Nimuoe yupi kati ya huyu mwenye degree na darasa la saba

mmh!ndo wale wale wanaopenda miteremko..hela yake unaipeeeda ee
sasa ndo unakuja kuomba ushauri wa kuoa
mxiii afu unatuhadithi jinsi ulivyompiga na kumuadhibu
mxiiii..ballax
hivi umewahi kupenda wewe?hata robo?
ngoja niishie hapa nisije vunja keyboard
 
naskitika kuwa jina lako haliendani na matendo yako,kama humtaki mtu ndo umpige!!kwani ungemwambia kwa ustaarabu asingekuelewa!?!naamini kati ya hao wawili una majibu ya yupi unaemuhitaji,nikipima maelezo yako std 7 unamfeel zaidi,,gudluck but u need to change uwe gentleman
WiseLady + Wiseboy =:A S-heart-2::peace:
 
mmh!ndo wale wale wanaopenda miteremko..hela yake unaipeeeda ee
sasa ndo unakuja kuomba ushauri wa kuoa
mxiii afu unatuhadithi jinsi ulivyompiga na kumuadhibu
mxiiii..ballax
hivi umewahi kupenda wewe?hata robo?
ngoja niishie hapa nisije vunja keyboard

Acha tu wadada wengine wanatia hata huruma wanapobembeleza penzi
 
Kwa jinsi ninavyojua wanawake

Huyo uliyempiga alafu amekuvumilia ... anakufaa zaidi

She knows u better than all of them included together.

U shud not do that agin though cz ukimpiga tena nitambembeleza alafu atakusahau.

Be wise,

kaa nae mwaka mmoja if she wont change her behavior hata akipata kazi, then YOU ARE LUCKY BOY

Ukimwacha utajutia mpaka siku unakufa
 
1.wanawake hawapigwi,mkuu acha kabisa tabia hiyo.unatutia aibu wanaume wenzio ebo?
2.oa mwanamke anaekupenda kuliko wote....utaishi kama mfalme
3.ukioa unaempenda sana sana,jiandae kuishi kama mtumwa.
Uchaguzi ni wako.
 
kabla ya kuoa nenda katubu kwanza madhambi yako,huna hata aibu kusema kwamba ulimpiga mwanamke kwa kosa la kukupenda?huo ni unyanyasaji,tubu,kisha mrudie MUNGU wako,muombe akupe mke.huenda kati ya hao hakuna ubavu wako hapo.na kama upo basi MUNGU atakufunulia.
 
Kaka, ridhika na ULIYE NAYE, anayekupenda kwa DHATI, kwani alikuvumilia hata pale ulipomwambia HUMTAKI. Ulimpiga, akakuganda. Moyo wake uko kwako. Huyo wa Darasa la Saba ni KIGEUGEU! Si alikuacha kwa sababu kasikia maneno ya watu? Sasa kakuona mtu wa maana, una wako ndani, wivu umemwingia, anataka KUKUHARIBIA! Muda wote huo hamjakuwa pamoja, hujui pengine AMEUKWAA? Ukimgusa atakuambia mwende PEKU PEKU, kumbe anataka KUKUINGIZA KWENYE GRIDI! UMEME KAKA! Ogopa!

Ushauri wangu, huyo uliyenaye, mmesoma wote, hata ukipata tatizo, kwa mfano, ukaumia, ukapata ulemavu, ataweza kukutunza. Huyo wa Darasa la Saba ana ELIMU GANI ya kukutunza wewe? Fikiria na ya baadaye, si ya LEO tu! Umenielewa mdogo wangu?

umeniboa!!! hapo kwenye bold hilo ni tusi!!!
Naona kama umemtukana mama yangu aliyekua anajua kuandika jina lake tu na kurudisha chenchi za waliokuwa wanakuja kununua maziwa pale kijijini kwetu!!! lakini alikuwa mwanamke wa pekee katika maisha yangu sijawahi kuona!!! na si yeye tu najua wapo watu wengi walioshia darasa la 7 lkn leo wanamaendeleo kuliko ww mwalimu mwenye degree yako ya Education!!!
 
hi jf members, mm ni mvulana nipo mwaka wa mwisho moja ya vyuo vikuu hapa Tz. Nilipokuwa 4m 5 na 6 nilikuwa na mchumba ambaye nilimpenda sana naye alinipenda. Nilipokuwa chuo mwaka wa kwnza akapewa udaku naye akaamua kunipotezea, basi nikamtongoza binti tuliyekuwa naye mwaka wa kwanza, japo huyu nililenga awe kuenjoy naye siku moja na kumuacha maana sikumpenda sana, ila baada ya ku do naye alinipenda ile mbaya na kuanza kuniganda kila ninapoenda. Kuona hvyo nikamtumia sms ya kumkataa pia hakusikia, nikampiga hadi kumuumiza pia hakuniacha. Ok nikaamua kuzuga naye maana nilichoka kutoa adhabu, baada ya hapo tukawa tunaishi km lovers kwa sababu yeye ananipenda sana hata hela zake ziko kwenye account yangu na tumenunua naye vitu vingi vya ndani mfn tv, kitanda, kabati, computer, nk. Pia hutumia mzazi wangu hela zake japo hajawahi kumuona. Wakati huo huo yule binti wa darasa la 7 naye aliniomba msamaha nikamsameha pia anasubiri nimuoe. Je nimuoe yupi kati ya hawa? nifaje ili roho yangu impende huyu wa chuo? plş

Kwanza inavyoelekea ni mmoja wa watu wasio makini katika mambo ya mahusiano. Kati ya vitu adimu katika uwanja wa mapenzi/mahusiano ni kijana wa kiume kupata "msichana anayempenda kwa dhati". Vijana wengi wa kiume hulazimisha kupendwa na wasichana na mara nyingi hutumia vishawishi kuwanasa. wewe unabahati kuwa umepata msichana anayekupenda na inaonyesha mmeshafika mbali kiasi ambacho hatua zozote utakazochukuwa kusitisha uhusiano huu wa mwanachuo utamuathiri sana huyu mwanachuo na wewe utakuathiri zaidi maana hutapata amani kwenye mahusiano mengine kwani utaachiwa lana na mpenzi utakayemuacha hivyo ndoa yako haitakuwa salama itakuwa ya misukosuko na mahangaiko kutokana na dhambi uliyoifanya.
 
asante dada kwa ushauri wako, huyu dada wa chuo ni mvumilivu sana, ni mcha mungu, anapenda ndg zangu ndo huwa anawatumia chumvi. Kwa kifupi wa drs la 7 anamzidi huyu uzuri kisura hicho pekee ndo kigezo

Kwa hiyo wewe unataka kuoa sura au unataka kuoa darasa??Mbona hueleweki??Kwenye mapenzi hakuna darasa la saba au masters.wangapi wenye phd hawajaolewa au kuoa??suala la mapenzi liko moyoni mwenu na hasa wewe ndio unajua nani ana nafasi kubwa kijamii.Humu huwezi kupata jibu la masaibu yako.USIKILIZE MOYO WAKO KISHA FANYA MAAMUZI.Bila kijali mengineyo mke anatakiwa awe mvumilivu,mcha mungu wa kweli,anayekupenda wewe na ndugu zako, ambaye nawe pia umempenda na kumridhia .chekecha
 
ulianza vizuri ukaharibu baadae...ulipokua kidato cha sita hukua na mchumba bali mzinzi mwenzio...well umekua na uliye naye ndo stahili yako kwa sasa...umeshamtumia sana,na kuchezea hisia zake as well as resources zake,sasa unataka kumwacha ili iweje! Na nikipe tu angalizo kua tabia ya kupiga wanawake ni ya kizamani na iliisha baada ya abolition ya slave trade!
 
Jamani hayo yote anayajua yeye, kusema huyu wa dr 7 hafai hatujui, vile vile na chuo anaweza kubadilika tu si bado anasoma subiri amalize awe na kidigrii chake atataka wa juu yake zaidi ukizingatia watakuwa level moja
 
Yaani angekuwa huyo mdada mwenye digrii ndio ameomba ushauri, ningemwambia aachane na wewe fasta, ndoa si lelemama, hapo hajazaa hata mtoto mmoja na anatumia muda wake mwingi na wewe unampa kichapo, je akianza kuwa bize na watoto si ndio utamuua kabisa. Ushauri wangu usioe yeyote hapo, huna sifa ya kuwa mume mzuri tafuta mgomvi mwenzio ndio muoane!
 
Mtu anaekupenda atakuvumilia (nadhani unahitaji sana uvumilivu)
Mtu unaempenda utamvumilia sana (unaweza?)

Yote ni hiari yako, hakuna kamili duniani, ukamilifu uko mbinguni,

Chagua na jifunze kuwa mtu mzima, huna haja ya kuanza maisha ya watu wazima na akili ya kitoto, utaanika mambo yako yote kwenye mawebsite
 
Nashukuru kwa michango yenu mbalimbali, nimezipenda zote positive na negative contribution zilizoelekezwa kwangu! kusema ukweli nimefunzwa kitu hapa na kimenisaidia sana kwani my love graph has increased to da one i have and i feel now comfortable. Asanteni sana na endeleeni kusaidia wengine kwa moyo mmoja.
 
Nashukuru kwa michango yenu mbalimbali, nimezipenda zote positive na negative contribution zilizoelekezwa kwangu! kusema ukweli nimefunzwa kitu hapa na kimenisaidia sana kwani my love graph has increased to da one i have and i feel now comfortable. Asanteni sana na endeleeni kusaidia wengine kwa moyo mmoja.

penda unapopendwa usijependa usipopendwa usije jutia utapotendwa .... huyo dada akimpata wa kuweza kumteka utakuja jutia maisha!! wifey material aint that many mdogo wangu ... yaani mtu unachezea almasi hivi hivi ukidai ni kioo?? ... jirekebishe fasta before its too late!! habari ndio hiyo!!
 
Back
Top Bottom