Nimrod Mkono kakisusia kijiji, JF okoeni kijiji hiki!

Bumangi na Zanaki kwa ujumla ina human resource kubwa sana, wengi wako hapo Dar, nadhani hawana utashi wa kuendeleza kijiji chao vingine wangeshatatua hiyo shida siku nyingi. Jaribu kuongea na watu hapo Dar utaelewa ninachosema.
Ushauri wangu ni kuwashawishi WAMANGI waliopiga hatua kubwa za kimaendeleo kukumbuka nyumbani. Achana na Mko huyo hana sera.

kitu ulichokiongea ni suala kubwa na lenye ukweli, i hope baadhi wapo humu walione hili........yani kijiji chetu kina wasomi wanaosifika but no one is bothered with the real situation ya bumangi, my God ligth upon me to success on this.
 
Ila nasikia nyie wa upande wa Zanaki (Bumangi, Makutano, Buhemba, Butiama, Butuguri, Kyarano, Lwamkoma, Bisyare, na wote along Musoma - Bunda road) hampendi huyo mbuge wenu, tofauti na watu wa upande wa ziwani, I mean Majita, that is why huyo mzee anawashiti sana, alichofanya amewajengea tu shule za sekondari nzuri na nyingi tu ili msome na muelimike - na ukizingatia mnamdharau kwa kuwa ni mzanaki mwenzenu na hamkumuona wakati mwl.akiwa hai (infact mnamsema kama mwl angekuwa hai wala asingekuwa mbuge kwa mnajua ni fisadi), wakati wenzenu wa ziwani wanakula maisha na wanamuona ni mkombozi na baba yao..and mind you huyo mzee alikubali jimbo lake liwe wilaya mbili Butiama na Musoma vijijini, ila hataki kuwe na majimbo mawili (musoma vijijini na Butiama) akiogopa nyie wazanaki mtamnyima kura kama atagombea jimbo la Butiama na wakati huo hawezi kwenda ziwani wakati yeye si asili ya huko..ushauri wangu, ombeni muwe na jimbo lenu la Butiama ili mtoe hukumu ya haki kwake, Ombeni kikao naye si cha kussurrender ila cha kumwambia ukweli kwamba tumekuchoka.
Ndugu mchangiaji nadhani hukufanya utafiti wa kutosha kabla ya kutoa maoni yako kuhusiana na mada hii.
Kama kuna eneo ambalo tangu nchi hii ipate uhuru limetelekezwa ni Musoma vijiji sehemu za Majita ambalo liko ziwani.
Eneo hilo halina huduma yeyote zaidi ya kibarabara ambacho nacho ni cha msimu kwa ajili ya kusaidia usafirishaji wa samaki wanaopatikana kwa wingi toka eneo hilo.Watu wa eneo hilo wanaishi kwa kunywa maji pamoja na Mifugo yao,hawana huduma za hospitali,umeme na hata Mazao yao yananunuliwa kwa bei ya kutupwa.
Mkono ameamua kutumia ukosefu wa huduma muhimu katika eneo hili kwa kuwagandamiza Wananchi wa Majita kwa kung'ang'ania Jimbo kutogawanywa pamoja na ukubwa wake na hii maana yake ni kwamba Majita itaendelea kubaki nyuma kimaendeleo.
 
Mtoa mada acha kulalamika Bumangi ni miongoni mwa vijiji vilivyosheheni wasomi wengi na wa kada mbalimbali. wasomi hao walipatikana wakati wa awmu ya kwanza na ya pili wakati Nyakiran'gani akiwa mwenyekiti wa scholarship board. wasomi wote mlio nao wameshindwaje kujimobilise mkapata maji na mbona usiwasemee watu wa Muriaza, Kizaru ambao kwanza hawwkupata upendeleo wa ndgu yako Nyakirang'ani.
Hivi kweli akina Tom Nyanduga na wenzake wote wanashindwa kupata wafadhili.kwa hili usimlaumu mkona hawezi kufanya yote. mengine wananchi nguvu zetu zinatakiwa,ebu tupe kwa ufupi ni juhudi gani zimefanywa na nyini wanachi ili mbunge awasaidie.

uko sahihi kabisa mkuu, tena inaonekana unajua kijiji hiki kwa ukaribu sana, kama nilivyowajibu baadhi ya wachangiaji hapo juu, ni kweli kwamba tuna watu waliosoma tena wana sifa kubwa lakini rudi kijijni kwao hakika hakilingani na hadhi na sifa walizonazo..........ikumbukwe sio wote tuna mawazo yanayolingana na kila mtu ana target zake, lakini binafsi napenda sana kuiangalia jamii yangu nilipotoka na matatizo yake na ndo maana nimefanya juhudi kama nilivyozitaja hapo juu, sijui una taka nifanye juhudi gani zaidi mimi kama mwananchi na ninayejaribu kutumia upeo nilio nao kutatua tatizo......tusilaumu wananchi wasiojua hili na lile ila tujilaumu sisi tunaojua nini cha kufanya lakini tumemua kuziba macho yetu kwa miwani ya mbao........nipo tiyari kuacha shughuli zangu endapo atapatikana mtu au mdhamini ili nisaidiane nae pamoja na wananchi wa bumangi kuhakikisha tunapata maji bumangi.............ngoja niwape na namba yangu kabisa kwa yeyote atakae kuwa tayari na ameguswa na hili suala kukutana na kulitafutia ufumbuzi pale inapobidi +255756282167
 
inawezekana kabisa wapo wengi sana maana hat huyu prof.dr. mj. wa hapa kama unaenda tegeta si nilisikia naye ni wa huko? anyway ngoja nimpigie bridedia mts anipe ufafanuzi,vinginevyo kila la kheri

ahsnte mkuu, kama unamfahamu mtu wa bumangi au una email yake please mforwadie hii thread, najua wapo akina nyanduga, mwasi, nyakirang'ani, msawa group na n.k.......nashukuru kwa wale walionipa link ya nimrod mkono, nimepata pale email yake na tayari nimeisha mtumia email yangu kuhusu kilio cha kijiji chetu.
 
Tafuta njia ya kuwakuitanisha wamangi hapo Dar muanzishe BUMANGI DEVELOPMENT FORUM nitakusaidia kukutafutia wamangi wenzako huku ughaibuni maana wamejaa tele na kuna wengine mpka wako jeshini USA

vile vile jaribu kumtumia Pasaka Erasto Nyamusika kupitia Coca Cola mpate msaada .
Vilevile kwanini kanisa la menonite hapo Nyamiselele lisipeleke agenda hii pale MEDA-Menonite Economic Development Agency maana hapo Bumangi ndo menonite hasaaa
 
Juzi nimekaona haka kazee kanarandaranda mitaa ya mlimani city,hakana mbele wala nyuma ilmradi tu anauza fuvu,kumbe jimboni kwake kuna shida ya maji hivyo. Shame on him,dhaifu.
Who is responsible to bring water to Bumangi, Mkono or serikali dhaifu?
 
Who is responsible to bring water to Bumangi, Mkono or serikali dhaifu?

mkuu kuleta maendeleo sehemu ni connection ya segment tofauttofauti ikiwemo wananchi wa eneo husika, viongozi na serikali kiujumla na pia hata mtu mmoja mmoja kwa nafasi yake
 
Tafuta njia ya kuwakuitanisha wamangi hapo Dar muanzishe BUMANGI DEVELOPMENT FORUM nitakusaidia kukutafutia wamangi wenzako huku ughaibuni maana wamejaa tele na kuna wengine mpka wako jeshini USA

vile vile jaribu kumtumia Pasaka Erasto Nyamusika kupitia Coca Cola mpate msaada .
Vilevile kwanini kanisa la menonite hapo Nyamiselele lisipeleke agenda hii pale MEDA-Menonite Economic Development Agency maana hapo Bumangi ndo menonite hasaaa

ahsante sana kidogo chetu kama kweli upo tayari kuwastua jamii ya kizanaki iliopo huko abroad juu ya khali halisi ya kwao, wambie bumangi ilipiga hatua kumi mbele hapo nyuuuma ila kwa sasa inarudi nyuma hatua 15 zaidi, ilikhaali wazawa tupo, tena wengi wao walisomeshwa kwa kukumbembelezwa na kupewa mahitaji yote, acha sisi tuliopigana wenyewe kufika hapa tulipo tena kwa kuandama bodi ya mkopo kila uchwao.........vile vile nitafurahi endapo wachangaaji mtani pm contact za watu mnaowajua (wahusika wa hili suaLA) ili iwe rahisi kuwafikishia hili suala.................kuhusu kikundi niliwahi kupata tetesi kuwa kilianzinshwa hapa dar japo goal yao kubwa ilikuwa ni masuala ya vifo, so i will work out kuhakikisha nawapata...................kuhusu kanisa la menonite ni kweli ndo dominant pale kijijini ila nilikuwa cjui kama wana michango katika sector ya maji, nadhani may be viongozi wa pale hawajiliweka hili katika kipao mbele.
 
hii ndo bumangi yetu, hapa ni kwenye vibao vya shule ya msingi na secondary bumangi, pls wamangi let us remember our home, jamii inapata shida while tupo tulowezeshwa na hii hii jamii kufika to the point we are
bumangi.jpg
 
Mkuu pamoja na uelewa wako wa maeneo hayo but u seem to miss something here, huko majita huyo jamaa hakuna kitu cha maana alichofanya hata sasa, zile shule amejenga kuenzi utemi wa watuguli na hana lolote, hebu taja shule moja nzuri aliyojenga huko Majita mkuu, vipi kuhusu Kyagata ambako hadharauliki kafanya nini cha maana huko?

nimechokoza ili muweze kumfikiria huyu jamaa (Mkono) vizuri, ila kwa shule zile alizojenga ni afadhali yake na ni hatua mojawapo aliyomaliza na kuanza ingine kwa ajili ya Majita na kiagata, safari ni hatua,
 
Kaka nafikiri ungejielekeza kwenye hoja kuliko kushambulia utu wa mtu. Jitahidi kuficha hisia zako kuhusu personality za watu.
Kanaudhi sana kazee, kamesoma sheria kana prestige zote.Badala kifurahie wengine kupata haki na heshima kinawatumia kama daraja la kupata diplomatic passport na kuendelea kandamiza nchi.Ndio maana hivi vitakataka vinamhofia Mengi sana.

Vinadhalilisha makabila yao,kuwa wakipata hawana uzalendo halafu vikienda sehemu vinadai kuwa sehemu zao hazikupendwa.Zipendwe vipi au kusaidiwa vipi iwapo watu wenye kufaidi nchi kuliko watanzania wa maeneo mengi wameshindwa fanya hata kile wafanyacho watanzania masikini.Kukumbuka na kuinua maeneo yao.

Hichi kizee hata bank yao haina adabu.hawataki wateja wa kampuni ndogo.Nadhani pia kingejitahidi kwa kutumia hela yake na sura yake ipate image anayoproject.Otherwise kipo kama kiganga aka sheikh yahaya
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom