Wadau mpaka sasa sioni mfumo wala harakati za nguvu za Wenje kujihakikishia ushindi hapa Nyamagana. Naanza kupata wasi wasi kama atashinda ingawa Masha hapa Nxamagana hatakiwi kabisa.
Tatizo la Wenje na CHADEMA hapa MZA sizioni juhudi zao kujitangaza na wala sioni mfumo makini wa kuwashirikisha raia kulinda kura. Nilikuwa Msoma last week, Nyerere pamoja na uhakika alionao anafanya kampeni ya nguvu sana na anawajengea raia uzalendo wa kulinda kura zao na people wamerespond positively saaana, tofauti na Wenje hapa Mwanza. Masha akishinda itakuwa kosa la CHADEMA NA SI WANANYAMAGANA.Kama Masha hatakiwi basi mshindi atakuwa mpinzani wake.
Mleta mada naona haeleweki anachohitaji hapa. Umetumwa kujua msimamo wa JF katika jambo hili?Kama Masha hatakiwi basi mshindi atakuwa mpinzani wake.
Hawa CHADEMA vipi......??? Nilishawahi kushuhudia uchaguzi mwingine Songea. Chadema walishinda ila kazi waloifanya ilionesha kweli wanataka ushindi, sasa huku sijui Yahaya yule mzee mchawi keshawachakachua!! Mkishindwa mi nasema msitafute mchawi.Tatizo kama hilo lipo hata busanda,Finias magesa nae kama vile amechakachuliwa na lolensia bukwimba,wanachadema msishangae kulikosa hilo jimbo,hakuna juhudi zozote,poleni sana chadema