Nimfanyaje huyu house girl wangu

Unastahili kupata yote hayo maana umezidi. Na naamini ulikuwa na akili timamu wala sio ulevi. Na huyo dada anastahili kukufanyia hayo anayokufanyia. Na ukimfukuza ujue habari imefika kwa mkeo na hapo anakuheshimu tuu wala sio kingine.
 
Naomba unipe huyo H/G jamani maana ni wachache wenye maadili kama huyu hongera zake ..
..Na pia tabia yako ni mbaya usisingizie maji.
Sakata umelianzisha mwenyewe inabidi utafute namna ya kusolve .
 
Khhhhhaaaaaaaaaaaaa mkuu si asavali hata ungeenda Meeda pale au Kona Bar Dada wa kazi !! mweeeeee umemdhalilisha sana mkeo, pole sana
 
...mimi nadhani umwambie ukweli mkeo ili awapatanishe.
Hakuna suluhu nyingine hapo, umekalia 'bomu!'
 
.............mke wangu alikuwa amelala hospitali akimuuguza ndugu yake

Yaani mke wako anauguza ndugu yenu na amelala hospitali wewe unaacha watoto na unakwenda kunywa hadi masaa ya lala salama? Umesahau ndugu ya mke wako ni wenu wote..na umesahau watoto..na umekumbuka pombe na HG?

Yaani bila aibu umeweza kuandika hapa.. duh! inataka moyo sana!
 
HIvi unauliza sababu hujui ao? Ukimkosea mtu unafanya nini? Hapo umemkosea housegirl sababu ulijaribu kutumia nguvu zako za boss na za kiume kwa kumnyanyasa kimapenzi. Kwa lugha nyingine it was sexual harrassement in a professional environment. Kama kweli you regret it and you are sure hauto rudi tena muombe msamaha.
Pili umemkosea sana mke wako kwa kumtaka mwanamke mwengine (bahati yako alikunyima). You had the intention of cheating on her. Yeye pia unatakiwa kumwambia na kumuomba msamaha (ila hapa nakushauri usubiri atoke hospitali na awe katika mood nzuri kidogo).
Ukimfuta dada sababu ya makosa yako utakua umemuonea ila kumweka hapo baada ya tukio hilo utafanya nyumba nzima iwe uncomfortable. Nakushauri umtafutie kazi else where au umtume kwao na hela kidogo akanze ka biashara ka kiushikaji.
 
Kabisa Russian. Hapo amefanya kosa kubwa sana. Wife yuko hospital anauguza badala hata ya kumfikiria kule aliko yeye tamaa yake ya ngono anataka kumbaka housegal. Hajawafikiria mke na ndugu aliyelazwa hospital na hata watoto wake yeye mawazo yake yako kwenye ngono.
Kwanza hakuwa na ulevi wowote ni tamaa yake ya ngono ilimtuma. Huwezi ukawa na ulevi uwe na jeuri ya kutaka kumbaka housegal.
 
kaka kwa usalama wako ni lazima ukomae ule mzigo huo,, ama sivyo uko kwenye hatari kubwa
 
Wandugu kwema?
Jamani mimi ni mdau wa humu siku nyingi sana ila nimekutwa na makubwa mwenzenu.

Siku tatu zilizopita mke wangu alikuwa amelala hospitali akimuuguza ndugu yake. Baada ya mimi kuwa huru basi nakaamua kutandika maji ile kisawasawa. Nilirudi majira ya saa tisa usiku nikiwa niko bati. Nilivyofika nyumbani dada akanifungulia mlango. Akili yangu ikanituma nimuombe dada penzi. Yule dada akawa mkali sana, nikajaribu kumlazimisha kwa kumshika akaning'ata mkono na kukimbilia chumbani kwake.

Basi nikaogopa watoto wasije wakaamka kwani walikuwa wamelala na bibi yao yaani mama yangu. Huyu dada sasa hivi namwona aibu na ninaogopa asije akamwambia wife. Shida ninayoipata nikamsalimia haitiki, nikimtuma kitu hafanyi kwa kweli ananidharau sana. Pia inabidi niwe karibu na wife mda wote kwani naogopa asije akamwambia.

Nimeomba ushauri kwa baadhi ya marafiki wengine wananiambia nikitaka niwe salama eti nihakikishe natembea nae na wengine wananiambia nimshawishi mama tumfukuze kazi.



Kama hii sio hadithi, , u get what u deserve. Yaani hata huoni aibu kuandika huu UPUPU. Na atakutengenezea fumanizi ndo utarudi hapa JF ukilia. SHAME on YOU.. yani mkeo kupata mgonjwa ndio imekuwa sherehe kwako. Watu wengine bwana ptuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu mbaaakaa. (kama nimekuuzi nipotezee tuu)
 
Ukware wako umekuponza,acha kusingizia pombe inaonesha mzee huchagui hubagui atakeyupa ni nani,acha ukware ndugu utakuja jidhalilisha buree
 
Naomba unipe huyo H/G jamani maana ni wachache wenye maadili kama huyu hongera zake .

Sio maadili huyo bosi mwenyewe mbayaaaaaaaa!!!! ole wako umpeleke kwako wakati maihazibendi wako handsome utajuuuuuta.
 
Mbona hapo kwenye rangi nyekundu pana tofauti kubwa sana na hapa pa bluu..!

Join Date : 3rd August 2011
Posts : 3

Rep Power : 0

Uongo kwenye jukwaa si mzuri... uadilifu uko wapi..?
Ukidanganya kwenye madogo utazoea utahamia kwenye makubwa...
Watu wabaya (wakiwemo na mafisadi) wanaanza hivi..!
 
Wewe Kwanza ni mtu wa ajabu kabisaaaaaaaaaaa, mdada huyo ni mtu nuhimu saana anasthili hata zawadi kwanza kakutia adabu cha mno alichonacho nini ambacho mkeo hana? na usiku mmoja tu ndo unafikia hata kumvunjia heshima mkeo! hakika wewe niwa ajabu mno! Ushauri wangu Jishitaki mwenyewe kwa mkeo na umweleze mkeo kuwa ulijaribu ukashindwa kwa sababu ya msimamo mzuri wa dada huyo nina hakika mkeo atakusamehe tu na dada huyo ataendelea kukuheeshimu maaana hata yeye sasa yuko kwenye tension akijua atafukuzwa tu maana ndio utaratibu wa wababa fake kama wewe mkijaribu mkashindwa mnawafukuza kwa visingizio, ukimfukuza ujue ajaye atakukubalia akuambukize UKIMWI UFE NA UMUUE NA MKEO NA FAMILIA IISHIE HAPO. Dada huyo big-up.
 
Wandugu kwema?
Jamani mimi ni mdau wa humu siku nyingi sana ila nimekutwa na makubwa mwenzenu.

Siku tatu zilizopita mke wangu alikuwa amelala hospitali akimuuguza ndugu yake. Baada ya mimi kuwa huru basi nakaamua kutandika maji ile kisawasawa. Nilirudi majira ya saa tisa usiku nikiwa niko bati. Nilivyofika nyumbani dada akanifungulia mlango. Akili yangu ikanituma nimuombe dada penzi. Yule dada akawa mkali sana, nikajaribu kumlazimisha kwa kumshika akaning'ata mkono na kukimbilia chumbani kwake.

Basi nikaogopa watoto wasije wakaamka kwani walikuwa wamelala na bibi yao yaani mama yangu. Huyu dada sasa hivi namwona aibu na ninaogopa asije akamwambia wife. Shida ninayoipata nikamsalimia haitiki, nikimtuma kitu hafanyi kwa kweli ananidharau sana. Pia inabidi niwe karibu na wife mda wote kwani naogopa asije akamwambia.

Nimeomba ushauri kwa baadhi ya marafiki wengine wananiambia nikitaka niwe salama eti nihakikishe natembea nae na wengine wananiambia nimshawishi mama tumfukuze kazi.
kwanza hata mimi tu hapa nishakuzaliwa sana maana kama ungekuwa una utimamu eneo la 'haya' ungeona aibu hata kutuuliza swali la namna hii ambalo limeweza kunionesha sura halisi ya tabia yako ilivyo mbaya
 
Dah! Kweli maisha ya ndoa yataka moyo. Wanaume kama nyie hivi ni lini mtawaheshimu mama zetu jamani? Yaani unamdhalilisha mkeo kwa kisingizio cha pompe kweli......jamani jamani jamani!!! Afu unataka hg akuheshimu ilhali we mwenyewe hujiheshimu. Ukweli ndo huu, we ulikuwa umempania tu huyo dada toka siku nyingi wala usisingizie pombe ni tamaa zako tu za kungonoka tena ningekuwa mi ndo hg ningekusiliba ngeu moja tu ya uhakika ili uje ujisemee mwenyewe kwa mkeo na kwa mama yako pia. Hizo dharau za hg inabidi uzizoee tu coz we ndo ulizitaka na vilevile hata ye ulimdharau pia lasivyo umuombe msamaha. Na ukimfukuza uje hapa ututaarifu pia utupe na adress yako ili kama umemfanyia ufirauni tukushikishe adabu!
 
Back
Top Bottom