Nina maumbile madogo mpaka najishangaa!

Tegelezeni

JF-Expert Member
Dec 31, 2009
268
124
Hata sijui sababu ni nini, maana kama ni kula nakula vizuri tu na mke wangu anajitahidi kunipikia mapochopocho mpaka basi lakini mwili wangu hauridhiki sijui kwanini, yaani nimekuwa na maumbile madogo wala sinenepi kabisaa mpaka ndugu zangu wanahisi kwamba huenda mke wangu hanipi chakula na ndio maana sinenepi kumbe binti wa watu anajitahidi kukalangiza lakini mwili wangu huu hauna shukurani.

Hebu nisaidieani, sababu hasa ya kukosa kwangu siha ni nini?
 
maumbile madogo yepi? zakari, tumbo, kichwa, miguu, vinyweleo, ubongo, kiuno au nini kingine?
 
Unene ni ugonjwa. Shukuru MUNGU u mwembamba wanene tunahangaika Na mijidiet eti tupungue, wengine mwautafuta, nyeee, MUNGU Kazi anayo.
Aisee Remmy nakubaliana na wewe lakini mimi ni mwembamba sana, mpaka natisha nahitaji kuongeza weight japo kidogo.
 
Last edited by a moderator:
namaanisha mwili wangu, kwani wewe ulidhani nazungumzia maumbile mgani?

mi nilizoea mtu akisema maumbile ni tafsida ya deepstick a.k.a mlizo
Nirudi kwenye mada,usipende kunenepa walio wanene wanatamani kupungua,upende mwili wako kunywa maji meng kwa siku ili mwili umelemete
 
Kweli kwenye miti hakuna wajenzi.
Mkuu Rogi hebu mcheki huyu jamaa hapa chini, huwezi kuamini kanizidi sana kwa unene

$(KGrHqR,!jYE-cm8By9PBPsJ!4LEe!~~60_35.JPG
 
Last edited by a moderator:
mi nilizoea mtu akisema maumbile ni tafsida ya deepstick a.k.a mlizo
Nirudi kwenye mada,usipende kunenepa walio wanene wanatamani kupungua,upende mwili wako kunywa maji meng kwa siku ili mwili umelemete
tatizo mke wangu analaumiwa sana na ndugu zangu, eti hanipi chakula na yeye hana amani kabisa
 
Julius amekaa Ikulu for 23 yrs hajawahi ever kuwa mnene, ama Kitambi !
Unadhani Maria hakua akimpa chakula ? Au alikua hajui makaangizo? Na akiwa (head of state) ungetegemea mwili wake uweje? Thn check aliyemfatia aliingia na body ya kawaida, lakini alimaliza muda wake akiwa kama Tembo.
 
tatizo mke wangu analaumiwa sana na ndugu zangu, eti hanipi chakula na yeye hana amani kabisa

mkubwa!nimegundua tatizo liko wap
Wewe ni mtu unaeishi kwa kusikiliza maneno ya watu,unaumizwa sana na majungu.nakushauri ishi utakavyo na si watu watakavyo,amini uyapangayo na si ndugu wakupangiayo,tumia kwa uwezo wako na si kwa kuwafurahisha ndugu.
 
Nimekuelewa mkuu, tatizo waifu ananung'unika mno!
 
Kama ni mrefu wastana no problem kama ni mfupi kazi kwako.next time weka jukwaa la mahusiano uzi wako,unaweka kwenye chit chat arhooo
 
Nimekuelewa mkuu, tatizo waifu ananung'unika mno!

wewe ndio wakumpa ujasiri shemeji,ukiwa jasiri na yeye atakua jasiri,ukiwa mwoga na yeye atakuwa mwoga,mabadiliko ya kweli huanzia kwako kisha kwa shemeji hadi kwa watoto.wote wanakuangalia wewe,wewe ndio kamanda wa kuongoza mapigano usiteteleke.ukimwambia shemeji kwamba hili HAKUNA TATIZO umaanishe na usimamie ulicho kisema,yaani shemeji akikuangalia kuanzia chini hadi juu na ndani ya moyo pate jibu kuwa mme wangu amemaanisha.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom