Nimfanyaje huyu dada? Yamenikuta leo asbh

Amekudhalilisha vipi kwa jirani yako?

she was trying to captivate you in love, she believes to be the only one and very unfortunately she thought her dreams failed unknowingly!msamehe jamani hakujua huyo ni nani na alikuwa na matumaini makubwa sana!haya ndo maisha yetu, sidhani na sijui ni kwanini watu tunakuwa a mawazo ya haraka sana kabla ya kuwa na uhakika wa mambo!vilevile na wewe unaweza kuwa ulimuonesha sana mambo fulani yakamteka si unajua!au alikuwa frastruted akahis utakuwa kimbilio lake!mambo ni mengi!
 
Kiukweli mazungumzo yenu kwenye gari ndio yatakayotusaidia sisi ili tuweze kukushauri vilivyo,anyway it happen
 
Alijua keshapata buzi, tena buzi lina gari! bahati ilioje, hapo ni kama umempa za uso. Achana nae kwani anakupunguzia nini amwache akajaribu kwingine ndoano yake inaweza kunasa
 
wewe lift unawapa wanawake tu???
au wanaume huwaonagi wakihangaika na tabu ya usafiri,...??
pole nadhani ulitaka kutumia gari yako kama chambo cha kupatia wanawake.....na ukawapata kweli.....
kifupi,usimpe huyo dada lift tena ukimuona uchune atajifunza kusonya watu asiowajua,uchune kabisaaa kama hujamuona kwanza una mtu mwingine wa kupiga naye stori kwenye gari (jirani) incase boredom ndio inakusumbua....
and second,jifunze kutokana na hii experience ya kusonywa kuwa OPEN,huyu dada wa pili asije akapata bichwa kwa kuona mwenzie 'kaachia ngazi' hivyo kumpa false hopes yeye kawa 'promoted' mwambie wazi kilichotokea na unafanya hivyo kama msaada tu na si vinginevyo...ili na yeye asipate matumaini ya kukuzoa...
mwisho OA uwe unampe lift mkeo tu.......ukionyesha udhaifu kuna wanawake ni mapapa yapo kuwinda tu shaurilo....
 
duh mkuu nje ya mji siwezi hata kuchangia
nawezaingia choo cha kike mpwa nje ya mji malizaneni na anje ya maji
 
kama leo kakususia wewe kesho unataka umpe lift ya nini? sema na wewe una lako jambo. hebu funguka maana unatuminyia hapa kiasi tunashindwa kukupa mawazo muafaka.

Ndg naombeni ushauri maana najua kesho tena naweza kumkuta eneo lile lile na sijui nichukue uamuzi gani wa busara, msaada pliz!
 
Mimi najiuliza huyo dada anamfahamu huyo jirani yako?isije ikawa walishagombana??....jamani kukosa lift na mvua ndo zimeanza kunyesha..mbona kazi?????
 
Ushauri wa bure. Achana naye atakuletea balaa kama angekuwa mkeo je? Kwa nini akasirike naye ulikuwa unamsaidia tu unless katika mazungumzo yenu katika siku mbili tatu ulizompa msaada wa usafiri ulitamka kitu ambacho kilijenga matumaini kwake!!
 
Gari yako, umenunua kwa hela yako unahangaika na hao viruka njiia wa nini. Piga mwenda usitoe lift kwani ana hisa kweye gari yako. Chunga sana what huyo angekuwa mkeo? Kuna vitu vingi hatutaki kuhoji ila huyo binti inaonekana umeshakula apple lake. Kwa heri!
 
Gari yako, umenunua kwa hela yako unahangaika na hao viruka njiia wa nini. Piga mwenda usitoe lift kwani ana hisa kweye gari yako. Chunga sana what huyo angekuwa mkeo? Kuna vitu vingi hatutaki kuhoji ila huyo binti inaonekana umeshakula apple lake. Kwa heri!

Kwani amesema ana ma apple Caroline....?
 
Hii ni kali!
Nimesoma hadithi nyingi, huwa zinaelekeana lakini ya kwako hii ni ya aina yake!
Wanawake wana wivu sana na ni roho mbaya kichizi!

Lakini wewe mwenyewe huenda hujatulia, unaweza kukuta unajieleza mambo mazuri tu, usikute ushalikoroga sana na huyo mdada wa watu siku za nyuma!...kwanini asonye wakati hajui kuwa huyo ni dada yako au shangazi yako?
Anaijua tabia yako huyo mkuu!..badilika!

You're genius bro.
 
Ni wiki chache zimepita tangu nihamie kwenye kibanda chungu nilichojenga nje ya mji. Kwa sababu ya umbali wa ninakokaa na foleni za magari, inanilazimu kuondoka nyumbani kumi na mbili kasoro kuwahi traffic jam. Siku ya kwanza nikiwa kwenye gari yangu nilikutana na huyu binti aliyesababisha leo niombe ushauri. Alikuwa anajitembelea pembeni ya barabara akielekea kazini. Kwa kuwa sikumfahamu, nilimpita.
Kesho yake muda kama huo nilikutana naye tena, aliniangalia sana, lakini nikampita. Siku ya tatu nikamkuta tena kwa huruma nikasimama, na kumkaribisha lifti mpaka mjini ambako kila mtu alielekea kzn kwake. Basi tangu siku hiyo ikawa ndo kupeana lifti na mazungumzo ya ndani yalikuwa ni salamu tu.
Juzi amehamia jirani mwingine mdada ambaye amejenga nyumba karibu na kwangu kabisa. Baada ya kutambulishana na jirani huyu, akaomba nayeye awe anapata lifti ya kwenda kazn. Nilimkubalia.
Cha kushangaza, leo nilimpa lifti jirani yangu huyu mpya ambaye alikaa siti ya mbele ya gari. Hatua chache mbele kidogo nikakutata na huyu mdada wa siku zote, kama kawaida nikasimama.
Akaja, akafungua mlango wa mbele, baada ya kugundua kuwa kuna dada mwingine amekaa siti ya mbele, akafyonza na kufunga mlango kisha akazira na kukataa kupanda gari.
Nauliza waungwana kosa langi ni lipi? Na nimtendeje huyu dada? Nahisi maenidhalilisha kwa jirani yangu!

Wasalaam,
HP

Are you serious bro?
 
Back
Top Bottom