Ninaomba wana jf tuijadili picha hii.

Haya ndo nilikuwa ninayasema hapo utakuta wanafanya shughuli zao ubalozini hizi CCM nje ya nchi zinaendesha balozi sasa
 
Watu huwa wanakosa vya kufanya huko Urusi. Ila nadhani hawa pia wanachosema na kufanya ni opposite , kwa hiyo picha ya raisi wao 'waliyoichakachua' hapo ukutani inaonyesha kweli hawamtambui ila wanajifanya kusema kinyume chake.
 
Hao ni wakereketwa au ni baadhi ya hao hao mafisadi waishio hapo? Alichokisema Capt Jaka kina mashiko zaidi kwani wajue kuwa wanapaswa kuwatumikia wananchi na si wananchi wawatumikie wao....
Hata hivyo inatia kichefuchefu kwa maneno yake haya ...''Mwenyekiti wa Tawi la CCM Urusi Dk. Alifred Kamuzora katika hotuba yake alihoji kuwa katika uchaguzi wa hivi karibuni, ambapo wapinzani wanadai matokeo yalichakachuliwa, isije kuwa wenyewe wanaotoa madai hayo ndio waliojichakachua wenyewe. Akisisitiza jambo, Dk. Kamuzora alisema Matokeo ya Uchaguzi kuanzia ya uraisi hadi wabunge na madiwani yalikuwa sio ya ubabaishaji na uchaguzi ulikuwa huru na, salama na Haki, hata taarifa ya waangalizi wa Umoja wa Ulaya, Umoja wa Africana SADC walithibitisha hilo. Aither Dr. Kamuzora alisisitiza kuwa katika kipindi cha mwanzo cha uongozi wa Raisi Kiwete CCM imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutimiza ilani yake ya uchaguzi''haya ni maneno ya mtu asiyekuwa na hekima na sidhani kama huo uwenyekiti wa tawi hakika litakuwa tawi la wajinga wenzie!

Kumbe wapo watanzania waishio nje ya Tanzania wanamawazo mgando kama haya? Inasikitisha sana!
Wewe unayejiita Dr. Alfred, Kura hukupiga na hao wenzako woote hamkupiga kura. Hamkuwa Bongo kwa nini mpige domo, wakati waliopiga kura, waliopigwa mabomu ambayo ni ndugu zenu walala hoi wa Bongo wanaamini kuwa wameibiwa? Shame on you guys if u are tired with mabox and u think that by praising the thieves u will accecc good position when u will be back mmechemsha
 
Wakati raia wa nchi nyingine wakifikiria namna ya kuwasaidia wenzao waliobaki kwenye hali ngumunchini mwao sisi wa kwetu wanafikiria kufungua matawi a CCM dunia nzima. Je, CCM ni biashara gani?
 
Nonsense wanafiki wakubwa. Sio ndio hao kipindi fulani walikuwa wanalalamikia pesa za kujikimu? Je wataacha kuwa wanafiki hili hali wanategemea handouts toka serikali ya JK? Dr gani anashindwa kuwa objective and analytical?
 
IMG_0196.JPG

Na Mwandishi wetu Happy
Katika hali iliyoonekana kuwavutia watanzania wengi waishio nchini Urusi, Tawi la CCM Moscow limefanya sherehe ya kumpongeza Mwenyekiti wa CCM na Raisiwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kwa ushindi mkubwa alioupata katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni. Sherehe hiyo iliyoanza majira ya saa kumi na moja jioni ya tarehe 27/11 na kumalizika majira ya saa kumi na mbili na nusu asubuhi ya tarehe 28/11 iliwavutia sii tuu watanzania waishio nchini Urusi na Maeneo ya jirani, bali pia natu wengine wasio watanzania.

Miongoni mwa wageni muhimu waalikwa na Capt. Mstaafu Jaka Mwambi ambaye pia aliwahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi Tanzania ikiwemo ukatibu mkuu msaidizi wa CCM Taifa. Mh. Mwambi katika htuba yake kwa wapenzi, wanachama na wakereketwa wa CCM waliohudhuria amesisitiza kuwa vijana sio tuu taifa la kesho, ila pia ni Taifa la Leo na la Keshokutwa. Mh. Mwambi amesema kuwa vijana wasifikirie kuwa kujiunga na chama ni kujinufaisha kifedha, bali ni kukomaa kimawazo na kisiasa na lengo kubwa ni baadae kuwatumikia wananchi na sio wananchi kuwatumikia.

Mwenyekiti wa Tawi la CCM Urusi Dk. Alifred Kamuzora katika hotuba yake alihoji kuwa katika uchaguzi wa hivi karibuni, ambapo wapinzani wanadai matokeo yalichakachuliwa, isije kuwa wenyewe wanaotoa madai hayo ndio waliojichakachua wenyewe. Akisisitiza jambo, Dk. Kamuzora alisema Matokeo ya Uchaguzi kuanzia ya uraisi hadi wabunge na madiwani yalikuwa sio ya ubabaishaji na uchaguzi ulikuwa huru na, salama na Haki, hata taarifa ya waangalizi wa Umoja wa Ulaya, Umoja wa Africana SADC walithibitisha hilo. Aither Dr. Kamuzora alisisitiza kuwa katika kipindi cha mwanzo cha uongozi wa Raisi Kiwete CCM imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutimiza ilani yake ya uchaguzi. Katika kauli mbiu ya CCM ya Maisha Bora kwa kila Mtanzania, CCM imeweza kuboresha huduma za hospitali, kuongeza shule za msingi, shule za sekondari kwa kila Kata na hata vyuo vikuu nchini vimeongezeka kutokana na sera na Ilani ya CCM.
Mengine ni uboreshaji wa mahakama huru, ambapo watanzania wameshuhudia hata watu waliowahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini wakisimama kizimbani, uboreshwaji wa chombo imara cha dola, jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi, na Jeshi la kujenga Taifa.
Aidha, CCM imeweza kuboresha elimu, maji, umeme, barabara nk. hayo ndio maisha bora yanayozungumzwa.

masikini wa fikra.

kwa kula kwao raha moscow wanafikiri na huku bongo tunakula kuku.
 
Sherehe imeanza saa kumi na moja jioni nakumalizika saa kumi na mbili asubuhi siku iliyofuata, kwa muda wa zaidi ya masaa 12 walikuwa wanakunywa vodka ulitegemea katika akili zao kutazaliwa nini kama si ulevi? Hayo ni maneno ya walevi.Angalia sura ya huyo dada wa tatu kutoka kushoto, ameoza kwa vodka.CCM ni chama cha walevi na mafisadi
 
Kijana wa 3 kutoka kulia mwenye skafu shingoni nahisi kuna tatizo kubwa la kibailojia
 
IMG_0196.JPG

Na Mwandishi wetu Happy
Katika hali iliyoonekana kuwavutia watanzania wengi waishio nchini Urusi, Tawi la CCM Moscow limefanya sherehe ya kumpongeza Mwenyekiti wa CCM na Raisiwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kwa ushindi mkubwa alioupata katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni. Sherehe hiyo iliyoanza majira ya saa kumi na moja jioni ya tarehe 27/11 na kumalizika majira ya saa kumi na mbili na nusu asubuhi ya tarehe 28/11 iliwavutia sii tuu watanzania waishio nchini Urusi na Maeneo ya jirani, bali pia natu wengine wasio watanzania.

Miongoni mwa wageni muhimu waalikwa na Capt. Mstaafu Jaka Mwambi ambaye pia aliwahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi Tanzania ikiwemo ukatibu mkuu msaidizi wa CCM Taifa. Mh. Mwambi katika htuba yake kwa wapenzi, wanachama na wakereketwa wa CCM waliohudhuria amesisitiza kuwa vijana sio tuu taifa la kesho, ila pia ni Taifa la Leo na la Keshokutwa. Mh. Mwambi amesema kuwa vijana wasifikirie kuwa kujiunga na chama ni kujinufaisha kifedha, bali ni kukomaa kimawazo na kisiasa na lengo kubwa ni baadae kuwatumikia wananchi na sio wananchi kuwatumikia.

Mwenyekiti wa Tawi la CCM Urusi Dk. Alifred Kamuzora katika hotuba yake alihoji kuwa katika uchaguzi wa hivi karibuni, ambapo wapinzani wanadai matokeo yalichakachuliwa, isije kuwa wenyewe wanaotoa madai hayo ndio waliojichakachua wenyewe. Akisisitiza jambo, Dk. Kamuzora alisema Matokeo ya Uchaguzi kuanzia ya uraisi hadi wabunge na madiwani yalikuwa sio ya ubabaishaji na uchaguzi ulikuwa huru na, salama na Haki, hata taarifa ya waangalizi wa Umoja wa Ulaya, Umoja wa Africana SADC walithibitisha hilo. Aither Dr. Kamuzora alisisitiza kuwa katika kipindi cha mwanzo cha uongozi wa Raisi Kiwete CCM imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutimiza ilani yake ya uchaguzi. Katika kauli mbiu ya CCM ya Maisha Bora kwa kila Mtanzania, CCM imeweza kuboresha huduma za hospitali, kuongeza shule za msingi, shule za sekondari kwa kila Kata na hata vyuo vikuu nchini vimeongezeka kutokana na sera na Ilani ya CCM.
Mengine ni uboreshaji wa mahakama huru, ambapo watanzania wameshuhudia hata watu waliowahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini wakisimama kizimbani, uboreshwaji wa chombo imara cha dola, jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi, na Jeshi la kujenga Taifa.
Aidha, CCM imeweza kuboresha elimu, maji, umeme, barabara nk. hayo ndio maisha bora yanayozungumzwa.

Hamna uzalendo wala mapenzi na nchi zaidi ya kuijipendekeza na kijikomba kwa CCM ili wapate vyeo vya bure na hilo wanapoteza muda kwani come next election huku watanzania wamebadilika na wanataka mabadiliko na wapiga kura wako huku na mechi inachezwa nyumbani. Endeleeni kupoteza muda kwa VODKA huko Urusi
 
Sasa nimeamini kua upinzani pia ndani ya ubalozi wa nchi upo kwakua nahisi hata huyo alieichana Picha ya Kikwete Macho ni mamluki anayejifanya yeye ni CCM damu damu kumbe ni sawa na chui aliyevaa ngozi ya Kondoo! Shame on you CCM mnajimaliza wenyewe! Hiyo picha jamaa walikua wanajipongeza tu Balozi kawaitia Ulabu waburudike!
 
IMG_0196.JPG

Aidha, CCM imeweza kuboresha elimu, maji, umeme, barabara nk. hayo ndio maisha bora yanayozungumzwa.

Yaani nyie mnaishi Urusi na mnataka kujidai mnayajua haya yanayotokea Bongo kuliko ambao wapo hapa Bongo???? Even though kama ungekuwa unafuatilia vyombo vya Habari usingeandika ulichokiandika..........

Mimi ntaeleza kwa uchache kutoka mistari miwili uliyoandika.

ELIMU: Kuanzia UNIVERSITY LEVEL mpaka Msingi hali ni mbaya. Tatizo ni walimu na usifikiri kutunikiwa PHD kwa JK UDOM kumeboresha hali. Bado walimu ni tatizo linalokikabili chuo kile. Ukija sec bado wenye fedha ndo wanapata elimu murua so hapa labda useme CCM bado inaongeza GAP kati ya Maskini na Tajiri...Msingi bado wanafunzi wa shule kibao wanakaa chini...

MAJI: Tusiende vijijini, huko itakua mbali sana. hapahapa DSM maji bado ni tatizo TBT, KIWALANI, MBAGALA nk ni baadhi ya maeneo ambayo bado hawajaipata huduma ya maji...labda mwenzetu unajua ilivyoboreshwa...waweza tujuza.

UMEME: Kwa hili ndo nimekudharau sana ulipolitaja, koz its just y'day TANESCO wametangaza mgao wa umeme nchi nzima baada ya Mitambo ya SONGAS kuzingua na kina cha maji kupungua PANGANI HYDRO POWER STATION. Kifupi JK na serikali yake hawajaongeza lolote katika sekta hii. bado anatumia HYDRO za NYERERE, Gas plants za MKAPA...yeye kama yeye hana jipya.

BARABARA: Sina kumbukumbu nzuri ila najua barabara zote ambazo ni ongoing na zilizo kamilika ni za MKAPA. Kifupi huyo jamaa unaemsifia hii miaka mitani amekula BATA kinyama zaidi ya mnavyofikiri.......
 
Mimi nimejiunga hivi karibuni jf.Labd niulize swali.Hivi kutukana kama kuwaita watu majuha,wapumbavu nk ndo kweli hoja zinazohitajika katika forum hii?
Nimegundua kuwa an jf wengi ni wapenzi wa cdm ambacho kinajiita chama cha demokrasia.Nielewavyo mimi Demokrasia ni pamoja na uhuru wa mawzo,sas inakuwje mtu akitoa mawzo badala ya kujibu hoja unatukana?
 
Back
Top Bottom