Nina mashaka na Gazeti Pendwa la Mwananchi.

Ndibalema

JF-Expert Member
Apr 26, 2008
10,956
4,647

Kumradhi Waziri Membe

MWANANCHI. Monday, 23 July 2012 21:00
Katika gazeti hili la tarehe 12/01/2011 tulichapisha habari yenye kichwa. Membe: Polisi walikiuka Maadili (Mabalozi waibana Serikali, wahoji polisi kutumia risasi za moto).

Habari hiyo ambayo ilifuatia tukio la vifo vya watu watatu na majeruhi kadhaa vilivyotokea mjini Arusha wakati polisi walipokabiliana na waandamanaji wa Chadema, ilidai kwamba Waziri Membe alililaumu jeshi la polisi kwa kukiuka maadili, kuvuka mipaka yake na kusababisha mauaji hayo ambayo yalitia doa Tanzania.

Aidha habari hiyo iliendelea kudai kwamba mabalozi wa nchi mbalimbali walimbana wakitaka tamko la Serikali juu ya tukio hilo.

Baada ya uchunguzi wa kina, gazeti hili limebaini kuwa, Waziri Membe hakusema maneno hayo na wala hapakuwa na mvutano wala madai yeyote ya Mabalozi juu ya jambo hilo.

Kutokana na hayo, tunachukua fursa hii kumwomba radhi Waziri Membe, Jeshi la Polisi, Serikali, Mabalozi wote na Wananchi kwa ujumla.

Aidha tunapenda kumhakikishia Waziri Membe na wasomaji wote kwa ujumla kwamba habari hii iliandikwa kwa bahati mbaya na kwamba gazeti hili litaendelea kufanya kazi yake kwa kufuata misingi ya Taaluma ya uandishi wa habari, Maadili na sheria za nchi bila kumwonea mtu au kushinikizwa na mtu yoyote kwa maslahi binafsi.
Mhariri

My take: Napata mashaka sana na umakini wa gazeti hili. Inawezekana vipi habari kama hiyo ichapishwe kimakosa?
Ikumbukwe kuwa Ni jana tu Mbunge wa Arumeru mashariki Joshua Nasari na yeye amelilalamikia gazeti hili la Mwananchi kuwa wameandika habari ya uongo juu ya ya kauli yake (Nasari) kuhusu Zitto na urais 2015
 
Dah, wamenikumbusha machungu ya udhalimu wa chama tawala.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Hata mimi nashangaa, wamewezaje kukumbuka na kuomba msamaha kwa habari ya karibia mwaka na nusu ! au wanahisi Membe anaweza kuukwaa uraisi!! na wameanza kujirudi!
 
Unaambiwa 'kambi za uraisi' ccm wamepatana, hizi media zetu wote waganga njaa, tunangojea kuona msimamo wa RaiaMwema.
 
Utaratibu huu utaendelea. Wanakuchafua - then wanauza gazeti. Harafu wanaomba radhi - na kuuza gazeti tena.
 
Halafu nimekumbuka kitu hawa jamaa c wanaongozwa na Tido mabaye anasubiri EL aingie madarakani ili arudi TBC kwa hiyo walikuwa katika vita ya kummaliza Membe mapema!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom