi katika mazingira magumu; na Kulikuwa na uhusishaji wa WAVIU katika Mwitikio wa Taifa hasa Uraghibishi na upunguzaji wa unyanyapaa na ubaguzi.

Hata hivyo, katika mwitikio wa jumla, bado kuna changamoto nyingi zinazohitaji kushughulikiwa kwa miaka ijayo. Miongoni mwa changamoto hizo ni: Upungufu wa utashi wa kisiasa katika ngazi ya kati na ya chini pamoja na uwajibikaji wa mwitikio wa VVU;

Programu chache na hafifu za VVU katika Wizara, Idara, Wakala na Mamlaka ya Serikali za Mitaa hasa katika ngazi za mikoa, wilaya na kufikia jamii; Chombo cha uratibu cha Kitaifa chenye majukumu mengi (TACAIDS); Kutotambuliwa na kutotumika kwa kanuni ya “Dhana Tatu” katika ngazi ya Serikali kuu na Wilaya. Uhusishaji mdogo wa vyama vya Kiraia na WAVIU hasa katika mipango na utekelezaji wa mwitikio wa VVU kwenye ngazi ya Wilaya na jamii; Ucheleweshaji wa mara kwa mara na matatizo katika kutoa fedha kwa wakati kwa Wilaya na Jamii; Uwezo mdogo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa wa kuandaa na kutekeleza mipango kabambe ya VVU na UKIMWI; Unyanyapaa na ubaguzi bado ni vya kiwango cha juu katika jamii; Juhudi za kinga hazikushughulikia kiasi cha kutosha masuala ya afya ya ujinsia na uzazi na mara nyingi hazikutekelezwa; Bado kumekuwa na matatizo ya matumizi sahihi na ya mara kwa mara ya kondomu na upatikanaji mdogo katika jamii nyingi za vijijini; Uenezaji mdogo wa juhudi za kinga katika maeneo ya vijijini, na; Upatikanaji wa Tiba ya kuongeza Kinga ya Mwili ulikuwa katika vituo vya mijini tu.
 
King unanichekesha sana eti unawajua kuwa ni HIV+ uliwapima?? for your information mimi nafanyakazi hapo na nikwambie kitu walio wengi hapo wamekuja na ndoa zao siku nyiiingi waliooa wakiwa TACAIDS ni wachache sana tena ni vijana. Hata mimi sijakwambia kuwa watu wote ni HIV+??? Na huyo unayesema amezaa na small hausi he he he sijawahi sikia maana mimi niko Admini ningekuwa na taarifa zote maana taarifa na kumbukumbu za wafanyakazi nazitunza mimi so ningekuwa na taarifa.

King kiukweli umenikwaza sana katika hili, eti watu wanatafuta wakuoa hivi kuna mtu hana mke/mume hapa TACAIDS?? Umenishangaza kweli aisee dah.

Hiyo bluu inahusika hapa niambie kama huo mpango wa kukutanisha watu upo hapo?

Zifuatazo ni kazi za TACAIDS: -
  1. Kutunga miongozo kwa ajili ya mwitikio wa mapambano dhidi ya janga la UKMIWI na usimamizi wa athari zake Tanzania Bara
  2. Kutayarisha mkakati kwa ajili ya mipango na shughuli za udhibiti wa VVU/UKIMWI kwa mujibu wa mkakati wa Taifa.
  3. Kukuza uhusiano wa kitaifa na kimataifa miongoni mwa wadau wote kupitia uratibu bora wa mipango na shughuli zote za kudhibiti UKIMWI kwa mujibu wa mkakati wa Taifa.
  4. Kutafuta, kugawa kulingana na mahitaji na kufuatilia matumizi yake.
  5. Kusambaza na kubadilishana taarifa kuhusu janga la VVU/UKIMWI na madhara yake nchini Tanzania ili tuweze kudhibiti janga hilo.
  6. Kuhimiza na kuimarisha utafiti, ubadilishanaji taarifa na nyaraka na utunzaji kumbukumbu kwa ajili ya kuzuia na kudhibiti VVU/UKIMWI.
  7. Kuimarisha program za uraghbishi na elimu kwa kiwango cha juu.
  8. Kufuatilia na kutathmini shughuli zote za VVU/UKIMWI
  9. Kuratibu shughuli zote za kudhibiti janga la UKIMWI nchini Tanzania kwa mujibu wa mkakati wa Taifa.
  10. Kuwezesha juhudi za kupatikana tiba na chanjo na kuimarisha upatikanaji wa huduma na matunzo.
  11. Kuilinda haki za jamii ya watu walioathiriwa na walioathirika na VVU/UKIMWI
  12. Kujenga mazingira wezeshi kwa wanaoishi na virusi vya UKIMWI waweze kukubali hali
  13. Kuishauri serikali kuhusu masuala yote ya udhibiti wa VVU/UKIMWI Tanzania bara.
  14. Kubainisha vikwazo vya utekelezaji wa afua za VVU/UKIMWI katika sera za kinga, mipango na kuhakikisha ufikiwaji wa malengo yaliyowekwa.
  15. Kuimarisha shughuli zote zinazohusu huduma za kinga na udhibiti wa janga la UKIMWI katika yafuatayo:
  • Huduma za afya na ushauri kwa watu wanao ugua UKIMWI
  • Ustawi wa wafiwa, yatima na wategemezi waliobaki.
  • Kushughulikia masuala ya kijamii, kiuchumi, kiutamaduni na kisheria yanayohusu janga la UKIMWI
Kutekeleza shughuli na majukumu mengine yeyote yanayohusu kinga na udhibiti wa UKIMWI katika Tanzania bara kama Tume itakavyoona inafaa.

King nadhani umenisoma ukitaka data zaidi tuwasiliane.

hizo siasa zenu huku huko.....mipango kibaaao mmekalia politics na facebook kama sio jf hamna kazi ya maana inayofanyika..samahni kama nimekuudhi maana nawe pia umeudhi!!sio muda wa kubishana na kutajiana kazi zenu mara elfu mngekua na icho kitengo cha kuwakutanisha watu walioathirika wakapata wenza wao kuiliko kuja hapa na kujisafisha eti hakuna hat ammoja...kw aiyo mnaona sifa kuwa nawafanyakazi amabo hawajaaathirika ilihali mnafanya kazi ya ukimwi?nyie ndo wale mnapiga chini wafanyakazi mkigundua wameathirika soon b4 employment...tena nna waswasi na uwezo wako kama vp ifute msg yako...mnajiona magreat thinker kumbe uharo tu!!

toa msaada husika sio kulumbana hapa..kwani TACAIDS kazi yake nini...ten ando mlipaswa ofisi nzima wawe WAATHIRIKA mtoe elimu nzuri zaidi............what the hell is TACAIDS..nimechuki asana
 
Inawezekana kuolewa ukazaa na mtoto asipate maambukizi, nina mifano ya PLHIV ambaye ameolewa mtu ambaye ni negative, wamezaa bila kuambukizana. unaweza kuni pm maelezo zaidi
 
utaolewa tu usiwe na wasiwasi,
endelea kujitunza na kumwomba MUNGU yote
yanawezekana.
 
Pole sana mpendwa.....

Nakushauri tembelea vituo vya ushauri nasaha kuna watu wengi wanaoishi kwa matumaini wanatafuta wenzi wa kuishi nao. Kuwa na VVU siyo mwisho wa maisha. Usikate tamaa, kaza moyo... Kama vipi nenda pale PASADA uonane na washauri nasaha... kuna dada yangu mmoja alijipatia mchumba pale, wameoana na wana mtoto ambaye hajaathirika.

Mungu aliye mbinguni akubariki na kukuongoza.

Nampongeza kwa kujua afya yake katika umri mdogo alionao, wengine wanaishi na ma ukimwi hawajitambui, kwangu mimi namuona shujaa wala asikate tamaa, kufa kupo, kwani wanaokufa wote ni waathirika? Ata maralai au inaua
 
mkimwomba mungu kwa imani mnauwezo wa hata kuhamisha milima,kwa dada yangu muombe mungu atakusaidia au hata kuondoa kabsa huo ugonjwa
 
La kuolewa Ni majaaliwa kwani wapi hata wazima hawana maambukizi na hawajaolewa ila kwako ikifika wakati utaolewa tu ila nnachojua Ni kwamba utazaa na mtoto atakuwa mzima Kama utahudhuria clinic mapema kuna mambo ya kufanya utashauriwa na Kuna DAWA utapewa ya kumzuia mtoto na mtoto atapewa DAWA baada ya kuzaliwa
 
utaolewa tu usiwe na wasiwasi,
endelea kujitunza na kumwomba MUNGU yote
yanawezekana.
Teh teh huyu ni mwanaume anawazingua tu hapa.nimeshindwa kuweka thread yake ipo humu analalamika mkewe hataki kumpa unyumba.teh teh teh watu mmemiminika kwa huzuni sana.
 
Teh teh huyu ni mwanaume anawazingua tu hapa.nimeshindwa kuweka thread yake ipo humu analalamika mkewe hataki kumpa unyumba.teh teh teh watu mmemiminika kwa huzuni sana.

Kweli bwana huyu jamaa ni mwanaume tena kwenye MAPENZI NA MAHUSIANO ana thread iliyo andikwa MKEWANGU HATAKI NIMGUSE!! USHAURI. huyu jamaa vipi anatuzingua bure.
 
Back
Top Bottom