Ninamtafuta ndugu yangu naomba msaada haraka hasa kwa walioko Vancouver-Canada

Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu

JF-Expert Member
Mar 8, 2006
1,211
230
Ndugu Wana Jamii forums!

Ninaomba msaada kwa yeyote yule anayeishi Canada au nje ya Canada anayemfahamu Ndugu anayefahamika kwa jina la TOSH au Daniel Musisi na anajua namba yake ya simu,Anuani au email Tafadhali sana naomba anifahamishe au Amwambie kuna kaka yako yupo jamiiforums anakutafuta na awasiliane nami mara moja.

Mara ya Mwisho kuwa na mawasiliano naye ya simu ilikuwa mwanzoni mwa mwaka 2009 na alipatwa na misukosuko mingi kabla ya hiyo simu ya mwisho.Mtiririko wa matukio yake kabla ya kupoteza mawasiliano ilikuwa kama ifuatavyo alikamatwa kwa tuhuma za domestic violence kwa kuripotiwa na rafiki wa mke wake na kitu ambacho hakikuwa kweli na aliachiwa huru na tuhuma kufutwa na hata kuruhusiwa kurudi kwenye nyumba na kutakiwa kuishi pamoja na mke baada ya awali kupigwa marufuku kuishi pamoja hadi kesi iliposikilizwa na kuonekana hakuna ushahidi.

Kabla ya tatizo hili kujiri alimkaribisha jamaa wa nyumbani, nyumbani kwake kwasababu alikuwa na matatizo ya makazi lkn baadaye jamaa mkaribishwaji akaanza kuleta fitina ndani ya ndoa na kupelekea tuhuma za uongo za domestic violence nilizozieleza awali.

Baada ya kuruhusiwa kurudi nyumbani mke alisema yeye anaona apange sehemu nyingine kwa muda ila lkn atakuwa anakuja tu na mara zote walikuwa wakiwasiliana na bado jamaa alkuwa akimpa fedha za matumizi kwasababu mke hakuwa na kazi na nilipata fursa kipindi hicho kuwasiliana nao wote yaani mke na mume.

Wakati wakiendelea kukaa mbali mbali siku moja usiku Ndugu TOSH akiwa amelala ndani ya nyumba yake alisituka kwa kutaka kwenda kujisaidia na kukuta nyumba ikiwa inawaka moto naye akiwa ndani ndipo alipowahi kutoka bila ya kitu chochote na nyumba ikiwa imeteketea na vitu vyote ikiwemo simu na kikosi cha wazima moto mbali na jitihada zao hawakufanikiwa kuokoa chochote zaidi ya wamiliki wa hizo nyumba zilizoungua kuwahi kutoka.

Siku hiyo ndiyo alinipigia simu na kunipa taarifa kupitia simu ya rafiki yake.Baada ya hapo nikipiga simu zote ya kwake ambayo iliungua lkn natumai angeweza kupata namba hiyo hiyo kama angeomba au labda aliamua kubadilisha sielewi,ya rafiki yake ambaye alitumia kuongea nami mara ya mwisho na namba ya mke wake ambayo mkewe alikuwa akiitumia kuwasiliana nami kabla ya tukio hilo.

Sasa karibu mwaka wa pili sina mawasiliano naye hivyo kwa yeyote yule anayesoma bandiko hili na anamfahamu mtajwa ambaye wakati haya yote yakitokea alikuwa akiishi Vancouver naomba tuwasiliane kupitia bandiko hili.

Tafadhalini Naomba Msaada wenu,Kwa wenye ndugu Canada naomba vile vile mniulizie kama wanamfahamu mtajwa na kama wanaelewa alipo au nini kilimsibu.Natanguliza Shukrani zangu za dhati!
 
Sasa kaka mara ya mwisho kuwasiliana naye umesema ni mwanzoni mwa 2009....mwishoni unasema sasa karibu mwaka wa pili huna mawasiliano naye...kweli?!
 
Hebu kama unajua majina yake yote jaribu ku google unaweza kumpata kwenye social forums nyingine.Pia unaweza ukawaandikia watu wa mambo ya ndani canada ukaona watakujibuje especially kama unakumbuka physical address yake ya mwisho
 
Huyo nduguyo ameingia mwaka gani Canada? Mji gani? Aliingia kusoma au kufanya nini? Alitokea nchi gani kabla ya kusettle Canada? Alikuwa akifanya shughuli gani? Majina aliyokuwa akitumia kwenye passport ni yapi?
Jibu vizuri hayo maswali tukusaidie.
 
Hebu kama unajua majina yake yote jaribu ku google unaweza kumpata kwenye social forums nyingine.Pia unaweza ukawaandikia watu wa mambo ya ndani canada ukaona watakujibuje especially kama unakumbuka physical address yake ya mwisho
Inawezekana alishampata maana ni kitambo
 
Huyo nduguyo ameingia mwaka gani Canada? Mji gani? Aliingia kusoma au kufanya nini? Alitokea nchi gani kabla ya kusettle Canada? Alikuwa akifanya shughuli gani? Majina aliyokuwa akitumia kwenye passport ni yapi?
Jibu vizuri hayo maswali tukusaidie.
Hakujibu huenda alimpata kama hajampata natumai atakuja kukutajia
 
Back
Top Bottom