Indume Yene
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 2,950
- 711
Inabidi urekebishe heading yako maana wengine tunashindwa kuelewa kama unauliza swali toka kwa wana JF au unawakilisha mashaka yako kuhusu CHADEMA kukamata dola 2015.
Mimi ni mtanzania niliyeichoka CCM, na siamini kama kwelli watanzania tunataka maendeleo kuichekea CCM iendelee kushika hatamu ya nchi.
Kwa kuwa suala la CCM kuondoka madarakani ni lazima, sasa mbadala wake ni Chadema, chama ambacho kinaonesha matumaini makubwa kwa watanzania, chama kinachofumua mengi ambayo watanzania tulikuwa tumefumbwa macho na kutawaliwa kama mazezeta huku tukiambiwa nchi yetu ni maskini.
Bila shaka nina imani kubwa na Chadema katika kuikomboa nchi hii, na sina shaka kama si 2015 basi very soon Chadema kitachukua uongozi wa juu kabisa wa nchi , yaani uraisi na kuongoza nchi.
Tunapozungumzia haya ni Chadema kitatoa watendaji wote wakuu na muhimu pindi kitakaposhika madaraka ya nchi.
Yaani kuanzia
- mawaziri
- makatibu,
- wizara,
- Mabalozi
- wakuu wa idara mbalimbali,
- mahakimu,
- wakuu wa mikoa na wilaya.
na wengineo wengi kwa ukubwa wa serikali yetu, tokea wizara, kanda mikoa hadi wilaya.
Suala ambalo hula linanijia kichwani mara kwa mara ni KUPWAYA kwa Chadema katika kusimamisha serikari hiyo. Na kwa kuwa mimi hufikiria mbele zaidi na napenda sana kuwa realistic huwa naichukua Chadema namna hii na naitapanya katika serikali kwa ukubwa wake, kwa kweli naona inapwaya, Haswa ukuzingatia kwamba chama hakijajikita katika katika kurecruit wanachama katika ngazi zote za ukubwa wa nchi.
Chadema kinapwaya si kwa sababu hakina viongozi na wanachama makini na wachapakazi la hasha, Chama kina watu makini, (Kuanzia, Dr Slaa, Mbowe, Tundu Lisu, Zitto Kabwe, Halima Mdee, John Mnyika, Godbless Lema na wengineo wengi) la hasha bali viongozi hawa makini na wenye uwezo mkubwa hawatoshi kufit katika nyadhifa na idara zote na kutengeneza serikali yenye ufanisi na kasi moja. kimsingi kwa idadi yao wanapwaya.
Ukichukulia mfano tu ile kambi ya upinzani bungeni, inayoongozwa na Mbowe, mgawanyo wamawaziri kivuli katika wizara kivuli hizo ambao ndio unatoa picha ya nani atashika nafasi gani kama Chadema itashika madaraka, waliochaguliwa utagundua kabisa kuwa Chadema hakuna NGUVU KAZI YA KUTOSHA. Kuna wengi ambao ni makini lakini sio 'the best' we can get kwa ajili ya kusimamia maendeleo ya taifa kwa ukubwa wake.
Wako wanaoweza kuwa mawaziri na viongozi makini sehemu mbali mbali serikalini, kama Zitto Kabwe, Tundu Lissu, Mnyika kiasi, Mbowe, Mdee kiasi........kimsingi hata ninavyoitaja hii list unaona kabisa kwamba tunarun out of options.....nguvu kazi inayohitajika haitoshi. Iitakapokuja katika suala la kuteua Nguvu Kazi kwa ajili ya nyadhifa zote kwa ukubwa wake, naona Chadema inapwaya. Labda waje kutumia kujuana, kitu ambacho hakitaleta tija katika maendeleo (najua Chadema haitafanya hivyo).
Nadhani, Suala la kurecruit wanachama wapya linahitajika kufanyika, tena kila sehemu hadi vijijini, Chama kirecruit wachapakazi, wanachama makini, kitoe mafunzo na warsha mbalimbali ili kuinspire vijana wengi zaidi na kupata nguvu ya kutosha kuendesha nchi wakati utakapofikia. Bila hivyo kwa kweli naona Chadema kinapwaya jamani, hebu nyie wenyewe semeni.
Tunapozungumzia haya ni Chadema kitatoa watendaji wote wakuu na muhimu pindi kitakaposhika madaraka ya nchi.
Yaani kuanzia
- mawaziri
- makatibu,
- wizara,
- Mabalozi
- wakuu wa idara mbalimbali,
- mahakimu,
- wakuu wa mikoa na wilaya.
na wengineo wengi kwa ukubwa wa serikali yetu, tokea wizara, kanda mikoa hadi wilaya.
Licha ya kutokuwa na watu wa kuongoza , CHADEMA a.k.a. MAGWANDA watakuwa wanaiona nchi hii kama uchi wa mtoto. Kwani mtoto akiwa uchi utakuwa wamtizama tu na huna la kufanya
Matatizo yako ni madogo sana. Una tatizo la kuabudu baadhi ya binadamu wenzako. Hata mimi naweza kuwa waziri, sijui wewe.
Ndugu yangu hadi mahakimu wanatoka CDM! unajua kweli unachoongea? Mbona ni sawa na kusema CDM ikiingia madarakani itabadili mipaka ya nchi. Hadi leo hujui kuwa mahakimu hawafuati maelekezo ya chama chochote katika majukumu yao?
Inabidi urekebishe heading yako maana wengine tunashindwa kuelewa kama unauliza swali toka kwa wana JF au unawakilisha mashaka yako kuhusu CHADEMA kukamata dola 2015.
Umenena vyema mkuu, ukiwa na Rais makini, Makamu wake makini, Waziri mkuu makini, Mawaziri makini na wachapakazi, kinachofuata ni kuweka utawala bora katika mikoa, wilaya na hata vijiji.Wanaosikika Chadema ni wachache lakini ndani ya Chadema kuna hazina kubwa sana ya viongozi bora, pia kuna wanachama na nje ya chama lakini kuna watu wenye mapenzi mema na nchi hii.Mfumo uliopo ndio unaoharibu nchi kukumbatia kwamba kila kiongozi lazima atoke ccm, hata kama kuna kiongozi mzuri kwa nafasi ya uwaziri laki hatoki ccm basi hapewi, who knows bwana kama Chadema ikikamata nchi inawezekana akina magufuli wakarudishwa kwenye uwaziri na wakajirekebisha walipo jikwaa na kuwatumikia watanzania, so hofu ondoa ndugu.
ushauri ameshautoa!!!
Kumbuka hivyo vichwa vichache vya chadema ulivyovitaja ni sawa na Baraza zima la jk. Ndo maana jk anahitaji mawaziri 60 kuunda serikali wakati chadema wanahitaji wasiozidi 20. Kukuondoa wasiwasi, mwaka 2015 tutakapounda serikali, wabunge wa Chama Tawala (CDM) watakua zaidi ya theluthi mbili ya wabunge wote. Maandalizi yameshaanza. Kumbuka, kabla ya uchakachuaji wa mwaka jana kulikua na wabunge 112 wa cdm walioshinda. Hali hiyo hatutairuhusu tena kaka.
Revolutionary,
Una hoja ya Msingi,watu kama ninyi mnasaidia sana katika kuimarisha upinzani hasa mnapo-expose doubt zenu ili kama kuna ukweli zifanyiwe kazi.
Chadema ni ni chama makini ni lazima kitumie jitihada zote kuhakikisha kwamba watanzania hawatakuwa na wasiwasi kama wakitupa ridhaa ya kuongoza.
Ila hapo kwenye suala la kupata watu wa kuongoza ni kwamba si lazima tufuate mfumo kama huu uliopo,inawezekana kiongozi mzuri aliye CCM akawa ndani yua serikali ya Chadema,CUF,NCCR n.k.Ni lazima tukomae katika hili.Kitakachowaongoza watu hawa kutoka vyama tofauti but the best brains ni sera na leadership values zitakazowekwa na Chadema.Uliona kule United States,Obama(Democrats) alimwacha Robert Gates waziri wa Ulinzi wa serikali ya Bush(Republican Party) katika portfolio yake kwa maslahi ya taifa.Kinachohitajika ni leadership values and commitment to the laid principles and values na uwezo wa chama na uongozi wa juu kufanya coordination and monitoring of Government machinery.
Hata hivyo,ukweli ni kwamba Chadema tunahitaji kujipanga zaidi ya hapa.Tuendelee kushirikiana,chaguzi zetu za ndani tutakazofanya kuanzia sasa tutakuwa tunafanya chaguzi zitakazotoa Taswira ya outcome ya general election 2015.Ni jukumu na wajibu wa Chadema kuhakikisha viongozi wote watakaochaguliwa wataongeza kasi ,na kurahisisha harakati za kuchukua dola.Uchaguzi wa ndani wa 2013 utakuwa ni uchaguzi pacha,yaani ni sawa na kupiga kura kwa ajili ya matokeo ya 2013 na kwa ajili ya matokeo ya uchaguzi mkuu 2015 yatakayoamua position yetu na Tumaini la watanzania kupata mabadiliko kupitia chama makini cha Upinzani
So,Watanzania waendelee kukiunga mkono Chadema kwa nguvu zote,tusaidiane kulikomboa Taifa Letu.Mjadala unaondelea sasa kuhusu kulazimishana posho na kutumia vitisho ni dhahiri kwamba sasa Watanzania wamejua ni chama gani na ni akina nani hasa wenye dhamira ya dhati katika kuwapigania,kuwajali na hasa wanyonge walio wengi
By the time they see us, they will know that something is happening in Tanzania and that people are ready for change. Let us never doubt what we can achieve if we work together. The time has come for change in Tanzania and we are the apostles of that change.We are asking Tanzanians to give us the opportunity to lead the country. If one party (Chama Cha Maapinduzi) has failed the nation, there are other Serious parties
jamaaa unaandika usichokijua, wewe nani alikwambia 2015 lazima cdm ichukue madaraka