Ninachompendea Kikwete Jakaya Khalfani ni hiki...

Naomba nitofautiane na wewe kidogo
Kumbuka kila kitu kina wakati wake
na mabadiriko ya sasa yaliyopo hata kama angelikuwa ni nani asingeweza kuyazuia
ni sawa sawa na maandamano yanavyotokea huko Kaskazini hayo hayana mkono wa mtu wala nini bali ni hali halisi ya wananchi wamechoka na kusema basi inatosha.

Hivi sisi tuna uhuru wa kuongea lakini viongozi wetu hawasikii wala hawafati tunachoongea ni kama mavuvuzela tu vile
N awale wasiokuwa na Uhuru wa kuongea lakini wanatimiziwa mahitaji yao yote ya mhimu
J eni yupi bora?
Sisis ni kweli tunaongea sana, lakini ukweli ni kwambba kila kitu ni kibaya zaidi, kila kitu ni siasa tu hakuna vitendo kabisa.
shule ndio hizo za kata za kufelisha asilimia 85, Hospitali si unaziona mwenyewe kama za mwananyamala zilizo jijini zinafanya yale madundu je zile za kule vijijini? najua unalo jibu.

JK hajawahi kuwahadaa ama kuwasuta watu wa media kama Mkapa, ameruhusu mno uhuru wa media nasi kujadili ndani-nje bila vikwazo juu ya utawala wake.

Hii JF yetu enzi za mzee Ben...ingalishafungwa kitambo na kusahaulika.
 
Umenikumbusha kitu: Jambo Forum! nayo hivi iliishia wapi na ulikuwa wakati wa utawala wa nani ??
Yaani wewe Hujui Jambo forum iko wapi??/ duh kumbe kunahitajika kuwe na somo hapa Jf ili kuwasaidia kuelewa wajukuu wanapoingia jukwaani
 
Kuhusu swala la noti za bandia kuna tatizo ,
N awala usitake kuwaambia watu waone vitu na wakae kimya ..hapana..tena hapan kabisa
Kunapokuwa na tatizo lolote liwe limesababishwa na wizara au watu wengine tu kama linaihisu wizara husika hatuna budi kuilaumu hiyo Wizara, na hilo ni suala la kawaida kabisa katika kila sekta, ndio maana unaona kwa nchi za wenzetu kunapokuwa na kashfa tu iwe ya kweli au ya uwongo kitu cha kwanza kwa mhusika huwa ni ku-step down.
Wao kama BOT wamefanyaje kuhakikisha watu wa vijijini kama mimi tunazijua hizo alama za hizo pesa mpya?
kwni kila mtu ana TV, redio au magazeti?
Hivi hujui kuwa magazeti yanasomwa mijini tu? je wananchi wa kawaida waatapata wapi tyaarifa maalumu kama hizo?
ni sawa wanaweza kusikia kwenye redio lakini je kusikia tu unaweza ukaweza kupambanua vizuri ukilinganisha zile ni pesa mpya???

Hapo ndio utagundua matatizo makubwa ya serikali zetu, ni kutokuwashirikisha wananchi wake ipasavyo.
Hao BOT walitakiwa kutembea nchi nzima na kuzinadi hizo pesa zao mpya natummaini wasingewapa mwanya hata hao maharamia kutengeneza hizo bandia.
Wanaozitengeneza hizo pesa wanatumia tu ule ujinga wa mwannchi wakawaida wa kutokujua alama zake kamili lasivyo wasingezitengeneza.
Mi nalala si unajua tena huko Pyongyang jua linazama masaa 6 zaidi yenu.

[QUOTE=Mbopo;1670900]hakika huu ndiyo umaskini wa akili. Suala na noti bandia jk anahusikaje kama siyo kudhihirisha chuki isiyo na sababu. Halafu unailaumu bot kwa lipi. Kwani hizo noti bandia zimetolewa na bot. Unashindwa kuelewa kwamba umepata uwezo wa kuzitambua noti bandia kwa sababu alama zilizopo kwenye noti halali za bot zinajipambanua vizuri na kwa urahisi na hizo noti feki.

Ukweli ni kwamba jk ametoa uhuru ambao hata mimi naujutia maana watu kama nyie hamkutakiwa kusikika kabisa maana kila mnaponyanyua mdomo mnayoyaongea ni pumba na maudhi tu. Huko ambako uhuru wa kuongea umaminywa nao wana katiba lakini mkono wa chuma wa watawala ndiyo unaowatia adabu. Waswahili wanasema samaki ndani ya maji haoni umuhimu wa maji mpaka pale wimbi la ukombozi linapomtoa kutoka ufukweni na kumrejesha baharini ndipo hugundua kwamba bila maji yeye hana maisha. Mtamkumbuka huyu! Nyie leteni tu chuki na ushabiki usio na maana![/QUOTE]
 
Amewapa raia uhuru wa kuzungumza. Hii ni tofauti kabisa na Gaddafi wa Libya ambaye hataki kusikia raia au paparazi anasema au kuandika chochote bila 'ruhusa' ya vibaraka wa Gaddafi. Raia wa Libya wana maisha bora kuliko hata raia wa Misri, lakini hawautaki utawala wa Gaddafi kwa sababu wananyimwa uhuru wa kuzungumza. Ukitaka kuzungumza lazima ufanye hivyo 'kwa hisani ya Gaddafi'.

Bravo Mkwere!! (Lakini naskitika sijawahi kukupigia kura, na hiyo haikuwa kwa bahati mbaya. hata ukigombea leo sikupi)

Kuwapa watu uhuru wa kuzungumza hakutoshi. Yafanyie kazi hayo ya muhimu yanayozungumzwa au daiwa.
Watu wamekuwa huru kuongea ya Dowans au Gongo la Mboto lakini JK utafikiri anaishi kwenye sayari ya Zebaki.
 
Ah wapi! Kikwete hakuwa na utashi, mabavu au ujasiri wa kufanya kitu chochote. Yeye mpaka sasa hivi hana habari kinachoendelea au kazi ya rais ni nini. Jamani kutofanya kitu si sawa na kufanya kitu. What do I mean? He didn't do sh*t about freedom of expression, ndo maana kila mtu anafanya anachotaka. Sasa humuhumu kuna religious incitement lakini wahusika hawachukuliwi hatua, hiyo ni freedom of expression?
Mfano mwingine ni hali ya uchumi, aliendelea tuuuu na sera zile zile za Mkapa hakuna alichokibuni au kuongeza, sasa unaona mipango imekamilika, mikataba ime-expire, mikakati imepitwa na wakati na hana jipya. Hebu nipeni mfano wa uwekezaji wowote wa maana uliofanyika ndani ya miaka hii 5 -6 ya JK? Kama si vituo vya mafuta vya kizushi kuongeza kwa wingi!
Let us not confuse inaction with action!
Kawekeza mitambo yake ya umeme wa dharula Richimonduri a.k.a Dowans.. japo kasema hawafahamu wamiliki wake... Usanii wa aina yake kama mkaidi aliyeshika jiwe ukimuambia alitupe anakuambia sijashika jiwe mimi....(J.K. Juma Kilaza)
 
Amewapa raia uhuru wa kuzungumza. Hii ni tofauti kabisa na Gaddafi wa Libya ambaye hataki kusikia raia au paparazi anasema au kuandika chochote bila 'ruhusa' ya vibaraka wa Gaddafi. Raia wa Libya wana maisha bora kuliko hata raia wa Misri, lakini hawautaki utawala wa Gaddafi kwa sababu wananyimwa uhuru wa kuzungumza. Ukitaka kuzungumza lazima ufanye hivyo 'kwa hisani ya Gaddafi'.

Bravo Mkwere!! (Lakini naskitika sijawahi kukupigia kura, na hiyo haikuwa kwa bahati mbaya. hata ukigombea leo sikupi)

I don't think this is something to congratulate Kikwete. These are our rights and your make mistakes to say that "Kikwete gave you this" Makosa makubwa kumpa raia yeyote nguvu za kuchukua na kukupa muda anaotaka yeye. Lazima tujue kwamba sisi tunao contribute humu kwenye JF tuna bring changes. Kuna mtu humu hajui kama ccm wapo humu na wanasoma? Hawataki wanavyo viona and they can't do nothing about it because we will fight and take them out in a second if they try to remove these rights. Tusilinganishe utawala wa nchi za kiarabu na utawala wa nchi yetu. Historia ya nchi za kiarabu kuna unyama wa ajabu na hapa sisi Tanzania tuna unyawa wetu kama "Downs" Yote haya ni makosa na kinyume cha haki za binadamu. There is no way nitampa Kikwete rights zangu kama hizi za freedom of expression. Kuna watanzania walipigania hizi Rights na wengine walikufa na Kikwete hakuusika katika haya mapambano. No matter what we say although sikubaliani na Mtikila kwa kila kitu, amechangia kuleta mabailiko ya sheria Tanzania. Freedom of Media Haishiii Mtanzania Kuongea ni Kila Swala Linalo Mhusu Mtanzania lisungumzwe kwa uwazi bila siri na vikao vyao.

Kikwete ni Mpingaji Mkubwa wa Free Media. Tangu Lini Tuliona Mijadala ya Policies na Mikataba Hadharani?
Kila Jambo Linafanyika Ofisi ya Raisi, BOT, Wizarani Kwa Siri Kubwa kwa Wananchi
 
JK hajawahi kuwahadaa ama kuwasuta watu wa media kama Mkapa, ameruhusu mno uhuru wa media nasi kujadili ndani-nje bila vikwazo juu ya utawala wake.

Hii JF yetu enzi za mzee Ben...ingalishafungwa kitambo na kusahaulika.
Hili swala la uhuru wa kuongea nakutoa maoni ni Haki yetu ya Kikatiba na ipo stated kwenye Katiba hatuipati kwa Hisani ya Mkwere so msimpe sifa za bure.Msome katiba mjue haki zenu gazeti la Raia mwema linatoa nakala ya katiba kila wiki J'tano.
 
Hata huo uhuru wa kujieleza (ambao unadai rais karuhusu) hatunao kivile, ndo maana hapa JF kuna aliases nyingi kuliko majina halisi. Moja ya sababu ya kutumia aliases ni kuogopa 'kushughulikiwa' kutokana na maoni mtu atoayo. So bado hatujawa na uhuru kamili wa kujieleza.
 
Sio vizuri kumsema mtu kwa kutaja kabila lake. Pamoja na matatizo yake lkn pia kuna mazuri amefanya.
 
Tatizo kubwa la JK ni timu yake..ina udhaifu karibu kila kona..pia hatujui timu yake anayoiamini yeye inatupeleka wapi..!?

Kwa mtazamo wangu ameshindwa kabisa kupata timu kamili ya wachapakazi wanaolijua hilo na ndio maana utaona utendaji wa serikali yake umejaa dharura nyingi.

Mambo yanaendeshwa kwa dharura.

Ndio maana wananchi wengi wamepoteza mapenzi, imani na matumaini kwa serikali yake.

JK hana serikali, ila alichonacho yeye ni baraza la mawaziri kwa mujibu wa sheria na katiba ya JMT. Angekuwa na serikali maendeleo wote tungeyaona na mfumuko wa bei ungedhibitiwa. Pengine ni jukumu la watanzania wazalendo na wasomi kumsaidia aweze kuwa na serikali kama ilivyokuwa kwa JK wa ukweli (mzee kifimbo), Ben na mzee rukhsa. The big gap tunayofeel katika taifa letu siyo ombwe la uongozi, bali ni kukosekana kwa government machinery! Hatuna serikali Tanzania, tuna rais na cabinet yake basi.
 
Amewapa raia uhuru wa kuzungumza. Hii ni tofauti kabisa na Gaddafi wa Libya ambaye hataki kusikia raia au paparazi anasema au kuandika chochote bila 'ruhusa' ya vibaraka wa Gaddafi. Raia wa Libya wana maisha bora kuliko hata raia wa Misri, lakini hawautaki utawala wa Gaddafi kwa sababu wananyimwa uhuru wa kuzungumza. Ukitaka kuzungumza lazima ufanye hivyo 'kwa hisani ya Gaddafi'.

Bravo Mkwere!! (Lakini naskitika sijawahi kukupigia kura, na hiyo haikuwa kwa bahati mbaya. hata ukigombea leo sikupi)
hata usimpompigia kura wala haimsaidii chochote hiyo kura yako,kura za wale wanaompigia zinamtosha,nandio anamalizia miaka yake 10 kwa mujibu wa katiba.
 
Amewapa raia uhuru wa kuzungumza. Hii ni tofauti kabisa na Gaddafi wa Libya ambaye hataki kusikia raia au paparazi anasema au kuandika chochote bila 'ruhusa' ya vibaraka wa Gaddafi. Raia wa Libya wana maisha bora kuliko hata raia wa Misri, lakini hawautaki utawala wa Gaddafi kwa sababu wananyimwa uhuru wa kuzungumza. Ukitaka kuzungumza lazima ufanye hivyo 'kwa hisani ya Gaddafi'.

Bravo Mkwere!! (Lakini naskitika sijawahi kukupigia kura, na hiyo haikuwa kwa bahati mbaya. hata ukigombea leo sikupi)

Umeua kabisaaaa hahahaha
 
Kama kuna free media access Dowans, EPA na hii mikataba fake imetoka wapi, why there was or is public discussions on every policies zinazo mhumu Mtanzania? Please hii analysis yani kera kufikia kuzungumzia very thin eyes...
 
Huyo JK wako naye hatumtaki hebu ona ma noti bandia yalivyozagaa
Sasa haya yote yamekuja sababu ya usimamizi wa huju JUMa Kilaza(JK) hakuna anachofanya mpaka tunaletewa mijinoti fake na BOT halafu wanayanadiiii bila hata aibu ptuuuuuuu.
Mkuu,
Jaribu sana kuepuka stereotyping!
Unakumbuka lile tangazo la "maimuna"?
Inaweza kuchekesha lakini "tunawahujumu" watu kisaikolojia....si mchezo mwema.
 
hakika huu ndiyo umaskini wa akili. Suala na noti bandia jk anahusikaje kama siyo kudhihirisha chuki isiyo na sababu. Halafu unailaumu bot kwa lipi. Kwani hizo noti bandia zimetolewa na bot. Unashindwa kuelewa kwamba umepata uwezo wa kuzitambua noti bandia kwa sababu alama zilizopo kwenye noti halali za bot zinajipambanua vizuri na kwa urahisi na hizo noti feki.

Ukweli ni kwamba jk ametoa uhuru ambao hata mimi naujutia maana watu kama nyie hamkutakiwa kusikika kabisa maana kila mnaponyanyua mdomo mnayoyaongea ni pumba na maudhi tu. Huko ambako uhuru wa kuongea umaminywa nao wana katiba lakini mkono wa chuma wa watawala ndiyo unaowatia adabu. Waswahili wanasema samaki ndani ya maji haoni umuhimu wa maji mpaka pale wimbi la ukombozi linapomtoa kutoka ufukweni na kumrejesha baharini ndipo hugundua kwamba bila maji yeye hana maisha. Mtamkumbuka huyu! Nyie leteni tu chuki na ushabiki usio na maana!

huyu jamaa inaonyesha tuko wote jobless corner mie nashukuru jk kwakuturuhusu kuwa na jf na google maanake nilikuwa china juzi kusearch protest tu ishu, bravo mkwere
 
Anaetoa uhuru wa kuzungumza na kuandamana si raisi bali haya na mengine yameainishwa kwenye katiba ya nchi. Ni haki yetu. Marais wliozuia haya ms mengine ni madikteta!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom