Nimsaidiaje Kaka yangu aliyelazimishwa kumuacha mkewe na vyombo vya dini?

Washawasha

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
16,652
13,076
Habari zenu wanajamii,
Ni hivi nina mdogo wangu alikuwa anafanya kazi kwa hawa watu wa kushikashika bunduki sasa alikuwa anajifanya anawapinga sana mafisadi basi wakamtengenezea scandal na mwishowe kumtimua kazi.
Basi akawa yupo yupo nyumbani tukamfanyia mpango akapata kazi katika kampuni ya ulinzi lakini kama mnavyojua mshahara wake ni mdogo huko aliko sasa
Basi mkewe akaanza kutoka nje baada ya kumuona jamaa kachacha kimtindo sababu maisha yalibadilika kwa kweli sio kama alivyozoea.akapata jamaa huko nje ambaye ana mshiko kinoma.
Basi siku moja kaka yangu akiwa anarudi kutoka kazini akakuta baadhi ya vitu chumbani kwake havipo na mke pia hayupo,ndipo alipowaliza majirani na kuambiwa kwamba mkewe kasema anaenda kwao,wakamuuliza kwani hajakuaga?
Jamaa presha juu,kesho akaenda kuomba ruhusa kazini na kwenda ukweni kujua kulikoni mbona bibie kaondoka bila ruhusa!
Lakini alipofika ukweni baba mkwe akamuonesha talaka ya kuwa mwanawe anasema kaachwa,kaka yangu huyo alipinga kwa nguvu zake zote lakini mtoto wa kike akawa anang'ang'ania kuwa kaachwa.
Basi ikabidi mzee kutokana kidogo ni mtu wa dini akaomba suala hilo likamalizwe na vyombo vya dini nakumuomba kaka yangu arudi cku ya ijumaa ili baada ya swala ya Ijumaa,waende ktk vyombo husika.
Ilipofika Ijumaa kama makubaliano yalivyokuwa kaka yangu akaenda na kwenda kwa vyombo husika,basi baada ya swala kuisha ndipo kikao kikafanyika na hiki chombo kiliipinga talaka ile maana ilisomeka hivi,
MPOKEE MWANAO NIMEMUACHA,NDIMI WASHAWASHA JR
Wakasema hii sio talaka bali ni maelezo,je talaka iko wapi basi ?kukawa na ubishani wa hapa na pale mpaka kushikishwa MSAHAFU na viapo juu lakini bibie alikomaa kuwa kaachwa na ndugu yangu aking'ang'ania kuwa hajaacha,ndipo kikao kikaghairishwa mpaka ijumaa nyingine,
Basi yule mtoto akaamua kusema ukweli ya kwamba hajaachwa na mumewe huyo hiyo talaka alimuomba rafiki yake amuandikie isipokuwa kampata kibosile mwingine ambaye anataka kumuoa na kuomba aje kumtambulisha
Jamaa akatambulishwa na kubomoa nyumba ya udongo na kujenga ya tofali na kule kwenye chombo cha dini akamwaga fedhwa,Ijumaa ilipofika kile chombo cha dini kikamuambia kaka yangu kuwa kaacha na ile ni TALAKA sahihi kwahiyo mke si wake.
Ndugu yangu anataka kwenda kuchoma moto ile nyumba na kuwafanya kitu mbaya huyu jamaa na huyo my wife wake kwasababu anayajua haya mambo vizuri mno na anataka kuwaumiza hawa watu wa dini,anaomba msaada wangu ,je nimsaidieje huyu WASHAWASHA JR?
VYOMBO VYA DINI MBONA MNATUANGUSHA ,SASA TUMUAMINI NANI JAMANI?
 
Sijui kiswahili au macho yana usingizi Washawasha bana haya
 
Whether kaka yako au mdogo wako - anamng'ang'ania huyo mwanamke wa nini?

Anachotafutwa ni kufungwa tu sasa
 
Sijui kiswahili au macho yana usingizi Washawasha bana haya
Lengo langu hapo ni kumaanisha huyu mdogo wangu ni dume ndio maana nikatumia neno kaka,samahani kwa wote ambao mtashindwa kuelewa hapo kwenye BLUE
 
Ndoa zingine matatizo matupu, inakuaje mtu anataka kuendelea kukaa na mtu kama huyo dada?

Kifupi huyo dada yuko after money..sasa kama huyo mdogo wako anataka kuendelea kuwa na mtu ambae ameshajua hampendi yeye kama yeye bali pesa yake basi mwambie ajitahidi kukusanya mkwanja wa kutosha kummiliki kifaa hicho.
 
sawa ndugu yangu mie itabidi nimuambie kuwa kumrudia huyo shemeji yangu ni kama kutaka kufanya mapenzi na tembo
 
Kiukwel wanawake wengi, hata hapa kwenye JF wapo after money. Tafakari.
 
huyo kaka ashukuru mara mia,ajue kwamba huyo si mke,kama talaka,amuongezee.ingawa ataumia na inaweza kuchua muda,baadae atampata anaemfaa wa shida na raha.
 
mwambie bro wako aachane naye, laana itamkuta huko huko pamoja na hao aliowanunua, alaa!
 
Back
Top Bottom