Ninatamani kuolewa, lakini ninaishi na virusi vya ukimwi

MBUFYA

JF-Expert Member
Aug 15, 2011
445
68
Wakuu, mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 25, kwa sasa ninavirusi vya ukimwi, ninatamani sana kuolewa na kuzaa watoto, nifanye nini? je ntapata mwanaume wa kunioa? na tukitaka kuzaa salama tutafanyaje?
naombeni msaada wenu wana jamvi.
 
Tafuta mwenzio mwenye hali hiyo. Si rahisi kwa anayejijua hajaambikizwa kukubali kukuoa labda umfiche.
 
kuolewa inawezekana dada, na kupata watoto pia. Yupo rafiki yangu mmoja naye anaishi na virusi vya ukimwi kaolewa na sasa ana watoto wawili mapacha na maisha yanasonga vizuri tu huwez jua. La msingi tembelea wataalam watakushauri dada.
 
pole sana rafiki
kwanza elewa kuishi na HIV sio mwisho wa maisha kubali kabisa ilo moyoni
kuhusu kuolewa utaolewa tu muombe mungu kila kitu humu duniani mungu ana mipango nacho.

wewe kama binadamu yeyote huna mapungufu yoyote nas utaishi na kutimiza ndoto zako zote hapa duniani kama kusudi la mungu lilivo
so amini utaolewa,na utazaa watoto wakati wa bwana ukifika
amen
 
Pole sana mpendwa.....

Nakushauri tembelea vituo vya ushauri nasaha kuna watu wengi wanaoishi kwa matumaini wanatafuta wenzi wa kuishi nao. Kuwa na VVU siyo mwisho wa maisha. Usikate tamaa, kaza moyo... Kama vipi nenda pale PASADA uonane na washauri nasaha... kuna dada yangu mmoja alijipatia mchumba pale, wameoana na wana mtoto ambaye hajaathirika.

Mungu aliye mbinguni akubariki na kukuongoza.
 
pamoja na ushauri woote utakaopewa humu vi vyema kabla hujayatolea maamuzi uende kwa wataalamu wa mambo ya ushauri nasaha yanayohusiana na HIV watakupa mwanga zaidi juu ya jambo hili...ingawa binafsi yangu nahisi linawezekana.....
pole sana..
 
Pole sana mpendwa. Fuata ushauri uliopewa hapa unaweza kukusaidia kufanikisha ulitakalo. Ukae kwa amani na kila la heri katika kutafuta utakacho.
 
njooo igekemaja au welamasonga kuna watu wenye hali kama ya kwako hivo itakuwa rahisi kupata wa kukuowa....!!
 
kwanza dada hongera sana kwa kuwa mtu ambaye unajielewa na unaamini kwa kilichopo , kwanza nakushauri nenda hosp ukapate ushauri kwani ni jambo linawezekana, kapate ushauri jinsi ya kujikinga na maambukizi kwa mtoto na jinsi ya kuweza kupata mtoto asipate maambukizi
 
Pole sana mpendwa.....

Nakushauri tembelea vituo vya ushauri nasaha kuna watu wengi wanaoishi kwa matumaini wanatafuta wenzi wa kuishi nao. Kuwa na VVU siyo mwisho wa maisha. Usikate tamaa, kaza moyo... Kama vipi nenda pale PASADA uonane na washauri nasaha... kuna dada yangu mmoja alijipatia mchumba pale, wameoana na wana mtoto ambaye hajaathirika.

Mungu aliye mbinguni akubariki na kukuongoza.

Touchy, sina la kuongeza!
 
Mdogo wangu haupo peke yako watu wengi sana wameathirika.Na wengi hawajijui Hongera wewe unaejitambua.
Inawezekana sana tena kwa asilimia 100% wewe kuolewa na mwanaume utakae pendana nae.Na kupata watoto.Tena kwa umri wako jihesabie Miaka 15 ya kuishi bila ARV.
Hivyo Vyama ni uzushii Mtupu achana nao Wengi wao wapo kimaslahi yao zaidi.Ww jiangalie wewe kama wewe nenda Hospital angalia afya yako yote kwa ujumla.

Kumbuka wagonjwa wazamani hawakuwa na ARvs wala kinga dhidi ya mtoto alie tumboni lakini siku hizi vitu hivyo vipo.Usikate tamaa.Na imani baada ya miaka kadhaa TIBA itapatikana.Matokea yanaonesha hivyo.Kikubwa Jitunze.

Nitumie Private mail.nikuelekezee zaidi na kukupatia msaada zaidi
 
we we mletata mada mbona umekula kona au ndio unasoma ushauri we nenda maeneo waliokushauri utapata tu mtu mwenye wazo kama lako amini nakuambia hilo bibie enjoy and feel your expressional
 
Wengi wanampa pole sijajua wanampa pole kwa ajili gani? Kwani amesema anaumwa? Dada usiwe na wasiwasi kuhusu kuolewa na kupata mtoto,vyote hivyo vinawezekana kwa 100% pale TACAIDS wapo watu ambao ni HIV+ wanatafuta wa kuwaoa cha msingi nenda pale utapata mtu.
 
Seconded 100%
 
Ndhani walio kujibu hapo mwanzo wamesha sema mengi, ningependa tu kukupa a positive link, inakuonesha hatua za kuchukua kama unataka kupata mtoto: gonga hapa
kwa kifupi wanakushahuri:
  1. Kufikiria kuhusu afya yako. fanya vipimo vyote vya HIV, na vya magonjwa mengine. kama una diabetis, deal with it. kama una tatizo la moyo au BP, deal with it. hakikisha afya yako is as good as possible before you conceive.
  2. Ongea na Daktari wako, akwambie njia zote za kuziwia tumwambukiza mtoto, na kama utachagua treatment ianze mapema.
  3. Wakati wa mimba doze your CD4 very often. usiwe na wasi wasi kama zinaenda chini, ni kawaida sana wakati wa mimba. you just need to monitor it.
  4. Mtoto akisha zaliwa atapewa AZT kwa miezi 6, na baada ya miezi 18 atapimwa. only that test can determine a negative HIV status.
Sababu it is a very hard situation to live, ningeshahuri utafute mume HIV affeted (One living with HIV or one who has been exposed to an HIV positive person in his life) sababu an HIV negative anaweza kuona it is a too dangerous and demanding experience...
Kila la heri mpendwa.
 
Wengi wanampa pole sijajua wanampa pole kwa ajili gani? Kwani amesema anaumwa? Dada usiwe na wasiwasi kuhusu kuolewa na kupata mtoto,vyote hivyo vinawezekana kwa 100% pale TACAIDS wapo watu ambao ni HIV+ wanatafuta wa kuwaoa cha msingi nenda pale utapata mtu.

King Katika watu niliokuwa nawaheshimu wewe ni mmoja wapo lakini leo nimekushusha thamani kabisa.

Una hakika kuwa wafanyakazi wa TACAIDS wapo HIV+ (Ninabisha na ninauthibitisho wa hilo ukitaka)

Sidhani kama unajua hata kazi wala majukumu yake. For your infomation TACAIDS hakuna mtu ambaye hajaoa wala kuolewa. Muwe mnazungumza vitu mlivyo na uhakika sio kuropoka hovyo hovyo tu.

Ushauri kwa mdada:

Wengi wamekwambia hapo juu nenda pima magonjwa yote moyo, sukari nk ili ujue uko katika hali gani ikiwamo kuangalia CD4 zako ziko kiasi gani kwa sasa usije kuchelewa ukakuta zimeshuka sana ukapata magonjwa nyemelezi kwa maelezo zaidi NI PM
 
Dena Samahani kama nimekukwaza kuhusu TACAIDS,sijakwambia wafanyakazi wote ni HIV+ me nawajua watu pale ni HIV+ na waeoana na mie nimekuja kujua baada ya mke kusema mwenyewe kisa m/me wake kazaa na m/ke mwingine(bi mdogo) sasa bi mdogo alivyokuja juu ndo bi mkubwa akampa makavu live kwamba anagombania nini? Mtu mwenyewe anayemgombania ni +,so ikabidi nikae nae chini yule bi mkubwa wa TACAIDS ndo akaniambia hadi jinsi walivyokutana kwamba kuna program kama mtu ni + unakutanishwa na + mwenzako(kama tu unaitaji),sio wote read btn the lines
 
we we mletata mada mbona umekula kona au ndio unasoma ushauri we nenda maeneo waliokushauri utapata tu mtu mwenye wazo kama lako amini nakuambia hilo bibie enjoy and feel your expressional

sijala kona mkuu, nimefurahi sana kwa ushauri wenu na wengine wame ni pm. ntawasiliana nao.
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom