Nimshughulikie au? Naombeni ushauri

We vipi hiyo ngoma unagonga! yeye ametaka mgongane kwani amekwambia anataka ndoa?
We zubaa zubaa Unaweza kuta hata mchumba wako wenzio wanakula, ndoa kitu ingine kabisa!
 
Man acha hizo hit and run jombaaa.Hivyo mbona vituo tu kwenye safari wakati inaendelea ila ndomu muhimu kaka.
 
Nilikutana na huyu binti kwa mara ya kwanza ndani ya basi moja maarufu lifanyalo safari zake kati ya Dar na Morogoro. Tulikaa nae siti zilizopakana, na sikuongea nae kwa takribani nusu saa nzima ya safari. Baadae akawa amepitiwa na usingizi na kunilalia kwa kuniegemea. Kama ilivyo kawaida ya wanaume walio wengi sikuthubutu kumkatiza usingizi wake kwa kumwamsha asiniegemee. Nilivumilia na robo saa baadae basi likapiga tuta akaamuka na kuniomba radhi kwa kuniegemea. Nilitabasamu nikamwambia usijali na hapo ndio ukawa mwanzo wa maongezi yetu yaliyo pelekea kufahamiana na hadi kubadilishana mawasiliano. Tumetokea kuwa marafiki wakubwa sana sijawahi kuona. Hadi watu walio wengi wanadai nina mahusiano nae ya kingono kwa jinsi nilivyo karibu nae.

Ilikuwa ni mwezi uliopita siku ya boxing day alinipa mwaliko maalumu kumtembelea katika chumba chake anachoishi. Hii haikuwa mara yangu ya kwanza kwenda kumtembelea na hata yeye alishawahi kunitembelea kwangu mara kadhaa. Kwa kweli kama ni zile sifa za uzuri zinazovuma mitaani naona zote anazo. Ninachokiona cha zaidi kwake ni ile sifa ya kumcha Mungu sana. Nilifika mida ya saa kumi jioni, nikabisha hodi bila kuitikiwa. Kwa kuwa mlango ulikuwa umeachama kidogo yapata uwazi wa sentimeta kumi hivi nilijua hayuko mbali yupo karibu tu. Lakini msukumo mkubwa ulioibuka mshindi ni ule ulionituma kuchungulia kwa kuongeza kidogo upenyo wa uwazi wa mlango. Baada ya kuufungua mlango mboni zangu za macho zikatua katika mwili wake uliositiriwa na kanga moja tu. Alikuwa amelala kifudifudi na ilionekana kama alikuwa amesinzia fofofo.

Nililazimika kumwita mpaka mara nne ndipo akastuka, akanikaribisha, nikaingia na kuketi. Tulibadilishana mawazo, tukaangalia music katika screen, tukacheka, nikala, nikanywa na ilipofika saa moja jioni nilimuaga. Alinisihi nimsubiri aoge ili anitoe kidogo maana nae alikuwa anataka kutoka jioni hiyo. Alikwenda kuoga na aliporejea na kanga yake moja hiyo hiyo nilitaka kumpisha ili avae lakini alikataa na kuvaa nikiwa ndani humohumo. Baadae akaniambia anataka anifanyie surprise lakini sharti nifumbe macho kwanza. Nilitii sharti kwa kuwa nilipatwa shauku ya kuiona surprise yenyewe. Baada ya dakika kama moja akaniambia nigeukie upande wa kitanda ndipo nifumbue macho, nami nikafanya hivyo. Sikuelewa elewa baada ya kufumbua macho kwa juu ya kitanda niliona vitu ambavyo sikutarajia kabisa kuviona. Nilikuta ametapakaza kitanda kizima vipakti vya mipira ya kiume. Nilipogeuka ili kumuuliza kulikoni nilijuta kugeuka. Nilikuta amevua nguo zake zote yupo mtupu kama alivyozaliwa.

Damu yangu ilichemka, akili ikawa sio yangu tena maana kwa kweli maungo yake hadharani yana sifa nzuri mno sijawahi kuona. Damu ilitembea mpaka kwa mwana wa pale kati akakasirika na kuamka. Ghafla iliniijia sura ya mchumba wangu ambaye ninae kwa miaka miwili sasa na mwezi wa kumi mwaka huu tunatarajia kufunga ndoa. Nikamwambia simuelewi mambo anayofanya, wakati huo nikiwa nimetizama pembeni. Tulijibizana huku akiniongelesha kwa sauti ya mahaba na hata akadhubutu kunifuata kwa nyuma na kunigusa gusa. Ili kuepusha mengi niliamua kumuaga huku nikielekea usawa wa mlango pasipo kuinua kichwa kumtazama. Nikakishika kitasa cha mlango na kukinyongea chini huku nikiuvuta mlango kwa ndani. Haukufunguka nikajua amefunga na kuutoa ufunguo. Kuikata stori iwe fupi, ilibidi niwe mpore busara ikatawala zaidi mpaka mdada huyu akaamua kuvaa nguo zake na mambo yakarudi kawaida. Akanisindikiza mpaka nikapanda daladala nae akarudi kwake.

Toka siku hiyo hakomi kunipigia simu na kunitumia meseji za kimahaba. Bahati mbaya mchumba wangu anasoma mwaka wa tatu na wa mwisho chuo kikuu Dododma nami nipo ninaishi Dar es salaam hivyo inakuwa vigumu hata kumchunia rafiki yangu huyu au kuwa na hofu na meseji zake anazonitumia. Toka tukio hili litokee nimekuwa mbali kidogo nae lakini yeye amezidi kuwa karibu sana. Kitu kimoja kikubwa ninachokihusudu toka kwake ni sifa ya urembo pamoja na kujichunga lakini nashangaa kwa nini mimi ananifanyia hivyo. Kuna watu wenye pesa wengi sana huwa wanamfukuzia na hajawahi kumkubalia mtu hata mmoja kati yao na kila kukicha idadi ya wanao ongezeka kwenye list ya wanaomtokea inaongezeka tu. Mda wote wa urafiki wetu sikuwahi kumuona na boy friend tofauti na mimi, na amekuwa akipenda sana kuwa nami na ndio kisa cha watu kusema nina mahusiano nae.

Ndugu zangu wapendwa hayo ndiyo yanayonisibu kwa wakati huu. Nimekamatika njia panda, watu wengi sana wanamtaka tena watu wazito kabisa na maarufu lakini hawajampata lakini kwangu mimi amekuja yeye mwenyewe! Sasa kila siku najiuliza sijui nimshughulikie? au sijui vipi? Naombeni ushauri wenu wana jamii forum wenzangu.
Aksanteni sana.

Ng`wana Madeleke! uyomba kenehe?
kula mzigo huo fastaa! unatudhalilisha wanaume! ebo!
 
Usimshughulikie wala nini, mweleze wazi kuwa una mchumba na ikiwezekana kata mawasiliano naye.
 
mmmh,siku hizi watu wa dini ni wachache.kama angekuwa mtu wa dini,asingekufanyia hivyo.nyege hizo nyege gani?inaonyesha aliyapanga hayo zamani.na wewe pia inaonyesha ni sitaki nataka.kwa nini usimwambie ukweli kama una mchumba wako?na mueleze msg za mapenzi asikutumie kwenye wewe na yeye sio wapenzi.kama kweli unampenda mchumba wako,jaribu kumkwepa.kama unavyosema ni mcha mungu,mmwagie mistari ya kidini dini

Kisukari, unafahamu kitu kinaitwa NYEGE BWIMA? au NYEGE MSHINDO? hizo zikikutembelea dini zote unasahau, tena usipoangalia unaweza kubaka mtu! waulize wanawake wenzio!

katika swala la nyege hamna cha padri wala sheikh wala sista! as long as you are a human being NYEGE ni NYEGE tu!

Huyo dada wa Morogoro inaionekana alikuwa na kiu ya kufa mtu, na since jamaa alikuwa ana play u gentleman, akashindwa kuendelea kusubiri mpaka aanze kutongozwa, akaamua ajilipue! wanawake wengi sana dunia ya leo kama kaku mind na anaona una domo zege, anajilipua tu!
 
Sasa Jiulize Condom Kazipata wapi na zanini kwa yeye mwanamke, mtu haukai nae mmekutana tu kwenye basi umejuaje kuwa ni muaminifu? Kwanza Surprise za kukaliana uchi ni za kimalaya tu, hakuna mtu aliyemwema akamkalia mwenzake uchi eti ana mu attract, chukua hatua na usipende kujiridhisha kwa kila unachokiona.
 
ukiona manyoya kashaliwa huyo anajificha kwa kivuli cha dini, dini anayo sasa ungesema dini gani maana siku hizi....
 
Nilikutana na huyu binti kwa mara ya kwanza ndani ya basi moja maarufu lifanyalo safari zake kati ya Dar na Morogoro. Tulikaa nae siti zilizopakana, na sikuongea nae kwa takribani nusu saa nzima ya safari. Baadae akawa amepitiwa na usingizi na kunilalia kwa kuniegemea. Kama ilivyo kawaida ya wanaume walio wengi sikuthubutu kumkatiza usingizi wake kwa kumwamsha asiniegemee. Nilivumilia na robo saa baadae basi likapiga tuta akaamuka na kuniomba radhi kwa kuniegemea. Nilitabasamu nikamwambia usijali na hapo ndio ukawa mwanzo wa maongezi yetu yaliyo pelekea kufahamiana na hadi kubadilishana mawasiliano. Tumetokea kuwa marafiki wakubwa sana sijawahi kuona. Hadi watu walio wengi wanadai nina mahusiano nae ya kingono kwa jinsi nilivyo karibu nae.

Ilikuwa ni mwezi uliopita siku ya boxing day alinipa mwaliko maalumu kumtembelea katika chumba chake anachoishi. Hii haikuwa mara yangu ya kwanza kwenda kumtembelea na hata yeye alishawahi kunitembelea kwangu mara kadhaa. Kwa kweli kama ni zile sifa za uzuri zinazovuma mitaani naona zote anazo. Ninachokiona cha zaidi kwake ni ile sifa ya kumcha Mungu sana. Nilifika mida ya saa kumi jioni, nikabisha hodi bila kuitikiwa. Kwa kuwa mlango ulikuwa umeachama kidogo yapata uwazi wa sentimeta kumi hivi nilijua hayuko mbali yupo karibu tu. Lakini msukumo mkubwa ulioibuka mshindi ni ule ulionituma kuchungulia kwa kuongeza kidogo upenyo wa uwazi wa mlango. Baada ya kuufungua mlango mboni zangu za macho zikatua katika mwili wake uliositiriwa na kanga moja tu. Alikuwa amelala kifudifudi na ilionekana kama alikuwa amesinzia fofofo.

Nililazimika kumwita mpaka mara nne ndipo akastuka, akanikaribisha, nikaingia na kuketi. Tulibadilishana mawazo, tukaangalia music katika screen, tukacheka, nikala, nikanywa na ilipofika saa moja jioni nilimuaga. Alinisihi nimsubiri aoge ili anitoe kidogo maana nae alikuwa anataka kutoka jioni hiyo. Alikwenda kuoga na aliporejea na kanga yake moja hiyo hiyo nilitaka kumpisha ili avae lakini alikataa na kuvaa nikiwa ndani humohumo. Baadae akaniambia anataka anifanyie surprise lakini sharti nifumbe macho kwanza. Nilitii sharti kwa kuwa nilipatwa shauku ya kuiona surprise yenyewe. Baada ya dakika kama moja akaniambia nigeukie upande wa kitanda ndipo nifumbue macho, nami nikafanya hivyo. Sikuelewa elewa baada ya kufumbua macho kwa juu ya kitanda niliona vitu ambavyo sikutarajia kabisa kuviona. Nilikuta ametapakaza kitanda kizima vipakti vya mipira ya kiume. Nilipogeuka ili kumuuliza kulikoni nilijuta kugeuka. Nilikuta amevua nguo zake zote yupo mtupu kama alivyozaliwa.

Damu yangu ilichemka, akili ikawa sio yangu tena maana kwa kweli maungo yake hadharani yana sifa nzuri mno sijawahi kuona. Damu ilitembea mpaka kwa mwana wa pale kati akakasirika na kuamka. Ghafla iliniijia sura ya mchumba wangu ambaye ninae kwa miaka miwili sasa na mwezi wa kumi mwaka huu tunatarajia kufunga ndoa. Nikamwambia simuelewi mambo anayofanya, wakati huo nikiwa nimetizama pembeni. Tulijibizana huku akiniongelesha kwa sauti ya mahaba na hata akadhubutu kunifuata kwa nyuma na kunigusa gusa. Ili kuepusha mengi niliamua kumuaga huku nikielekea usawa wa mlango pasipo kuinua kichwa kumtazama. Nikakishika kitasa cha mlango na kukinyongea chini huku nikiuvuta mlango kwa ndani. Haukufunguka nikajua amefunga na kuutoa ufunguo. Kuikata stori iwe fupi, ilibidi niwe mpore busara ikatawala zaidi mpaka mdada huyu akaamua kuvaa nguo zake na mambo yakarudi kawaida. Akanisindikiza mpaka nikapanda daladala nae akarudi kwake.

Toka siku hiyo hakomi kunipigia simu na kunitumia meseji za kimahaba. Bahati mbaya mchumba wangu anasoma mwaka wa tatu na wa mwisho chuo kikuu Dododma nami nipo ninaishi Dar es salaam hivyo inakuwa vigumu hata kumchunia rafiki yangu huyu au kuwa na hofu na meseji zake anazonitumia. Toka tukio hili litokee nimekuwa mbali kidogo nae lakini yeye amezidi kuwa karibu sana. Kitu kimoja kikubwa ninachokihusudu toka kwake ni sifa ya urembo pamoja na kujichunga lakini nashangaa kwa nini mimi ananifanyia hivyo. Kuna watu wenye pesa wengi sana huwa wanamfukuzia na hajawahi kumkubalia mtu hata mmoja kati yao na kila kukicha idadi ya wanao ongezeka kwenye list ya wanaomtokea inaongezeka tu. Mda wote wa urafiki wetu sikuwahi kumuona na boy friend tofauti na mimi, na amekuwa akipenda sana kuwa nami na ndio kisa cha watu kusema nina mahusiano nae.

Ndugu zangu wapendwa hayo ndiyo yanayonisibu kwa wakati huu. Nimekamatika njia panda, watu wengi sana wanamtaka tena watu wazito kabisa na maarufu lakini hawajampata lakini kwangu mimi amekuja yeye mwenyewe! Sasa kila siku najiuliza sijui nimshughulikie? au sijui vipi? Naombeni ushauri wenu wana jamii forum wenzangu.
Aksanteni sana.

Ndugu yangu kama kweli ulifanya hivyo, nivema, lkn inanwia vigumu pia kumuamini huyo mchumba wako kwani uchumba c ndoa, pia chuo ni jini kwa wasichana, hasa wa leo, kwani kuna quiz na hom wks pamoja na mitihani ya mwisho inajazwa na walimu wenyewe, unaweza mkataa huyo leo kumbe mchumba anamtazamo hasi, lkn ni vema ukautii moyo wako kwani wanaume waliopita kama ww wengi na wakashinda.
 
hili jamvi linazid kuchafuliwa kila siku na mihadithi ya kufikirika utafikiri kurasa za shigongo kweny global publishers.sas unaomba ushaur kweny li hadithi lako la kiboya peleka kwa shigongo sio hapa.
download complete..
 
acha kuendekeza zinaa, itakuangamiza,

ww amekudanganya kuwa wengine amewakatalia lengo ni kuteka hisia zako ili uone kuwa ww ndo wa kwanza kufungua kitabu wakati sivyo. hata kama ingekuwa hivyo huo ujasiri wa kukufanyia hivyo umetoka wapi, kama sio mtu mzoefu

kila aziniye na mwanamke hana akili, anajipalia makaa ya moto katika kifua chake akidhani hataungua kumbe sivyo mithali 6

kama zinaa inakusumbua nashauri uoe na utulie na mke wako
 
mmmh,siku
hizi watu wa dini ni wachache.kama angekuwa mtu wa dini,asingekufanyia
hivyo.nyege hizo nyege gani?inaonyesha aliyapanga hayo zamani.na wewe
pia inaonyesha ni sitaki nataka.kwa nini usimwambie ukweli kama una
mchumba wako?na mueleze msg za mapenzi asikutumie kwenye wewe na yeye
sio wapenzi.kama kweli unampenda mchumba wako,jaribu kumkwepa.kama
unavyosema ni mcha mungu,mmwagie mistari ya kidini dini
Anamlea tu na msg zake za mapenzi halafu mchumba akirudi atakuja kuomba ushauri Anatumiwa msg za mapenzi akiwa na mpenzi wake afanyaje? Its now or never! Mpige stop sasa hivi na kama mnaendelea kuwa marafiki weka mipaka. Ukitembea nae tu ujue amekuganda.
 
Acha uwongo wewe dogo, ulikua unatoka kupiga mzigo aften posten ndani ya T-ban ukakutana na huyo binti naye kachoka kurusha, ndio mkaamua muende kupunguza uchovu kwa kula mzigi, dogo acha kuzuga wewe! Sinsen na morogoro wapi na wapi bana!! acha hizo wewe kula tu mzigo basi!
 
Mkuu kuna dosari....uliwahi kumuuliza kama ana boyfriend? kwa sifa na urembo ulioumwaga hapa ni lazima angekuwa committed. Jambo la kumcha mungu lisikufanye ujiaminishe, chukua tahadhari.
 
Mimi naamini haukuwa mkweli na huyo binti, kama ungeweka wazi kama relation ni platonic asingepagawa. Naamini kuwa hajui pia kama uko engaged, umelikoroga sasa linywe.....
 
mmh hapo kuna namna ucjecheka na nyani ukavua mabua heri ya jana kuliko leo,be wise men
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom