Nina mashaka na uwezo wa CHADEMA kuongoza SERIKALI 2015

Kaka cjaona hoja hapa! Subir 2takapochukua nchi ndio utaona kama kuna watendaji au hakuna na ucpende kuishi kwa hisia
 
Mkuu ni hivi, tuanze na kwenye uwaziri, ni wazi kwamba Chadema has limited options, wapo wachapakazi hawa tunaowajua kila leo,lakini kimsingi hawatoshi, angalia mfano tu wa baraza kivuli kule bungeni, kama ingekua ni kuformulate a full government nakosa watu wa kuwaongezea watoshe nyadhifa zote za kisiasa serikalini..... Pia ni mabadiliko makubwa yanayotakiwa hata kwenye idara zisizo za kisiasa serikalini, so unataka kunambia bila kujua a potential number of candidates watu ambao KIMSINGI wanaweza kuwa wanachama wa Chadema, kwani ni maamuzi yao, na wakaenda kutekeleza kazi za kiserikali bila tatizo.

hujafafanua ni idara zipi ambazo unataka wakuu wake wawe wanachama wa chadema? mashirika, makampuni, taasisi za umma au?
 
Mtoa mada kumbuka kuwa ukitoa mawaziri ambao. Ni lazima wawe wabunge kwa ticket ya chama fulani, makatibu wakuu,wakuu wa mikoa na wakuu wa idara mbalimbali hawatakiwi kuwa na itikati za vyama....imekuwa hivyo sbb ya mfumo mbove tulio nao...na kumbuka chini ya serikali ya CDM wakuu wa wilaya watafutwa...so huhitaji kuogopa, tujipange kwa ajili ya kuisuport CDM 2015 maana ndilo tumaini pekee lililobaki

Umenena vyema mkuu, ukiwa na Rais makini, Makamu wake makini, Waziri mkuu makini, Mawaziri makini na wachapakazi, kinachofuata ni kuweka utawala bora katika mikoa, wilaya na hata vijiji.

Wanaosikika Chadema ni wachache lakini ndani ya Chadema kuna hazina kubwa sana ya viongozi bora, pia kuna wanachama na nje ya chama lakini kuna watu wenye mapenzi mema na nchi hii.

Mfumo uliopo ndio unaoharibu nchi kukumbatia kwamba kila kiongozi lazima atoke ccm, hata kama kuna kiongozi mzuri kwa nafasi ya uwaziri laki hatoki ccm basi hapewi, who knows bwana kama Chadema ikikamata nchi inawezekana akina magufuli wakarudishwa kwenye uwaziri na wakajirekebisha walipo jikwaa na kuwatumikia watanzania, so hofu ondoa ndugu.
 
Ninawasiwasi hata kama umesoma sio tu kuelewa nilichokiandika, waliosoma wameelewa, muulize Mukandara. Na usikurupuke siishi kwa hisia, ila I am a realist, naexplore all the options, I think divegently.....tofauti yetu nadhani unategemea kudra za mwenezi Mungu!

Kaka cjaona hoja hapa! Subir 2takapochukua nchi ndio utaona kama kuna watendaji au hakuna na ucpende kuishi kwa hisia
 
Hii thread Kivuli na ina mawazo kivuli, ngoja wananchi vivuli wachangie mawazo vivuli.
 
Kwanza Serikali inaundwa na wanasiasa (mawaziri) na wataalamu (professionals) kV makatibu wakuu (watendaji wakuu wa wizara), wanasheria/mahakimu/judges n.k. Kumbuka hwa hawatakiwi kijiuhusisha na siasa na akitaka kufanya hivyo inabidi ajihuzuru.

Pili watendaji wengi serikalini ni bendera fuata upepo utendaji wao unategemea aliye juu ya yao. Kukosekana kwa uwajibikaji kunatokana na mfumo uliopo ambao chanzo chake ni katiba ya sasa inayompa madarka makubwa rais kuteuwa karibu watendaji wakuu wote wa serikali; hivyo rais na chama chake wakiwa wepesi serikali nzima inakuwa nyepesi na kinyume chake ni sahihi.

Suluhisho ni:
1. Katiba mpya yenye kuzingatia hayo yote
2. Rais makini kama Dr. W.Slaa mwenye kutenda kama asemavyo (Walk the talk)
3. Chama makini chenye uwezo wa kumkemea rais na serikali aliyoiunda.

Kwa ujumla wake watendaji wengi ni hawa hawa watanzania waliokosa viongozi ila wana watawala.
 
Nakubaliana na wewe, lakini je hiyo inamaanisha Chadema mtachagua watu waliopo sasa katika nyadhifa au, hao watu Chadema itakao chagua watatoka wapi? ni akina nani? nataka tufikirie hivyo!

Sikatai Chadema ina hadhina kubwa, hazina ipi hiyo? hebu kuwa straight to the point! çause najua Chadema bado haijaexploit hazina kubwa sana. Hao wanaosikika wenyewe hawatoshi, hebu angalia serikalini kuna Nyadhifa ngapi halafu, hao unaowaita wanasikika wapange wote utaona kama wanajaa hawajaii?

Umenena vyema mkuu, ukiwa na Rais makini, Makamu wake makini, Waziri mkuu makini, Mawaziri makini na wachapakazi, kinachofuata ni kuweka utawala bora katika mikoa, wilaya na hata vijiji.

Wanaosikika Chadema ni wachache lakini ndani ya Chadema kuna hazina kubwa sana ya viongozi bora, pia kuna wanachama na nje ya chama lakini kuna watu wenye mapenzi mema na nchi hii.

Mfumo uliopo ndio unaoharibu nchi kukumbatia kwamba kila kiongozi lazima atoke ccm, hata kama kuna kiongozi mzuri kwa nafasi ya uwaziri laki hatoki ccm basi hapewi, who knows bwana kama Chadema ikikamata nchi inawezekana akina magufuli wakarudishwa kwenye uwaziri na wakajirekebisha walipo jikwaa na kuwatumikia watanzania, so hofu ondoa ndugu.
 
Tunapozungumzia haya ni Chadema kitatoa watendaji wote wakuu na muhimu pindi kitakaposhika madaraka ya nchi.
Yaani kuanzia
- mawaziri
- makatibu,
- wizara,
- Mabalozi
- wakuu wa idara mbalimbali,
- mahakimu,
- wakuu wa mikoa na wilaya.
na wengineo wengi kwa ukubwa wa serikali yetu, tokea wizara, kanda mikoa hadi wilaya.
Nadhani kosa lako ni kuangalia mfumo wa uongozi wa CCM na kutaka CHADEMA nayo iufuate huo huo. Mfumo wa CCM una ukiritimba mkubwa sana ambao pamoja na mambo mengine umejengwa kwenye msingi wa uswahiba. Hivyo rais anafungua nafasi nyingi za uongozi ili azigawe kwa maswahiba wake.

Kimsingi wa utawala wa kidemokrasi, Makatibu wakuu, wakurugenzi, makamishna, wakuu wa maidara, na mahakimu ni watu ambao hawatakawi kuwa wanachama wa chama chochote bali ni watendaji wanaaoteuliwa kutokana na uwezo wao wala siyo kwa ushabiki wao. Kwa hiyo CHADEMA ina haki ya kumweka mtu yeyote mwenye uwezo bila kuangalia itikadi yake, na kama akiingiza siasa katika kazi basi anafukuzwa.

Kuhusu mawaziri, wanatakiwa wasiwe wabunge, bali wateuliwe kulingana na uwezo wao. Na hata kama ni lazima wawe wabunge, bado hilo halihindikani kama CDAM ikiing'a CCM madarakani basi itakuwa na wabunge wengi hasa ukizingatia kuwa CDM isingependa kuunda serikali kubwa ya CCM.

Swala la wakuu wa miko na wa wilaya kuteuliwa na rais ni kubinya demokrasi huko mikoani. Nafahamu kuwa mojawapoa ya melengo ya CDM ni kubadili vyeo hivi ili wakuu wa mikoa (au majimbo) wawe wanachaguliwa na wanachi huko huko mikoani.
 
Najua unajua kwamba serikali ni kitu kimoja, na ingawa haitakiwi kuteua wanachama kuwa viongozi, lakini lazima uteue watu with the like mindset, wanaojua Tanzania inahitaji nini, yawezekana si wanachama lakini wanaamini katika kile wanachoamini Chadema, katika kulinda maadili ya kazi na uwajibikaji, hawa watu unawatoa wapi Tanzania (ukiondoa wale wateule wa serikali ya CCM ambao siamini kama watatupeleka popote) kama si kuwarecruit in some sense! au tayari kuna program hii, tujuzeni watu wa ndani ya Chadema!

Revolutionar
Wajua kuwa hao wote unaosema ni watendaji katika serikali na jua kitu kimoja serikali sio CCM au CDM tu serikali ni yawote na wale walioko sasa wanaweza endelea wako wengi wenye uchungu na nchi hii. ila wafanyeje wakati wanapelekwa ila siku utakapo sikia CDM imeshika dola utajua kuwa CDM wako wengi na wengio walikuwa wanataka mabadiliko kaka. usijali ni sehemu ya mipango na hakika kila kitu kitakuwa sawa
 
Mimi ni mtanzania niliyeichoka CCM, na siamini kama kwelli watanzania tunataka maendeleo kuichekea CCM iendelee kushika hatamu ya nchi.

Kwa kuwa suala la CCM kuondoka madarakani ni lazima, sasa mbadala wake ni Chadema, chama ambacho kinaonesha matumaini makubwa kwa watanzania, chama kinachofumua mengi ambayo watanzania tulikuwa tumefumbwa macho na kutawaliwa kama mazezeta huku tukiambiwa nchi yetu ni maskini.

Bila shaka nina imani kubwa na Chadema katika kuikomboa nchi hii, na sina shaka kama si 2015 basi very soon Chadema kitachukua uongozi wa juu kabisa wa nchi , yaani uraisi na kuongoza nchi.

Tunapozungumzia haya ni Chadema kitatoa watendaji wote wakuu na muhimu pindi kitakaposhika madaraka ya nchi.
Yaani kuanzia
- mawaziri
- makatibu,
- wizara,
- Mabalozi
- wakuu wa idara mbalimbali,
- mahakimu,
- wakuu wa mikoa na wilaya.
na wengineo wengi kwa ukubwa wa serikali yetu, tokea wizara, kanda mikoa hadi wilaya.

Suala ambalo hula linanijia kichwani mara kwa mara ni KUPWAYA kwa Chadema katika kusimamisha serikari hiyo. Na kwa kuwa mimi hufikiria mbele zaidi na napenda sana kuwa realistic huwa naichukua Chadema namna hii na naitapanya katika serikali kwa ukubwa wake, kwa kweli naona inapwaya, Haswa ukuzingatia kwamba chama hakijajikita katika katika kurecruit wanachama katika ngazi zote za ukubwa wa nchi.

Chadema kinapwaya si kwa sababu hakina viongozi na wanachama makini na wachapakazi la hasha, Chama kina watu makini, (Kuanzia, Dr Slaa, Mbowe, Tundu Lisu, Zitto Kabwe, Halima Mdee, John Mnyika, Godbless Lema na wengineo wengi) la hasha bali viongozi hawa makini na wenye uwezo mkubwa hawatoshi kufit katika nyadhifa na idara zote na kutengeneza serikali yenye ufanisi na kasi moja. kimsingi kwa idadi yao wanapwaya.

Ukichukulia mfano tu ile kambi ya upinzani bungeni, inayoongozwa na Mbowe, mgawanyo wamawaziri kivuli katika wizara kivuli hizo ambao ndio unatoa picha ya nani atashika nafasi gani kama Chadema itashika madaraka, waliochaguliwa utagundua kabisa kuwa Chadema hakuna NGUVU KAZI YA KUTOSHA. Kuna wengi ambao ni makini lakini sio 'the best' we can get kwa ajili ya kusimamia maendeleo ya taifa kwa ukubwa wake.

Wako wanaoweza kuwa mawaziri na viongozi makini sehemu mbali mbali serikalini, kama Zitto Kabwe, Tundu Lissu, Mnyika kiasi, Mbowe, Mdee kiasi........kimsingi hata ninavyoitaja hii list unaona kabisa kwamba tunarun out of options.....nguvu kazi inayohitajika haitoshi. Iitakapokuja katika suala la kuteua Nguvu Kazi kwa ajili ya nyadhifa zote kwa ukubwa wake, naona Chadema inapwaya. Labda waje kutumia kujuana, kitu ambacho hakitaleta tija katika maendeleo (najua Chadema haitafanya hivyo).

Nadhani, Suala la kurecruit wanachama wapya linahitajika kufanyika, tena kila sehemu hadi vijijini, Chama kirecruit wachapakazi, wanachama makini, kitoe mafunzo na warsha mbalimbali ili kuinspire vijana wengi zaidi na kupata nguvu ya kutosha kuendesha nchi wakati utakapofikia. Bila hivyo kwa kweli naona Chadema kinapwaya jamani, hebu nyie wenyewe semeni.

Licha ya kutokuwa na watu wa kuongoza , CHADEMA a.k.a. MAGWANDA watakuwa wanaiona nchi hii kama uchi wa mtoto. Kwani mtoto akiwa uchi utakuwa wamtizama tu na huna la kufanya
 
Nakubaliana na wewe, lakini je hiyo inamaanisha Chadema mtachagua watu waliopo sasa katika nyadhifa au, hao watu Chadema itakao chagua watatoka wapi? ni akina nani? nataka tufikirie hivyo!

Sikatai Chadema ina hadhina kubwa, hazina ipi hiyo? hebu kuwa straight to the point! çause najua Chadema bado haijaexploit hazina kubwa sana. Hao wanaosikika wenyewe hawatoshi, hebu angalia serikalini kuna Nyadhifa ngapi halafu, hao unaowaita wanasikika wapange wote utaona kama wanajaa hawajaii?

Inaelekea bado hujafahamu nini maana ya serikali, kuna watu wamekueleza hapa, Chadema haitakuja kufumua uongozi wote katika nchi, yaani fukuza, RC wote, DCs wote, Makatibu, wakurugenzi, wakuu wa mashirika na taasisi mbali mbali, la hasha.

Ukiona wamechukua nchi Rais ametoka chadema wao wanaanza kusimamia sera zao, wanaunda baraza la mawaziri, wanateua wakuu wa ulinzi na usalama wapya na watakao tii mamlaka iliyopo, then watangalia RC na DCs (tena hapa kuna watu wengine hata hatatakiwa kuwepo, why DC wakati una Mkurugenzi and why RC wakati kuna RAC) wanachapa kazi wataendelea wazembe tupilia mbali kwa hiyo ndugu hata wewe pia ni kiongozi lakini pengine hujapewa nafasi na mfumo uliopo kwa kuwa wewe sio miongoni mwao, hupendi sera zao.

cha Muhimu kama kweli wewe unapenda mabadiliko kuanzia moyoni kwako saidia Chadema kushika Dolla na utashuhudia makubwa.
 
NDG SIO WOOTE WALIo CHAMA CHA MAGAMBA WANA MAGAMBA HIVYO KUNA WATENDAJI WENGI TU WAZURI LAKINI WAMEKOSA DIRA NDO MAANA MHESHIMIWA DR.(PHd) alisema kama unakumbuka angeshinda(alishinda ila mzee wa kaya alichakachua tunalijua hilo hata makame shahidi)angeandaa kitu kama semina ya kurudisha uadirifu kazini
 
2. Rais makini kama Dr. W.Slaa mwenye kutenda kama asemavyo (Walk the talk)
.

Dr.Slaa kutembea kwenye yale ayasemayo??a u serious?

....kitendo cha Dr.Slaa kuupinga mshahara wa Wabunge na baadae kuomba kulipwa mshahara unaoendana na wa Mbunge kimemuondolea sifa ya kutembea kwenye maneno yake, amebaki tu kuwa kama opportunists wengine wanaoongea pasi kutembea kwenye gharama za maneno yao....
 
Mkuu hoja yako imejikita kwenye idadi ya waliopo bungeni tu na viongozi wa Chama. You are missing the point. Naungana na aliyekupa mfano wa Nyerere wakati wa uhuru, Kagame, Museveni na wengine wengi. System haiendeshwi kwa njia hiyo tu unayofikiri wewe. Hao wachache ni usukani tu. Lakini utashangaa wako wengi sana ambao baada ya ushindi huo wa CDM, watateuliwa na hata kupatikana na kuweza kuendesha nchi. Nchi hii ni kubwa mno, lakini zipo pia system za nchi eg intelligence etc,kuhakikisha nchi inaendelea, provided ni chama gani kitashika nchi. Angalia nchi zingine ambazo zimekuwa zikifanya uchaguzi wa kidemokrasia na ikawepo smooth transition of power, mfano Ghana n.k. Widen your scope of thinking!
 
Hilo halina ubishi ndio maana yeye hivi sasa ni rais kivuli

Yaani akili za watu wa MAGWANDA ni chache mno kiasi cha kwamba unashangaa hivi kama chenyewe kina watu wa namna hii basi wote wanahitajika kufika hospitali kupimwa
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom