Nimfanye nini huyu Mwanamke?

Mimba ya mkeo imetoka kwa sababu ya mshtuko wa kufiwa na kaka yake, ila kwa kuwa haiwezi kutoka siku hiyo hiyo ndo maana matokeo yakaonekana akiwa safarini. Hivyo basi msamehe na maisha ya aendelee.. hata asingesafiri hiyo mimba ingetoka tu.. trust me!
Mayasa good point, lakini mpeni pole huyo mwanamke mwenzenu aliye olewa na mwanaume kama huyo mtoa mada.
 
Wewe ni Mwanaume,kuna tofauti kati yake na wewe,Wanawake ni viumbe dhaifu,ishi nao kwa akili
Hizi double standards huwa zinanifurahisha sana, yaani mwanamke anakuwa dhaifu only for her own convenience. Kila siku mnapiga mikelele me=ke ila zinapokuja ishu kama hizi, mnaleta ishu za mwanamke dhaifu sijui nini, Mi nadhani inabidi ifikie mahali tuset standards tu either ke ni kiumbe dhaifu au ke=me kuliko hii michanganyiko iliyopo sasa hivi.
 
Mke wangu nimedumu naye kwa miaka minne sasa, katika ndoa yetu tumebahatika kupata mtoto wa kiume mmoja, na baada ya mtoto kutimiza miaka mitatu, tuliamua tupate mtoto mwingine. Tumefanya majaribio kadhaa kwa takriban miezi tisa lakini mke wangu hakushika mimba. Tukaenda kwa wataalamu na baada ya kushauriwa na kupewa tiba, ndipo mimba ikashika, lakini ilianza na matatizo na akahitajiwa akae Bed Rest.

Wakati ujauzito wa mke wangu ulipotimiza miezi miwili, hivi karibuni akapata msiba wa kaka yake aliyemlea. Mimi sikuwepo mjini kwa sababu nilisafiri kikazi mikoani. Alinipigia simu kunipa taarifa za msiba na akanijulisha kwamba mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda kijijini kwao kwa mazishi. aliniaga kwamba na yeye atasafiri na mwili wa marehemu kwenda kuzika. Nilimshauri asisafiri kutokana na hali yake, na nilimuhakikishia kwamba nitakaporudi nitafanya utaratibu ili twende tukahani msiba. Alikataa katakata na akanioana mimi ni mbaya kwa sababu nimemkatalia kwenda kumzika kaka yake aliyemlea na kumsomesha. Nikamwambia aende lakini sitahusika na lolote litakalotokea akipata matatizo.

Ni kweli aliamua kwenda lakini akiwa njiani alipata matatizo na ikabidi akimbizwe hospitai ya karibu na ule ujauzito ukatoka. Hakumudu kuendelea na safari na wala hakuhudhuria mazishi ya kaka yake. Nimezipokea taarifa hizi kwa uchungu sana. Sasa najiuliza nikirejea nimfanye nini huyu mwanamke?
Ukipenda, tukio hili linaweza kuwa sababu tosha ya wewe kuwa mwanaume anayeheshimiwa na kusikilizwa zaidi duniani na mkeo. Kama bafuni vile, unaweza zungusha kitufe cha maji ya moto au ukazungusha kitufe cha maji baridi. The choice is yours!
 
The Boss nakubaliana na wewe, lakini pale ambapo mume anatoa ushauri tena wa msingi halafu ukapuuzwa, basi hapo kuna walakini. Na huyu amekuwa mtovu wa nidhamu, kushindwa kumtii mumewe wa ndoa.

Mhhhh! kweli "kuishi kidogo unaona mambo mengi", mkuu ni wakati gani hatakiwi kutomtii mume/mke! kwa wale ambao "common sense zao ni common" wataona kabisa huyu mama/mdada hakukaidi amri/hana makosa!
hebu huyo bwana avae kiatu cha mkewe alafu aseme yeye angefanyanye!
pia akumbuke kuwa chochote atachomfanya hakitarudisha mimba! akubaliane na ali halisi,
wengina uzaa kabisa na bado watoto wanakufa! mengine yako ndani ya uwezo wa Mungu!
 
Nature ya kazi yangu huwa nasafiri kikazi mara kwa mara, na kutokana na hali hiyo nimemuwekea wasichana wa kazi wawili, yote hiyo ni kutaka kuhakikisha anakuwa akihudumiwa wakati wote. Naamini nimekujibu FF
Jibu ni zuri sana na nimeridhika. Kwa hiyo, Kama wewe umeona nature ya kazi yako ni bora na ukubali kuwa na na yeye nature yake ni kumzika kaka yake. Hilo la kumuwekea wafanyakazi sio muhimu sana kwani kwanza, hukumuwekea, mmewaweka. Halafu pili hiyo mimba ni yako na kuitunza ilibidi uwe karibu nae wakati wote, kilichokuzuwia ni "nature" ya kazi yako.
 
Mimba ya mkeo imetoka kwa sababu ya mshtuko wa kufiwa na kaka yake, ila kwa kuwa haiwezi kutoka siku hiyo hiyo ndo maana matokeo yakaonekana akiwa safarini. Hivyo basi msamehe na maisha ya aendelee.. hata asingesafiri hiyo mimba ingetoka tu.. trust me!

Mayasa acha uongo, kwani mimba inachukua siku ngapi ili itoke! wiki, mwezi!
 
Asiyesikia la mkuu,msamehe tu,naamini hakutegemea kama ujauzito ungetoka.Akili yote iliishia kwenda kumzika kaka yake.BIBLIA INASEMA "ENYI WAUME ISHINI NA WAKE ZENU KWA AKILI MAANA NI VIUMBE DHAIFU"

Na ni vumbe dhaifu kinomaaa!
 
Mke wangu nimedumu naye kwa miaka minne sasa, katika ndoa yetu tumebahatika kupata mtoto wa kiume mmoja, na baada ya mtoto kutimiza miaka mitatu, tuliamua tupate mtoto mwingine. Tumefanya majaribio kadhaa kwa takriban miezi tisa lakini mke wangu hakushika mimba. Tukaenda kwa wataalamu na baada ya kushauriwa na kupewa tiba, ndipo mimba ikashika, lakini ilianza na matatizo na akahitajiwa akae Bed Rest.

Wakati ujauzito wa mke wangu ulipotimiza miezi miwili, hivi karibuni akapata msiba wa kaka yake aliyemlea. Mimi sikuwepo mjini kwa sababu nilisafiri kikazi mikoani. Alinipigia simu kunipa taarifa za msiba na akanijulisha kwamba mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda kijijini kwao kwa mazishi. aliniaga kwamba na yeye atasafiri na mwili wa marehemu kwenda kuzika. Nilimshauri asisafiri kutokana na hali yake, na nilimuhakikishia kwamba nitakaporudi nitafanya utaratibu ili twende tukahani msiba. Alikataa katakata na akanioana mimi ni mbaya kwa sababu nimemkatalia kwenda kumzika kaka yake aliyemlea na kumsomesha. Nikamwambia aende lakini sitahusika na lolote litakalotokea akipata matatizo.

Ni kweli aliamua kwenda lakini akiwa njiani alipata matatizo na ikabidi akimbizwe hospitai ya karibu na ule ujauzito ukatoka. Hakumudu kuendelea na safari na wala hakuhudhuria mazishi ya kaka yake. Nimezipokea taarifa hizi kwa uchungu sana. Sasa najiuliza nikirejea nimfanye nini huyu mwanamke?

shukuru mungu mkeo hajafa mzee..mtoto utapata mwingine ningekuelewa kama huyo mtoto angekuwa adult na umemgharamikia malezi na elimu na akafa kabla hajaanza hata kazi...kikubwa ni kumshukuru mungu kwa kuzidi kumpa uhai wife... Fikiria ungekuwa ni wewe ndo una ujauzito na kaka ako kafariki na unjihisi una weza kwenza kuzika usingeenda??
 
Samehe broda, kama ni fundisho amekwisha pata

Sent from my HTC Incredible S using Tapatalk
 
The Boss nakubaliana na wewe, lakini pale ambapo mume anatoa ushauri tena wa msingi halafu ukapuuzwa, basi hapo kuna walakini. Na huyu amekuwa mtovu wa nidhamu, kushindwa kumtii mumewe wa ndoa.
Nimesoma kwa kina hii post yako, nimesoma comments za waungwana weingine pia. Kauli yangu kwa hili, mkeo anastahili kupewa suspension ya hata 3 months...naongea hivi nikiwa nimeoa na mtoto juu. Huu ni ujinga kusingizia eti kuchanganyikiwa, upendo etc etc, nani hajawahi kufiwa na mtu wa karibu kuweza ku experience the same feeling ambazo wengi husingizia eti ndiyo sababu kama baadhi yetu tunavyotaka kujenga hoja. Huu ni utovu wa nidhamu, na dharau kwa sura nyingine. Mme kashauri kwa maana ya kuona nini mbele kinaweza tokea lakini matokeo yake ndiyo hayo wote tunasikia mhusika akiyalalamikia.....by the way kuwahi au kutowahi mazishi kunasaidia nini, kama mtu kafa kisha kufa tayari, so what? Ujinga na visingizio ndiyo imekuwa utamaduni wa Watanzania..tunapaswa kubairika sana. Na personally kama ni mimi hatua ya kwanza ni kwenda Likizo akajifunze kuelewa nini mwenzi wako anasema na kwa wakati gani na sababu zipi.POLE SANA MTU MZIMA, JIPE MOYO MUNGU ATAKUSAIDIA NA UTAPATA TU KAMA ALIVYOKUATIA WA KWANZA.
 
Lakini lazima nimuonyeshe kwamba amenikosea, na hivyo lazima apate adhabu japo kidogo!

Kuna wanaume mna roho mbaya huku duniani.Umpe adhabu kwani yeye mtoto wa darasa la kwanza,hapo wewe kinachokuuma ni
mtoto tu wala siyo hali ya mke wako,eti
tumetumia gharama,gharama kitu gani mbele ya
afya ya mke wako.

Ila nimejifunza kitu kumbe dili sio kuolewa tu, ila ni unaolewa na mtu wa aina gani.Asante Mungu kwa kunifunulia hili.
 
Nimesoma kwa kina hii post yako, nimesoma comments za waungwana weingine pia. Kauli yangu kwa hili, mkeo anastahili kupewa suspension ya hata 3 months...naongea hivi nikiwa nimeoa na mtoto juu. Huu ni ujinga kusingizia eti kuchanganyikiwa, upendo etc etc, nani hajawahi kufiwa na mtu wa karibu kuweza ku experience the same feeling ambazo wengi husingizia eti ndiyo sababu kama baadhi yetu tunavyotaka kujenga hoja. Huu ni utovu wa nidhamu, na dharau kwa sura nyingine. Mme kashauri kwa maana ya kuona nini mbele kinaweza tokea lakini matokeo yake ndiyo hayo wote tunasikia mhusika akiyalalamikia.....by the way kuwahi au kutowahi mazishi kunasaidia nini, kama mtu kafa kisha kufa tayari, so what? Ujinga na visingizio ndiyo imekuwa utamaduni wa Watanzania..tunapaswa kubairika sana. Na personally kama ni mimi hatua ya kwanza ni kwenda Likizo akajifunze kuelewa nini mwenzi wako anasema na kwa wakati gani na sababu zipi.POLE SANA MTU MZIMA, JIPE MOYO MUNGU ATAKUSAIDIA NA UTAPATA TU KAMA ALIVYOKUATIA WA KWANZA.

Afadhali wewe umeliona hili, watu humu wamenishambulia sana na kunifanya kama situmii akili. Nilishasema, nitamsamehe lakini lazima a-face concequences, nikimuacha hatakoma huyu, ataendelea kuniletea dhereu. Mimi ni mstahimilivu, na ananijua, lakini pale ninapooneshwa dhereu tena za wazi, huwa nakasirika kupita kiasi na maamuzi yangu yanakuwa ni mazito. analijua hilo!
Hata mimi huwa akinionya jambo kwa kunieleza kwa makini madhara ya kufanya jambo hilo naacha mara moja. nakumbuka kuna siku ilikuwa nisafiri kwenda Congo DRC kikazi akanishauri nisiende kutokana na hali ya usalama ya kule. nilifuata ushauri wake na nikatafuta sababu na ile safari akapewa mwenzangu na mimi nikabaki Dar. yule mwenzangu aliyesafiri alifika salama, lakini wakielekea kwenye eneo la kazi, gari liliowabeba lilipinduka na wenzake wawili walipoteza maisha, yeye na dereva wa gari lile walipona lakini waliachwa na majeraha mengi mwilini. Taarifa zile zilituifikia, na zilitushtua sana. Nilimetumia muda mwingi kumtahadharisha juu ya uamuzi wake wa kusafiri ilhali alitakiwa kuwa bed rest, lakini akakaidi. Je hizi si dhereu?
 
Mwanaume una roho wewe.
Eti aface concequences. . .
Kwani unadhani yeye anachekelea kumpoteza huyo mtoto?Kumbuka yeye ndie mama, yeye ndie aliekua amebeba hiyo mimba kwahiyo usijifanye unajua uchungu sana kuliko yeye. Kama una sababu nyingine zakumlipukia bora useme kuliko kusingizia sijui dharau na mengineyo.Hizo gharama unazolalamika mmetumia akisema atakurudishia je hasira zitakuisha?Maana umeng'ang'ania sana gharama.Kama huyo mtoto was not meant to be angeweza akampoteza hata akielekea chooni.

Kuhusu adhabu hicho kitendo cha kupoteza kichanga chake tu ni adhabu tosha.Kama huwezi kuelewa hilo basi wewe ni mwanaume wa ajabu sana na huna huruma wala mapenzi kwa mkeo hata chembe. Unajali gharama tu, mwambie akurudishie gharama zako basi, au mnyime chakula mwaka mzima ili ufidie gharana zako na amani irudi.
 
Ckia 2 kua mwenzio kafiwa lakin ucfiwe wewe! Km hakua ridhiki yenu mimba ingetoka 2 4 any mins. Msamehe mkeo coz yeye anaumia zaid yako. Kapoteza kaka ake pa1 na mwanae.
 
Mwanaume una roho wewe.
Eti aface concequences. . .
Kwani unadhani yeye anachekelea kumpoteza huyo mtoto?Kumbuka yeye ndie mama, yeye ndie aliekua amebeba hiyo mimba kwahiyo usijifanye unajua uchungu sana kuliko yeye. Kama una sababu nyingine zakumlipukia bora useme kuliko kusingizia sijui dharau na mengineyo.Hizo gharama unazolalamika mmetumia akisema atakurudishia je hasira zitakuisha?Maana umeng'ang'ania sana gharama.Kama huyo mtoto was not meant to be angeweza akampoteza hata akielekea chooni.

Kuhusu adhabu hicho kitendo cha kupoteza kichanga chake tu ni adhabu tosha.Kama huwezi kuelewa hilo basi wewe ni mwanaume wa ajabu sana na huna huruma wala mapenzi kwa mkeo hata chembe. Unajali gharama tu, mwambie akurudishie gharama zako basi, au mnyime chakula mwaka mzima ili ufidie gharana zako na amani irudi.

Halafu wewe nakuona hata hujaelewa nini kinagombewa hapa...issue siyo gharama issue ni kutokusikiliza mwenzi wako anasemaje.
 
Ingekua sehemu aliyokua anataka kwenda ni harusini, bar, sokoni ningeelewa kwasababu hizo ni sehemu ambazo sio lazima. Msiba ni ishu nyingine kabisa, ndio maana watu hua wanatumia maelfu ya dollar kusafiri kuzika ndugu zao, kinachosababisha hayo yote ni umuhimu na ukaribu kati ya huyo kaka na dada yake. Kama wewe binafsi huwezi kufanya hivyo ni sawa kwako, ila huwezi lazimisha kila mtu awe na hisia zinazofanana na zakwako.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom