Nimetokea mahabusu kumuona Lema leo

Good, Big up sana! Kwa msimamo wako nimejifunza kitu.

Hakika umeonesha uwakilishi imara, ww ni mbunge pekee Tz usiyeogopa, kwa asiyejua unacho kifanya ni rahisi kusema unajikweza na kutafuta sifa.

Tunayafahamu maovu wanayotendewa wananchi ambao hawana wa kuwasemea, umefika wakati wa ukombozi wao. Vijana tusimame imara.
 
Naona wewe Ritz unashikishwa ukuta na huyo Nape anyekulipa mshahara kwa kuongea pumba tumia kamati kuu ya akili yako kufanya uamzi wewe ni moja ya vijana wapumbavu nchii hii

Tumewazoea CHADEMA, ndio wakati wenu wa kijipromoti kwa wapiga kura, maana mara mtoke bungeni mara mpige huyu leo mnakataa dhamana ili mradi mpate huruma ya wananchi ,mmekuwa bidhaa mbovu? Maana bidhaa mbovu inamatangazo mengi sana.....

Kwanza wewe lema ungetambua maovu yako ucngali tatufa umaarufu kwa njia hy, hapo ulipo ni sheria nzuri zinazokulinda hata mpaka unatambuliwa kama mbunge , nyuma yako unamadhambi ambayo huwezi kupewa hata ujumbe wa nyumba kumi.

Na wala hulingani na Mzee Mandela kama wanavyokulinganisha naye wajinga wenzio... Kaa humo utatoka kwa mujibu wa sheria tuu
 
Ukienda tena mwambia hivi tarehe 14 asikubali kuja mahakamani..

Siku moja tu kaishanza kulalamika kaa miaka mitatu at least ndio uanze kulalamika

kalalamika wapi wewe uko bias mpaka basi kwani lazima uchangie?
 
NGOROMIKO kikwetu hili jina linamaana ya UHARO! Bado kidoogo CHANGE will start from Arusha!
 
Homeboy ndo kitu gani? Sitaki kuhusishwa na homeboy kanjanja wa kisiasa kama Godbless. Mrudisheni shule kwanza huyo dogo wenu, anatutia aibu hapa Arusha.
Kama mtu ambae hajasoma naweza kufanya vitu vilivyofanya na Lema basi kumbe hakuna haja ya kusoma.....Bona dr, dr, dr, dr, Kikwete ameshindwa kuchukua maamzi mazito...
 
Dah! Huyu LEMA anadamu ya ajabu na pekee sana. Kama kweli nia yake ni njema basi siku moja italipa tu
 
Kesho kutakuwa na mgomo wa daladala kumuunga mkono kwa uamzi wake huo...CCM wana haha kuwa bembeleza wasigome

Hapa ndipo tunapataka, wakianza A town, Mza wajibu, Mbeya wajibu Dar wajibu timbwili la siku moja tu utaona moto. hawa jamaa wa dala dala kama watagoma kweli, watakuwa wametupa somo na sie wengine nini cha kufanya, kwenye sector zote ni kugoma tu basi!! ni zaidi ya kuandamana.
 
Wacha aendelee kukaa huko jela kama alivyotaka.
Pale ndipo panapomstahili yeye na wahalifu wenzake.
Nadhani alikuwa amewa-miss sana machalii waliofungwa siku nyingi....sijui walimpokeaje.

Arusha is a better place without Lema!

wewe sema Arusha is better place without lema,soon will Arusha is a bitter place without mafisadi sisiem,nyambafu.
 
Big up kamanda sisi wanavyuo wote tupo nyuma yako,mapinduzi ni lazima! Wanataka hawataki, kaza moyo kaka.
 
tumewazoea cdm , ndio wakati wenu wa kijipromoti kwa wapiga kura, maana mara mtoke bungeni mara mpige huyu leo mnakataa dhamana ili mradi mpate huruma ya wananchi ,mmekuwa bidhaa mbovu?

Maana bidhaa mbovu inamatangazo mengi sana.....kwanza wewe lema ungetambua maovu yako ucngali tatufa umaarufu kwa njia hy, hapo ulipo ni sheria nzuri zinazokulinda hata mpaka unatambuliwa kama mbunge , nyuma yako unamadhambi ambayo huwezi kupewa hata ujumbe wa nyumba kumi. Na wala hulingani na Mzee Mandela kama wanavyokulinganisha naye wajinga wenzio...

Kaa humo utatoka kwa mujibu wa sheria tuu

Madhambi yake ni yapi yataje ueleweke na kwa nini humshitaki!?
 
ASANTE KAKA Nimetokea magereza kuu ya mkoa wa Arusha, Kisongo ambako nilikwenda na mke wa Lema na watoto wake. Watoto wake wawili Allbless na Brilliant hawakuruhusiwa kumuona baba yao na wamelia kwa uchungu mkubwa sana wakati askari magereza walipowazuia.

Lema yupo Imara na still msimamo wake uko palepale. Ameona na azidi kujifunza mengi, amewakuta watu wengi wanaolalama kwa kubambikiziwa kesi, amewakuta maskini kibao ambao wamefungwa kwa sababu ya kushindwa kulipa faini ya pesa kidogo na ameomba watu wenye nia njema wachange fedha kuwasaidia watu hao waondoke magereza.

Amewakuta wafungwa wanawaKe wakikosa huduma muhimu kama vitambaa vya kike yaani pedi na hali ni mbaya sana.

Wakati tunaondoka alimwambie mke wake "BE STRONG, The purpose of life sio kisses na maisha mazuri. BE STRONG KAMA MKE WA MARTIN LUTHER CORETTA KING"

Wanaonibeza wacha wanibeze lakini kukaa gerezani kuna maana kubwa sana kwangu.

Nawasilisha
 
Anakusanya data magerezani kwa ajili ya kushusha hotuba kali nyingine ya kambi ya upinzani kuhusu wizara ya mambo ya ndani. Ukimaliza kazi na kutoka naomba namba yako nitume pesa kwa m pesa uwafikishie wafangwa hao wa kike, nakushauri uanzishe NGO ya kusambaza pedi kwa mama zetu wafungwa iwe kwa nchi nzima, nipo tayari kufanya kazi kwa kujitolea kwenye NGO hiyo.

Nina mengi ya kuongea na Lema anayejua namba yake airushe. HONGERA SANA KAMANDA LEMA.
 
Poa kakanakuombea kwa mungu. Wasiwasi wangu ni namna unavyoishi huko na chakula unacho kula mh hadi huruma lakini mungu yupo
 
Nafikiri hao mama zetu watakuwa wanatumia nguo wanazopewa kwa ajili ya mazoezi kujistili. Pole sana sana ukumbukwe hao mama zetu walioko huko ni wale hata hiyo pedi hawaijui na wao wanaona kawaida tu inatisha kaka
 
All will be well with those who are tortured fighting for what they believe...
source, Wambura. ni hayo tu
 
tumewazoea cdm , ndio wakati wenu wa kijipromoti kwa wapiga kura, maana mara mtoke bungeni mara mpige huyu leo mnakataa dhamana ili mradi mpate huruma ya wananchi ,mmekuwa bidhaa mbovu? Maana bidhaa mbovu inamatangazo mengi sana.....kwanza wewe lema ungetambua maovu yako ucngali tatufa umaarufu kwa njia hy, hapo ulipo ni sheria nzuri zinazokulinda hata mpaka unatambuliwa kama mbunge , nyuma yako unamadhambi ambayo huwezi kupewa hata ujumbe wa nyumba kumi. Na wala hulingani na Mzee Mandela kama wanavyokulinganisha naye wajinga wenzio... Kaa humo utatoka kwa mujibu wa sheria tuu
Ushambenga mtaacha lini? kama unayajua maovu yake nani kakukataza kuyaweka wazi kama watu wengine wanavyoweka wazi ufisadi wa viongozi wa CCM?

Kama madhambi yake hayana nafasi hata kumpa ujumbe wa nyumba kumi mbona hamkuweka pingamizi wakati wa kupitisha fomu NEC? ni upuuzi kupoteza muda kwa kuandika habari za kufikirika na za uzandiki.

Mpende msipende Lema kaonyesha njia kuwa kama mlidhani Magereza ndio silaha yenu ya vitisho basi yeye kaenda mwenyewe hivyo na wengine hawataogopa kitu kinachoitwa JELA wakati wakitetea haki.

Kama hao madereva wa daladala watafanya mgomo wao waliosema watafanya, Hakika nawaambieni Arusha itaingia kwenye vitabu vya historia kama mahali ilipo asisiwa Tanzania mpya tunayoitaka
 
MKOA WA KINONDONI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM

Tamko la katibu wa mkoa wa Kinondoni Kanda Maalum ya Dar es salaam

Ndugu zangu wanahabari

Nimewaita hapa leo kwa lengo la kuwapa watanzania msimamamo wangu na
wa chama ngazi ya mkoa kuhusu tukio la kukamatwa na kupelekwa magereza
kwa Mhe. Godbless Lema Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini.

Imekuwa ikizoeleka kwa muda mrefu sasa kwamba waheshimiwa wabunge wa
CHADEMA na wale wanaaotokana na vyama vya upinzani wamekuwa
wakinyanyaswa sana kwa lengo la kuwafanya wajute kuingia katika siasa
za upinzani Tanzania.

Hii kwa CHADEMA haitokei tu kwa waheshimiwa wabunge bali hata kwa
viongozi wa ngazi zote. Inaonekana kuwa sasa serikali ya Chama Cha
Mapinduzi imeamua kutekeleza kwa vitendo mkakati wa kuwatesa kwa siri
na kwa wazi wale wote wanaoipinga siasa kandamizi na zisizowalazimisha
watawala kuwajibika kwa wananchi.

Mkakati huu umetungwa na CCM, unasimamiwa na usalama wa taifa na
unatekelezwa na jeshi la polisi. Kwa hakika hatuhoji tena kwamba jeshi
la polisi ni kitengo cha kusimamia maamuzi na maelekezo ya CCM badala
ya kulinda raia na mali zao.

Mheshimiwa Godbless kama mbunge wa wananchi wa jimbo la Arusha Mjini
amekuwa akifuatwafuatwa na jeshi la polisi kila mara na kufanyiwa
vitendo vingi vya udhalilishaji na unyanyasaji hasa kwa kupitia OCD wa
Arusha Mjini Zuberi.
Mathalani wiki iliyopita siku ya ijumaa tarehe 28/10/2011 Mhe.
Godbless lema akitoka mahakamani alisindikizwa na wananchi wake kutoka
mahakamani hadi ofisini kwake. Wafuasi wake walipomfikisha ofisini
waliondoka na kurejea makwao. Huko ofisini aliwakuta wananchi
wakimsubiri ili awahudumie kama mbunge wajimbo lao. Wakati akiongea na
wananchi ghafla polisi walifika na kuwakamata wananchi wote waliokuja
kuomba usikivu wa mbunge na kuwapeleka kituo kikuu cha polisi.

Mbunge Lema alipokwenda kituo cha polisi kwa lengo la kuwawekea
dhamana naye aliwekwa chini ya ulinzi kwamba eti amefanya maandamano
bila kibali.

Tunahoji: Ni maandamano yapi hayo ambayo Lema aliyafanya na wananchi
wake akiwa angali ofisini kwake? Je maandamano wanayoyazungumzia ni
kuondoka na wananchi mahakamani hadi ofisini kwake? Je kama kuondoka
kwake na wafuasi wake mahakamani ni kosa kisheria; Je kwa Mhe Ole
Sendeka alipokuwa akitoka mahakamani, alikuwa akiondoka na kundi kubwa
la wafuasi wake na kusindikizwa na OCD huyu huyu? Vile vile Mwenyekiti
wa UV-CCM mkoa wa Arusha amekuwa akienda kituo kikuu cha polisi
akisidikizwa na kundi kubwa la wafuasi wake wa CCM. Polisi hawakuwahi
kuwakamata wala kuwaonya. Sasa haya yote yalikuwa maandamano ama
matembezi ya hisani? Maana Arusha kuna msiba mkubwa wa CCM kukataliwa
na wananchi.

Kwa hakika tukio la kukamatwa kwa Mhe Lema, kupelekwa mahakamani na
hatima ye kupelekwa gerezani ni ushahidi wa kutosha kwamba jeshi la
polisi sasa linakamilisha sehemu kubwa wa wajibu wake wa kuibaka
demokrasia.

Hata hivyo tunalitaka jeshi la polisi na serikali ya CCM wajue kwamba
kitendo cha kumpeleka Lema magereza ni ushindi tosha katika harakati
za ukombozi wa taifa hili. Maana hakuna silaha yoyote duniani ama
jeshi la polisi popote pale duniani ambavyo viliweza kushinda vita
dhidi ya ukweli, haki na uwazi.
Ndugu zangu watanzania
Tunawaunga mkono wana Arusha kwa kumpata mbunge ambaye anayatetea
maslahi yao kwa mzigo hata pale inapobidi kwenda gerezani kwa ajili ya
watu wake na hata ikibidi kifo anaweza kusimamia hilo. Alisema Martin
Luther King Jr. 1963 “A man who wont die for something is not fit to
live” na akaendelea kusisitiza “Nobody can give you freedom, nobody
can give you justice or right or anything. You take it!” (STAND UP;
STAND UP 4, UR RIGHT) Hayo yalikuwa maono ya bob marley ambayo
aliyaona mwaka wa 1973,baada ya kuwa amekaa katika mto mmoja huko
jamaica akaona samaki wanapita katika maji lakini samaki wakubwa
wakawa wanawaonea samaki wadogo,hivyo akaona hata hapa duniani hata
wa2 walio juu wanawaonea watu wa hali ya chini.

Kwa watu wanaopinga ama kukejeli maamuzi ya Godbless lema kukataa
dhamana, Wathubutu kufanya ziara huko Mahospitalini wavae sura za
uhasilia wa kibinadamu wakaone watu waliokuwa kama wao jinsi
wanavyotaabika kwa kukosa matibabu ile hali ni walipa kodi wa taifa
hili. Kwanini Godbless asiende jela wakati anasimamia mambo ya msingi
na hayatekelezwi, tukiandamana tunaonekana tunavunja sheria ni
afadhali kwenda sehemu wanayodhani tunaogopa kuliko kukaa kimya kumbe
hatuogopi. Mungu yupo upande wetu na tunaelekea kushinda unyanyaswaji
huu.

Kama ambavyo alivyowahi kusema Martin Luther king jr, ndivyo tunavyo
wahakikishia wana wa Arusha, we will work together; we will stand up
together, we will go to jail together, until justice runs down like
water. maana mateso tunayoyapata ni makubwa kuliko huko jehanam
tusipopajua.

Kwa kuonyesha tuko pamoja katika harakati hizi za kudai demokrasia ya
kweli tunampogeza Godbless lema mbunge wa Arusha mjini kwa kupeleka
ujumbe kwa watawala wanaodhani wanaweza kutumia magereza kama sehemu
ya vitisho kurudisha harakati zozote zile nyuma.

Ujumbe huu uwafikie watawala yakuwa jela sisehemu ya kumtishia mtu
yeyote Yule mwenye akili timamu, mpenda haki bali ni sehemu ya kawaida
ambapo binadamu yeyote Yule anaweza kwenda.

ASANTENI ASANTENI NA MUNGU AWABARIKI WATANZANIA WENZANGU
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom