Nimuache au nimvumilie

zacharia elieza

New Member
May 4, 2012
2
0
kumpenda nilimpenda sana mpaka nilifikia hatua ya kumtorea barua ili awe wangu wa kufa na kuzikana,ila tatizo likaja baada ya kutoa barua kwao binti kawa na kiburi kama nini sijui,tofauti kabisa na mwanzo yaani anataka kufanya vitu anavyotaka yeye ukisema umuelekeze kosa hapo ni ugomvi tu!sasa mi nashindwa kuelewa ndo kagundua kuwa nampenda ndo maana analeta visa au nini.Sasa ndo najiuliza nimuache au nivumilie atakuja kubadilika
 
kumtorea = kumtolea

unaposema 'ulimpenda' ina maana mapenzi yamekwisha?

Moja ya silaha ya mahusiano ni communication, je umezungumza na mwenzio kuhusu mabadiliko yake ya tabia?
Umezungumza nae jinsi unavyojisikia?

Kwa upande wako unazungumza nae vipi? Kwa heshima na upole au kwa ukali na kushurutisha?
Kumbuka heshima ni pande zoye mbili na ukishurutisha pia huleta kutokuelewana.

Je anapokataa kufanya yale unayomweleza, na kufanya anavyojisikia , hayo anayoyafanya ni kwa manufaa yenu wote wawili? Je yanalengo la kuboresha future yenu?

Vunja ukimya mkuu, zungumza na mwenzio, ndipo utakapopata jibu kama umwache au uendelee nae, bila kusahau yapaswa ujinguze pia mapungufu yako na urekebishe.

Future ya mahusiano yenu ipo mikononi mwenu
 
ongea nae muelewane inawezekana ameshampata kilaza ma mjini
 
Ongea nae labda ulikuona mshamba wa mapenzi ndio kiburi kikazidi.
 
tishia kumpiga chini... akichukulia poa ujue huna chako, chapa lapa
 
muwekee misimamo ya kiume, hataki kujirekebisha mwambie nakumwaga japo nimeleta barua kwenu usiogope kwamba atasema uhusiano uishe kwani hapo ndo utajua kama kweli anakupenda au la...yataka moyo kidogo hasa kwa mtu unayempenda lkn itakusaidia kujua ukweli
 
jamani mbona uko too general? ila kama alivyo sema boss ni utani lakin kweli. mwambie humpendi tena uone atakavyo act.

lakini pia nikupe angalizo, kuna mabinti ambao ni good pretenders ambao hawa huwa wanaweza kupretend for a while hadi apate anachokitaka. na huenda yeye kajua kuwa kutolewa barua basi ndio mwisha kashakuwa mke na usikute kashaanzataratibu za kuandaa k/party na s.off wakati wewe huko bado hujafika. kuwa makini sana mwambie kabisa tabia yake inamfanya upendo wako kwake upotee. yawezekana yuko kimaslahi zaid. stail ya mjin si unaijua?
 
Wewe hujabadilika??maana usijekuta wewe mwenyewe ndio chanzo cha mabadiliko..
Zungumza nae kwa upole,mueleze kilichopo kwenye moyo wako kama anakupenda kweli atajirekebisha..
 
pole ila katika mahusiano a hasa kuelekea kwenye ndoa kuna mambo ya msingi yapaswa uyaelewe na ndo yatakupelekea kwenye maamuzi
  1. heshima
  2. kusikilizana
  3. kuelewana
  4. kuthaminiana
  5. kujitambue
  6. nk
sasa kama hamwezi kusikilizana kwa sasa je baada ya ndoa kitafuata nini????
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom