Sinkala
JF-Expert Member
- Dec 22, 2008
- 1,773
- 683
Kumekuwepo na wimbi la uchafuzi wa jiji la Dar es Salaam kunakofanywa na masangoma ambao huwa hawachagui mahali pa kuyaweka matangazo ya shughuli zao, wanaweka popote tu hadi Airport kuna vitambaa vya matangazo. Sasa mimi ninauliza, ni mamlaka gani inayodhibiti uwekaji wa mabango? Hivi zile billboards za makampuni ya simu et al, si huwa zina utaratibu wa kulipia matangazo; hawa sangoma wanalipia? Nilitaka niweke picha mbili hapa, lakini nimeogopa kwani bado familia inanihitaji.