Nimuoe yupi kati ya watatu hawa?

Wewe bado unasoma na huyo wa daploma bado yupo shula wengne achana nao utawapotezea muda mabinti bure.acha ulaghai kijana
 
yaani umeingia humu uchaguliwe mke au iyo nayo ni kama kampuni inayohitaji shareholders.
 
Unakopa, unajikopa bila kujua. Hivyo v2 wanavyokuhonga hao wadada ipo ck utakuja kuvilipa either direct or indirect! Uwe kakini
 
Mmoja amegraduate Udom mwaka huu,ananisisitiza sana nimuoe kwani tayari ameniona nafaa kua mumewe.

Wa pili anachukua diploma ya ualimu mwaka wa kwanza,huyu tayari amewajulisha wazazi wake kua tayari amepata mchumba na si siku nyingi amewahidi kunipeleka kwa utambulisho.

Mwingine na watatu,ni darasa la saba ila ni mfanyabiashara,hapendi kuona mimi napata taabu pale ninapokua na tatizo na hujitahidi kunitumia pesa kama hivi nilivyo hapa chuoni.

Nisaidieni kimawazo,kwani wote pia wanaupendo wa dhati pamoaja nami.Kwa mfano:aliopo diploma amenitumia simu wiki ilopita,wa udom alinipatia sana fedha ya kula nikiwa field,wakati huo bodi ya mikopo walikua hawajanipa fedha na watu mwanzoni mwa wiki alinitumia 20,000/=kukabiliana na matatizo madogo-madogo.

Nifanyeje mimi,mwenzenu.Napata wakati mgumu kujua nimuoe nani na niwache wakinani!

marudio kwa ID mpya au copy from forwarded chain of mails
 
Mwenye matatizo ni wewe! Utakataje (booking) tickets katika ma'bus ma3 tofauti kwa safari na wakati mmoja? Kisha ubabaike bus la kupanda? Huoni huo ni mzaha au comedy flani?
 
usipende pesa penda mtu oa unayempenda zaidi ya wengine tena fanya haraka sana wajipange
 
Kama unataka kuoa si uende Moshi ujue mbovu na mbichi. Achana na hao katafute upareni au Machame uone huo ujinga wako kama hautakuishia. Unataka kula vya wenzio siyo. Kaoe huko nilikokwambia uone watakavyokuletea ma-uncle kila siku usijue kumbe washikaji zao.
 
unapenda kuhongwa eh? mwingine anaeza asikupe kitu na bado akawa ndo mwenye mapenzi ya dhati.. true love ndo inamatter who do u think u can stand spend the rest of ur lif with
 
Mmoja amegraduate Udom mwaka huu,ananisisitiza sana nimuoe kwani tayari ameniona nafaa kua mumewe.

Wa pili anachukua diploma ya ualimu mwaka wa kwanza,huyu tayari amewajulisha wazazi wake kua tayari amepata mchumba na si siku nyingi amewahidi kunipeleka kwa utambulisho.

Mwingine na watatu,ni darasa la saba ila ni mfanyabiashara,hapendi kuona mimi napata taabu pale ninapokua na tatizo na hujitahidi kunitumia pesa kama hivi nilivyo hapa chuoni.

Nisaidieni kimawazo,kwani wote pia wanaupendo wa dhati pamoaja nami.Kwa mfano:aliopo diploma amenitumia simu wiki ilopita,wa udom alinipatia sana fedha ya kula nikiwa field,wakati huo bodi ya mikopo walikua hawajanipa fedha na watu mwanzoni mwa wiki alinitumia 20,000/=kukabiliana na matatizo madogo-madogo.

Nifanyeje mimi,mwenzenu.Napata wakati mgumu kujua nimuoe nani na niwache wakinani!

Kwanza, maelezo uliyoyatoa hayaonyeshi kama kuna upendo wa kweli kati yako na hao wachumba zaidi ya wao kukusaidia kifedha...kwa maana nyingine upedo haupimwi na fedha. Pili, inawezekana vipi ukawa na wachumba watatu kwa wakati mmoja...samahani nadhani bado hujawa tayari kuoa.
 
Hi everyone.

Mimi ni mgeni humu javini naomba kuchangia hii mada.

Kifupi acha kuwapotezea muda hao kinadada. Wewe si muoaji. ungekuwa muoaji muda mrefu ungekuwa umefanya maamuzi wa yule ambaye ulianza naye. kwanza unasema unawanawake 3 uliwapata kwa pamoja au kwa nyakati tofauti? nimekuona bonge la **** kwa kuchezea feeling za watu. mwanamke akisema anawanaume watatu mnasema mhuni. vip kuhusu wewe tukuiteje ilihali bado mwanafuzi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom