Nimfanyaje huyu dada? Yamenikuta leo asbh

mkuu ina maana baada ya salamu, hakukuwa na maongezi mengine ndani ya gari na huyo binti wa njiani ?
Its so strange afyonye bila ya sababu.
 
siku ingine ukikutana nae mtangulize kabisa nyumba ya kulala wageni maana anakutaka live...usichezee hiyo bahati ya mtende!!!! wengine wanaililia sana iyo bahati..
 
Je umeoa? Na kama bado huyo mpenda lifti anajua kuwa upo upo? Si unajua tena eligible bachelors wanazidi kupungua. Lol.

Ila kweli amekudhalilisha kwa kumssonya jirani yako.. Dawa ni kupiga tinted hiyo gari hakuna kumpa mtu lifti; watakutega hao, kuna wasichana wana ugonjwa wa magari na wengine kama alivyosema mdau majini visigino na wengine manyoya. Lol.

Jamani, naapa kabisa sijawahi kumwambia neno lolote huyu dada isipokuwa salamu na kumjulia hali yeye na familia yake. Ni huruma tu ya kumsaidia lifti nahisi ndiyo imeniponza.
 
Jamani, naapa kabisa sijawahi kumwambia neno lolote huyu dada isipokuwa salamu na kumjulia hali yeye na familia yake. Ni huruma tu ya kumsaidia lifti nahisi ndiyo imeniponza.
Lift haiponzi bana..........
lazima kuna mbwembwe nyingine....
wakati wa kurudi mlikuwa hampitiani nyie??
kabla ya kuingia home, moja moto moja baridi??!!!

Funguka kaka..........funguka!!
 
au huyo jirani naye alimuonyesha zarau?si unajua tena dada zetu walivyo na wivu usio na maana
 
Hii ni kali!
Nimesoma hadithi nyingi, huwa zinaelekeana lakini ya kwako hii ni ya aina yake!
Wanawake wana wivu sana na ni roho mbaya kichizi!

Lakini wewe mwenyewe huenda hujatulia, unaweza kukuta unajieleza mambo mazuri tu, usikute ushalikoroga sana na huyo mdada wa watu siku za nyuma!...kwanini asonye wakati hajui kuwa huyo ni dada yako au shangazi yako?
Anaijua tabia yako huyo mkuu!..badilika!
Inawezekana mhusika kuna ukweli ameuficha, lakini all in all huyo dada atakuwa ni mswahili tu.
 
Ndg naombeni ushauri maana najua kesho tena naweza kumkuta eneo lile lile na sijui nichukue uamuzi gani wa busara, msaada pliz!
 
Inawezekana kutokana na maongezi yenu aliamini kwamba uko interested na yeye.

Kuna watu bwana (wanawake kwa wanaume) hata ukimchekea tu basi anadhani ndo umempa ndio. . . achilia mbali kumpa lift. Kwahiyo inawezekana sana wewe hukua interested na wala hukuonyesha dalili ila kwa vyovyote vile huyo dada anaamini ukarimu wako ulikua dalili za wewe kumtaka.

Cha maana mpotezee asije akakwendea bwagamoyo bure.
 
Ndg naombeni ushauri maana najua kesho tena naweza kumkuta eneo lile lile na sijui nichukue uamuzi gani wa busara, msaada pliz!
Don't judge each day by the harvest you reap but by the seeds that you plant.
 
Kama ni ujenzi wa ghorofa la matumaini, basi dada alikuwa kwenye rosheni ya kumi na mbili.

Ila sijaelewa kitu kimoja, huyo dada anawafahamu nduguzo wote?
 
Achana naye tupa kuleeeeeeeeeeeee!
Siyo jukumu/wajibu wako kumbeba garini mwako.
Amejijengea dhana kuwa mna kitu kati yenu - wewe kwani ulimpa picha gani au uliwahi kumtongoza?
 
Inawezekana kutokana na maongezi yenu aliamini kwamba uko interested na yeye.

Kuna watu bwana (wanawake kwa wanaume) hata ukimchekea tu basi anadhani ndo umempa ndio. . . achilia mbali kumpa lift. Kwahiyo inawezekana sana wewe hukua interested na wala hukuonyesha dalili ila kwa vyovyote vile huyo dada anaamini ukarimu wako ulikua dalili za wewe kumtaka.

Cha maana mpotezee asije akakwendea bwagamoyo bure.

mmh...bwagamoyo kuna nini tena huko...!!??....just curious...
 
Lift haiponzi bana..........
lazima kuna mbwembwe nyingine....
wakati wa kurudi mlikuwa hampitiani nyie??
kabla ya kuingia home, moja moto moja baridi??!!!

Funguka kaka..........funguka!!
Hhahahaha!!!
 
Mbona mkuu HP hiyo kesi imeisha toka pale alipozira na kukataa kupanda gari!...au nini unataka zaidi ya hilo?kama lifti ulitoa kwa huruma yako,mpewaji sasa haitaji wewe unatafuta kitu gani kingine?....au mkuu kuna kitu zaidi ya lifti ambacho unaona utapoteza kutokana na hilo tukio?.....yeye kapotezea then wewe potezea zaidi yake....hakuna kesi hapo kiongozi.
 
Back
Top Bottom