Nimfanye nn shemeji yangu huyu?

Washawasha

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
16,652
13,077
Habari zenu wanajamvi natumaini ni wazima wa afya. Jamani leo yamenikuta mwenzenu nikiwa namuaga kwa d*nda zito My nyumba ndogo wangu shemeji yangu wa kiume akaniona na kuniambia ya kuwa sio vizuri ninachokifanya na kuondoka zake na kwenda kumuambia dada yake ya kuwa ameniona,bac kidume kufika nyumbani nikakutana na kesi,mie nikakataa kuwa hakuniona na wala cna demu nje,ikabidi aitwe na kuulizwa anakubali kaniona na mie nakataa ya kuwa hakuniona na wala ckufanya hiyo kitu,mpaka sasa sijalala napigiwa kelele natishwa,nafinywa,napigwa na mito yaani vurugu humu ndani amani ishaanza kutoweka na My wife wangu kawa mkali ajabu. Je? Nimfanyeje shemeji yangu huyu.
 
nimfanyeje shemeji yangu maana yeye ndiye aliyekwenda kumuambia dada yake
 
nimfanyeje shemeji yangu maana yeye ndiye aliyekwenda kumuambia dada yake
sasa mkuu unataka kumpelekea sister wake mifugo ya HIV halaf unataka azime radio? mimi nahisi alikuheshim sana, kuna kes kama yako ilitokea , yule shemeji alimramba vichwa mume wa sister wake mbaya sana. mpaka leo kesi inaendelea, shemeji yuko nje kwa zamana
 
Oohhh dear
nimecheka ila
sijui ni kwa nini hata

Nway
Kumbuka damu ni
nzito kuliko maji dada atamwamini
kaka yake saa yeyot e. .
Anaweza akuache wewe lakini kaka
yake atakuwa naye milele..

Mie naona umwite huyo
Shem kesho uongee naye
Kikubwa na si kumtishia..
kwa sasa tembea kwa magoti
usiku uwishe..
 
Habari zenu wanajamvi natumaini ni wazima wa afya. Jamani leo yamenikuta mwenzenu nikiwa namuaga kwa d*nda zito My nyumba ndogo wangu shemeji yangu wa kiume akaniona na kuniambia ya kuwa sio vizuri ninachokifanya na kuondoka zake na kwenda kumuambia dada yake ya kuwa ameniona,bac kidume kufika nyumbani nikakutana na kesi,mie nikakataa kuwa hakuniona na wala cna demu nje,ikabidi aitwe na kuulizwa anakubali kaniona na mie nakataa ya kuwa hakuniona na wala ckufanya hiyo kitu,mpaka sasa sijalala napigiwa kelele natishwa,nafinywa,napigwa na mito yaani vurugu humu ndani amani ishaanza kutoweka na My wife wangu kawa mkali ajabu. Je? Nimfanyeje shemeji yangu huyu.

Umfanye nini kwani kakufanya nini??Si kasema kweli yake yaani we unaona unachofanya ni sahihi tuuu??Kamuombe msamaha na uache tabia ya Nyumba ndogoz maana Babu wa Loliondo umri unasonga usimtegemee saana kukuponya magonjwa yako utakayoyakwaa!!
 
Mpe zawadi huyo shemeji yako kafanya vizuri sana ivi wewe mdogo wako angemkuta mkeo anapigwa denda angekuambia lingekuwa kosa? mimi nafikiri huyo shemeji yako muombe msamaha na mpongeze kwa kufikisha ujumbe kwa dada yake inaonekana si mnafiki,. Na wewe punguza bwana kufanya hayo mambo hadharani by the way umeoa unamdhalilisha mkeo si tu shemeji kukuona hata majirani wakikuona ni aibu sana,,,. :crying:
 
Yote yeshasemwa.
Omba msamaha kwa mkeo na shemejio. Tena namsifu shemejio, kilichokuwa kinafuata ni Small house wako kupata kipigo.
 
Kitu cha kusikitisha, huoni kama umemosa!
Ulishafikiria kuwa mkeo ndio angefanya hivyo?

Unahitaji majuto ya kweli, ndipo uombe msamaha na kwa Mungu pia, if you have one!
 
hahahaha shemeji hana koromeo yeye yanamuhusu nini...
Wakifa na ngoma, yeye ndie atakaye achiwa watoto awatunze.

Yeye ndie atakaye hangaika na hospital bills.
Au wewe ndie utakaye lea yatima?
 
Omba msamaha kwa mkeo, akusamehe yaishe.Kumbuka kweli itakuweka huru siku zote na utakuwa mwenye amani na furaha tele maishani mwako.
 
Dah, wanaume??????
Sina hata cha kushauri manake mi naona umekosa, wakati wewe huoni kama umekosea!!!!!
 
Mie najiweka pembeni kabisa, kweli umekosa lakini huyo shemeji yako nae mmmhhh ana kiherehere kwani dada yake hayajui hayo siku zote?? Hata kama umekosa angekufata akwambie nyie wote wanaume manatakiwa kuzungumza kiume sasa yeye mbio kwa dada YATAMSHINDA na huo ni umbea hata kama anasema kweli inahuuuuu????? Mambo ya ndoa za watu waachie wenyewe kha???? Dume zima mdomo waaa hana haya huyo mtoto wa mama nini??? Mwanaume anakuwa hana siri hata kama ni mbaya kiasi gani???
 
Habari zenu wanajamvi natumaini ni wazima wa afya. Jamani leo yamenikuta mwenzenu nikiwa namuaga kwa d*nda zito My nyumba ndogo wangu shemeji yangu wa kiume akaniona na kuniambia ya kuwa sio vizuri ninachokifanya na kuondoka zake na kwenda kumuambia dada yake ya kuwa ameniona,bac kidume kufika nyumbani nikakutana na kesi,mie nikakataa kuwa hakuniona na wala cna demu nje,ikabidi aitwe na kuulizwa anakubali kaniona na mie nakataa ya kuwa hakuniona na wala ckufanya hiyo kitu,mpaka sasa sijalala napigiwa kelele natishwa,nafinywa,napigwa na mito yaani vurugu humu ndani amani ishaanza kutoweka na My wife wangu kawa mkali ajabu. Je? Nimfanyeje shemeji yangu huyu.
Huna kitu cha kumfanya, maana alikuwa sahihi kumjulisha dada yake kitu alichoona ili dada yake ajihadhari na wewe. Kumbuka wewe sio ndugu wa hao wawili yaani (mkeo na shemejio). Kwanza nafikiri huyo shemeji yako alikuheshimu sana maana kama ni hao mashemeji waliopinda, naamini usingekwepa adhabu ya kipigo. Najua huwezi kuiacha nyumba yako ndogo maana tayari umeshikwa na "adui" Kama ni wale wenye hofu ya mungu ningekuambia uache tabia hiyo mara moja maana ni hatari kwako na familia yako. Majuto ya haya mambo ya kuhangaika ni mabaya kupita unavyofikiri.
 
Wakifa na ngoma, yeye ndie atakaye achiwa watoto awatunze.

Yeye ndie atakaye hangaika na hospital bills.
Au wewe ndie utakaye lea yatima?

wewe unaona tatizo ngoma tu ambayo hata ukipata haufi kesho,na hizo hosp bills uliambiwa ukiwa na ukimwi peke yake ndio utapaswa kuzilipa,vipi kuhusu malezi ya watoto ambao wazazi wametalakiana kwa upumbavu wa shemeji unafikiri wao hawana haki ya kuishi na wazazi wao wawili,tufikiri kabla hatujatenda na tuachane na mambo ya watu hata kama ni kakako au dadako hayatuhusu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom