Nina wivu nashindwa hata kumeza mate!

Pole mwanangu
Wivu siyo kitu kibaya hata kidogo. Ila wivu wako wewe unatokana na obsession na insecurity. Lakini inaelekea mwenzako analiona hilo na ndiyo maana ana ridhia mabadiliko unayoyafanya na vilevile kukuridhia utakalo. Lakini ninaomba nikutahadharishe kuwa uelewe kuwa naye ni binaadamu hivyo uhakikishe ile kamba inayowaunganisha ni imara na wewe ndiye wa kuhakikisha inakuwa hivyo maana kamba hiyo [inayojumuisha mapenzi/urafiki/mwenza/msiri/ nk] haikatiki kwa kumfanyia vitu ambavyo vitakuwa kero kubwa kwake. Kwani ikifikia hapo ataanza kubadilika tabia na vitendo na wewe bila kujua utadhani amepata mwingine na utafanya mambo ambayo yatazidi kuweka umbali kati yenu na mwishowe hatima ya mapenzi kwisha na kasheshe na visa kuanza.
 
Abunwasi, asante sana kwa mawazo mazuri. Ukweli nimeliona hilo, kwamba na yeye ni binaadam na wivu wangu unaweza kuwa ni kero kubwa kwake hivyo kuhatarisha mahusiano. Ndio maana pamoja na kujitahidi kumridhisha na kufanya mahusiano yetu yaimarike siku hadi siku, pia nahitaji kubadilika - nipunguze au niache wivu wa kupindukia. Nashukuru sana kwa mawazo yako naamini yatanijenga.

Asante sana,

Annina
 
Nashukuru sana kwa kutambua hilo kwani wengi wanaumi moyo au kufanya mambo ambayo hawakutarajia kutokana na kutojifahamu.
Mama, nina uhakika mtaishi vizuri sana kama mtaamua kufunga pete ya maisha.
Nakutakia maisha mema na mwenza.
 
Asante sana Abunwasi, naomba Mungu hilo litimie na atujaalie ndoa yenye amani na upendo.

Asante sana,

Annina
 
Asante sana Abunwasi, naomba Mungu hilo litimie na atujaalie ndoa yenye amani na upendo.

Asante sana,

Annina

Kila la heri Annina...kila siku ukumbuke, "Too much of anything is harmful."
 
Asante BAK,

Nimekusoma, nitajikumbusha hilo kila mara.

Annina
 
Back
Top Bottom