Nimpe? Naomba ushauri

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,144
[h=3]Nimpe?[/h]

Je, ni muhimu wanandoa kusalimiana mnapoamka asubuhi?
Kwanza fahamu kwamba wanandoa wanapokaa muda mrefu baadhi ya vitu huanza kuchakaa kimapenzi. Hata hivyo upendo na wema husaidia kurudisha moto wa mapenzi na wanandoa kujiona wapya kila umri unavyozidi kuongezeka.
Matendo yanayoonesha wema kwa wanandoa ni gundi inayoshikisha wawili kujiona wapo karibu na moja ya tendo la wema ni kumsalimia mwenzako wakati mnaamka hata kama mmelala kitandani kimoja na hata mlikumbatiana usiku mzima au ulimuweka mwenzi wako kifuani usiku mzima.
Anayesalimiwa hujiona anapendwa, ana thamani na pia appreciated.
++++++++++++++++++++++++++
Tupo kwenye new millennium kiasi ambacho watu tupo busy hata kuamka tunahitaji kuweka alarm ituamshe hata hivyo badala ya kukimbia bathroom kuoga ni muhimu kumpa kwanza salamu mwenzi wako ndipo uendelee na kazi zingine au na ratiba yako.
Tafiti zinaonesha wanandoa ambao husalimiana asubuhi wanajiona ndoa yao ni nzuri sana na wana mahusiano yanayoridhisha.
++++++++++++++++++++++++++++++++
Je, nini kinafanya maneno ya salaamu ya asubuhi kuwa muujiza katika ndoa na mahusiano?
Unapomsalimia mwenzi wako maana yake unamwambia na kumpa ujumbe kwamba ni asubuhi njema tumeamka pamoja katika upendo na furaha na kwamba unajisikia vizuri kuanza siku mpya na mtu wako na pia unaweza msingi mzuri wa mawasiliana kwa hiyo siku mpya
 
waswahili wanasema salamu ni kitu cha bure. hata kama mmelala na ugomvi, ni ustaarabu wa kibinadamu kusabahiana asubuhi, tofauti yaweza kuwa kuwepo ama kutokuwepo kwa mabusu, tabasamu na maongezi kidogo. by the way, ukiskia alarm tu ukaruka kitandani unaweza anguka kwa mstuko wa moyo ama kizunguzungu.so hata kama humpendi sana ulienae kitandani,mtumie kujiamsha hadi utampenda. muamshe na kabusu on the lips,muulize umeamkaje,msimulie umeota nini,spit what is on ur mind kama una wasiwasi kuhusu ile issue then run to the bathroom.ukiudi hukawii kukuta kakuletea na bfast kabisaa,lol (leo najua sitochapwa,lol!)
 
Kama kuna wanandoa hawasalimiani asubuhi basi hiyo ndoa inakaugonjwa fulani. Msiposalimiana na kujuliana hali halafu watu wakakuuliza kama mkeo/mmeo hajambo unajibuje? Unadanganya kuwa hajambo?
 
Hapa kuna suala la utamaduni maana acha mke kuna vitoto vingine hata asubuhi havisalimii wazazi wao,yaani we acha tu maana wake wengine kichwa ngumu kama jiwe la buzwagi,mkiwa na kabifu utatamani uhame nyumba hadi gogoro liishe maana hata kama ana shida anakulima kimemo na kukuwekea dressing table,jamani ndo hizi!
 
Mi naonaga kimyakimya tu, labda kuagwa kwa busu na wakati mwingine tunapiga free tu
 
mi naonaga kimyakimya tu, labda kuagwa kwa busu na wakati mwingine tunapiga free tu

gaga embu tupe free style jamani tuokoe nanii za watu pengine zinaleta matanisho mtu akaacha kushika miguu ili kumuamsha mwenza kisa ajue anamwaga mwaya wangu nikiaga nikaoana kimya nabamizaga mlango kwa nguvu nikiwa natoka nasikia

hny ubarikiwe mungu akuhifadhi ..nakwambia nikisikia hilo hata insuarance iishe traffic akiona gari anaakimbia kwanza
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom