Nimrod Mkono na Mkono Advocates watch

huyu nae fisadi.. alafu yupo Power Pool.. Tenga jambazi mpare yule.trust me.

Kwani law firms dar ni ya huyu mpare na mkono, mbona law firms zingine hawapewi tender kubwa kubwa kama hizi... Hapa lazima kutakuwa na mambo ya 10 percent
 
Date::8/3/2009

Serikali yaionya Benki Kuu

Na Ramadhan Semtawa

SERIKALI imeonya Benki Kuu (BoT), isithubutu kutoa kiasi cha fedha takriban Sh 60 bilioni kwa mfanyabiashara Devram Valambhia, nje ya mahakama.

Onyo la serikali kwa BoT limekuja wakati kumekuwa na shinikizo la Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, kutaka BoT imalize kesi hiyo ya Valambhia nje ya mahakama kwani tayari imetumia kiasi cha Sh 8 bilioni za uwakili hadi mwaka jana Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), alivyofanya ukaguzi.

Wakati kamati hiyo inayoongozwa na mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, ikitoa msimamo huo kurejea ule wa Kamati ya Fedha na Uchumi, Gavana wa BoT Profesa Benno Ndulu, ametoa msimamo akisema tayari wamepata maelekezo ya serikali yakionya benki hiyo isitoe fedha zake kwa Valambhia nje ya mahakama.

"CAG alionesha wasiwasi kuwa pesa ambazo wakili alilipwa zilikuwa ni nyingi mno kulingana na kesi yenyewe. Kesi yenyewe inagharimu Dola za Marekani 55 milioni na mpaka ukaguzi unafanyika wakili alikuwa amelipwa Sh 8 bilioni," ilisema kamati ikisisitiza umuhimu wa kesi hiyo kumalizwa nje ya mahakama.

Valambhia anaidai serikali kiasi cha dola 55 milioni kutokana na kuiuzia Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, magari kutoka Chekoslovakia.

Hata hivyo, akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu ofisini kwake jijini Dar es Salaam wiki iliyopita, gavana Ndulu alisema tayari wamepata maelekezo hayo ya serikali ikionya fedha zake zisiguswe.

"Serikali yenyewe ambayo ndiyo yenye fedha zake, imekataa tusilipe nje ya mahakama..., kwa hiyo ndiyo msimamo uliopo sasa tunaoutekeleza," alifafanua gavana. Gavana alisema BoT siyo yenye dhamana ya kulipa fedha za Valambhia, kwani yenyewe inahifadhi fedha za watu ambazo ni za serikali.

Akifafanua, gavana alisema kama serikali ikitoa idhini BoT haitakuwa na pingamizi, lakini hadi sasa haiwezi na wala haina mpango wa kulipa fedha hizo nje ya mahakama.

"Mwenye pesa kakuonya usiguse fedha zake halafu mwingine aje akwambie uzichukue ukamlipe mtu, hapana... hatwendi hivyo," alisisitiza. Kwa msisitizo, alisema anafahamu lipo shinikizo kutoka kwa watu mbalimbali ambao (ukiacha Kamati ya Bunge), wana maslahi yao.

"Najua kuna watu wanashinikiza hili kwa maslahi yao binafsi, tunawajua, lakini msimamo ni kwamba, I can't do that (siwezi kufanya hivyo)," alisisitiza gavana.

Kamati hiyo ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma katika taarifa yake ya kwanza mwaka huu, imeitaka BoT kumaliza kesi hiyo nje ya mahakama ili kuepuka gharama zaidi za uendeshaji kesi kwa kulipa mawakili.

Hata hivyo, BoT iliijulisha kamati kuwa ilisitisha mkataba na Kampuni ya Mkono tarehe 22 Januari mwaka 2008 na kuteua kampuni nyingine ya Uwakili ya Law Associates, kuitetea BoT katika kesi zake zote.

Sehemu ya taarifa ya kamati ilisema, "Kamati ilifuatilia agizo la Kamati ya Fedha na Uchumi ililolitoa kwa Benki Kuu mwaka 2007 kuhusiana na malipo makubwa ya ada kwa kampuni ya uwakili ya Mkono and Company Advocates. Malipo haya yalitokana na kesi iliyokuwa na inayoendelea mahakamani kati ya Benki Kuu na ndugu Devram Valambhia."

"Kesi hii ni ya siku nyingi sana na inatokana na uamuzi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa kununua magari kutoka nchini Chekoslovakia."

"Kamati iliona kuwa ni vema kesi hii ikamalizwa nje ya mahakama kwani iwapo itachukua muda mrefu zaidi gharama za kesi zitazidi thamani ya kesi yenyewe. Kamati ya Fedha na Uchumi iliiagiza Benki Kuu kufanya mazungumzo na kampuni ya Mkono ili kupunguza gharama za kesi na hatimaye kuimaliza kesi hiyo nje ya mahakama.

Hata hivyo, kamati ilifafanua kwamba inakubaliana na uamuzi wa BoT kusitisha mkataba na kampuni ya uwakili ya Mkono, lakini ikasisitiza iwapo juhudi hazitawekwa kumaliza kesi hiyo ya Valambhia nje ya mahakama, kampuni ya uwakilii iliyopewa kazi hiyo nayo italipwa fedha nyingi na kwenda zake na ikawa ni mtindo wa mawakili kufaidika na kesi za BoT ambazo haziishi.
 
Nadhani maagizo ya Rais JK juu ya kutochanganya BIASHARA NA UTUMISHI WA UMMA yatungiwe sheria ndipo tutakapoona wapi tumesimama: Mhe. Nimrod Mkono kampuni yake ya Mkono Advocates ilipewa Tenda na BOT kuitetea... moja ya kesi zinazozungumzwa sana ni ile ya Devram Purshotam Valambhia dhidi ya BOT na AG ambapo eti Mh. Mkono aliitetea BOT isimlipe $ 60.0 Milioni lakini yeye akawa anavuta asilimia ambayo hadi mkataba unasitishwa alishavuta asilimia 20 ya den la BOT kwa Valambhia. Kampuni ya Bw. Marandu na Mwenzake ndio waliokuwa Wakimtetea Valambhia ( sasa marehemu) gavana wa BOT wakati ule, Balali alihukumiwa kwa kudharau amri ya mahakama na kutozwa faini sh.400,000 au kwenda Jela... Wadau ebu tuchimbe kesi hii nayo imefikia wapi????

Mkanganyiko huu wa maslahi ya utumishi wa Umma na Maslahi binafsi yataka upatiwe ufumbuzi ili kuondoa harufu ya giza na rushwa na kuleta mwanga na uwajibikaji.
 
Last edited:
"Najua kuna watu wanashinikiza hili kwa maslahi yao binafsi, tunawajua, lakini msimamo ni kwamba, I can't do that (siwezi kufanya hivyo)," alisisitiza gavana.

Swali ni kwamba hao wanao sisitiza BOT imlipe Valambia US 60 Mil wanainterest gani kwenye hiyo kesi na ni wa kina nani hasa hii inapaswa kueleweka wazi wazi.Kwa kuwa kampuni iliyosupply hayo magari jeshini ni kampuni ya Valambia na kama kudai wanadai wao kwa kazi walioifanya hao wengine kinawahusu nini.Sasa hawa wengine wanaoishinikiza serikali ilipe interest yao ni nini hasa?

Au ndio wale wale wamaotaka kushinikiza malipo halafu wapate chajuu kwa kufanikisha deni kulipwa.Watanzania bwana ni watu wa ajabu kweli kweli,ubinafsi ndio uliowajaa wengi.Hapa kinachogomba ni maslahi ya watu binafsi, maskini Valambia wa watu amesota wee mpaka akapoteza uhai kwa kufuatilia deni lake.

Huku nyuma watu wanashinikiza deni lilipwe ili nao wafaidi huu nao ni ufisadi wa aina yake.Ingekuwa vizuri kama Gavana wa BOT akiweka majina ya hao wanaoweka shinikizo hadharani ili jamii iwatambue.
 
"Najua kuna watu wanashinikiza hili kwa maslahi yao binafsi, tunawajua, lakini msimamo ni kwamba, I can't do that (siwezi kufanya hivyo)," alisisitiza gavana.

Swali ni kwamba hao wanao sisitiza BOT imlipe Valambia US 60 Mil wanainterest gani kwenye hiyo kesi na ni wa kina nani hasa hii inapaswa kueleweka wazi wazi.Kwa kuwa kampuni iliyosupply hayo magari jeshini ni kampuni ya Valambia na kama kudai wanadai wao kwa kazi walioifanya hao wengine kinawahusu nini.Sasa hawa wengine wanaoishinikiza serikali ilipe interest yao ni nini hasa?

Au ndio wale wale wamaotaka kushinikiza malipo halafu wapate chajuu kwa kufanikisha deni kulipwa.Watanzania bwana ni watu wa ajabu kweli kweli,ubinafsi ndio uliowajaa wengi.Hapa kinachogomba ni maslahi ya watu binafsi, maskini Valambia wa watu amesota wee mpaka akapoteza uhai kwa kufuatilia deni lake.

Huku nyuma watu wanashinikiza deni lilipwe ili nao wafaidi huu nao ni ufisadi wa aina yake.Ingekuwa vizuri kama Gavana wa BOT akiweka majina ya hao wanaoweka shinikizo hadharani ili jamii iwatambue.

Ahsante sana kwa mchango wako mzuri. Ndullu inabidi ayaweke majina ya hao wanaoishinikiza BoT ili ilipe hizo pesa ili Watanzania tuwajue ni akina nani badala ya kuwaficha wahusika hao.
 
Mimi nafikiri wafanye kazi za kisiasa kwa sababu hizo firm zao zinawanyima watu wengine fursa kwa vile hawana ubavu wa kushindana nao katika kutafuta kazi
 
Compare with this which happened in Greece

The applicant is a 72-year-old Greek national who lives in Athens. The application concerns his forfeiture of his parliamentary seat on the ground that carrying on a professional activity disqualified him from holding such office. Mr Lykourezos has been a member of the Athens Bar since 1960. In April 2000 he stood in the parliamentary elections in the first constituency of Athens as a candidate on the "Nea Dimokratia" party's list. He obtained 44,387 votes and was elected as a member of parliament for a four-year term.

In 2001 a revision of the Constitution made all professional activity incompatible with the duties of a member of parliament. Such a disqualification is provided for in the new Article 57 of the Constitution, although the relevant implementing legislation has yet to be passed. In February 2003 a constituent lodged a complaint against the applicant with the Special Supreme Court, arguing among other things that, under Article 57 of the Constitution, his practising as a lawyer disqualified him from holding parliamentary office.

In a judgment of 3 July 2003 the Special Supreme Court allowed the complaint and ruled that the applicant had forfeited his seat. In particular, it dismissed the applicant's argument that he could not be deemed to be practising a profession as he no longer received any fees. Accordingly, the applicant was replaced as a member of the Chamber of Deputies by his substitute in July 2003.

Relying on Article 3 of Protocol No. 1, the applicant complained that his forfeiture of his parliamentary seat had infringed his right to be elected to the national parliament and had deprived his constituents of the candidate they had elected before his term of office had expired. He also alleged that the fact that he had forfeited his seat in order to be able to carry on his professional activities had amounted to unjustifiable interference with his private and professional life, in breach of Article 8.

Article 3 of Protocol No. 1
It was not the Court's task to state its view on the general prohibition on practising any profession. It confined itself to observing that the disqualification created by the new Article 57 of the Constitution, whereby members of parliament were prohibited from carrying on a professional activity, was rarely encountered in other European states.

However, the Court could not overlook the fact that the applicant had been elected in conditions not open to criticism, in accordance with the electoral system and the Constitution as in force at the time. Nobody could have imagined that his election might be called into question while his term of office was in progress on the ground that his simultaneously carrying on a profession was incompatible with his duties as a member of parliament. The applicant's disqualification on professional grounds during his term of office had therefore come as a surprise both to him and to his constituents.

In those circumstances, the Court concluded that by considering the applicant's election under the new Article 57 of the Constitution without taking into account the fact that he had been elected in 2000 in accordance with the law, the Special Supreme Court had caused him to forfeit his seat and had deprived his constituents of the candidate they had chosen freely and democratically to represent them in Parliament, in breach of the principle of legitimate expectation. The Greek Government, moreover, had not advanced any grounds of pressing importance to the democratic order that could have justified the immediate application of the absolute disqualification.

The Court therefore held that there had been a violation of Article 3 of Protocol No. 1.

Article 8
Having regard to its finding of a violation of Article 3 of Protocol No. 1, the Court did not consider it necessary to consider the case under Article 8 as well.

Article 41
Under Article 41 (just satisfaction) of the Convention, the Court awarded the applicant 20,000 euros (EUR) for pecuniary damage and EUR 14,000 for costs and expenses.
 
Hapa nina wasiwasi na umakini wa chadema

Maana wanamtuhumu huyu mkono kuwa ni fisadi mara wanakuja kwa kushangilia kuwa amesign pendekezo la kumtoa waziri mkuu pinda

This is to low kwa mkono na chadema
 
Back
Top Bottom