Nimetimuliwa na baba mkwe

Huyo baba anakutimua wewe kwamba ni maskini yeye ana uwezo gani? wazee wengine wa ajabu sana.
 
Nina mchumba ambaye nimemchumbia na tuko kwenye mikakati ya kufunga ndoa hapo mwezi wa sita mwakani.
Jana jioni nilitoka na mchumba wangu kwa ajili ya matembezi ya jioni.
Nlipofika nyumbani kwao nikamkuta babake yupo kibarazani na mama yake.
Nikawasalimia lakini baba hakuitikia, akaanza kunigombeza kuwa mimi ni kapuku na sina vigezo vya kumuoa mwanae, akaniambia hapo hapo ulipo, toka nje.
Nikafungua geti na kuondoka.
Binti akawa nanipigia simu haongei chochote analia tuu.
Je niendelee na uhusiano huu au nijiondokee na umasikini wangu/

Mzee ni chadema , wewe umekwenda na jezi la ccm, badilisha jezi mkuu
 
haha haha ha ha ha ha a.
jamaa wenzake ukweni wanaenda na suti yeye anaenda na bukta, hii ni hatari
 
wiki mbili zilizopita kuna rafik yangu alikuwa anafunga ndoa.....siku ya harusi ilipofika si kuna ile maharusi wanaenda saluni asubuhi then saa nane ndo ndoa inafungwa...basi bwanakumbe baba wa binti alikuwa mahali za watu wawili...huyu jamaa yangu ndo akafanikiwa kuoa...sasa siku hiyo binti anatoka saluni na mpambe wake wanaelekea kanisani....mim na bwana harusi tayari tuko kanisan... yule jamaa aliyechukuliwa mahali then akakataliwana n wazaz wa binti akiwa na nduguze... waliliteka gari la bibi harusi + mpambe.....wamekaa nao kusiko julikana kwa wiki nzina na juzi ndo wametelekezwa mahali usiku.....

mpaka mda huu ninaoongea bwana harusi yuko hosp kalazwa.......

presha iko juu sana...........
tutolee story za kijiweni hapa
 
Mtie mimba huyo binti baba atakukubali tu mazee,mahari kala alafu analeta za kuleta ?.

Hiyo hapana aise. Braza angu flani alifanyaga hivyo, alikuwa na mchumba wake walikutana Muhimbili wakiwa wanasomea udaktari, binti wa kinyakyusa. Sisi wengine tuliona wanapendana sana, na hata mi nishafika kwao Upanga mara mbili tatu kumsalimia shemeji. Kumbe dingi yake ambaye ni kigogo wa CCM hampendi jamaa, ati anadai ni mzaramo hana maana. Braza alimpa mimba yule binti na akazaa mtoto, lakini haikusaidia kumbadili msimamo dingi yake, alikataa katakata, jamaa akapigwa marufuku asionekane maeneo. Hadi leo yule dada anakaa kwa babake na analea mwanaye kule, na braza baada ya kushindwa uvumilivu aliamua kutafuta msichana mwingine akaoa, sasa yuko na familia yake. Kuna madingi wana dharau mbaya uspime!
 
Msiwaseme vibaya wazee, kuweni na heshima japo kidogo. Jichunguze na jidadisi kwa nini utimuliwe kama mbwa?
lazima kutakuwa na kosa umelitenda
 
Msiwaseme vibaya wazee, kuweni na heshima japo kidogo. Jichunguze na jidadisi kwa nini utimuliwe kama mbwa?
lazima kutakuwa na kosa umelitenda

Hapana, wengine ni ubaguzi tu! Hivi kwa mfano kuwa mzaramo ni kosa gani? Dingi anamwambia binti yake kuwa yule mzaramo sitaki mumwona nyumbani kwangu! Kisa tu ni mzaramo, hilo ni kosa? Yule mdingi nilikuwa namheshimu lakini kwa hili alinisababisha kumdharau kabisa, imagine mzee kigogo wa chama tawala ndivyo anavyoendesha mambo home kwake, nashangaa hao wenye chama chao wamemwaminije mtu mbaguzi hivyo!
 
safi sana,wababa wa JF mjifunze...mkiona mkwe hana muelekeo mnampotezea...msiache mabinti zenu wakahangaika.......alichofanya huyo baba ni sawa,mtu yeyote mwenye mapenzi na mwanae would do that...!:teeth::whoo:
 
Huyo Baba mkwe hajui hata Carlos Slim Helu alianzia chini ..wazee wengine ni matatizo tupu:redfaces:
Lakini ni sababu hiyo tu ya umaskini ndio imemfanya akutimue?
mie nimeona tatizo kwako Mikela

safi sana,wababa wa JF mjifunze...mkiona mkwe hana muelekeo mnampotezea...msiache mabinti zenu wakahangaika.......alichofanya huyo baba ni sawa,mtu yeyote mwenye mapenzi na mwanae would do that...!:teeth::whoo:

If you do me...i do you!

Nimeikubali signecha yako dada! Hakuna kuremba.
 
Nina mchumba ambaye nimemchumbia na tuko kwenye mikakati ya kufunga ndoa hapo mwezi wa sita mwakani.
Jana jioni nilitoka na mchumba wangu kwa ajili ya matembezi ya jioni.
Nlipofika nyumbani kwao nikamkuta babake yupo kibarazani na mama yake.
Nikawasalimia lakini baba hakuitikia, akaanza kunigombeza kuwa mimi ni kapuku na sina vigezo vya kumuoa mwanae, akaniambia hapo hapo ulipo, toka nje.
Nikafungua geti na kuondoka.
Binti akawa nanipigia simu haongei chochote analia tuu.
Je niendelee na uhusiano huu au nijiondokee na umasikini wangu/

Hapo kwenye red bado kuna utata. Huyo Baba Mkwe mlishawahi kuonana nae? Kwa sababu kwa mtazamo wa kawaida hawezi kukufukuza kama mahari ulishatoa. Mwezi wa sita mwakani sio mbali kama uhai ukiendelea kuwepo, kwa hiyo kuna mambo mengi sana mmeshafanya au kuyazungumza baina yako na huyo mchumba wako na mengine wazazi wa huyo binti watakuwa wamehusishwa.

sasa from no where baba mkwe anakutimua, unajua haiingii akilini...Inawezeka kana kuna something else ambocho huja-disclose hapa jamvini ambacho kime-lead wewe kutimuliwa.

Toa maelezo zaidi utapata ushauri....vinginevyo inaoneka kama ni "TAMTHILIA ZA KINA NGOSWE - PENZI KITOVU CHA UZEMBE."
 
dah! kamanda nilizani washakupoteza, mimi bana if you do me i double do you. hakuna kuremba

Sasa ukimdabo do naye akakutripo do.....si utachungulia kaburi ukiwa na gloves zako mkononi?

Hehehe, nani anipoteze kamanda? Mi nikiamua kupotea napotea kwa Osama style.

Shemejio mpya alikuwa kanificha sehemu.
 
safi sana,wababa wa JF mjifunze...mkiona mkwe hana muelekeo mnampotezea...msiache mabinti zenu wakahangaika.......alichofanya huyo baba ni sawa,mtu yeyote mwenye mapenzi na mwanae would do that...!:teeth::whoo:

Sasa huyo mwenye mapenzi na mwanae kamwachanisha na mchumba, sasa hivi binti yuko anapuyanga na mabwana wa kuazima tena waume za watu, wakati mchumba wake yule aliyeambiwa ni mzaramo hafai sasa hivi ana maisha mazuri kaoa ana familia nzuri yenye upendo, na ana kazi nzuri analipwa in USD tena mafungu ya maana. Kiko wapi?
 
Sasa ukimdabo do naye akakutripo do.....si utachungulia kaburi ukiwa na gloves zako mkononi?

Hehehe, nani anipoteze kamanda? Mi nikiamua kupotea napotea kwa Osama style.

Shemejio mpya alikuwa kanificha sehemu.
heheh aminia kamanda, majuzi nilikwoti lile signecha lako ili kuelimisha jamii. i hopu haliko kopiraited , lile you better have plain waifu, acha nikaongeze uzito mwilini bana, hapa natumia imajensi protini za uzazi, tangu usku wa jana sijalamba menu.
 
Nina mchumba ambaye nimemchumbia na tuko kwenye mikakati ya kufunga ndoa hapo mwezi wa sita mwakani.
Jana jioni nilitoka na mchumba wangu kwa ajili ya matembezi ya jioni.
Nlipofika nyumbani kwao nikamkuta babake yupo kibarazani na mama yake.
Nikawasalimia lakini baba hakuitikia, akaanza kunigombeza kuwa mimi ni kapuku na sina vigezo vya kumuoa mwanae, akaniambia hapo hapo ulipo, toka nje.
Nikafungua geti na kuondoka.
Binti akawa nanipigia simu haongei chochote analia tuu.
Je niendelee na uhusiano huu au nijiondokee na umasikini wangu/

Mzee wa Kichagga

duh pole sana mzee,nilipata maswahibu kama yako kwa kupata mkwe wa dizaini hii na kabila hilihili,lakini uzuri mchumba niliyepata ndie aliyenipa plani moja kubwa sana ili nikubalike kwa mzee.baada ya hapo tulimpiga mzee usanii wa hali ya juu sana tukakubalika na kuendeleza mapenzi,ila baadae binti alinigeuka maana tulishindwa ku proof kama kweli niko well-off.na mzee ananisaka mpaka leo atoe hasira zake za kuingizwa mjini.
mbinu niliyotumia sikushauri,ushauri wangu msikilize binti anasemaje,mkielewana yeye ndio wa kumpiga chini huyo mzee wake kisha aambatane na wewe,vinginevyo we endelea na maisha kuna mabinti wengi wazuri wanatafuta kuolewa hata hapa jf utapata ukitaka.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom