Nina kamtoko, lakini...!

platozoom

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
9,364
11,150
Mtoko wenyewe wa kawaida lakini hayo maandalizi ya huyu bi mdada balaa. Kuanzia saa 6 mpaka sasa anajiandaa. Ingekuwa ni mara ya kwanza ningesema ni sawa..............Lakini ni mtu wangu yapata mwezi sasa.

Hapa nilipo nilimaliza shughuli zangu tokea saa 5 kwa ahadi ya kukutana mida ya saa 6 ili tupige lunch kabisa na baadaye jioni tushangaeshangae maghorofa mjini.......akapiga simu akasema yuko bado salon anajiweka sawa kwa hiyo hata hiyo lunch tutapiga saa 8, lakini sasa inaelekea saa 10 halafu anasema "usijali dear ndio nimemaliza nakuja.....khaa".

Nimechoka na nimemwambia mtoko umefutwa ili ajifunze......maana hii ni mara ya pili anaunguza muda wangu! Sijataka kujua reaction yake.

Sijui niko sahihi au hasira tuu!
 
sasa kama amestukia kuwa unataka kumpa sapraiz ya pete ya uchumba unataka asijiandae? Wacha ajipambe ili upate heshima mjini.Ni kawaida mkuu kwa dada zetu hata usipanick baadae mfundishe kuwa time ni mtaji popote!
 
Jamani umekosea sana kufuta huo mtoko.. Napata picha ndio ingekuwa mie.. Duh ningenunaje! Maandalizi yote hayo halafu holaaaaaa...! Wee ungemvumilia tuu kwa leo halafu wakati wa maongezi ndio ungemwambia kuwa ni muhimu kwenda na muda, angekuelewa tuu mkuu..!

Mmmmmh... Kama ameweka na kope za kubandika ili atokelezee imekula kwake..Lol
 
Inaudhi sana masaa 5 na bora angesema mapema kuwa atachelewa. Picha niliyopata ni kama hajali hivi.
 
Itabidi hayo tuyaongee wakati mwingine........sasa hivi mind yangu imeishiwa hamu kabisa
 
Mpigie simu bana, umwambie walau muonane jioni..! Yaani mwenzio kakesha anachagua mpalo wa kutokelezea nao kwenye mtoko na wewe halafu kirahisi rahisi tuu unaghairisha..! Dah....! Yaani hapa nampatia picha jinsi atakavyokuwa amesikitika..!

Wadada ndivyo tulivyo jamani... Mtuzoeage tuu na kuturekebisha taratibu sio kutuadhibu namna hiyo..!
 
Inaudhi sana masaa 5 na bora angesema mapema kuwa atachelewa. Picha niliyopata ni kama hajali hivi.
Mi naamini unampenda na ndiyo maana unaona anapochelewa inakuuma,sasa kwa kuwa anachelewa mpe nafasi mkuu,polepole ndio mwendo.Akija fanyeni mlopanga kuyafanya mkimaliza ongea nae taratibu kwa kumuelewesha kuonesha kwamba hali hiyo inakukera sana na usingependelea lijirudie wakati mwingine.
Tambua pia bado yupo kwao kama si kwa wazazi basi walezi so yawezekana anataka kufanya timing awe amekamilisha mambo fulani fulani.Ili aweze kuwa mkeo mwenye sifa uzitakazo tumia pia muda wako kumfunza mambo mazuri ulonayo nawe pia jifunze mazuri yake.ILi kudumu lazimu mvumiliane!
 
Uliyosema sahihi, lakini kumpigia simu sasa hivi itakuwa kama nimeweka msimamo wangu rehani
 
Mpigie simu bana, umwambie walau muonane jioni..! Yaani mwenzio kakesha anachagua mpalo wa kutokelezea nao kwenye mtoko na wewe halafu kirahisi rahisi tuu unaghairisha..! Dah....! Yaani hapa nampatia picha jinsi atakavyokuwa amesikitika..!

Wadada ndivyo tulivyo jamani... Mtuzoeage tuu na kuturekebisha taratibu sio kutuadhibu namna hiyo..!

Kiswahili kigumu wenzangu!!, Hapo kwenye nyekundu sielewi, naona kama TUSI!!
 
Sipati picha shosti kanunajeeeeeee! Ndivyo alivyo hajui kutunza muda bt mchukulie alivyo na kamwe usitegemee kumbadili, its how she is!!
 
Shida ya M-bongo n kwamba kupanga mtoko tayari keshapanga na kum-do mtoto wa watu. Sasa akiona muda unaenda anaona atalipia eneo la tukio bila kupata maximum enjoyment.
 
Hao ndo wanawake mzee wangu alipenda sana kusema ukitaka kutoka na mwanamke kama safari ni saa moja mwambie unaondoka saa 12 kasoro.. Hapo mtachelewa lakini sio sana..
 
Wala siyo lengo langu na kama kuwa naye ni zaidi ya mwezi sasa. Leo ilikuwa ni siku ya kusafisha macho mjini basi
 
Hao ndo wanawake mzee wangu alipenda sana kusema ukitaka kutoka na mwanamke kama safari ni saa moja mwambie unaondoka saa 12 kasoro.. Hapo mtachelewa lakini sio sana..

Hata mimi nili-expect atachelewa lakini si kwa kiasi hiki.
 
Kumbe huwa unasusaga? Haipendezi hiyo mwanaume mzima. Halafu mtoko gani wa Monday!
 
Back
Top Bottom