Ninatafuta kazi, nisaidie.

Oct 27, 2012
62
18
Habarini Wakuu,
Mimi ni kijana, 23, ninayetaraji kuhitimu elimu yangu ya chuo kikuu ngazi ya Shahada hivi karibuni (BA English). Lakini Nina walakini kidogo kiasi cha kuhitaji msaada wenu.

Masomo yangu yanafadhiliwa na HESLB kwa asilimia zote (100%), lakini nimekuwa mmoja wa wahanga wasiolipiwa ada ya mwaka mzima kwa mwaka wa masomo 2012/2013.

Ufuatiliaji haujazaa matunda yoyote hadi sasa na taarifa iliyopo ni kwamba transcript haitatolewa kwa ambaye ana deni ama la bodi au binafsi. Kwa maana ya kwamba ninatakiwa kuilipa mimi binafsi.

Sina pesa wala chanzo chake kwa sasa. Ninamaliza mwezi July nikiwa kama Form VI leaver tu, kwa minajiri hiyo.

Akili yangu kwa sasa in kutafuta hata tempo au contract work japo kwa mwaka au miwili niweze kujilipia chuoni. Sasa ninaomba sana msaada wa connection kuanzia sasa.

Ninaweza kufanya Writing, editing and proofreading, Translation, Interpretation (English to Kiswahili), Photography, TV Production na Graphic Design (vyote nimesomea darasani).

Msaada wenu tafadhali

Ni PM, tutaongea. Utakuwa umenisaidia sana.

Email: manpeters@ymail.com
 
Hakika, ninatafuta kwa bidii zote wakuu. Isije kuwa nimepoteza miaka yangu mitatu kwa bure.
 
Back
Top Bottom