Nina nusu eka naomba msaada

AHAKU

Member
Jan 28, 2010
26
1
Nawasalimu wana JF
Kwa taadhima naomba kuuliza nina eneo la nusu ekari mahala panaitwa Msongola katika wilaya ya Ilala. Naomba kujua kwa eneo hili la ardhi naweza kufanya kilimo gani kinachoweza kunipatia senti za hapa na pale. Kwa ajira niliyo nayo nina uwezo wa ku save Sh laki moja kila mwezi
Asanteni
 
Kutokana na hali ya hewa na ardhi ya dar, mimi nadhani uwe na mtizamo kwenye ufugaji. Kama vile kuku wa kisasa.
 
Je eneo hilo lako unaweza kuchimba kisima? Kama liko tambalale na unaweza kuchimba kisima,fanya yafuatayo. Fuga kuku wachache wakupe mbolea, kisha anzisha kilimo cha mchicha kitalaamu. Mkuu kama utalima mchicha vizuri na maji unayo na vikuku viwili vitatu vya kutoa mbolea na kitoweo nakuhakikishia utapiga bao zuri.
 
lima mboga mboga adimu,do a survey bei wanazonunua watu wa mahoteli makubwa,then unafanya direct delivery ,ila wanataka quality kwa hiyo usimamizi inabidi uwe mzuri.
 
Back
Top Bottom