Syllogist,Halitafakariki hili...
Pamoja na kua inauma hili halina nafasi yake kwenye siasa za Tanzania
Kwa wale wanaotaka kuamini na kudekeza hayo yaliyoandikwa, atabakia kama alivyo!
Kwa wale watakao kubaliana na mimi kuwa huyo mwandishi mwenyewe alihitimisha kuwa 'hao waafrika' hawata soma hilo, linatubakisha kwenye kundi tofauti kabisa ...kwani tumesoma na tunaweza kuchambua pumba zake elekevu kwa walengwa wasiolengeka!
Hivyo kama umesoma, hautabakia kwenye kundi hilo analodai mwandishi.
Kusudi kubwa, la mwandishi huyo, kwa maoni yangu ni la kichochezi kutaka kutafuta mdahalo, ambao upo na unajadiliwa kila kukicha na wadau. Hivyo kumbakisha kwenye kusudi lisilo na mwelekeo maalum!
Hakuna jipya analolisema pamoja na madai lukuki aliyoambatanisha.
Mie huwa "Ninapojiuliza kuhusu Waafrika...." Nafurahi sana! Kwani Afrika ndio mama wa fikra zangu.
Ahsante
Mi nakubaliana na wewe kabisa. Napinga dhana kwamba sisi waafrika/watu weusi tuko duni kiakili tukilinganishwa na watu weupe. Hakuna uhusiano wowote wa lazima kati ya weupe/weusi na umakini/uduni. Nashangaa kuona baadhi wameongea kwa conviction kabisa kwamba mtu mweusi ni duni mbele ya weupe. Ajabu!
Kusema mtu mweusi ni duni maana yake ni ku-affirm kwamba si mtu kamili, ni mtu nusu kwani mtu kamili ni yule mwenye akili na utashi. Aliye na uwezo wa kutumia faculties zake kuyatawala mazingira yake na kuubadili ulimwengu. Siamini kwamba sisi waafrika ni watu nusu, na kwamba wazungu ni watu kamili. Kushikilia mawazo haya ni kujidhalilisha na kuogopa kuukabili ulimwengu.
Mwafrika ni mwerevu kama watu wa race nyingine. Mwandishi anaposema kwamba watu weusi ni WAJINGA, WALAFI (greed) na WABINAFSI kwa hakika hajaongea cha PEKEE kinachomtofautisha mwafrika na watu weupe. Kama ni ujinga, hakuna anayezaliwa na maarifa. Wote tunazaliwa tukiwa tabularasa. Tunaanza kupata maarifa kwa milango 5 ya fahamu.
Mwandishi anasema waafrika hawasomi vitabu. Ajue kwamba kusoma vitabu ni njia mojawapo ya kujipatia maarifa. lakini ziko njia nyingi tu kama za informal education, "kusoma" kwa kutazama na kuelewa mambo, kwa kusikiliza, nk. Pengine hatujatumia sana njia kusoma vitabu. Lakini hii ni kwa sababu ya mazingira yanayowanyima wengi nafasi ya kusoma vitabu. Kumbe mwandishi anaposema tu wajinga na si wapumbavu sioni kama ni kitu kibaya sana kwa sababu mjinga anafundishika (he has the potentials to be knowledgeable). Mpumbavu ni yule asiyefundishika kwa sababu hana uwezo wa kupokea maarifa. Si tuna uwezo wa kupokea maarifa.
Mwandishi anasema weusi ni watu WABINAFSI. Wote (all races) tunazaliwa na ubinafsi (umimi . . . wenye lengo la kujilinda for survival). Lakini jinsi tunavyokua na malezi tunayoyapata tunaanza kuushinda ubinafsi na kutoa nafasi kwa watu wengine. Tunajifunza kujinyima kidogo kwa ajili ya wengine.
Hakika ubinafsi si wa mwafrika tu. Mzungu ni mbinafsi zaidi kuliko mtu mweusi na ndiyo maana amejenga taratibu za kibinafsi katika kufaidi mali ya dunia hii. Fikiria juu ya ubepari, ukolonimamboleo, utandawazi, nk. Kama waafrika wanakuwa wabinafsi ni kwa sababu WAMEIGA na WANAENDELEA KUIGA mifumo ya kimagharibi ya watu weupe. Kwa sababu kutokana na malezi yetu ya tangu zamani waafrika tumefundishwa kuwa wakarimu, kuwa WAJAMAA. Na ndio maana Tanzania tulijaribu kuujenga ujamaa, kitu ambacho hakikuwa kipya kabisa kwa waafrika. Ulishindwa kwa sababu ya athari za kimagharibi na hasa MAWAKILI watanzania wa mfumo wa kimagharibi wakishirikiana na watu wa magharibi.
Mwandishi amezungumzia greed (labda Ulafi - kisw.). Wazungu ndo walafi wa walafi. Waafrika tunajua starehe na anasa kuwazidi wao? Siamini kabisa.
KUMBE kusema waafrika tu WAJINGA, WALAFI NA WABINAFSI kana kwamba ni SIFA za PEKEE kwa waafrika tu SI KWELI. Ndiyo nakubali wapo baadhi ya waafrika/watu weusi wenye kasoro hizi kama walivyo baadhi ya weupe wenye kasoro hizo pia. Lakini kusema waafrika wote ndivyo walivyo ni ku-generalise mno na kukosa breki katika conclusions. Mbaya zaidi ni kule kusema kwamba kasoro hizi ni inborn yaani tumezaliwa nazo kama race (weupe hawana), ni sehemu ya hulka yetu ndani ya damu, mifupa, genes na cells. Hii si kweli!! Kusema hivo ni kukataa dynamism of the human being. Mwafrika ni mtu anayebadilika kama watu wa race nyingine, anaelekea kuzuri. Kama kuna kasoro ni za kimazingira, ambazo hata kwa hao wazungu zimekuwepo kwani si weupe wote wameendelea kwa wakati mmoja na kwa namna moja. Hata wao wamepishana. Sasa utasema kwamba hao walio nyuma wamezaliwa na kasoro kutoka matumbo ya mama zao? Nawasilisha.