Ninapomwona dada yangu na mwanaume moyo unaanza kuuma.

Viol

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
25,426
18,228
Habari zenu humu Jamvini.

Mbona mi nikimwona dada yangu au mdogo wangu wa kike na mwanaume/boyfriend wake moyo unauma?yaani nahisi kama atakuja kutendwa au kuharibiwa malengo yake,halafu mi nikifukuzia dada za watu naona iki poa tu,hivi na nye mnaumia mnapoona dada zenu au wadogo zenu wa kike na boyfriend zao?
Halafu nye wadada mkiwaona kaka zenu na girlfriends zao mnawaonea huruma kuhofia watakuja kutendwa?
 
hahahaha.... Unawafanyaga nini watoto wa wenzio hadi unakua na woga hivo? lol
 
Habari zenu humu Jamvini.

Mbona mi nikimwona dada yangu au mdogo wangu wa kike na mwanaume/boyfriend wake moyo unauma?yaani nahisi kama atakuja kutendwa au kuharibiwa malengo yake,halafu mi nikifukuzia dada za watu naona iki poa tu,hivi na nye mnaumia mnapoona dada zenu au wadogo zenu wa kike na boyfriend zao?
Halafu nye wadada mkiwaona kaka zenu na girlfriends zao mnawaonea huruma kuhofia watakuja kutendwa?
heri mnasema wenyewe mi nikisema
smile naonekana mbaya
heri mnaconfess wenyewe
wanaume ndo zenu hizo kumbe mnajua
 
heri mnasema wenyewe mi nikisema
smile naonekana mbaya
heri mnaconfess wenyewe
wanaume ndo zenu hizo kumbe mnajua

hapo labda akikutana na mtu ambaye is not matured,halafu hajielewi,but kama anajielewa nadhani hakuna baya litatokea
 
mie niliwahi kumdunda jamaa kisa anatoka na mdogo wangu..mbaya zaidi..jamaa akachukua jumla na mm nikapokea posa na kumkabidhi...na kutoa ujumbe kwenye harusi....dah...
 
Mdogo/mtoto wa kike anauma sana, ila wa kiume unamuona jembe tu acha lilime.
 
mie niliwahi kumdunda jamaa kisa anatoka na mdogo wangu..mbaya zaidi..jamaa akachukua jumla na mm nikapokea posa na kumkabidhi...na kutoa ujumbe kwenye harusi....dah...

teh teh afadhali huyo alikuwa na nia kabisa,wengine wa msimu,wanapita tu,hapo ndo inauma
 
Mimi huwa moyo hauumi ila huwa nawaonea huruma tu, mapenzi siku hizi ni kutumiana kwenda mbele, kama sister ataona poa kutumiwa sijali sana ni maisha yake, mimi zangu ni SODA YA KOPO, nikimaliza kunywa natupa.
 
Hahaha hahahha hahhaha,
Wanaume bana dah!
Dada zenu roho inauma ila kwa dada za wenzenu mnaona poa tu,
Vumilien tu kwani mnachofanya kwa dada za wenzenu ndio hicho hicho dada zenu wanafanyiwa atii!

Kwa kaka yangu nitaumia km akiangukia mwanamke atakayekua anamnyanyasa na kumpelekesha kaka yetu!
 
Kwa maneno ya mwanafalsafa mashuhuri J.M.Kikwete(Ph~D) ''Usipokuwa tayari kuliwa kidogo huli,sasa wewe unataka kula tu bila kuliwa haiwezekani"
 
Ila si utampata kaushari?ili akipuuza asikulaumu
 
Hahaha hahahha hahhaha,
Wanaume bana dah!
Dada zenu roho inauma ila kwa dada za wenzenu mnaona poa tu,
Vumilien tu kwani mnachofanya kwa dada za wenzenu ndio hicho hicho dada zenu wanafanyiwa atii!

Kwa kaka yangu nitaumia km akiangukia mwanamke atakayekua anamnyanyasa na kumpelekesha kaka yetu!
teh teh we acha tu,tunapenda tuwafanyie wengine ila tukifanyiwa sisi inauma
 
Kwa maneno ya mwanafalsafa mashuhuri J.M.Kikwete(Ph~D) ''Usipokuwa tayari kuliwa kidogo huli,sasa wewe unataka kula tu bila kuliwa haiwezekani"

mkuu nadhani hiyo falsafa haitafanya kazi kama huna dada
 
Back
Top Bottom