Nimezipenda solution za January Makamba kiukweli

KAMATI ya Nishati na Madini imeamuru kuwashwa mara moja kwa mitambo ya kuzalisha umeme ya Kampuni ya Dowans ili kupunguza tatizo la mgawo wa umeme.
Hatua hiyo ni kati ya maazimio na mapendekezo 30 yaliyofikiwa na kamati hiyo na huku ikisisitiza kuwa iwapo serikali itayatekeleza kwa haraka itasaidia kuiondoa nchi katika athari za kiuchumi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati hiyo kilichofanyika kwa muda wa siku 12, Mwenyekiti wa kamati hiyo na Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba (CCM), alisema kutokana na mitambo hiyo kuwepo nchini ni muhimu serikali iiwashe mara moja ili kuepukana na matatizo ya kiuchumi.
Alisema mapendekezo yaliyotolewa ni yale ya dharura, ya kati na ya muda mrefu ambapo katika moja ya mapendekezo ya dharura, kamati hiyo inataka kupunguzwe megawati 125 zinazotumika katika migodi 4 ya madini ili umeme huo uelekezwe kwa matumizi ya wananchi.
Makamba alisema migodi hiyo haijawahi kuathiriwa na tatizo la umeme hivyo kwa sasa inatakiwa ipunguziwe megawatts 50 na kusisitiza kuwa hatua hiyo inaweza kufanyika hata sasa.
“Katika migodi hiyo hawajawahi kujua wala kuonja makali ya mgawo hivyo serikali ikiamua kulitekeleza hilo linawezekana hata leo hili megawat hizo zikafidie maeneo yenye mapungufu,” alisema.
Alisema mbali na hiyo pia serikali inatakiwa kuhakikisha inatoa mafuta ya kutosha katika mitambo ya kuzalisha umeme ya IPTL ambapo hadi sasa inazalisha kati ya megawat 10 hadi 50 huku ikiwa na uwezo wa kuzalisha megawat zaidi ya 80 hadi 90.
Alieleza kuwa iwapo serikali itashindwa kutekeleza mapendekezo hayo kuna uwezekano wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kupoteza kiasi cha sh bilioni 840 iwapo mgawo huo utaendelea katika kipindi cha mwaka huu.
Alisema mapato ya taifa yamepungua kwa asilimia tano ya pato la taifa ambayo ni sawa na dola bilioni 1.1.
“Mapendekezo na maazimio tuliyotoa ni yale ya kati, dharura na ya muda mrefu na iwapo serikali itatekeleza mapendekezo hayo basi tatizo la umeme litaisha katika kipindi cha wiki moja,” alieleza.
SOURCE:TANZANIA DAIMA
Nilivyokuwa mwanafunzi mlimani ilikuwa kuna kitu tunakiita kuzima moto.. ikimaanisha kusoma ile ya overnite halafu unaingia katika exam.. Nahisi kama serikali inafanya the same katika kutatua tatizo la umeme! Mungu atatufikisha salama japo chombo chetu chenda mrama!
 
Uyo Makamba ni kama baba yake akuna kitu anatafuta sifa tuu kujipendekeza kwa mafisadi, atuna imani nae uyo
 
Back
Top Bottom