Nina bifu na admin

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,136
4,292
NA BIFU NA ADIMINI.

1)nione sina adabu,ukweli nikuambie.
Niseme kilo nisibu,upende na uchukie
Acha nipige ulabu,na haya inikimbie.
Na bifu na adinimi,natamani nikuteke.

2)ni mbaya yako tabia,niseme usizuie.
Hivi ulishatubia,shetani akukimbie.
Ona unavyochukia,wataka nikuchunie.
Na bifu na adimini,matamani nikuteke.

3)kisa kundi li ni lako,basi chako siyo chake.
Kundi halina mashiko,kama kaa la mashuke
Adimini ka tambiko,si ni bora uondoke.
Na bifu na adimini,natamani nikuteke.

4)kazi kututoa toa,lini nawe uondoke.
Wengi wetu twachukia,hatutaki turopoke.
Hapa tulipo fikia,twatamani uanguke.
Na bifu na adimini,natamani nikuteke.

5)adimini ka mganga,nyota yako si mashuke.
Roho mbaya ka kipanga,kama bomu ulipuke.
Hivi unakula unga,kama teja la temeke.
Na bifu na adimini,natamani nikuteke.

Shairi=NA BIFU NA ADIMINI.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Aruaha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.coa
 
NA BIFU NA ADIMINI.

1)nione sina adabu,ukweli nikuambie.
Niseme kilo nisibu,upende na uchukie
Acha nipige ulabu,na haya inikimbie.
Na bifu na adinimi,natamani nikuteke.

2)ni mbaya yako tabia,niseme usizuie.
Hivi ulishatubia,shetani akukimbie.
Ona unavyochukia,wataka nikuchunie.
Na bifu na adimini,matamani nikuteke.

3)kisa kundi li ni lako,basi chako siyo chake.
Kundi halina mashiko,kama kaa la mashuke
Adimini ka tambiko,si ni bora uondoke.
Na bifu na adimini,natamani nikuteke.

4)kazi kututoa toa,lini nawe uondoke.
Wengi wetu twachukia,hatutaki turopoke.
Hapa tulipo fikia,twatamani uanguke.
Na bifu na adimini,natamani nikuteke.

5)adimini ka mganga,nyota yako si mashuke.
Roho mbaya ka kipanga,kama bomu ulipuke.
Hivi unakula unga,kama teja la temeke.
Na bifu na adimini,natamani nikuteke.

Shairi=NA BIFU NA ADIMINI.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Aruaha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.coa
Mkuu aruoha ndo wapi!!
Na hiyo gmail .coa ndo mtandao gani!!
 
Jicho limekutoka,hebu nihurumie
maneno yakutoka,kama whatsap umetengeneza wewe
nipishe nifanye yangu,yako nimekuachia

group nimetengeneza mie,yanini uingilie..?
weka pozi,upate konzi
mi mdonzi,nakupa dozi
usilete upuuzi,mb nanunua mwenyewe

sorry leo weekend niko dug!!:eek::eek::eek::eek:
 
we kaka jikatae,ukisemacho ni pumba.
admin umeongelee,amekuibia mchumba?
naomba usiendelee,nitakunyonga kwa kamba.
na nguvu zikulegee,ivi una undugu na lipumba?
 
we kaka jikatae,ukisemacho ni pumba.
admin umeongelee,amekuibia mchumba?
naomba usiendelee,nitakunyonga kwa kamba.
na nguvu zikulegee,ivi una undugu na lipumba?
adimini unalia,kisa vocha za mkopo.
ubabe watuletea,ukipaa kama popo.
mchana watuchekea,kisa umetoka depo.
hivi umesema nani,sinaga undugu nae.
 
Jicho limekutoka,hebu nihurumie
maneno yakutoka,kama whatsap umetengeneza wewe
nipishe nifanye yangu,yako nimekuachia

group nimetengeneza mie,yanini uingilie..?
weka pozi,upate konzi
mi mdonzi,nakupa dozi
usilete upuuzi,mb nanunua mwenyewe

sorry leo weekend niko dug!!:eek::eek::eek::eek:
nilijua utasema,kisa group ni lako.
ungetwambia mapema,tukuache peke yako.
group lako ni chama,chetu wala siyo chako.
adimini acha hizo,ubabe wala hufai.
 
adimini unalia,kisa vocha za mkopo.
ubabe watuletea,ukipaa kama popo.
mchana watuchekea,kisa umetoka depo.
hivi umesema nani,sinaga undugu nae.
nahisi una kichaa,we ni mmoja wa wanne.
we Idd nakushangaa,tabia zako ka' za mwanne.
mdomo unaukunjua,kisa admin umnene.
ukileta za kuleta,nitakuondoa kundini.
 
nahisi una kichaa,we ni mmoja wa wanne.
we Idd nakushangaa,tabia zako ka' za mwanne.
mdomo unaukunjua,kisa admin umnene.
ukileta za kuleta,nitakuondoa kundini.
kama mambo ndiyo hivyo,basi bora nitulie.
 
kama mambo ndiyo hivyo,basi bora nitulie.
na utulie kweli,usirudie upuuzi.
nitakupaka pilipili,hadi utokwe na mashuzi.
najua huna akili,wewe ni zaidi ya mpuuzi.
admin nina hasira,nitakutoa kundini.
 
nilijua utasema,kisa group ni lako.
ungetwambia mapema,tukuache peke yako.
group lako ni chama,chetu wala siyo chako.
adimini acha hizo,ubabe wala hufai.
Hapa kazi tu,nakufunza chuo kikuu
peke yako walalama,unashindwa na kina mama..?
mikono juu chutama,kama hutaki hama!

tuache wajuvi tujilipue,we mpuuzi tusikujue
moto umeuwasha,wacha ukulipue
kicheko si chako,mapengo halali yako!
kundi si lako,yanini ujishebedue..?
mwaka huu utahama,nakukimbia kama ndama
naona unaisoma,mpaka unaumwa homa
hapa umefika,lazima utikise kichwa

shabab ndo mie,kwanini nisijisikie..?
admin wao ndie mie,
wacha nijivunie
misifa wanimwagie,mchele nijilie

mwiba nakuchoma,siku nyengine usirudie
rudi kwenu dodoma,huku mjini tuachie
nakuona unavyohema,nyangema nacheka mie
 
Wewe wachokonoe tu,
Utapigwa Ban Takatifu...
Shauri yako
huyu ni mwehu,'tapigwa ban takatifu.
hili ni safina la Nuhu,linabeba hadi siafu.
mjinga aliyekubuhu,anapenda sana bifu.
admin nina hasira,nitamuondoa kundini.
 
Kundini nakuadi, matusi unakoleza
Baadae nkikutoa, adimini ni mbaya
Mapovu mnatupa, nidhamu pembeni
Nchi ni ya viwanda, hatupendi ujinga.
 
Kundini nakuadi, matusi unakoleza
Baadae nkikutoa, adimini ni mbaya
Mapovu mnatupa, nidhamu pembeni
Nchi ni ya viwanda, hatupendi ujinga.
unataka tuogope,na tuache kukusema.
na sisi tule viepe,wewe minofu na nyama.
admin acha mapepe,hi si ya kibabe zama.
eti Trump ni nduguyo,mbona mwafanana sura ?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom