Nimrudishie pesa zake?

Kiutu ... ungerudisha tu hizo fedha na
ku mwambia penzi la kweli halinunuliwi..

Kisheria.. hizo fedha ni kama zawadi .
Hujamuomba wala hujakopa.
Kwa hiyo hata akitaka kukushtaki hana kesi..
kama hakufanya internet transition basi atakuwa na deposit slip tu. .
Hamna paper uliosaini.

Kwa hiyo maamuzi ya mwisho ni yako ..
 
Mkuu pole na yaliyo kusibu zamani ujue uamuzi wako kama ulikuwa na uamuzi sahihi na mimi nakushauri usiwe fisadi wa nafsiyako na maliyako uliyoitafuta kwa tabu hivyo usichanganye halali na haram yake anataka kukununua hiyo ni hongo hata kama unashida uskubali kununuliwa mrudishie pesa zake hii ingine ni mitihani toka kwa mungu anakupima imaniyako mkuu hiyo sio halaliyako fkitia je mumewe anajua hilo ukipata jibu ligeuzie upande wako ungelikuwa wewe unafanyiwa hivyo
 
Kama hauna mpenzi tafta na umtambulishe kwake, siku akikutafta mpe simu mpenzi wako awe anapokea simu. Hela ifanyie biashara au toa msaada. am out
 
mkuu usirudishe pesa. Kama bado unayo, nina kistarlet changu twaweza fanya biashara ukabaki na ukumbusho wa fedha zake.
 
kula hela iyooo na akijileta we mpotezee ila uwe na majibu akiuliza kwanini ulikula hela zangu..!
 
Chanzo cha magonjwa hichi! Huyo dada kashgudundua kuwa Mme wake dinya dinya hovyo inje ya ndoa...yeye anakuitaji ili umtulize; Ukila hiyo hela tuu umekwisha..."Ukishatoka kwenye nyumba inayoungua usirudi kumuokoa mtu" utakufa wewe! Rudisha hela. Tena mwambie atunze ndoa yake! good day
 
Wakuu, nilitendwa na dada mmoja miaka mitatu iliyopita. Nilipata secondment Nigeria kikazi kwa kama miezi kumi hivi, baada ya kurudi nikamkuta na kitumbo cha miezi 3. Huyu alikuwa mtarajiwa wangu ambaye tulifahamiana na kuaminiana sana kiasi hata cha account na vipato vyetu kuwa wazi kwa wote. Baada ya kutendwa sikuwa na hamu tena ya kuwa na mahusiano, maana sikuwa nawaamini wadada tena. Niliamua kufocus kwenye shughuli zangu binafsi ambazo kimsingi zimenipa maendeleo kiasi.

Pamoja na kwamba dada huyu aliolewa, lakini kwa kama miezi 14 sasa, amekuwa akinitafuta mara kwa mara
akiomba msamaha na kusisitiza kuwa bado ananipenda. Nimekuwa nikimkwepa sana lakini hakati tamaa kila ninakojificha, hunitafuta mpaka kunipata. Nilimkalisha chini na kumuonya kuwa kamwe siwezi kumrudia maana amekuwa mke wa mtu na ni hatari kucheza na wake za watu.
Cha ajabu nimekuta kaniwekea kwenye akaunti yangu fedha taslim kama 4m na kasha kunitext
pole kwa yote, fungu hilo likufariji. Baadaye alituma ujumbe kwa email akionyesha masikitiko yake kwa aliyoyafanya na kusema nipokee hizo hela na wakati wowote nikiwa na shida nimtafute maana yuko tayari kwa lolote.

Kwa ufupi nimeapa SIMTAFUTI hata kwa dawa. Wadau mnanishaurije, nimrudishie pesa zake?

Wasalaam,
HorsePower Kufakunoga

Msamehe bana,....
Kwa tafsiri nilivyokusoma hapo juu
anakuomba msamaha umsamehe,
SIO mrudiane bana.

Hizo 4m/= ni kifuta machozi Kwakuwa imekuwa ngumu kwako kumsamehe.
Mrudishie na mwambie umemsamehe bila gharama yoyote ili
nyote wawili muishi kwa amani kila mmoja na njia yake.

Kila la heri.
 
Wakuu, nilitendwa na dada mmoja miaka mitatu iliyopita. Nilipata secondment Nigeria kikazi kwa kama miezi kumi hivi, baada ya kurudi nikamkuta na kitumbo cha miezi 3. Huyu alikuwa mtarajiwa wangu ambaye tulifahamiana na kuaminiana sana kiasi hata cha account na vipato vyetu kuwa wazi kwa wote. Baada ya kutendwa sikuwa na hamu tena ya kuwa na mahusiano, maana sikuwa nawaamini wadada tena. Niliamua kufocus kwenye shughuli zangu binafsi ambazo kimsingi zimenipa maendeleo kiasi.

Pamoja na kwamba dada huyu aliolewa, lakini kwa kama miezi 14 sasa, amekuwa akinitafuta mara kwa mara akiomba msamaha na kusisitiza kuwa bado ananipenda. Nimekuwa nikimkwepa sana lakini hakati tamaa kila ninakojificha, hunitafuta mpaka kunipata. Nilimkalisha chini na kumuonya kuwa kamwe siwezi kumrudia maana amekuwa mke wa mtu na ni hatari kucheza na wake za watu.
Cha ajabu nimekuta kaniwekea kwenye akaunti yangu fedha taslim kama 4m na kasha kunitext pole kwa yote, fungu hilo likufariji. Baadaye alituma ujumbe kwa email akionyesha masikitiko yake kwa aliyoyafanya na kusema nipokee hizo hela na wakati wowote nikiwa na shida nimtafute maana yuko tayari kwa lolote.

Kwa ufupi nimeapa SIMTAFUTI hata kwa dawa. Wadau mnanishaurije, nimrudishie pesa zake?

Wasalaam,
HorsePower Kufakunoga



kuRa heRa hizo wewe usiwe faRa, na akiReta zingine wee' kuRa tu hadi akome kuziReta hayo mengine ni maamuzi yako binafsi....!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom