Nimetoa Ushauri Jamani, Lakini sijui kama ni sawa!!

chiko

JF-Expert Member
Feb 24, 2010
580
245
Nina Rafiki yangu tumejuana kitambo, kwa sasa ni zaidi ya ndugu. Ni mtu mzima amenizidi ki-umri. Bwana huyu amekua mgonjwa wa Figo kwa muda zaidi ya miaka Minne sasa. Ka talaka mke wake wa kwanza, na ana watoto watu wazima. Kaoa tena kama miaka mitatu iliopita, mama mmoja ambae aliachwa pia.

Huyu bwana kila mwezi akija matibabu mjini mimi ndio humsimamia, na humsaidia. Juzi kaja kama kawaida kwa matibabu, akanitobolea siri, kuwa ana mambo mazito yanayomsumbua. Akanambia mke alienda kupima HIV, akapatikana Positive, kaja nyumbani na kuzusha war!, bwana akawa mpole kwa sababu huwa anapimwa kila mara akija matibabu, na anajua hali yake ni Negative. Wote wawili wakaenda kupimwa pamoja, Bibi Positive na bwana Negative. Wakaambiwa warudi tena baada ya miezi mitatu(Incubation Period), majibu yalikuwa vile vile. Bibi karudi chini, lakini bwana, hasira zikampanda...utapata talaka, kwanza nani kakupatia haya maradhi, na mimi mgonjwa, hata unyumba wenyewe wanishinda!.

Bwana kaja kwangu, anataka ushauri, lakini moyoni amejaa hasira ya kutendewa, akaniambia amewacha bibi akilia nyumbani, hajui afanyeje.

Mimi ushauri wangu ni kamwambia, akirudi nyumbani asiwe na hasira, akae chini na mkewe, wazungumze maisha ya baadae, kwa vile ameomba msamaha, amwachie mungu, atahukumu na waendelee kuishi pamoja na kusaidiana, kwani wote wagonjwa, haina haja kuachana, waendelee na matibabu, kila mtu amsaidie mwenziwe kwa ushauri!.

Sijui wanajamvi, kama nilitoa ushauri mzuri ama nilikosea..... Nyinyi mungemshauri vipi?????????
 
Aiseee!!
Wayaongee kama hayatatuliki mzee wa watu aachane nae ajipumzikie asije akafa siku si zake.Na hivi ana matatizo tayari aweke afya yake mbele zaidi kwa faida ya wanawe!
 
wanawake kama hawa wako kibao,hata mimi mke wangu ananipigia kelele kila siku nikapime,kwa vile sijapata ujasiri wa kwenda kupima,siku nikienda kupima halafu sina ujue nitamwondoa yule muhehe,huyo jamaa kama wamezaa aende kwa fundi seremala pale jirani amtengenezee kitanda chake
 
Ngekuwa mie ndo huyo mama nlishaenda kwa babu kitambo kweli , mwambie aende kwa babu ila awe anaamini mie mwenyewe kuna sister angu walikuwa ivo na bana ake sister voltage zinasoma shem hazisomi so wakenda loliondo wakipiga kikombe kwenda kupima baada ya mwezi woote wako pouwa wanasubiri awamu ya pili mwezi wa saba ili waendelee kula bata.
 
Ushauri mzuri!, Lakini nafikiri kwanza, wakae chini na kushusha pumzi
 
Aiseee!!
Wayaongee kama hayatatuliki mzee wa watu aachane nae ajipumzikie asije akafa siku si zake.Na hivi ana matatizo tayari aweke afya yake mbele zaidi kwa faida ya wanawe!

Mke yualia na kusikitika, amuomba mzee asimwache, kwani aibu ataipata, na huenda akaaga mapema kabla siku zake!!!!
 
Mke yualia na kusikitika, amuomba mzee asimwache, kwani aibu ataipata, na huenda akaaga mapema kabla siku zake!!!!
Aibu ndo anaijua leo...acha aipate asije akmharakisha baba wa watu kaburini!
 
Huo ushauri uliompa hauna tatizo lolote ila jamaa inatakiwa awe makini.....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom